Hakuna sababu ya kuzisifu Shule Binafsi

Hakuna sababu ya kuzisifu Shule Binafsi

Umeongea vema,.na kwa kuongezea,hzo shule binafsi utakuta interview ya kuingia kidato cha kwanza wanafanya wanafunzi kama laki mbili hvi eg marian,kati ya hao laki mbili wanachukuliwa kati ya 40 hadi 90 hvi,maana ya wanachukua wale ni bora ambao hata wangesoma shule zingine wangefanya vzuri na hapo wana wachuja tena kuwapata bora zaidi ukichanganya na mazingira lazima wafaulu sanaa,..,.hizi shule zinafanya biashara tu ila hazisaidii taifa maana hao wanaochukua ni ambao wana uwezo tayari,wao hawazalishi wale wa kawaida kuwafanya waweze kufaulu vema

Well said mkuu!

Wanachukua cream na cream wanaendelea kuichuja zaidi.

Wanachokifanya ni kuboresha A tu na si kubadilisha F to A.
 
Kwani mtihani wenyewe wa form four si mchujo pia kuchuja nani aendelee na kidato cha tano na kozi zingine au arudi nyumbani kulala.
 
Habari:

Toka matokeo ya kidato cha nne kumekuwa na mjadala kwanini Shule ya binafsi zimefanya vyema zaidi .

1. Kwanza si kweli kwamba hizi shule hazitoa zero bali wanachofanya ni kuzihamisha.

Hizi shule wanachukua wanafunzi na kuanza kuwachuja..... Hapa wanaoshindwa kuwafundisha wanachuja na kuwaondoa... Hapa ina maana wangebaki lazima wangetaga.

2. Shule za serikali hawachagui wanafunzi wanaowataka, wanaletewa..

Pia hawana mamlaka ya kuwachuja... Naamini nao wangekuwa wanaruhusiwa kuchagua watoto na kuwachuja wangetoa A na Kaizerege.

Kaizerege inachofanya ni kuchukua wanafunzi wenye A na kuziboresha... Ili tuwajue kama wanafundisha vyema wachukue wanafunzi wenye zero na kuwawezesha kupata A (From 0 to A).

Mfano:

Wachukuliwe wanafunzi wa shule X ya Kata wahamishiwe Kaizerege na wasiruhusiwe kuwachuja tuone kama watatoa A..

Elimu ya Tanzania ni Usanii Mtupu.
unamaanisha barcelona akiifunga arsenal keshokutwa hamna haja ya kuisifia maana barcelona wana worldclass players,
 
Halafu wakimaliza form six wanaenda imtu au St .......university waambie waende Sua au muhimbili wakaone mziki wake kule no spoon feeding
 
Habari:

Toka matokeo ya kidato cha nne kumekuwa na mjadala kwanini Shule ya binafsi zimefanya vyema zaidi .

1. Kwanza si kweli kwamba hizi shule hazitoa zero bali wanachofanya ni kuzihamisha.

Hizi shule wanachukua wanafunzi na kuanza kuwachuja..... Hapa wanaoshindwa kuwafundisha wanachuja na kuwaondoa... Hapa ina maana wangebaki lazima wangetaga.

2. Shule za serikali hawachagui wanafunzi wanaowataka, wanaletewa..

Pia hawana mamlaka ya kuwachuja... Naamini nao wangekuwa wanaruhusiwa kuchagua watoto na kuwachuja wangetoa A na Kaizerege.

Kaizerege inachofanya ni kuchukua wanafunzi wenye A na kuziboresha... Ili tuwajue kama wanafundisha vyema wachukue wanafunzi wenye zero na kuwawezesha kupata A (From 0 to A).

Mfano:

Wachukuliwe wanafunzi wa shule X ya Kata wahamishiwe Kaizerege na wasiruhusiwe kuwachuja tuone kama watatoa A..

Elimu ya Tanzania ni Usanii Mtupu.
Lazima tuzisifu kwa maana zinamfumo mzuri wa kuhakikisha mwanafunzi anaelewa kile anachojifunza. Ni muhimu kwa serikali kuiga mfumo huo maana utasababisha wanafunzi wajitume kwa bidii ili matokeo yao yawe mazuri. Big up shule za private kwa kutoa elimu bora na sio bora elimu[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Halafu wakimaliza form six wanaenda imtu au St .......university waambie waende Sua au muhimbili wakaone mziki wake kule no spoon feeding

Wanaenda vyuo vyao hivyo hivyo vya kuwabeba....
 
Zamani ukienda private ulionekaje mbele ya wanaoenda za serikali? mambo hubadilika kulingana na nyakatia
 
Zamani ukienda private ulionekaje mbele ya wanaoenda za serikali? mambo hubadilika kulingana na nyakatia
 
Kuna watu katika jamii wanatupa lawama kwa serikali juu ya shule za kata kuanguka katika matokeo na kuziacha private zikitamba kumi bora, madai yao ni ukosefu wa walimu, miundo mbinu mi bovu, ukosefu wa vitendea kazi ndo unafanya shule hizi ziboronge lakini wanasahau huwenda kwakutojua au kwa makusudi sababu kuu ni moja tu hizo zingine ni mbwembwe tu zisizo na ukweli wowote.

Katika shule za private ili mwanafunzi huingie ni lazima ufanyike mchujo mkali wale wasiojiweza wanaondoka wenye uwezo mkubwa wanabaki ndo maana fedha inawanafunzi waliomaliza 72 tuuu lakini walioomba kujiunga ni zaidi ya 1000 ao 1000 walitupiliwa mbali katika mtihani wa mchujo.

