Half rey unajua wewe ni mwepesi kuliko kapi

Half rey unajua wewe ni mwepesi kuliko kapi

Mkuu umeandika maneno ya vizuri sana, ila tambua tu kila jambo chini ya jua linawezekana. Kaa utulie utazame movie ndio uje na conclusion. Jambo la msingi tu ni kwamba huwezi jua yeye anasilaha gani kwahiyo kaa kwa kutulia mkuu. Tuiache vita zidi ya wahuni iishe salama.
Jambo la msingi tu ni kwamba huwezi jua yeye anasilaha gani kwahiyo kaa kwa kutulia mkuu. Tuiache vita zidi ya wahuni iishe salama.
 
Mimi sielewi kitu mnachomnanga hamfrei

Jamaa anapambana na wahuni walioko kwenye chama na wala siyo raisi wa nchi

Ulichoandika ni pumba tu. Sijawahi kumsikia hamfrei anapinga jitihada za raisi samia wala sirikali

Yeye anapambana na wabaya wake kina nape na wengine....

Msizoeee kila mtu atakuwa muoga kama nyinyi kama kufa kila mtu atakufa

Yani kwa mara ya kwanza ndugu mshana umeandika uzi usiojielewaaa kbsaaaa
Asante endelea kufuatila mjadala na hongera kwa mchango
 
Ngoma unayocheza ni ya kitoto mno.. Haina ubavu wa kukesha.... Huna uwezo wa kucheza mnanda au mchiriku siku hizi wanaita singeli.. Hizo ndio ngoma za kihuni sasa.. Kama huna pumzi unaumbuka...!
Salamu kidogo ulizotumiwa ni onyo la kishkaji sana, hizi sio nyakati za jiwe hizi ni nyakati za watoto wa mjini hawakutoi damu wala manundu wanakunjia tu yai kwenye mpasuko kisha wanakupiga picha...
Hakuna anatakayekudhuru hata ukucha ila utabadilishiwa tu santuri za mjini tena kwa mitindo tofauti tofauti.. Wewe ni chawa tena yule kiroboto.. Wanakujua vema.. Ndio maana wameamua kukucheza shere japo kiduchu.. Hizo ni salam tuu ..kama unagutuka gutuka sasa!.. Ukiendeleza ushamba wako hakuna rangi utaacha kuona.. Utasagiwa mpaka kunguni

Hili dubwana linaloitwa SIRIKALI lione hivi hivi...! Unamsikia tena Gwajiboi? Hajaguswa hata ukucha Lakini umeona alivyopoa kuliko marehemu mochwari? Vp na mzee wa PhD famba ya kupigwa? Cheza michezo yako yote lakini ukifika kwenye kibao kilichoandikwa SIRIKALI.. Brother nakushauri ufyate kama mbwakoko ugenini..!

Brother sikio litabaki kuwa sikio.. Kamwe halitakaa lizidi kichwa... Kuna viungo bandia vya kila aina lakini sio sikio lililozidi kichwa! Labda liwe la mdoli...! Ukinyonga na ukigeugeu wako vinasadifu ufinyu wa fikra ulionao.. Dr. Bashiru aliyeamua kukaa kimya sio mjinga..AMEJITAMBUA...!!!
Ulipewa salio la msg ukataka na kifurushi cha internet..! Ulikaribishwa upenuni, ukajiingiza sebuleni sasa unataka kuingia chumbani..Thubutuu.. Hizi adabu umefunzwa wapi? Na nani?

Kama walozi wenyewe tunaigwaya serikali wewe ni nani mpaka ujitie kifutu? Brother angalia na makinika usije ukawa na tabia za kenge! Maana kenge hasikii mpaka damu zimtoke masikioni...!

Usije ukajaribu kuinua kichwa tena.. Rungu zito zaidi litatua juu yake kwa style zilezile za watoto wa mjini...
Leo kuna mtu alikuwa akisema yy anafkr ni move flan ya kutengenezwa na walio upenunini ipi kuwahadaa wa upande wa pili waingie king kumkarbsha kwao kama waliopta ili kutengeneza njia ya uchaguz ujao.......imenifkrsha xana hii pia
 
Screenshot_20211216-065808.jpg
 

Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji. Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.

