Hali ni tete Mtwara Leo, Sakata ya Gesi

Kipanya+kuhusu+umeme++2.jpg
Kuingia na kutoka vyote vinafanana na ukitembea umeinama yawezekana ukajiona uko sahihi kumbe kituko.
 
alafu mlio hapo kongo mbona hatuwaoni hapa kwenye picha au mshayapatia maisha uku town
 
Ni baada ya kukunwa na hotuba ya waziri wa nishati wakati anawasilisha hotuba yake kuwa gesi itawanufaisha kwanza wanamtwara na mikoa ya jirani kabla ya maeneo mengine ya nchi..vijana wanasherehekea mitaani na kumpongeza muhongo

Wenzako wapigwa mabomu au ndo sherehe unayoisema?
 
swali, kwani wazimiwe umeme tokea jana? ina maana sirikali ilipanga kupambana na wananchi badala ya kuwaelimisha. gesi haitoki hata kwa bomba la peni, mtwara kwanza bagamoyo baadae
 
Kama watu wanaweza kutoka mtwara kwenda dar kununua mizigo,kwa nini ishindikane kutoka dar kwenda kununua gesi mtwara?serikali itumie tu busasa iwatumie wapinzani wazungumze na hawa watu..unajua sasa hivi wananchi wengi wanaamini kuwa ccm wote ni wezi,kwa hiyo ni vigumu kuwaambia kitu wananchi wakawaamini..
 
Hamna litakalowashinda kama umoja na msimamo utakuwepo mkilemaa yaliyowakuta watu wa mara na dhahabu yao na nyie msubirie komaeni
 
baada ya kutoridhishwa na bajeti ya nishati na madini vurugu zimeshaanza mitaa ya Magomeni, Soko kuu na Coco beach Pande za mtwara ....
nimetulia ndani naskizia mabomu yanavurumishwa ...
for more updates stay tuned ....

Tatizo bado liko ni kwa nini hiyo bajeti haikusomwa hiyo jana. Wameenda kufanya EDITING ili waje wawahadae watu wa Mtwara. Wanawona kama vile hawana akili. Serekali ya CCM imetoa ahadi likuki tangu mwaka 2005 mpaka sasa hawajaweza kutimiza leo uje uifanye Mtwara kuwa kama Ulaya? Haya ni matusi makubwa tena ya nguoni kwa wanamtwara. Walikua wapi siku zote wasiifanye iwe Ulaya leo hii ndio wafanye iwe ulaya. Wana uhakika gani hao CCM kama watakua madarakani ifikapo 2015 na wawe na bunge lenye maamuzi na Serukali ya kubabaosha kama ilivyo sasa. Wananchi wa Mtwara msikubali biashara ya kuchunga nyumba alafu mwenyumba anakwambia nikirudi nitakuletea peremende. Hiyo eremende ndani ya dakika tano itakua imeisha na pia haishibishi. Komaeni hata kama ni huyo Obama Ahirishe kuja Tanzania.
 
wengi

wenu mnaowapa sapoti watu wa Mtwara wala hamuishi Mt,yaani mpo nje ya
Mtwara,sasa nyie wanamtwara jidanganyeni tu eti mnaandamana mkidhani mpo
wengi!kwanza wengi wenu mna comment mkiwa ndani ya nyumba zenu,ndio
isitoke kweli?HAMUNA AKILI NYIE.
hv mnashindwa hata kujiuliza,ni sehemu gani Tanzania raia waliwazidi
askari ktk mapambano?..KUMBE MNAFANYA MIZAHA NA SMG,Madhara yake
mutayajua kesho kwenye misiba mtakapoo waona watoto wanalalamika kufiwa
na wazazi wao,nani atawalea?
 
Huko tunakoelekea wizara ya mambo ndani itakuwa inatenga 90% ya bajeti yake kwa ajili ya kununulia mabomu ya machozi maana wanayatumia kwelikweli

Wewe umenena! pia unajua kwanini ata polisi wanashabikia sana hayo mabomu na kuwakusanya hata wsiousika? ndipo nawao wanapopatia rushwa.
Iringa ilirindima mabomu jumapili na watu kibao wakachukuliwa walio na hatia na wasio na hatia matokeo yake waliobakia ndani waendesha mashtaka wameanza kuomba mlungula hasa dpp J yupo hapo maakamani yaani ni aibu kweli.
Yaani hatuna ata pa kukimbilia wananchi ni full kunyanyaswa.
 
Nimesikia wamekata matangazo ya Radio na TV huko Ntwara ili wasisikilize kinachoendelea Bungeni.
mlioko huko tupeni habari kamili.

Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania inaelezea kuhusu Haki ya Uhuru wa Mawazo, ukisoma kuanzia (a)- (d) na hasa kipengele (d) inasema kila mtu "anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii"- Ikiwemo kusikia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini..

Kwa mantiki hiyo, ni kukiuka Sheria mama (Katiba) endapo ni kweli kuwa unyimifu huo wa habari umefanywa kwa makusudi! jambo ambalo nadhani serikali hii iliyopo madarakani haiwezi kufanya labda watendaji wake baadhi kwa maslahi yao binafsi. Nawasilisha.
 
Sababu za vurugu:

1) Kukatishwa kwa Matangazo ya TBC 1 ili watu washindwe kuona Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Hiyo ilitokana na vipeperushi vilivyokuwa vinasambazwa mkoani Mtwara vya kuhamasishana watu wasiende makazini ili kuangalia Bajeti ya Wizara hiyo ikisomwa siku ya leo.

2) Wananchi wanalalamika ya kuwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo haina faida kwao kwani haijaonyehsa kutatua matatizo ya gesi mkoani Mtwara.

Je, TBC 1 mna maana gani kukatisha matangazo kwa watu wa Mtwara?

Mmefanya hivyi ili iweje? Je, wananchi wa Mtwara hawana haki ya kuona matangazo ya Televisheni?

Kuna siri gani kwenye Hotuba ya Wizara ya Nishati?Tuwe waangalifu..TV ni ya Umma na si ya watu wachache.

Na inaendeshwa kwa kodi za Watanzania.

Nawasilisha.
 
Busara, hekima, utu, uzalendo vingetawala toka mchakato wa kuanza kuchimba gesi...wala Wanamtwara na watanzania kwa ujumla tusingefikishwa hapa...!
 
Back
Top Bottom