Hakuna sababu ya kuzisifu Shule Binafsi

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,600
5,803
Habari:

Toka matokeo ya Kidato cha Nne kumekuwa na mjadala kwanini Shule ya binafsi zimefanya vyema zaidi .

1. Kwanza si kweli kwamba hizi shule hazitoi zero bali wanachofanya ni kuzihamisha.

Hizi shule wanachukua wanafunzi na kuanza kuwachuja..... Hapa wanaoshindwa kuwafundisha wanachuja na kuwaondoa... Hapa ina maana wangebaki lazima wangetaga.

2. Shule za serikali hawachagui wanafunzi wanaowataka, wanaletewa..

Pia hawana mamlaka ya kuwachuja... Naamini nao wangekuwa wanaruhusiwa kuchagua watoto na kuwachuja wangetoa A na Kaizerege.

Kaizerege inachofanya ni kuchukua wanafunzi wenye A na kuziboresha... Ili tuwajue kama wanafundisha vyema wachukue wanafunzi wenye zero na kuwawezesha kupata A (From 0 to A).

Mfano:

Wachukuliwe wanafunzi wa shule X ya Kata wahamishiwe Kaizerege na wasiruhusiwe kuwachuja tuone kama watatoa A..

Elimu ya Tanzania ni Usanii Mtupu.

=========
Maoni mengine:
Kuna watu katika jamii wanatupa lawama kwa serikali juu ya shule za kata kuanguka katika matokeo na kuziacha private zikitamba kumi bora, madai yao ni ukosefu wa walimu, miundo mbinu mi bovu, ukosefu wa vitendea kazi ndo unafanya shule hizi ziboronge lakini wanasahau huwenda kwakutojua au kwa makusudi sababu kuu ni moja tu hizo zingine ni mbwembwe tu zisizo na ukweli wowote.

Katika shule za private ili mwanafunzi huingie ni lazima ufanyike mchujo mkali wale wasiojiweza wanaondoka wenye uwezo mkubwa wanabaki ndo maana fedha inawanafunzi waliomaliza 72 tuuu lakini walioomba kujiunga ni zaidi ya 1000 ao 1000 walitupiliwa mbali katika mtihani wa mchujo.

Hivyo wanafunzi wanaosoma fedha ni sawa na kuchukua wanafunzi 72 katika shule 72 wanaoshika nafasi za kwanza. Hao 72 ndo wale ambao wangesoma shule za kata wangetoka na A sasa wamekusanywa fedha wamekusanywa alliance we unategemea nini?

Shule za kata hazina mi chujo hiyo ya fedha au alliance wao ukifika basi ni tiketi ya form four uwe unajua kusoma, hujui twende kazi, uwe unadaraja la chini au la juu wao twende kazi afu utamfananisha na wafedha ambaye ameingia si kwakigezo tu chakufaulu la saba kule Igomaa au Isangawana primary school bali ujiniazi ndo unakupa ticket.

Kuna baadhi za shule nyingine za private zimeanguka si kwasababu ya vitendea kazi na Mishahara la bali kwasababu hazina sheria za michujo mikali wao wanajali pesa.

0764408795
 
Habari:

Toka matokeo ya kidato cha nne kumekuwa na mjadala kwanini Shule ya binafsi zimefanya vyema zaidi .

1. Kwanza si kweli kwamba hizi shule hazitoa zero bali wanachofanya ni kuzihamisha.

Hizi shule wanachukua wanafunzi na kuanza kuwachuja..... Hapa wanaoshindwa kuwafundisha wanachuja na kuwaondoa... Hapa ina maana wangebaki lazima wangetaga.

2. Shule za serikali hawachagui wanafunzi wanaowataka, wanaletewa..

Pia hawana mamlaka ya kuwachuja... Naamini nao wangekuwa wanaruhusiwa kuchagua watoto na kuwachuja wangetoa A na Kaizerege.

Kaizerege inachofanya ni kuchukua wanafunzi wenye A na kuziboresha... Ili tuwajue kama wanafundisha vyema wachukue wanafunzi wenye zero na kuwawezesha kupata A (From 0 to A).

