Hali ni tete Mtwara Leo, Sakata ya Gesi

baada ya kutoridhishwa na bajeti ya nishati na madini vurugu zimeshaanza mitaa ya Magomeni, Soko kuu na Coco beach Pande za mtwara ....
nimetulia ndani naskizia mabomu yanavurumishwa ...
for more updates stay tuned ....


Kwenye red hapo kama uko ndani tutapate updates????????????????????????????


kama sio za kutunga!:kev:
 
mbona naona wamejaa vina wetu wale wanaopewa 5000 ili wafanye fujo hii siyo ya mtwara nzima bali ni kundi la wahuni.
 
wengi

wenu mnaowapa sapoti watu wa Mtwara wala hamuishi Mt,yaani mpo nje ya
Mtwara,sasa nyie wanamtwara jidanganyeni tu eti mnaandamana mkidhani mpo
wengi!kwanza wengi wenu mna comment mkiwa ndani ya nyumba zenu,ndio
isitoke kweli?HAMUNA AKILI NYIE.
hv mnashindwa hata kujiuliza,ni sehemu gani Tanzania raia waliwazidi
askari ktk mapambano?..KUMBE MNAFANYA MIZAHA NA SMG,Madhara yake
mutayajua kesho kwenye misiba mtakapoo waona watoto wanalalamika kufiwa
na wazazi wao,nani atawalea?

acha utoto, nguvu ya umma siku zote hailinganishwi na askari. Asikari wenyewe hawafiki hata laki mbili wa majeshi yote. Je utalinganisha na raia zaidi ya milion 30 wenye uwezo wa kupigana? nyie ndo mnawapa watu hasira na baadae watu wakiamua kufanya kweli mnabakia kuwayawaya Unafikiri misri, tunisia na kwingineko kulikuwa hakuna askari ? jifunze busara na si zarau za kitoto hizo zinazoweza kuleta madhara makubwa .
 
Mji mkongwe wa Mikindani hali ni ngumu. Vurugu zimetawala na ofisi za serikali ze mitaa karibia yote zimeteketezwa kwa moto ikiwemo ofisi ndogo ya Mbunge wa Mtwara mjini.

Polisi wameingia Mikindani kupitia bahari baada ya barabara zote zinazoingia na kutoka kufungwa na wananchi wenye hasira. Hali ni tete kwani kuna boti mbili zinapeleka askari kwa wingi huko.

Chanzo: Ndugu aliyeko huko.
 
Cvm wanayataka wenyewe .. Suala la kutumia diplomasia kulimaliza wao hawataki hawajali wanatumia nguvu.. No wonder hadi bungeni wanamwaga mitusi ya nguoni
 
acha utoto,
nguvu ya umma siku zote hailinganishwi na askari. Asikari wenyewe
hawafiki hata laki mbili wa majeshi yote. Je utalinganisha na raia zaidi
ya milion 30 wenye uwezo wa kupigana? nyie ndo mnawapa watu hasira na
baadae watu wakiamua kufanya kweli mnabakia kuwayawaya Unafikiri misri,
tunisia na kwingineko kulikuwa hakuna askari ? jifunze busara na si
zarau za kitoto hizo
zinazoweza kuleta
madhara makubwa .

tumia akili,kwani mtwara mpo watu m 30?
unadhani bunduki moja ya askari ina replace raia wangapi wenye mawe?MTU UMEJIFUNGIA NDANI HALAFU UNAPIGA KELELE ETI,HAITOKI,!Hizo c ndizo kelele zenyewe za chura?
 
Ni milio ya risasi na Mabomu kila kona Polisi wanapambana na Wananchi wenye hasira baada ya serikali kutangaza azma yao ya kusafirisha gesi kwa bomba kwenda Dar.kauri za wanasiasa zilizo jaa jazba wakiongelea mbali na eneo la tukio wamekwisha sababisha maafa.Nani wa kutunusuru na balaa hiliiiii
 
Hakuna haja ya kunusuliana,mambo mdundo kama syria,acha tuharibu vizazi vijavyo watarekebisha.
 
