Mchujo ni lazima ndiyo maana kuna kuna mitihani, Mtoto akifeli anarudia darasa shida iko wapi?Habari:
Toka matokeo ya Kidato cha Nne kumekuwa na mjadala kwanini Shule ya binafsi zimefanya vyema zaidi .
1. Kwanza si kweli kwamba hizi shule hazitoi zero bali wanachofanya ni kuzihamisha.
Hizi shule wanachukua wanafunzi na kuanza kuwachuja..... Hapa wanaoshindwa kuwafundisha wanachuja na kuwaondoa... Hapa ina maana wangebaki lazima wangetaga.
2. Shule za serikali hawachagui wanafunzi wanaowataka, wanaletewa..
Pia hawana mamlaka ya kuwachuja... Naamini nao wangekuwa wanaruhusiwa kuchagua watoto na kuwachuja wangetoa A na Kaizerege.
Kaizerege inachofanya ni kuchukua wanafunzi wenye A na kuziboresha... Ili tuwajue kama wanafundisha vyema wachukue wanafunzi wenye zero na kuwawezesha kupata A (From 0 to A).
Mfano:
Wachukuliwe wanafunzi wa shule X ya Kata wahamishiwe Kaizerege na wasiruhusiwe kuwachuja tuone kama watatoa A..
Elimu ya Tanzania ni Usanii Mtupu.
=========
Maoni mengine:
Serikali imezembea yenyewe, Mtoto hajui kusoma wala kuandika then unasema kafaulu hii ni akili ya mtu timamu kweli? Tuna akili sisi ?
Mitihani ya darasa la nne ilipoanzishwa mwanafunzi alikuwa akifeli anarudishwa darasa hata mara kumi mpaka aelewe, vilevile form two kulikuwa na mtihani akifeli anarudia leo hii hamtaki mnawapeleka tu wakifeli mnaanza kulalama wakati haya ni mafuno ya mlichopanda.
Hebu acheni utani nyie.