Sasa kiki ya penalt tayari, mpira wetu Polepole ana hanjahanja, goli nani analifunga!

======

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji huku kamati hiyo ikisimamisha kipindi chake cha Shule ya uongozi na kumpa masharti ambayo anapaswa kuyatimiza ili kirudi hewani.


Akisoma hukumu hiyo, baada ya kusikiliza upande wa Kamati na Upande wa Utetezi, Mwenyekiti wa Kamati, Habbi Gunze amesema maudhui ya kipindi cha shule ya uongozi yalikuwa ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.

"Kuhusu kuwapanga wamachinga, Humphrey Polepole Online TV iliwatuhumu viongozi wa Serikali kuhusu kutofuata maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu ya kuwapanga vizuri wamachinga. Kituo hiki kimevunja kanuni na maadili ya uandishi na utangazaji kwa kutowapa nafasi viongozi hao kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma alizotoa.

"Polepole alitoa maneno ya uongo na udharirishaji kwa viongozi akisema ni waoga na hawajitokeizi kutoa ufafanuzi kuhusu deni la Taifa bila kuwapa nafasi viongozi hao kufafanua madai yake wakati viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Waziri wa fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba mwezi Juni alisema bungeni kuwa deni la taifa ni himilifu.

"Katika utetezi wake alisema amejikita katika utoaji wa elimu tu bila kuzingatia mizania na kwamba TV yake si kama vyombo vingine vya habari vinavyotoa maudhui ya habari, yeye anatoa elimu tu. Pia alidai kanuni hazijitoshelezi kwani hazielezi kwa mtu anayetoa maudhui ya elimu afanyeje, jambo ambaloi si kweli kwani kanuni zinajitosheleza na zinatoa mwongozo wote.

"Kamati imebaini kuwa Polepole TV haina waandishi wenye taaluma ya uandishi wa habari hivyo kukikua misingi ya uandishi na imemuelekeza ahakikishe anazingatia uchaguzi wa maneno yenye sitaha, kuzingatia misingi, kanuni na maadili ya utoaji maudhui mtandaoni.

Maamuzi ya Kamati

Kama imejiridhisha kuwa Polepole TV imekiuka shria za mawasiliano kwa njia ya kieletroniki, hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 44, kifungu kidogo cha kwanza, sehemu G cha sheria ya mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania, sura ya 172, na marejeo yake ya mwaka 2017, na kanuni ya 21, kanuni ndogo ya tatu na sehemu A ya kanuni tajwa hapo juu, Kamati inatoa adhabu zifuatavyo.

Kituo kinapewa onyo kali. Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole TV kusimamishwa kwa muda mpaka pale atakapofanya yafyatayo. Kuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi wa habari na utangazi na kuleta tija na ufanisi katika vipindi vyake. Kuhakikisha vipindi vyake vyote vinazingatia sheria, misingi na kanunia za uandishi na utangazaji wa habari pamoja na masharti ya leseni yake.

"Baada ya kuzingatia maelekezo hayo Kituo cha Humpohrey Polepole kitatakiwa kutoa taarifa TCRA ambapo TCRA ikijirishisha kuwa maelekzo yote yamezingatiwa kipindi cha Humphrey Polepole kitajrejea na kitakuwa chini ya uangalizi wa TCRA kwa muda wa miezi sita.

Uamuzi huu umetolewa leo jijini datr es Salaam, uamuzi wa kukata rufaa kupitia FCT upo wazi ndani ya siku 21.

Mwenyekiti wa Katai ya Maudhui ya TCRA, Habbi Gunze.
 
Usije ukajaribu kuinua kichwa tena.. Rungu zito zaidi litatua juu yake kwa style zilezile za watoto wa mjini...
 
 
Back
Top Bottom