Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Aisee acha kuongea ujinga!! Una utafiti uliofanya usiongee mambo ambayo yanausisha utafiti! Ccm mnapumzika imetosha, kutowachagua nyie tutaokoa ata maisha ya wanyama wetu, kama tembo simba na nk.

Una akili nyingi sana
 
Msimtukane jamani pambaneni kwa hoja ayo ni maoni yake lakini afanye utafiti japo kidogo tuu aweze kujua katiba ,sera,na ata miundo ya nchi alizotolea mfano ikoje ndio aweze kutueleza kwa undani .
 
Kama ccm ingetusaidia kufikia maendeleo kama ya nchi hizo zingine tungeendelea kuichagua tu,na tungependa iendelee kubaki tu, but not this time my friend!!they must go,no matter what.
 
Mwaka huu magamba yatakufa...Thread zote yanayoanzisha yanamuongelea Rais Edward Ngoyai Lowassa.....na sisi hatuna habari....tunapata upepo wa bahari....mwaka huu si wa propaganda kwetu maana ukweli tulishauongea wananchi wakauelewa.
 
Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!
Na kwanini hicho chama kiwe CCM? Kabla ya msimu Wa uchaguzi kashfa kibao kuteteana, kulindana, kukashfisha hadi benki kuu bado unatuambia waendelee CCM!
 
Computer inaundwa na software na hardware....kwa mfano
tuchukue Tanzania kama computer ambayo ina software
(serikali) na hardware (wananchi)...Tuje kwenye software
(serikali) inayoongoza hardware kufanya kazi kama
antivirus kuuwa wadudu(takukuru na polisi) na software
nyingne kama graphics design,vlc, data backup softwares,
browsers na nyingnezo( wizara zote za kujenga na kuicontrol
nchi).....sasa computer hii ina operating software ya zaman
sana (CCM) na ina virus ndani yake ambao wamefanya had
antivirus na malware remover kuwa nazo kama virus pia
(Polisi na takukuru)......sasa kama hii computer (Tanzania )
haitoangaliwa itakuwa slow kwenye ufanyaj kazi
(maendeleo),
mafile yataliwa (rasilimali) au kucorrupt kabisa (crisis).......
...,.......................... .............................. ......................,.......
..solution n kupiga
chin window iliyopo (CCM) na kuinstall upya kwa kuhakksha
antivirus (Takukuru na Polisi? zilizowekwa n Kali zinazuia
wadudu......................au kuinstall window nyingine mpya
(Ukawa) ambayo ni Ubuntu.. Isiyowapa nafasi virus kufanya
kaz kabsa kama wapo......... ### Zamu Yako 2015###

CCM KAGEUKA MKOLONI MWEUSI!
 
Ziko nyingi na kwanza zote zilizoendelea na nimeshazitaja nazirudia Korea Kusini, Ujapani (ingawaje haitawaliwa lkn inaongozwa na Chama kimoja siku zote), Singapore, Taiwani, Malaysia n.k

Vipi kuhusu tz
 
Mtu asiyetaka mabadiliko kuna maslahi anapata haiwezekani kenya petrol tsh 1400 hapa tsh 2200 hujiulizi!
 
Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!
Shida ni elimu yako na ndio maana unafikiri kama darasa la saba B!! Unafahamu faida za multiparty system? Uingereza imekuwa ikibadilisha vyama mara kwa mara kati ya CONCERVATIVE NA LABOUR PARTY na ndio maana wapo pale kimaendeleo! Marekani wana DEMOCRAT NA REPUBLICAN,vyama hivi hubadilishana kushika dola mara kwa mara,kila kimoja hujitahidi kikae madarakani muda mrefu lakini wamarekani wasipo ridhika na performance yake wanakiondoa madarakani!!
 
naomba na mimi nikusaidie ...hizo nchi kweli zimeongozwa na chama kimoja( japan walitoka 2009 wakarudi 2012 kama sijakosea ) hivi maendeleo yao waliyonayo ni sawa na TANZANIA tungekuwa na maendeleo kama yao watu wasingesema hayo wanayoyasema......maendeleo hakuna ndo maana watu hawaoni tatizo kuweka wengine maana hamna cha kupoteza..watu wako madarakani kwa manufaa yao binafsi zaidi...
 
