Hali ni mbaya, waziri Bashe chukua hatua

Jana nimepita maduka mengi ya jumla huku maeneo ya mbezi yalikuwa hayana mchele zaidi ya wiki, wanasema huko wanakochukua umeisha wanategemea wakulima wavune kwanza. Duka nililobahatisha kupata mchele ule mzuri unauzwa 3,600/= kwa kilo, na inasemekana kuna wanaouza hadi 4000/-.Hivi mwananchi wa kawaida atamudu kweli kuishi kwa bei hizi za vyakula?

Halafu waziri anafanya siasa kwenye jambo nyeti la chakula eti anasaidia wakulima wakati kiuhalisia anawaneemesha madalali na walanguzi wa mazao ambao wana ma-godown ambayo wanayatumia kununua na kuhifadhi mazao ya wakulima kwa bei chee ili waje wayauze kwa bei ya juu nje ya nchi kwa bei wanayotaka.
 
Ahsante sana mkuu,, ila hapa pia kuna watu wanatetea huu uamuzi ngoja tusubr hiyo disemba tuone itavyokuwa
 
  • Je unajua gharama ya kulima heka moja ya mahindi, mpunga, maharage n.k?
  • Je gharama za kilimo zinarudishwa kwa bei ya soko kwa sasa?
  • Kulima si hisani inayofanywa na NGO's ndg; ni uwekezaji.
  • Vijana wawezeshwe kulima ili uzalishaji ukue; na bei uwe inatabirika si kuzipa promo bidhaa za mchina: bodaboda
Mkuu Gharama zipo Juu sana, mwaka huu jua limeathiri sana Mazao yetu Shamba I, timerudia kupanda baadhi ya sehemu. Mbegu zipo Juu, Mafuta ya disiel yapo Juu, madawa yapo Juu, mbolea ipo Juu. Jee kwanini mtake kutumiza sisi wakulima? Wacha soko liamue kama bidhaa zingine zinavyokuwa, Usiangalie Chakula tu angalia Bei ya cement, nondo, mabati, sukari, ngano kutoka nje , sukari? Leo Hii mkulima anatumia zaidi ya shilingi Milioni Moja Kulima Hadi kuvuna ekari Moja ya mahindi kipato chenyewe ni kuanzia Gunia 4 Hadi 14 halafu unasema serikali ipange Bei ya mahindi? Utakuwa na matatizo makubwa ya akili kama hujue changamoto za wakulima. Mtu kama Anaona wakulima wanafaidi karibuni tulime wote Bei ishuke!!
 
Ahsante sana mkuu,, ila hapa pia kuna watu wanatetea huu uamuzi ngoja tusubr hiyo disemba tuone itavyokuwa
Hao wanaokupinga ni kawaida yao, walishajipanga humu jukwaani......kila ukianzishwa uzi wa namna hii wanakuja kumshambulia mtoa mada wakisema wanamtetea mkulima. Lakini ukifuatilia wengi wanakuwa ni madalali na walanguzi wa mazao ambao wanajificha kwenye kichaka cha kumtetea mkulima.

Wakulima tunaowajua huwezi kuwakuta huku JF hasa kipindi hiki cha mavuno.
 
Jana nimepita maduka mengi ya jumla huku maeneo ya mbezi yalikuwa hayana mchele zaidi ya wiki, wanasema huko wanakochukua umeisha wanategemea wakulima wavune kwanza. Duka nililobahatisha kupata mchele ule mzuri unauzwa 3,600/= kwa kilo, na inasemekana kuna wanaouza hadi 4000/-.Hivi mwananchi wa kawaida atamudu kweli kuishi kwa bei hizi za vyakula?

Halafu waziri anafanya siasa kwenye jambo nyeti la chakula eti anasaidia wakulima wakati kiuhalisia anawaneemesha madalali na walanguzi wa mazao ambao wana ma-godown ambayo wanayatumia kununua na kuhifadhi mazao ya wakulima kwa bei chee ili waje wayauze kwa bei ya juu nje ya nchi kwa bei wanayotaka.

