Nikilewa mniache
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 19,305
- 51,965
Mada nimeielewa vizuri.Hii mada ukiisoma vizuri utaielewa. Kama wewe ni Baba kwa sasa isome tena huenda ukaelewa mantiki ya mtoa post
Kama unao uwezo wa kuwasaidia wazazi wako wasaidie
Kama kipato chako kinakutosha wewe na familia yako tu, basi waheshimu na uwaoneshe upendo
Asilimia kubwa ya wenye vipato na wenye elimu hawakufika hapo kimiujiza tu!
Wapo wazazi waliouza mifugo yao, mashamba na wengine waliokuwa na akiba kidogo walifunga mikanda na kuwasomesha.
Wazazi wetu walishindwa kununua hata pikipiki ya kuendea shamba kwa sababu ili kutusomesha wakiwa na mawazo ya kuja kufarijiwa na watoto wao uzeeni nyie mnasema wapambane na hali zao kweli?
Wazazi wetu wangeamua kufanya starehe kwa kutumia hizo pesa kidogo walizotusomesha nazo leo hii tungekuwaje?
Alafu muelewe sio kwamba nyinyi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pindi mnapopata ajira bali hata nyinyi mkiyumba mnakimbilia kwao
Maisha ni kuwa nayo makini tu maana hatujui kesho itazaa nini