Hakuna Magufuli anachofanya ambacho hakukisema!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kumekuwa na baadhi ya kelele kutoka kwa baadhi ya watu kuhusu utendaji wa Raisi Magufuli kana kwamba hawakuyategemea haya!

Hakuna chochote au hatua yoyote ile ambayo rais Magufuli ameichukuwa mpaka sasa hivi ambayo hakuiahidi kwenye kampeni zake, kama ni bomoa bomoa kila mtu alijua tangu hata Magufuli hajawa Rais, amekuwa akisisistiza ufwataji wa sheria na amesema kila mahali na rekodi zipo kwamba kama br. imekufwata utalipwa fidia lkn kama umeifwata hakuna kulipwa fidia.

Kama ni kufukuzwa kwa wafanyakazi papo kwa hapo aliyasema haya mara nyingi sana kwenye kampeni zake kabla ya uchaguzi kwamba yeye (Magufuli) akikukuta umeharibu kazi hata kuhamisha au kuunda tume bali atakufukuza moja kwa moja.

Kama ni mawaziri kuzunguka nchini na kuwa site na kufanya safari za kushtukiza aliyasema pia kwamba Mawaziri wake hawatakaa ofisini bali watakuwa vijijini na mijini kwa wananchi hivyo basi haya yote tuliyajua kabla ya kupiga kura lkn bado tukamchagua kwa maana hiyo hatuna sababu ya kulalamika kwani tumeyakubali yale yote aliyoyasema na ndiyo maana tukampigia kura kwa wingi wetu, Magufuli ameweza kumshinda fisadi Lowassa kwa tofauti ya kura milioni kadhaa!

Hivyo nawasihi muache kulia lia kwani Hakuna ambacho kinafanyika ambacho Rais Magufuli hakukiahidi kwa kifupi anatimiza yale yote aliyotuahidi!
 
Hii inawafaa zaidi akina Salum Mwalim na kundi lake linalodai Dr Magufuli anatekeleza sera zao. Siwashangai hata hivyo kwa sababu hawakuwahi kumsikiliza Dk Magufuli kwenye kampeni zake
 
Wanaolialia ni wale walizoea kusikia maneno bila kutenda.sasa huyu alisema na anatenda.wanaopiga kelele ni wale majizi na mazurumati.hivyo hizo siyo lawama wala
 
Nimekudharau kwa kusema Magufuli alimshinda Lowassa kwa kura milioni ishirini, ungekuwa umeendika tu kwa tarakimu ningejua umekosea kwa bahati mbaya, lakini ulichosema kwa maneno ndio hichohicho ulichoandika kwa namba! Idadi ya waliopiga kura nchi nzima wenyewe hawakufika milioni 20. Hata kama ni kulazimisha kile anachokifanya Magufuli ni lazima upotoshe na huo utetezi wako finyu.

Kila mtu anapenda sheria zifuatwe lakini inakuwaje sheria zinaangalia, nilitarajia wakwepa kodi waliogundulika wangechukuliwa adhabu kali, lakini inaonekana wameambiwa warudishe basi yakaishia hapohapo. Kwanza mchezo ulikuwa huuhuu tukambiwa kodi iliyokwepwa ni ya 80b lakini siku zilivyokwenda ikashuka mpaka 12.5b! Ni lazima mpate sifa kwa kutumia uongo?
 
Kabla ya kuangali hiyo video kumbuka maneno ya Mlm.Nyerere kwamba ,,tunataka raisi ambaye shida, mateso na umaskini wa Mtanzania unamuuma na hicho ndicho kimsukume kugombea uraisi." Mwisho wa kunukuu!




 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongeza tu. Hakuna anachokifanya ambacho hakipo kwenye ilani ya CCM.
 
Tanzania ya viwanda ipo wapi mahakama ya mafisadi ipo wapi anyway ni mwanzo ila tunavitaka


Duh! wewe kweli mtoto wa masikini na siyo tu wa mali mpaka akili! Kwa hiyo TanZania ya viwanda uliitegemea ijengwe kwa siku 30?
Hata kama kiwanda cha kwanza kingeanzwa kujenga siku raisi alipoapishwa kingekuwa bado hakijakamilka kujengwa
leo hii lkn bado unalalamika kwamba hakuna TanZania ya viwanda baada ya mwezi mmoja madarakani?
 
Mh. RaisiJPM anayaishi kivitendo Maneno yake Usichoke Mh.Raisi Umma wa Watanzania upo Nawe.
 
Kwa kuongeza tu. Hakuna anachokifanya ambacho hakipo kwenye ilani ya CCM.

Kwenye ilani ya ccm kuna kipengele cha kuwabana wafanyabiashara wafadhili wa CCM? Kama ni hivyo mbona ilikuwa haifanyiki mpaka mnawaruhusu wanapitisha mizigo bila kulipa kodi?
 
ukweli hua haujifichi mengi anayofanya raic yametokana na upinzan kwa kiasi kikubwa tu tusiwe wapingaji wa kila kitu kma malofa
 
Kwa kuongeza tu. Hakuna anachokifanya ambacho hakipo kwenye ilani ya CCM.

huyu mtu huwa simuelewi kabisa utawala wa kikwete alikuwa anasifia sana wakati tunaona kama alikuwa kawakumbatia mafisadi
 
Back
Top Bottom