Kama hao walanguzi wamenunua bei chee umeshindwaje na wewe kununua kwa bei chee pia?
 
Hao wanaokupinga ni kawaida yao, walishajipanga humu jukwaani......kila ukianzishwa uzi wa namna hii wanakuja kumshambulia mtoa mada wakisema wanamtetea mkulima. Lakini ukifuatilia wengi wanakuwa ni madalali na walanguzi wa mazao ambao wanajificha kwenye kichaka cha kumtetea mkulima.

Wakulima tunaowajua huwezi kuwakuta huku JF hasa kipindi hiki cha mavuno.

Hao walanguzi wananunua bei chee na wewe kanunue bei chee pia huko huko kwa wakulima si umesema wananunua bei chee wanaweka godown sasa na wewe nunua kwa bei chee ila nunua kiasi kidogo cha kula wewe mwenyewe
 
Huku
Ulichokisema Ni sahihi, hali ya bei ya chakula bado sio nzuri,na kusema kwamba mkulima anafaidika nadhani si wakulima wote,asilimia kubwa ya wakulima wa Tz ni wakulima wadogo wadogo,na hao ndio wanalisha nchi kwa kiasi kikubwa,swala la bei ya mazao kuwa nzuri si kweli kwamba wanafaidika nayo,wanaofaidika sanasana ni walanguzi na wakulima wa kubwa,mkulima mdogo akivuna anahifadhi kidogo kwa ajili ya chakula kingine anauza kwa walanguzi kwa bei ya kawaida, na mwisho wa siku mkulima huyo huyo akiishiwa chakula anakuja kununua kwa bei kubwa sana, kwahiyo ili swala liangaliwe upya, wachache sana ndio wanaofaidika wananchi wengi wanabaki wanaumia na mfumuko wa bei ya chakula
Wakulima wanauza direct kwenye soko Mahindi yanakwenda Dar es salaam Sasa tumeanza kuvuna tunauza Kwa Bei nzuri , hatutaki hiyo Bei ya serikali kg Moja NFRA
Hao wanaokupinga ni kawaida yao, walishajipanga humu jukwaani......kila ukianzishwa uzi wa namna hii wanakuja kumshambulia mtoa mada wakisema wanamtetea mkulima. Lakini ukifuatilia wengi wanakuwa ni madalali na walanguzi wa mazao ambao wanajificha kwenye kichaka cha kumtetea mkulima.

Wakulima tunaowajua huwezi kuwakuta huku JF hasa kipindi hiki cha mavuno.
Wakati nalima Shamba Inawekeza pesa zangu na muda wangu wote , tabu na mateso ya kulala porini , aje mjinga Moja anipangie Bei huo ni upuuzi na ujuha wa Hali ya Juu, Kwanini Usiangalie factors za production zinzopandisha gharama za kilimo Cha Mazao mbalimbali?
Bei ya mbegu za mahindi unazijuwa ?
Bei ya Disiel kwenye Kulima ?
Bei ya mbolea ya DAP, Urea, CAN na S A unazifahamu? Unamfahamu Bei ya viwatilifu ? Gharama za kupalilia , gharama za kuvunia, gharama za kupuchulia Mahindi, gharama za kubeba kutoka Shambani ,viroba vya kuhifadhia, Huyu mkulima anauza Mazao yake Alipe madeni, anunue nguo, Alipe ada za shule ,vyuo, na matumizi mengine hiyo ndio ajira yake, Hapati Hela za Bure za kukaa ofsini bila kufanya kazi kama wengine wenu,
Gharama ya Gunia Kwa msimu Kwa mkulima ni zaidi ya Tshs 65000/= wewe unataka mkulima apate hasara lazima mwaka huu Gunia halitapungua 75000/= Kwa Sasa Mahindi yameanza na 95000/= mashambani
 
Jana nimepita maduka mengi ya jumla huku maeneo ya mbezi yalikuwa hayana mchele zaidi ya wiki, wanasema huko wanakochukua umeisha wanategemea wakulima wavune kwanza. Duka nililobahatisha kupata mchele ule mzuri unauzwa 3,600/= kwa kilo, na inasemekana kuna wanaouza hadi 4000/-.Hivi mwananchi wa kawaida atamudu kweli kuishi kwa bei hizi za vyakula?

