Huu ni mwezi May kuna baadhi ya maeneo yanafanya uvunaji wa mazao tayari, kanda ya ziwa wameshavuna mahindi 80% ya mashamba yao sasa hivi wapo wanaendelea na uvunaji wa mpunga ambao upo 40%
70% ya mazao yanayotumika sana nchini kwetu ni mahindi, mchele na maharage haipiti siku waTanzania 7 kati ya 10 wasitumie moja wapo ya haya mazao, Maeneo yanayolima sana ndio yapo kwenye uvunaji mda huu
Mikoa ya kiuzalishaji kama Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Morogoro pia imeanza kuvuna mda huu lakini hatuoni bei ikishuka kwa asilimia kubwa, ikumbukwe nchi yetu inapata mvua vipindi viwili tu kwa mwaka (vuli na masika) vuli hutangulia kuanzia september mpaka disember (maanaake vuli imeshapita) sasa tupo mwishoni mwa mvua za masika mvua hizi zilianza mwezi february na zitaisha rasmi mwishoni mwa mwezi huu
Asilimia kubwa ya wakulima tulokuwa nao nchini wanategemea mvua na hapa tukubaliane kwamba hatutapata tena mda wa kuzalisha mazao mengine mpaka mwishoni mwa mwaka, maanaake mazao haya yaliyopo yanatakiwa yatupeleke mpaka mwaka kesho mwezi kama huu
Kama wakulima wapo wanavuna shambani lakini bei hazishuki na hii inatoa picha kabisa kuwa mazao yaliyopatikana msimu huu bado ni kidogo na bahati mbaya wakulima walokuwa wengi wanauzia mazao shambani maanake tayari wafanyabiashara wa mazao mameshajimilikisha mazao ya msimu huu
Nimepita baadhi ya maeneo haswa kanda ya ziwa mkoani Geita halmashauri ya Geita DC mpunga unavunwa bei ya mchele imepungua lkn sio kwa ukubwa huo huko kg 1 ya mchele wanauza kwa Tsh 2000- Tsh 2500 hii ni bei ya mchele mpya kutoka shamba tuna mwezi mmoja na nusu tu wa uvunaji hali ni mbaya
Hapa serikali inatakiwa izuie moja kwa moja soko la nje, tusijidanganye kuwa tunamsaidia mkulima tutaua watu kwa njaa, kama mwezi may bei ni hii vipi mwezi disember? Soko la ndani bado ni kubwa sana linatosha kuuza mazao ikiruhusiwa mazao kwenda nje trust me mazao hayatashikika
Inawezekana serikali inataka kuvutia watu waingie kwenye kilimo sawa lkn lazima tuwe na mgawanyo wa kazi, watu walime mazao tupate chakula, watu wasome tupate wataalamu, watu wafanye michezo tupate wacheza mpira, riadha ndodi nk
Kuna watu wengine hawawezi kujikita kwenye kilimo ila wanachangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa mambo mengine, hebu tuwawazie vijana wanaojenga majengo (mafundi) wanajitoa sana kuijenga nchi yetu tumeona kilichofanyika Dodoma mji unajengwa kweli kweli, vijana hawa kipato chao kipo pale pale hata mh Rais hajagusia masilahi yao leo hii pale Morogoro ataweza kununua chakula kikipanda bei ikiwa pesa anayolipwa ni ile ile miaka yote
Tusichukulie poa hali itakuwa mbaya sana kuanzia mwezi september mwaka huu