Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Siku nyingine ukikosa vitu vya maana ni bora ukae kimya au usome za wenzio. Huu ni utumbo!

Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!


Basi kama Muanzisha Mada naifunga kama inawezekana kwa kusema hivi Wote mnaotukana na kukebehi nawaambia hivi tatizo ni ninyi na wala siyo CCM au TanZania ni kama vile mtoto aliyeshindwa maisha halafu anaishi siku zote kwa kumlaumu baba yake kwamba ndiyo sababu ya yeye kuwa na maisha magumu!

Kila la heri na fisadi Lowasa!


 
Nani alikudanganya Msumbiji hawajabadilisha chama?? Nenda kafanye home work yako tena.. Kichwa chako si bure kimejaa udongo..

Uchaguzi wa majuzi tu hapa FRELIMO kimeangushwa na RENAMO.. Na kama CCM itabaki madarakani kwa miaka mingine mitano ijayo si ajabu Msumbiji wakatuacha kama walivyotuacha Kenya. Fanya assignment Miticash ya Msumbiji ilikuwa inabadilishwa kwa Shilling ya Kitanzania kwa bei gani 2005 then njoo leo uone Miticash anavyoigaragaza Shilling ya Tanzania..

Kaskazini mwa Msumbiji kuna Madini mengi na Mafuta na Gesi pia.. Wao miswada yao ya mafuta na gesi si ya kipuuzi kama hii iliyopitishwa kwetu. Miaka 10 ijayo Mreno atakuwa anapewa mikopo na Msumbiji kama anavyopokea kutoka Angola pia.

CC: Washawasha
Hapana mkuu,Frelimo bado wapo madarakani na Rais wa MSUMBIJI ni FELIPE JACINTO NYUSI anatokea chama cha Frelimo,pia ndio chama chenye wabunge wengi wakifuatiwa na Renano na MDM.
Nalog off
 
Back
Top Bottom