Halafu waziri anafanya siasa kwenye jambo nyeti la chakula eti anasaidia wakulima wakati kiuhalisia anawaneemesha madalali na walanguzi wa mazao ambao wana ma-godown ambayo wanayatumia kununua na kuhifadhi mazao ya wakulima kwa bei chee ili waje wayauze kwa bei ya juu nje ya nchi kwa bei wanayotaka.
Nenda kalime
 
Huu ni mwezi May kuna baadhi ya maeneo yanafanya uvunaji wa mazao tayari, kanda ya ziwa wameshavuna mahindi 80% ya mashamba yao sasa hivi wapo wanaendelea na uvunaji wa mpunga ambao upo 40%

70% ya mazao yanayotumika sana nchini kwetu ni mahindi, mchele na maharage haipiti siku waTanzania 7 kati ya 10 wasitumie moja wapo ya haya mazao, Maeneo yanayolima sana ndio yapo kwenye uvunaji mda huu

Mikoa ya kiuzalishaji kama Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Morogoro pia imeanza kuvuna mda huu lakini hatuoni bei ikishuka kwa asilimia kubwa, ikumbukwe nchi yetu inapata mvua vipindi viwili tu kwa mwaka (vuli na masika) vuli hutangulia kuanzia september mpaka disember (maanaake vuli imeshapita) sasa tupo mwishoni mwa mvua za masika mvua hizi zilianza mwezi february na zitaisha rasmi mwishoni mwa mwezi huu

Asilimia kubwa ya wakulima tulokuwa nao nchini wanategemea mvua na hapa tukubaliane kwamba hatutapata tena mda wa kuzalisha mazao mengine mpaka mwishoni mwa mwaka, maanaake mazao haya yaliyopo yanatakiwa yatupeleke mpaka mwaka kesho mwezi kama huu

Kama wakulima wapo wanavuna shambani lakini bei hazishuki na hii inatoa picha kabisa kuwa mazao yaliyopatikana msimu huu bado ni kidogo na bahati mbaya wakulima walokuwa wengi wanauzia mazao shambani maanake tayari wafanyabiashara wa mazao mameshajimilikisha mazao ya msimu huu

Nimepita baadhi ya maeneo haswa kanda ya ziwa mkoani Geita halmashauri ya Geita DC mpunga unavunwa bei ya mchele imepungua lkn sio kwa ukubwa huo huko kg 1 ya mchele wanauza kwa Tsh 2000- Tsh 2500 hii ni bei ya mchele mpya kutoka shamba tuna mwezi mmoja na nusu tu wa uvunaji hali ni mbaya

Hapa serikali inatakiwa izuie moja kwa moja soko la nje, tusijidanganye kuwa tunamsaidia mkulima tutaua watu kwa njaa, kama mwezi may bei ni hii vipi mwezi disember? Soko la ndani bado ni kubwa sana linatosha kuuza mazao ikiruhusiwa mazao kwenda nje trust me mazao hayatashikika

Inawezekana serikali inataka kuvutia watu waingie kwenye kilimo sawa lkn lazima tuwe na mgawanyo wa kazi, watu walime mazao tupate chakula, watu wasome tupate wataalamu, watu wafanye michezo tupate wacheza mpira, riadha ndodi nk

Kuna watu wengine hawawezi kujikita kwenye kilimo ila wanachangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa mambo mengine, hebu tuwawazie vijana wanaojenga majengo (mafundi) wanajitoa sana kuijenga nchi yetu tumeona kilichofanyika Dodoma mji unajengwa kweli kweli, vijana hawa kipato chao kipo pale pale hata mh Rais hajagusia masilahi yao leo hii pale Morogoro ataweza kununua chakula kikipanda bei ikiwa pesa anayolipwa ni ile ile miaka yote