Hivyo wanafunzi wanaosoma fedha ni sawa na kuchukua wanafunzi 72 katika shule 72 wanaoshika nafasi za kwanza. Hao 72 ndo wale ambao wangesoma shule za kata wangetoka na A sasa wamekusanywa fedha wamekusanywa alliance we unategemea nini?

Shule za kata hazina mi chujo hiyo ya fedha au alliance wao ukifika basi ni tiketi ya form four uwe unajua kusoma, hujui twende kazi, uwe unadaraja la chini au la juu wao twende kazi afu utamfananisha na wafedha ambaye ameingia si kwakigezo tu chakufaulu la saba kule Igomaa au Isangawana primary school bali ujiniazi ndo unakupa ticket.

Kunabaadhi za shule nyingine za private zimeanguka si kwasababu ya vitendea kazi na Mishahara la bali kwasababu hazina sheria za michujo mikali wao wanajali pesa.

0764408795
 
Walimu wapo kwenye mgomo baridi.. Unawezaje kutegemea ngombe akupe maziwa wakati unashindwa kumuhudumia vizuri! Walimu hasa wa serikali wanachangamoto nyingi sana.. Tunaishi nao tunaona wanayayoyapitia.. Lakini kingine pia wanafunzi wenyewe wa siku hizi ni majanga.. Hasa hawa wa uswahilini..
sana Mkuu walimu waakidai maslahi yao wanatishiwa kufukuzwa kazi na ukicheki kipato chao ni kidogo basi wananywea kimya wakiogopa kupoteza na kidogo walichonacho. Hapo kinachofuata ni mgomo wa kimya kimya tu ila impact yake ndiyo hyo.
 
Shule ya lowassa imekua ya ngapi kitaifa maana alituambia elimu elimu elimu

Fafanua kidogo,Shule ya Lowassa kwa maana ya umiliki,au ni yale majengo ya kata mnayoyaita Shule ambayo mnayapachika majina ya watu tena bila hata ridhaa ya mwenye jina?

Punguza "ashkmajinoon", maana unalitaja jina la Mh.Lowassa mara nyingi zaidi ya unavyolitaja jina la mumeo,vipi Binti au mumeo hawajibiki kikamilifu kwako?
 
Shule za Kata wanapokea wanafunzi 200... Kati yao 10 ni wazuri 190 ni wabovu.

Mwalimu anapambana na wale 190 mwisho wa siku na wale 10 wanaanza kushuka ili kuendana na kasi ya wale wengi...

Shule za Private ni Usanii Mtupu.
 
Fafanua kidogo,Shule ya Lowassa kwa maana ya umiliki,au ni yale majengo ya kata mnayoyaita Shule ambayo mnayapachika majina ya watu tena bila hata ridhaa ya mwenye jina?

Punguza "ashkmajinoon", maana unalitaja jina la Mh.Lowassa mara nyingi zaidi ya unavyolitaja jina la mumeo,vipi Binti au mumeo hawajibiki kikamilifu kwako?

Hawa ni wale wanaoumwa Lowasaphobia... Uchaguzi umeisha lkn bado wanasumbuliwa na jina la Lowasa.
 
Nini Kifanyike[/u]

1. Serikali iboreshe Elimu ya Msingi .... Hatuwezi kukomali Elimu ya Sekondari ikiwa wanafunzi wanamaliza darasa la 7 wakiwa wamevurugwa .. Wamekata tamaa.

2. Shule za Private zikatazwe kuchuja... Mwanafunzi achujwe kwa viwango vya serikali tu....
 
Nakubaliana na wewe...mchujo uwe wa serikali tu...form two na form 4...kuna wazazi wanalazimika kuamisha watoto shule sababu eti wamekosa marks za kuendelea form 2...kasema nani? huu ni ujanja wa kuwatupia wenzao mizigo....utasikia motto akikosa wastani wa 60 anabaki darasa lile lile...hii ni biashara sasa...na ukiangalia mtoto ndio umri unasonga utamtafutia shule nyingine ...na ndio wanachotaka hasa...afu kesho wanatamba tuna one na two tu....huku wanafunzi wasio na akili wamewa force wahamie shule nyingine....
 
Kwi kwi kwi kwi,,, yaan ukifika kaizilege mjengo Wa darasa tu ni division two ukija zile za kata mvua ikinyesha mnalowana
 
Nakubaliana na wewe...mchujo uwe wa serikali tu...form two na form 4...kuna wazazi wanalazimika kuamisha watoto shule sababu eti wamekosa marks za kuendelea form 2...kasema nani? huu ni ujanja wa kuwatupia wenzao mizigo....utasikia motto akikosa wastani wa 60 anabaki darasa lile lile...hii ni biashara sasa...na ukiangalia mtoto ndio umri unasonga utamtafutia shule nyingine ...na ndio wanachotaka hasa...afu kesho wanatamba tuna one na two tu....huku wanafunzi wasio na akili wamewa force wahamie shule nyingine....

Huu ni wizi wa wazi wazi....

Kwanini waniambie mtoto wangu hajafikisha wastani ikiwa wao ni mabingwa wa kufundisha.

Hapo wanakwepa fedheha wanakulazimisha uhamishe zero kwingine.
 
Back
Top Bottom