Mfano:

Wachukuliwe wanafunzi wa shule X ya Kata wahamishiwe Kaizerege na wasiruhusiwe kuwachuja tuone kama watatoa A..

Elimu ya Tanzania ni Usanii Mtupu.
Hata Feza wanafanya hivyo, tena wanatangaza hivi mtoto atakaepata maksi za juu atasoma bure, wanapeleka tangazo kila shule.....watoto wanafanya mtihani siku yakwenda kuchukua majibu kama kapata maksi za juu anaulizwa wazazi wako wanafanya kazi ipi ....ku determine kama wana uwezo kulipa ada milioni 6.

Wazazi wengi hupeleka watoto ambao kwenye mashule watokapo huwa wanashika nafasi za top 5 na kuja kuwa surprised na hicho kipengele cha kipatao.
 
mtihani wa taifa unatakiwa upigwe marufuku na kuwepo mitihani ya kimkoa kama wafanyazo wamarekani. huu mfumo wa nchi na elimu tulionao tayari uanafanya ubaguzi kati ya walio nacho na wasio nacho.wenye uwezo wanapata elimu bora wale kkipato cha chini wanapata elimu ya ovyo. kuna kijiji flani shule ilikuwa na walimu wanne tu kiasi kwamba ili walimu waweze kuwasaidia wanafunzi wakawa wanafundisha masomo mengine yasiyo wahusu. haiwezekani uniambie katika 74% waliopata iv-0 hawa wote wanazidiwa akili na wanafunzi wa feza na shule zingine za binafsi.
 
Habari:

Toka matokeo ya kidato cha nne kumekuwa na mjadala kwanini Shule ya binafsi zimefanya vyema zaidi .

1. Kwanza si kweli kwamba hizi shule hazitoa zero bali wanachofanya ni kuzihamisha.

Hizi shule wanachukua wanafunzi na kuanza kuwachuja..... Hapa wanaoshindwa kuwafundisha wanachuja na kuwaondoa... Hapa ina maana wangebaki lazima wangetaga.

2. Shule za serikali hawachagui wanafunzi wanaowataka, wanaletewa..

Pia hawana mamlaka ya kuwachuja... Naamini nao wangekuwa wanaruhusiwa kuchagua watoto na kuwachuja wangetoa A na Kaizerege.

Kaizerege inachofanya ni kuchukua wanafunzi wenye A na kuziboresha... Ili tuwajue kama wanafundisha vyema wachukue wanafunzi wenye zero na kuwawezesha kupata A (From 0 to A).

Mfano:

Wachukuliwe wanafunzi wa shule X ya Kata wahamishiwe Kaizerege na wasiruhusiwe kuwachuja tuone kama watatoa A..

Elimu ya Tanzania ni Usanii Mtupu.
point,.......
 
Hoja yako nyepesi sana,kwani serikali inashindwa nini kuwachuja wanafunzi wake??(kuwatenga kulingana na uwezo ili kuwasaidia kwa ukaribu??Ndio maana tulikuwa na shule maalumu,leo hii shule maalumu ziko wapi?Nenda amerika hata ulaya,mfumo wakubagua na kuwatenga wanafunzi kulingana na uwezo wao upo.
Shule maalum zipo haziperform kama zaman. Kifupi kodi tunakatwa tupate public services including elimu ila ndo bora liende
 
Pamoja na hayo uliyosema shule binafsi zinafundisha kuliko za serikali! Wanakuwa na wastani wa juu ambao ukishindwa kuufikisha kweli unaondoka lakini wanafunzi kwa kufahamu hilo wanajitahidi kusoma ili kuufikia

Shule binafsi wanajali muda zaidi kuliko za serikali huku wakiendelea kufanya real practical kuanzia madarasa ya chini

Waalimu wao wanajali muda na pia wanakuwa na motisha tofauti na shule zetu za serikali

Japo ni kweli kwamba shule binafsi wanamboresha zaidi yule mtu ambaye ni clever kutokana kuanza mchujo kutokea wanapo wadahili wanafunzi
 
Dunia hakuna usawa nyinyi mnataka usawa.kwa kila jambo.. serikali nayo huchuja kwani ina shule za vipaji maalum....mzumbe ,ilboru,kilakala na msalato.
Hao waliofaulu ni watoto watqnzania kwahiyo tujivunie ....kwani ud mbona nayo inachikuwa cream tu?
 
Pamoja na yote shule zote zilizo chini ya serikali uwajibikaji walimu ni F kabisa....Kuna shule mdogo wangu anasoma katika mitihani ya muhula akipata chini ya wastani wa marks 60 mzazi unaitwa shule na unasaini kabisa kwamba matokeo ya namna hiyo yakijurudia mtoto wako tunamfukuza...Hiyo itampa yule mtoto changamoto kubwa sana hata kulala hatolala na makundi yasiyo serious atayaacha..So Private wanajitahidi mno, Ama we unaona ni sawa serikali inavyowapitisha tu watoto hadi form na mtoto hajui hata kusaoma?
 
Hao watoto waliofanya vizuri shule za private ni watoto wetu kama hao wa public schools hatuna haja ya kusaga meno hapa kwa uchungu. Tujiulize tatizo liko wapi ili shule zetu za serikali ziweze nazo kufanya vzr? Kikubwa hapa sio kuangalia sekondari macho yetu wote yaangalie shule za msingi wanafunzi wanapata MAARIFA WANAYOSTAHILI KUPATA? leo mtoto anamaliza shule ya msingi hajui kusoma au anababaisha kusoma. Hajui kuandika wala kuhesabu vizuri lakini kwa MAAJABU ya dunia mtoto huyo anafaulu na kujiunga na kidato cha I. Kwa syllabus ya sekondari ni vigumu kumsaidia mtu asiyejua kusoma na kuandika so mtoto atasoma kwa kubahatisha mpk form 4. HOJA ya eti ni kwa kuwa sekondari lugha inabadilika hakuna mashiko. Miaka ya nyuma tulikuwa tunamaliza msingi tumeiva tukiingia sekondari miezi michache ya mwanzo unakuwa upo vizuri shule inaenda. Leo mtoto anaingia sekondari hata alfabet hajui kuzisoma. Serikali KWA UTULIVU KABISA IANGALIE UPYAAA SHULE ZA MSINGI WAONE NINI KIFANYIKE...vinginevyo tutabaki kulialia tu na jamii yetu inaangamia kwa kukosa elimu na maarifa.
 
Hoja yako nyepesi sana,kwani serikali inashindwa nini kuwachuja wanafunzi wake??(kuwatenga kulingana na uwezo ili kuwasaidia kwa ukaribu??Ndio maana tulikuwa na shule maalumu,leo hii shule maalumu ziko wapi?Nenda amerika hata ulaya,mfumo wakubagua na kuwatenga wanafunzi kulingana na uwezo wao upo.
Ni kweli kabisa mkuu serikali imeshindwa nn kuwachuja na kuwasaidia?
 
Mbona naona umeandika pumba tu, iyoiyo yaku wachuja ndio inabidi wapongezwe, we hujui kama mwanafunzi anaongeza bidii akijua mwisho wasiku anaweza asiendelee mbele ? Chakufanya ni kushauri serikali ifanye mambo kama yA shule binafsi na kuweka mazingira mazuri yA mtoto kusoma
 
Tusiukimbie ukweli..Shule nyingi za binafsi wanajitahidi kutoa elimu bora..Kuna shule za serikali za vipaji maalumu ambapo upelekwa watt wenye ufaulu mzuri(sijui kama ipo hivi siku hizi) lakini still kuna ziro zinapatikana huko..Kumbuka hawa walichujwa nao
 
Walimu wapo kwenye mgomo baridi.. Unawezaje kutegemea ngombe akupe maziwa wakati unashindwa kumuhudumia vizuri! Walimu hasa wa serikali wanachangamoto nyingi sana.. Tunaishi nao tunaona wanayayoyapitia.. Lakini kingine pia wanafunzi wenyewe wa siku hizi ni majanga.. Hasa hawa wa uswahilini..
 
Back
Top Bottom