Tusichukulie poa hali itakuwa mbaya sana kuanzia mwezi september mwaka huu

Demand and Supply vinapambanaga vyenyewe mara nyingi
 
N muda wa wakulima kutajirika...vjn wapo mjn wanauza vwembe hawatak kulima...serikali isiingilie swala hili...atakayekufa njaa na afe... BASHE ALISEMA KBS HAWATAINGILIA KAT BEI YA MAZAO..watu tumekuwa tukiwekeza kwenye kilimo lkn outcome miaka yote n ndogo achaaa kila mtu ashinde mechi zake...over
Mkulima hatajiriki, wanatajirika mabepari na wafanyabiashara, labda waangalie namna nyinyine kuhakikisha mkulima anatajirika kama mnavyoimba.

Wakulima hali zao ni zilezile.
 
Hao walanguzi wananunua bei chee na wewe kanunue bei chee pia huko huko kwa wakulima si umesema wananunua bei chee wanaweka godown sasa na wewe nunua kwa bei chee ila nunua kiasi kidogo cha kula wewe mwenyewe
Languzi jingine hili hapa.
 
Mkulima hatajiriki, wanatajirika mabepari na wafanyabiashara, labda waangalie namna nyinyine kuhakikisha mkulima anatajirika kama mnavyoimba.

Wakulima hali zao ni zilezile.
Wanataka kutuingiza chaka wapate justification ya kutorosha mazao kwenda nje, hawa hawana tofauti na wahujumu.
 
Labda watueleze, ni wakulima gani hao wanaonufaika na hiki kinachoendelea.

Kule Nyehunge mwezi wa kwanza kuna jamaa yangu katoka kuingia mkataba na wakulima kwa kuwakopesha fedha kwaajili ya kuendeshea kilimo chao, 45K kwa gunia moja la mpunga watakapovuna. Sasa fikiria 450K tu magunia yanakuwa 10, kisha uangalie bei ya mpunga ilivyo sokoni.

Wakulima wa nchi hii hawatawahi kuja kunufaika.
 
N muda wa wakulima kutajirika...vjn wapo mjn wanauza vwembe hawatak kulima...serikali isiingilie swala hili...atakayekufa njaa na afe... BASHE ALISEMA KBS HAWATAINGILIA KAT BEI YA MAZAO..watu tumekuwa tukiwekeza kwenye kilimo lkn outcome miaka yote n ndogo achaaa kila mtu ashinde mechi zake...over
Kama wangekuwa wanatajirika wangekufa kwenye queue wakisuburi mbolea ya rezuku
 
Jana nimepita maduka mengi ya jumla huku maeneo ya mbezi yalikuwa hayana mchele zaidi ya wiki, wanasema huko wanakochukua umeisha wanategemea wakulima wavune kwanza. Duka nililobahatisha kupata mchele ule mzuri unauzwa 3,600/= kwa kilo, na inasemekana kuna wanaouza hadi 4000/-.Hivi mwananchi wa kawaida atamudu kweli kuishi kwa bei hizi za vyakula?

Halafu waziri anafanya siasa kwenye jambo nyeti la chakula eti anasaidia wakulima wakati kiuhalisia anawaneemesha madalali na walanguzi wa mazao ambao wana ma-godown ambayo wanayatumia kununua na kuhifadhi mazao ya wakulima kwa bei chee ili waje wayauze kwa bei ya juu nje ya nchi kwa bei wanayotaka.
Kama huwezi kununua mchele kwa Tsh 4,000 kwa kilo jua kuwa wewe si mlengwa. Usilazimishe kununua mchele wakati kipato chako ni kidogo. Vyakula vyenu vipo vingi tu kama magimbi, viazi utamu, choroko, unga wa mahindi nk.

Hatuwezi wote kuendesha Mercedes, ndiyo maana na Toyota zipo, na yote ni magari.

Usiige kunya kwa tembo utapasuka msamba. Mchele siyo saizi yako
 
Back
Top Bottom