Ndugu mtoa mada kwa akili ya kawaida na utafiti usio hitaji mahesabu mengi utangundua nchi yetu chini ya CCM inarudi nyuma badala ya kwenda mbele . Viashiria kwamba nchi inaendelea ni pamoja na kuwa na viwanda vyetu vinavyoweza kukidhi mahitaji ya ndani na ku export nje ikibidi, elimu bora na kuwa na wataalamu wetu, mgawanyo wa rasilimali unao nufaisha wananchi walio wengi , fursa za kibiashara na ajira , shillingi imara na mfumuko wa bei wa kueleweka , miundo mbinu bora na viashiria vinaendelea. Najua ndugu muandishi inaonekana unajua sana historia lakini jiulize swali rahisi kama CCM ingiweza kutimiza hata viashiria vichache nilivyovitoa hapo juu unadhani CHADEMA/UKAWA wangekuwa na hoja yoyote ya kuongea ? Miaka hamsini iliyopita nchi kama Singapore ilikuwa ya kawaida kabisa lakini jaribu kuifuatilia siku za hivi karibuni uone hatua iliyopiga. CCM haioneshi ya hivi karibuni haioneshi kama ina nia ya kweli ya kutaka kumuendeleza Mtanzania, atleast ya Mwl. Nyerere ilikuwa inaonesha dira na kwa vitendo hii ya siku hizi imejaa maendeleo ya vitabuni ndo mana tunaona hiki kinachoendelea sasa.
 
Mtoa thread unakua kama kipofu aliejifanya kipofu yeye mwenyewe. unapoongelea mifano ya nchi maskini eti kisa zinabadirisha vyama uwe makini. Kenya kwa maendeleo kiuchumi iko ktk top 10 Africa wakati Tz haimo. Kenya imetuzidi sana kiuchumi na kimaendeleo ya mtu mmoja mmoja, sasa sijui unaongelea Kenya ya wapi? Je kiuhalisia India ni sawa na Tz kimaendeleo?? Pia unapoongelea kuwa chama kimoja ndio mwalobaini wa umaskini, je Uganda iliyo chini ya chama kimoja kwa miaka 30 sasa ina maendeleo gani ya maana? So which is which? I think there is no one size fits all. We need political dynamism, tuwe na fikra tofauti na kuona nani atatuletea mabadiriko tuyatakayo na sio kuishi ktk fikra mgando tukikalia hadithi za kuwa CCM imeleta amani tuliyonayo,...so what? 54 years of independence mkulima bado anategemea jembe la mkono huku mikoa mingine kama Simiyu wakiishia kuona barabara za lami kwenye vitabu na Tv na unatuaminisha eti CCM ndo italeta maendeleo. Tanzanians are fed up of CCM
 
Wananchi wameamua kubadilisha chama wewe endelea na mifano yako ya ulaya
 
Chama hakibadilishwi kwa sababu ya kubadilisha tu (for the sake of it) tunabadilisha kwa kushindwa kazi iliyopewa na kupuuza maoni ya wananchi ili kulinda maslahi yake (rasimu ya Warioba). Kama CCM ingetumia rasilimali za nchi vivuri ingebaki madarakani hata miaka mia kwa sababu wananchi wngeridhishwa na utendaji wake. CCM inavuna ilichopanda hata ikitumia bao la mkono, wananchi wamechoka na patachimbika.
 
Computer inaundwa na software na hardware....kwa mfano
tuchukue Tanzania kama computer ambayo ina software
(serikali) na hardware (wananchi)...Tuje kwenye software
(serikali) inayoongoza hardware kufanya kazi kama
antivirus kuuwa wadudu(takukuru na polisi) na software
nyingne kama graphics design,vlc, data backup softwares,
browsers na nyingnezo( wizara zote za kujenga na kuicontrol
nchi).....sasa computer hii ina operating software ya zaman
sana (CCM) na ina virus ndani yake ambao wamefanya had
antivirus na malware remover kuwa nazo kama virus pia
(Polisi na takukuru)......sasa kama hii computer (Tanzania )
haitoangaliwa itakuwa slow kwenye ufanyaj kazi
(maendeleo),
mafile yataliwa (rasilimali) au kucorrupt kabisa (crisis).......
...,.......................... .............................. ......................,.......
..solution n kupiga
chin window iliyopo (CCM) na kuinstall upya kwa kuhakksha
antivirus (Takukuru na Polisi? zilizowekwa n Kali zinazuia
wadudu......................au kuinstall window nyingine mpya
(Ukawa) ambayo ni Ubuntu.. Isiyowapa nafasi virus kufanya
kaz kabsa kama wapo......... ### Zamu Yako 2015###

CCM KAGEUKA MKOLONI MWEUSI!

nimeipenda hii itengeneze itupie watsaap
 
Back
Top Bottom