Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Hivi jamani ni ccm wanachelewesha maendeleo au hata sisi wanaichi tunaopewa dhamana serikalini na taasisi na kuanza kufanya ufisadi,hivi waajiriwa wote wale ni ccm?,maana niaminicho ni kuwa waajiriwa wako ktk itikadi tofauti tofauti na si kweli kama wanaofanya uhalifu wa kifisadi ni wafuasi wa ccm tu,ukija ngazi za juu makatibu wa wizara si wote wafuasi wa ccm kuna wa upinzani nao ndiyo waharibifu kabisa,hivyo ai vizuri kusema ccm ndiyo wameturudisha nyuma kimaendeleo,hata ukawa mkija ni same story labda muajiri wale wa ukawa tu na bado wataleta shida pia,kikubwa ni sote tufanye kazi kwa bidii,tuunganishe nguvu tuijenge nchi na kuwa waaminifu,kwanza watu washukuru ccm inahuruma pia,maana kwa ufisadi watu wangwkuwa wananyongwa tu sasa sijuu ingekuwaje
 
Kawadanganye kwenu... Uelewa huo Sasa tunao.. Na jibu ni kinyume... Hakuna nchi Tajiri duniani iliyoongozwa na majuha wale wale miaka yote..
 
we ugoro umefaribu mfumo wako wa fahamu kwanza india sio masikini pili china na taiwan na malasiya hazina mfumo wa demokrasia ya ukweli
 
Tukisema watanzania walio wengi ni MATAHIRA wanasema tunajidharau.hv hapa mtoto wa form 4 HAWEZI ANDIKA UTUMBO KAMA HUU
 
Dhana ya kubadirisha chama sio kwamba ndio formula ya kuleta maendeleo. Kuna nchi zimeongozwa na zinazidi kuongozwa na chama kimoja na zimepata maendeleo thabiti ya kiuchumk yanayoonekana dunia nzima na kuwafaidisha watu wake. Mfano mzuri ni China inayoongozwa na Chama cha Kikomunist kwa miaka mingi sasa na tahari wana maendeleo kiuchumi na influence ya wachina imeonekana dunia yote. Kwahiyo kwa dhana ya maendeleo na kuwaridhisha wananchi, ni dhahiri chama hicho kikaendelea kuwa madarakani(labda pia kwa kuwa China ni de facto one party state, huenda wangechagua chama kingine). Sasa hapa kwetu Tz, unataka kutuaminisha kuwa CCM inafaa kuendelea kushika dola kwa maendeleo gani waliowafanyia watanzania kwa miaka 54 sàsa? "Watanzania wanataka mabadiriko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM". #Time for change. R.I.P CCM
 
Acha uongo, developed countries zimekuwa hivyo sababu ya kubadilisha chama.
Mojawapo ni America, kuna republic na democratic hivi vyama vinachuana kila uchaguzi.
Utakuwa CCM wewe si bure. Mie sina chama chochote, ila CCM na utawala wake nimeuchoka.
 
Mfa maji haachi kutapatapa,Kenya imeendelea sana huwezi kufananisha na Tz na ni baada ya kuiondoa KANU.
 
Nisome vizuri tena kama ukipenda nimesema hakuna nchi iliyoendelea leo hii ambayo iliwahi kubadilisha Chama, sasa Kenya ni nchi iliyoendelea?
ANC ndiyo ilojenga SA au ni wazungu wabaguzi ndiyo walifanya ikawa vile?
 
Nani alikudanganya Msumbiji hawajabadilisha chama?? Nenda kafanye home work yako tena.. Kichwa chako si bure kimejaa udongo..

Uchaguzi wa majuzi tu hapa FRELIMO kimeangushwa na RENAMO.. Na kama CCM itabaki madarakani kwa miaka mingine mitano ijayo si ajabu Msumbiji wakatuacha kama walivyotuacha Kenya. Fanya assignment Miticash ya Msumbiji ilikuwa inabadilishwa kwa Shilling ya Kitanzania kwa bei gani 2005 then njoo leo uone Miticash anavyoigaragaza Shilling ya Tanzania..

Kaskazini mwa Msumbiji kuna Madini mengi na Mafuta na Gesi pia.. Wao miswada yao ya mafuta na gesi si ya kipuuzi kama hii iliyopitishwa kwetu. Miaka 10 ijayo Mreno atakuwa anapewa mikopo na Msumbiji kama anavyopokea kutoka Angola pia.

CC: Washawasha
 
Last edited by a moderator:
ujerumani na uingereza ni tajiri na hizi nchi kama zilivyo nyingi za ulaya zilijengwa na wafalme (monarch) ambao walikuwa hawabadilishwi haya mambo ya kubadilisha vyama wameanza siku hizi baada ya kuwa nchi tajiri tayari lkn wakati wako ngazi ya maendeleo kama yetu kulikuwa na wafalme tu ambao walikuwa wana absolute power na walikuwa hawabadilishwi!

Na nchi za asia zote ambazo zimeendelea hivi karibuni zimeiga ulaya nazo zote zimejengwa na chama kimoja hakuna hata moja ambayo ni tajiri leo iliyowahi kubadilisha chama si japani, korea kusini wala singapore na wale ambao wanabadilisha vyama kila siku kama india, pakistani, sri lanka bangladeshi ni masikini!
usa!!?
 
Pumba tupu! Ni dhahiri bin shayiri kwamba elimu yako na upeo wako wa ufahamu katika global affairs ni mdogo sana, rudi huko shule za kata ukasome tena!

Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!
 
Vipi Marekani, Uingereza na Ujerumani? . Narrow minded.
Kweli umeamua kudanganya watu kwa hoja dhaifu. Hivi hujui kuwa uchumi wa Kenya umeimarika baada ya kuiondoa KANU? Leo hii Kenya imetoka kwenye uchumi wa chini hadi wa kati kwa chama gani? Vipi nchi za Magharibi?
 
Marekani na Uingreza huwa hakuna mabadiliko?Kenya je wamerudi nyuma baada ya kufa KANU?
 
wewe utakuwa ni gamba uliye kubuhu na ndo maana huwezi kuandika tofauti na ulichoandika, mwaka huu mnalo
 
Back
Top Bottom