Hakuna sababu ya kuzisifu Shule Binafsi

Hakuna sababu ya kuzisifu Shule Binafsi

Mdogo wangu kabla hajahitimu bachelor yake ya mathematics,miezi miwili kabla tayari ameshaingia kwenye payroll ya shule binafsi. Walienda kucheck output iliyo bora kwa ajili ya shule yao, wakaridhika naye na kumpa mkataba mnono.

Shule za serikali mpaka umalize ukae nyumbani usikilizie weee, ndo maana walimu wanaoenda zinakuwa ni product hafifu ambazo nazo zitatoa product hafifu vilevile.
 
Kwahiyo hoja ni kwamba tuanzie kuboresha misingi
Ndio hivo mkuu. Na sio zoezi la mda mfupi ni lazima liwe zoezi endelevu. Unakumbuka serikali ilipoanza kuharibu elimu yetu? Ni pale walipokuwa wanachagua na kukubali hadi mwenye div 4 ya mwisho kusomea ualimu wa msingi. Ikawa sasa hata raia tu mtaan wakiona mtoto amefeli wanamshangaa kwa kumuuliza "yani umekosa hata ualimu?" Kwa hyo ualimu ikawa ni fani ya kudharaulika na kuongezea chumvi kwenye kidonda maslahi ni duni na mazingira ya kazi ni balaaa. Msingi kwanza
 
MWENGINE ANAINGIA MAABARA KUANZIA FORM ONE NA MWINGINE MAABARA MPAKA AFIKE FORM 4 AFU UNAWAPIMA KWA MTIHANI MMOJA NOT FAIR


Wanafunzi wengi wa shule za kata hata wakiingizwa maabara kila siku bado watataga tu.
 
Ukweli mtupu, shule hizi mtoto akipata chini ya B anatolewa. Sasa hapo kunakufundisha au usanii tu.


Wanachofanya ni kuziboresha A na wala si kuwafanya wasiojua wajue.


Ndio maana wanawachuja walioshindwa kuwabadilisha.
 
Hata Feza wanafanya hivyo, tena wanatangaza hivi mtoto atakaepata maksi za juu atasoma bure, wanapeleka tangazo kila shule.....watoto wanafanya mtihani siku yakwenda kuchukua majibu kama kapata maksi za juu anaulizwa wazazi wako wanafanya kazi ipi ....ku determine kama wana uwezo kulipa ada milioni 6.

Wazazi wengi hupeleka watoto ambao kwenye mashule watokapo huwa wanashika nafasi za top 5 na kuja kuwa surprised na hicho kipengele cha kipatao.



Halafu baadae wanasema ni mabingwa wa kufundisha..
 
Ufauru wa mtoto unaanzia kwa mzazi. Haiwezekani mtoto anashinda kwenye vigodoro afu afauru. Wazazi tukiwa serious na watoto toka wakiwa wadogo elimu itaenda. Hivi usha wahi ata kumsaidia mwanao kwenye masomo yake mpaka huyo mtoto alaumiwe. Mie najua mtoto akiwa na msingi mzuri na usimamizi bora toka kwa mzazi tangu akiwa darasa la kwanza ata fauru mpaka chuo. Nakumbuka akati nasoma chuo karibia asilimia 70 ya wanafunzi walikuwa watoto wa walimu. Sisemi kuwa watoto wa walimu hufauru sana hapana. Ila hapa nataka kuonyesha jinsi mzazi navochangia performance ya mtoto. Ukimkazania mwanao na kuweza kumcontrol kwenye mambo ya kijinga lazima afauru tu. Kama ata hatofanya vizuri basi ni bahati mbaya na huwa hawaferi kabisa utaona wanapata ata divII lakin tukiacha jukumu kwa walimu swala la ufauru wa watoto utakuwa historia tu.
 
Watoto wanapata kila kitu watashindwa vipi kufaulu!? Mimi form 4 nilipata I ya 11 Azania. shule ambayo wakiingia darasani walimu wawili kwa Siku ni wengi. Shule za serikali zimekuwa makambi ya watoto kupotezea mud a.
 
Motisha mdogo kwa walimu wa shule za serikali. Hivyo walimu wanaanzia huko GoT wakipata uzoefu wanaondoka au kununuliwa na hizo shule binafsi kwani kwao ni biashara.
 
Habari:

Toka matokeo ya kidato cha nne kumekuwa na mjadala kwanini Shule ya binafsi zimefanya vyema zaidi .

1. Kwanza si kweli kwamba hizi shule hazitoa zero bali wanachofanya ni kuzihamisha.

Hizi shule wanachukua wanafunzi na kuanza kuwachuja..... Hapa wanaoshindwa kuwafundisha wanachuja na kuwaondoa... Hapa ina maana wangebaki lazima wangetaga.

2. Shule za serikali hawachagui wanafunzi wanaowataka, wanaletewa..

Pia hawana mamlaka ya kuwachuja... Naamini nao wangekuwa wanaruhusiwa kuchagua watoto na kuwachuja wangetoa A na Kaizerege.

Kaizerege inachofanya ni kuchukua wanafunzi wenye A na kuziboresha... Ili tuwajue kama wanafundisha vyema wachukue wanafunzi wenye zero na kuwawezesha kupata A (From 0 to A).

Mfano:

Wachukuliwe wanafunzi wa shule X ya Kata wahamishiwe Kaizerege na wasiruhusiwe kuwachuja tuone kama watatoa A..

Elimu ya Tanzania ni Usanii Mtupu.

Well said Mkuu
 
Tusiukimbie ukweli..Shule nyingi za binafsi wanajitahidi kutoa elimu bora..Kuna shule za serikali za vipaji maalumu ambapo upelekwa watt wenye ufaulu mzuri(sijui kama ipo hivi siku hizi) lakini still kuna ziro zinapatikana huko..Kumbuka hawa walichujwa nao

Sawa walichujwa lkn ni kwa matokeo ya drs la saba....c wanavyoingia shuleni hata kama ni shule ya kipaji....na cha kujiuliza aliyekwenda shule ya kipaji ni kwa akili yake???au??
 
Motisha mdogo kwa walimu wa shule za serikali. Hivyo walimu wanaanzia huko GoT wakipata uzoefu wanaondoka au kununuliwa na hizo shule binafsi kwani kwao ni biashara.



Je unafikiri shule za kata wangekuwa wanaletewa "cream" na wakaruhusiwa kuchuja wasingefaulu wote???
 
Back
Top Bottom