Mtu aliyejipata kimaisha ni yupi?

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,837
Kumekuwa na mijadala mingi sana hapa jukwaani ya kimaisha ikihusisha swala la watu kujipata kimaisha, huku suala la umri na muonekano wa mtu vikiwekwa katikati ya mijadala hiyo kama kipimo cha kuashiria mtu kuwa na nafasi ya kufeli kimaisha au kutokuwa na lake tena katika mapambano ya kimaisha. Wengine wameenda mbali na kuibuka na hoja kuwa mtu ukiwa na mvi na kipara na hujajipata basi Huna lako tena kibongo bongo!.

Swali langu ni " je mtu ili awe amejipata kibongo bongo anapaswa kuwa na uwezo kiasi gani kimaisha"? "anapaswa kuwa na vitu gani hasa ili waungwana mseme ametoboa?

Nikirejea baadhi ya mabandiko humu jukwaani, yanayokebehi umri wa kaka zetu na dada zetu baadhi wenye 35yrs > na wale watu wenye vipara na mionekanao ya kizee kuliko uhalisia wao napata jibu moja tu, ni either waandishi wa mabandiko hayo hawajui tafasiri kamili ya neno maisha kwa watu walioko kusini mwa jangwa la sahara au ni vijana wa mwaka 2000's wanaofikiri maisha yanaangalia umri ulionao, au walimwengu wana huruma na muonekano wako, hell no!!, kijana jua uko hapa duniani to be tested to the limit, your age doesn't count, na wewe ni prey wakati huohuo ni predator inategemea umeegemea tawi gani.

Mtu aliyejipata ni yupi? swali kwako kijana mwenye <35yrs ,? Je ni kuwa na mshara wa mil 1.4 kwa mwezi baada ya kodi, na kiusafiri uchwara cha mil 25, plus mke na watoto na kibanda cha kulala au, huwa mnamaanisha nini mnaposema mtu amejipata?
Sababu kiuhalisia kama Huna Mali zenye thamani ya walau zaidi ya tsh billion 5, jua wewe bado unajitafuta na hata wanao wanahatari ya kuja kuteseka tu duniani!

Je hapo ulipo na hiyo miaka yako 18, unahisi unauwezo wa kufikia net worth ya 5 billion tsh.
 
Back
Top Bottom