TUMI EPAFRA
Member
- Jul 12, 2020
- 59
- 56
Hakuna Rais atakaye tatua tatizo sugu la ajira ila sisi wenyewe kama watu wa China walivyo jielimisha, hata kama CCM ikiondoka madarakani. Kwa sababu tatizo la ajira linatokana na ukosefu wa uzalishaji mali barani Afrika, ukosefu wa wataalamu wa viwanda ingawaje tuna wasomi wengi.
Rais wa kupambana na hili lazima aanzie kwenye mfumo wa elimu, kuhamasisha wanafunzi kusoma technology, la sivyo Rais yoyote atakaye ingia bila hii sera atazidisha umasikini kwa kutegemea mikopo ya nje, na kula chote kidogo tulichonacho mwenyewe na watu wake.
Wapinzani wote ni maneno matupu na wanategemea Ulaya kuiongoza nchi hii kiuchumi na kisiasa, jambo ambalo ni kinyume kabisa kwa nchi yeyote ya Afrika kufanya hivyo sasa, ni kuturudisha kwenye utumwa wa remote control.
Tatizo la Afrika sote tunakimbilia elimu zinazotuelimisha kuajiriwa sio kuajiri, kujiajiri au kuunda bidhaa zozote, mpaka leo tunaaigiza kila kitu toka Ulaya, kuanzia madawa mpaka chupi za kuvaa, sasa wanawake wanaagiza hata nywele za Ulaya
Angalau Magufuli anadumisha sera ya viwanda, lakini viwanda hivi inabidi viajiri wataalamu toka nje kuvisimamia na kuvirekebisha, na spare parts zake zinaagizwa toka Ulaya, Marekani au Asia.
Siku nchi yetu itakapozalisha kila kitu bila kutegemea nchi za nje, kuanzia madawa mpaka mavazi, peni na mashine za viwanda, simu na magari hata radio na fridges, tutapounda barabara zetu wenyewe, mungu akijalia tutakapo tengeneza hata computers, ndipo umasikini na ukosefu wa ajira utakapoisha.