Nimekudharau kwa kusema Magufuli alimshinda Lowassa kwa kura milioni ishirini, ungekuwa umeendika tu kwa tarakimu ningejua umekosea kwa bahati mbaya, lakini ulichosema kwa maneno ndio hichohicho ulichoandika kwa namba! Idadi ya waliopiga kura nchi nzima wenyewe hawakufika milioni 20. Hata kama ni kulazimisha kile anachokifanya Magufuli ni lazima upotoshe na huo utetezi wako finyu.
Kila mtu anapenda sheria zifuatwe lakini inakuwaje sheria zinaangalia, nilitarajia wakwepa kodi waliogundulika wangechukuliwa adhabu kali, lakini inaonekana wameambiwa warudishe basi yakaishia hapohapo. Kwanza mchezo ulikuwa huuhuu tukambiwa kodi iliyokwepwa ni ya 80b lakini siku zilivyokwenda ikashuka mpaka 12.5b! Ni lazima mpate sifa kwa kutumia uongo?