Serikali Mtwara haipo kwa sababu mkuu wa mkoa angejitokeza na wananchi wakakaa kwenye uwanja wa wazi wasikilize wote hotuba ya waziri wa nishati na madini ,ili kwa pamoja weka usalama wa mtwara sasa serikali mtwara imejificha imeacha jeshi la polisi wameteka mji wanadhani wananchi watakubali hawawezi kukubali
 
Sababu za vurugu:

1) Kukatishwa kwa Matangazo ya TBC 1 ili watu washindwe kuona Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Hiyo ilitokana na vipeperushi vilivyokuwa vinasambazwa mkoani Mtwara vya kuhamasishana watu wasiende makazini ili kuangalia Bajeti ya Wizara hiyo ikisomwa siku ya leo.

2) Wananchi wanalalamika ya kuwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo haina faida kwao kwani haijaonyehsa kutatua matatizo ya gesi mkoani Mtwara.

Je, TBC 1 mna maana gani kukatisha matangazo kwa watu wa Mtwara?

Mmefanya hivyi ili iweje? Je, wananchi wa Mtwara hawana haki ya kuona matangazo ya Televisheni?

Kuna siri gani kwenye Hotuba ya Wizara ya Nishati?Tuwe waangalifu..TV ni ya Umma na si ya watu wachache.

Na inaendeshwa kwa kodi za Watanzania.

Nawasilisha.

TBC Kuna watendaji wa ovyo sana wasiojua saikolojia. Ilipaswa sana leo hii wananchi hawa waachwe wasikilize hotuba yooooote bila kuingiliwa ili wasikie Waziri atasemaje kuhusu gesi ya Mtwara. Hata kama hotuba hii ingezungmza mazuri kwa wana Mtwara na gesi yao TBC kuzima matangazo ya TV kumeleta hisia mbaya kwamba kitakachosemwa kitakuwa hakina maslahi kwao. TBC huku wakidhani kuzima matangazo kungesaidia kuleta amani ikifananishwa na ndege aina ya kware ambaye huficha kichwa chake akiwa amefumba macho akidhani haonekani kisa kwasababu yeye mwenyewe haoni kumbe kwasababu kafumba macho, ndivyo TBC walichokifanya. TBC wamejaribu kuzima matangazo yao lakini siyo hisia za wana Mtwara na umoja wao.

Sasa kama kawaida CCM kupitia Nape watakuja na yao kwamba waliochoma ofisi hizo ni CUF au CHADEMA. La hasha si hao bali ni MAGAIDI
.
 
Serikali Mtwara haipo kwa sababu mkuu wa mkoa angejitokeza na wananchi wakakaa kwenye uwanja wa wazi wasikilize wote hotuba ya waziri wa nishati na madini ,ili kwa pamoja weka usalama wa mtwara sasa serikali mtwara imejificha imeacha jeshi la polisi wameteka mji wanadhani wananchi watakubali hawawezi kukubali
kwa jinsi wana mtwara walivyodanganyika, hata kama serikali itaamua kumjenge nyumba kila mtu na kumpa mtaji wa biashara, hawatakubali. wamedanganyika kweli. hivi kwa ile speech ya leo ya waziri wa nishati na madini kulikuwa na sababu kweli ya wana mtwara kuleta fujo? au kwa vile ndo hawajaisikia
 
kwa nini sasa jengo la ccm lichomwe moto? hawa watu wana malengo gani?
Unashangaa hilo mbona Masasi walichoma ofisi ya Halmashauri, magari yaliyokuwepo mpaka jengo walilokuwa wanatumia manesi wanafunzi kama hosteli. Haya na manesi wanahusika vipi hapo?
 
Tanzania nzima TBC 1 haionekani mpaka kwa satelite usije sema ni mtwara kwa 7bu ya badget unakosea ila kama umefanikiwa kuwa na king'amuzi umeona badgeti iko poa na wala sina tatizo nayo kama itafanikishwa kwa yaliyosemwa na waziri. Ila TBC kukatisha matangazo ni nchi nzima sio kusini pekee jarb kuwa mtafitiii

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom