Hakuna Kwetu Kwingine...

Kwetu kamwe sikubali,si kwetu ni kwa wenzetu,
Sio yale ya awali,tukiwa na utu wetu,
Kwa sasa hawatujali.tunaswagwa kwa mtutu,
Kwetu palikuwa kwetu,kwa sasa ni kwa wenzetu.

Hawatujali wenzetu.kwetu wameshapauza,
Hawatabakiza kitu,vyote wataangamiza,
Tubaki kama Wahutu,wakuja wala wasaza,
Kwetu palikuwa kwetu,kwa sasa ni kwa wenzetu.

Si ardhi si wanyama,urithi wetu asili,
Madini yetu wachuma,kwa kejeli na kibuli,
Ni wezi waso huruma,kwa zetu rasilimali,
Kwetu palikuwa kwetu, kwa sasa ni kwa wenzetu.

Baba keshauza nyumba,pamoja na wapangaji,
Kigamboni inayumba,wameuziwa walaji,
Wao wanao wajomba,pasi mbili na mtaji,
Kwetu palikuwa kwetu,kwa sasa ni kwa wenzetu.

Kwetu Mola pabariki,wanao twaangamia,
Kwa sasa hapakaliki,ni pazuri palikua,
Wageuze hambiliki,wabadili zao nia,
Kwetu palikuwa
kwetu kwa sasa ni kwa wenzetu.
 
Mwanakijiji sikia , maneno yenye hekima
Maisha ni kutulia, popote penye hatima
Mrume acha kulia, vita si lelemama
Mwanajeshi makini; vita kasimamia

Wajitia uhayawani, usiozaliwa nao
Rudi zako mkoani, kijana mtu wa kwao
Tanga ni burudani, maisha kwa raha zao
Mwanajeshi makini, vita kasimamia

Mangula yupo mahiri, ccm ameishika
Mafisadi wamekiri, vilio vimewashika
Namalizia shairi, maneno yangu hakika
Mwanajeshi makini, vita kasimamia

Sawa mkuu ila hapo kwa mangula, mmmh!
 
Hakuna kwetu kwingine, ila humu kwenye chaka.
Hakuna kwetu kwingine, tunaliwa tukicheka.
Hakuna kwetu kwingine, wanyonge twadhihakika.
Hakuna kwetu kwingine, si mbali ni Tanzania.
 
Chako ni chako jamani, hata kama maskini
Kikiwemo mfukoni, au uchimbie chini,
Kiwe cha kubwa thamani, au bei magirini,
Ni chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyumba ya kwako ni yako, hata iwe msituni,
Ya kwake siyo ya kwako, hata iwe ni peponi,
Ya kuazima si yako, hata kama ghorofani,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Kilicho chako cha kwako, hata watu wakucheke
Kidogo bado ni chako, wala usidanganyike,
Usiachie cha kwako, hata lije libeneke,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima

Mwizi kaingia ndani, kwenye nyumba ya kwako,
Utahamia uani, eti ni yake si yako?
Au wende kwa jirani, useme nyumba si yako?
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyoka umkute ndani, kwenye uvungu chumbani,
Utahamia jikoni, umuache kitandani?
Hutamtoa jamani, na kumpiga kichwani?
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.

Cha kwako bado cha kwako, hata kibovu watani,
Kizima kisicho chako, wakitamani kwa nini?
Tengeneza kilo chako, ujivunie moyoni,
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.

Ahsanteeee!
 
1. Hakuna kwetu kwingine, kwanza nawasalimia,

Hakuna kwetu kwingine, ujumbe nawaambia,
Hakuna kwetu kwingine, wa Kijiji naingia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

2. Hakuna kwetu kwingine, hata tukiwa Asia
Hakuna kwetu kwingine, tukiwa na Arabia,
Hakuna kwetu kwingine, Na nchi za Yuropia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

3. Hakuna kwetu kwingine, na siye wa Amerikia,
Hakuna kwetu kwingine, na popote Afrikia,
Hakuna kwetu kwingine, katika hii dunia,
Hakuna kwetu kwingine ila kwetu Tanzania.

4. Hakuna kwetu kwingine, kwetu kwa kupigania
Hakuna kwetu kwingine, kwetu kwa kung'ang'ania,
Hakuna kwetu kwingine, kwetu tusikochukia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

5. Hakuna kwetu kwingine, tunakokushabikia,
Hakuna kwetu kwingine, tunakokuulizia,
Hakuna kwetu kwingine, tunakokufuatilia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

6. Hakuna kwetu kwingine, kwingine kwetu na pia,
Hakuna kwetu kwingine, kwetu tusikogaia,
Hakuna kwetu kwingine, Ni Bongo nawaambia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

7. Hakuna kwetu kwingine, sababu ya kubishia,
Hakuna kwetu kwingine, hivyo twawang'ang'ania,
Hakuna kwetu kwingine, kamwe hatutaachia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

8. Hakuna kwetu kwingine, kwetu kwa kushabikia,
Hakuna kwetu kwingine, kwingine kwa kuchangia,
Hakuna kwetu kwingine, chochote tukipatia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

9. Hakuna kwetu kwingine, utawalaye sikia!
Hakuna kwetu kwingine, ukweli tutakwambia,
Hakuna kwetu kwingine, na hata ukichukia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania,

10. Hakuna kwetu kwingine, hata mkitutishia,
Hakuna kwetu kwingine, hofu haitoingia,
Hakuna kwetu kwingine, bado tutawashukia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

11. Hakuna kwetu kwingine, mafisadi mtalia,
Hakuna kwetu kwingine, vikaragosi vyenu pia,

Hakuna kwetu kwingine, hadi mje kukimbia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

12. Hakuna kwetu kwingine, beti zangu zatimia,
Hakuna kwetu kwingine, ni dazeni siyo mia,
Hakuna kwetu kwingine, nafunga na kutulia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Tarumbeta ya Kijiji)

Ki-ukweli MJJ hukunitendea haki manake ubeti wa mwisho mstari wa mwisho ilitakiwa umalizie kwa kusema
KWETU NI KWETU, HAKUNA KWETU KWINGINE, ILA KWETU TANZANIA!
 
nami nimejongea ili kuwashabikia
mwanakijiji nyumbani pia
hakuna kupakimbia
 
Mzee Mwanakijiji;5141543]Chako ni chako jamani, hata kama maskini
Kikiwemo mfukoni, au uchimbie chini,
Kiwe cha kubwa thamani, au bei magirini,
Ni chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyumba ya kwako ni yako, hata iwe msituni,
Ya kwake siyo ya kwako, hata iwe ni peponi,
Ya kuazima si yako, hata kama ghorofani,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Kilicho chako cha kwako, hata watu wakucheke
Kidogo bado ni chako, wala usidanganyike,
Usiachie cha kwako, hata lije libeneke,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima

Mwizi kaingia ndani, kwenye nyumba ya kwako,
Utahamia uani, eti ni yake si yako?
Au wende kwa jirani, useme nyumba si yako?
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyoka umkute ndani, kwenye uvungu chumbani,
Utahamia jikoni, umuache kitandani?
Hutamtoa jamani, na kumpiga kichwani?
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.

Cha kwako bado cha kwako, hata kibovu watani,
Kizima kisicho chako, wakitamani kwa nini?
Tengeneza kilo chako, ujivunie moyoni,
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.

Kama mkewe na Uli, Daudi kesha chukua,
Kakubakizia mwili,roho yako ameua,
Hakupi hata dalili, kujipanga kapasua,
Si chako si chako tena,kakuwahi mwenye nacho.
 
Hapa sasa sio petu,bali kwa wawekezaji,
Mabonde hata misitu, madini hata na maji,
Wanatamba mbele yetu, eti hatuna mitaji,
Tunataka ukombozi, kurudisha mali zetu.
 
Kwetu kwangu ni popote, mambo yakininyookea,
Kwetu mtu si chochote, wezi wanajiibia,
Kwetu sioni lolote, ni jina limebakia,
Ingawa kwetu ni kwetu, kwetu kwangu ni popote.

Kwetu niwe mkimbizi, wageni wawe wenyeji,
Hili hujalimaizi, hebu jaribu kuhoji,
Kwetu ilikuwa enzi, kwa sasa sina uenyeji,
Ingawa kwetu ni kwetu, kwetu kwangu ni popote.

Leo sitasema mengi, kwani si mahali pake,
Jambo moja la msingi, yabidi tubadillike,
Kwetu kweli kwa msingi, tupambane pakomboke,
Ingawa kwetu ni kwetu, kwetu kwangu ni popote.

Si mchezo.
Aluta continua. Lazima Tanzania tuikomboe kutoka ukoloni wa CCM na ukoloni wa kimagharibi maana vyote vinatutafuna. Lol, rasilimali za nchi zinashambuliwa kila kukicha, kwa kasi hii watanzania wa mwanza 2100 watakuta mabua tu. Shame on you CCM maana ndo umetufikisha hapa.
 
Wakiwa nacho wenzetu, kama ni chetu ni chetu,
Ya kwetu bado ni yetu, akitawala mwenzetu,
Hatukatai cha kwetu, akikipora mwenzetu,
Hata akiwa mwenzetu, hatumwachii chetu.
 
Wakiwa nacho wenzetu, kama ni chetu ni chetu,
Ya kwetu bado ni yetu, akitawala mwenzetu,
Hatukatai cha kwetu, akikipora mwenzetu,
Hata akiwa mwenzetu, hatumwachii chetu.

Wajipa nyingi huzuni; usije jipa maradhi
Wote tupo vitani; fisadi kakosa radhi
wanatia ubayani, chako nakihifadhi
Panga najitwalia, fisadi kumkabili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom