Kwa nyakati hizi ni ajabu kukuta mwanamke yupo single,ila si ajabu kukuta mwanaume yupo single.
Haya ni matokeo ya mifumo ya malezi ya kisasa ambayo imetengeneza mtazamo feki kuwa mwanamke awe nacho asiwe nacho ni tunu na mwanaume asiye nacho ni takataka na aliyenacho athaminiwe kwa anachimiliki.
Kwa mwanaume kukaa single kiroho na kimwili ni jambo takatifu sawa na mtu anae detoxify mwili kutoa taka mwili na kusafisha fikra zake na kujenga msingi mpya kwasababu mwanaume amepewa mafungu 70 (miaka kumi kumi) kuyaanza upya maisha yake kama atatuliza kichwa chake na kuzungumza vema na muumba wake.
Kinyume chake mwanamke kukaa single haina faida na ni uelekeo wa kufeli uwiano wake ni kama vile nguo inayokimbiza trend kwenye fashion kuwekwa kabatini hadi fasheni yake ipite. Fasheni ikipita hiyo nguo haitakuwa na thamani tena mbele ya macho ya wanunuzi kwasababu watavaaje nguo iliyo nje ya fasheni na trends,wachekwe?
Imagine mwanamke akae single akijitafuta na uchumi wa kati akamiliki nyumba,gari,na biashara,halafu awe bikra. Wewe mwanaume wa miaka 40 mwenye uwezo na mali zako ukaletewa huyo mwanamke wa miaka 35 mwenye mafanikio na ni bikra na pembeni ukaletewa binti wa miaka 23 bikra na mwenye maadili na heshima na mafunzo ya kuishi na mume na anatoka familia yenye heshima,utachukua yupi?🤔
So, mwanamke kuishi akiwa single ni kupoteza muda na mwanaume kuishi akiwa single ni kujiongezea thamani. Mwanamke olewa na Jenga familia katika umri sahihi (miaka 16 hadi 26) hiyo ndio wife material deadline. Chini ya hapo si sawa juu ya hapo ni bahati nasibu.
Mwanamke kuigizia kuwa single ni kubet na future yako.
Je ukishawahi kusikia nikihadithia kile kisa cha muuza nyanya aliyekuwa akiringa akiwaiga wauza nazi,akasahau kuwa nyanya ya leo si sawa na nyanya ya kesho kwa ubora wakati nazi ya leo na ya mwezi ujao hazina tofauti ya ubora.
Tuishi kwa kuzifuata Hekima na sio kutengeneza mifumo yetu nje ya hekima