Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

Baba mwema huacha urithi mpaka kwa wana wa wanae yaani wajukuu.

Hiyo ni kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu.

Sasa kama hadi wajukuu wanakuta mali ya babu/ bibi huyo baba atalalamika saaa ngapi? Mali zake zitazidi kumsaidia maisha yake yote.
Sasa ukiona baba analalamika kutokuhumiwa ujue hakuwajibika vyema mahali fulani kwenye maisha yake.


Watakupiga mawe shauri yako
 
Wazee wetu huko nyuma hawakuwa na makosa bali nyakati na na exposure ndogo ndio ziliwafikisha hapo hatuna haja kuwalaumu ni kuwaombea mbele za Mwenyezi Mungu awabariki na kuwasamehe makosa yao..

Kizazi cha sasa kuanzia miaka 50 kushuka chini tuna kila kitu na hatuna haja ya kushindwa kuandaa uzee na kuandaa vijana wetu... tuna exposure, nyakati bora, fursa za kutosha kinachotakiwa ni uthubutu na kujitoa kutengeneza maisha yako binafsi ya uzeeni na watoto wako..


Kusema hawakuwa na makosa ni kuamua kujidanganya
 
Mkuu Baba ni Baba tu labda kama hakukuzaa yeye na kukupatia huduma zilizokufanya ukafika ulikofika kimaisha!
Shida kubwa ya vijana walio wengi huwa tunaangalia tu pale tulipo sasa lakini hatuangalii tulikotoka!
Pia tunachelewa kugundua kuwa treatment tulizopata kwa wazazi wetu ni sehemu ya contents zilizotujenga hadi kufika mahala tulipofika,!
Unakuta mtu unazamia mijini hata miaka 10 bila kwenda kumjulia baba yako hali eti kisa alikuwa anakuchapa sana wakati wa umri wa utoto lakini unasahau kwamba kipindi hicho yeye alikuwa na uwezo wa kutafuta pesa wakati wewe hata kuchoma muhogo tu ulikuwa hujuwi achilia mbali kuugharamia!
Tuwathamini wazazi wetu ndugu hata wakitukosea pa kubwa kiasi gani, thamani yao haina scale ya kupimia!
 
Hili uko sahihi, hata lile la bikira pia uko sahihi
 
Hili uko sahihi, hata lile la bikira pia uko sahihi
 
wakuu nimesoma post na comments zote neno kwa neno, mstari kwa mstari na pia nukta kwa nukta.
Niwapongeze wote mliotoa maoni humu,
Mleta uzi hakuwa na nia mbaya kutukumbusha,
Ila pia nimeona kila mtu amelichukulia kwa uelewa wake na utashi wake!
Tukumbuke kuwa humu hatufanani uelewa pia na utashi, kumbuka tunatoka katika malezi tofauti, hapa tupo rika tofauti, dini tofauti, ila pia mazingira tunayotoka ni tofauti.
Tusameheane kwa yote wakuu!
Kuna kisa nimekutana nacho sehemu naomba sote tukisome ni kifupi sana huenda pia kuna la kujifunza kwetu!
Kutokana na huu uzi!
Ahsanteni
IMG_9599.jpg

IMG_9600.jpg

IMG_9602.jpg

IMG_9603.jpg

IMG_9605.jpg

IMG_9606.jpg

IMG_9608.jpg

IMG_9609.jpg
 
Ha ha ha..baba naona umekasirishwa kweli kweli
Mfate 42 sijakasirishwa nilieleza tu mtazamo wangu. JF ni sehemu ya kupunguza stress siyo kusababisha mtu akasirike. Kama unaweza kuwa unakasirishwa na comments za JF basi utakuwa na matatizo makubwa zaidi yanayohitaji ushauri nasaha.
 
Kwa mtazamo wangu,

Hua ni msomaji wa vitabu vyote ninavopata vya dini, kuanzia Biblia, Quran, Torah (torat) na hata vya Monks. Na ni mpenzi wa vitabu vya falsafa na siasa.

Nashukuru kwa kunisaidia mwandishi kwa kuweka vipande vya Biblia katika uzi wako.

Ningependa kuwakumbusha haya machache ambayo niliyakuta katika Quran kuhusu wazazi (Yani Baba Na Mama)

Sura ya 17: 23... Inasema hivi "Na mungu wenu amewa amrisha msimuabudu yoyote isipokua yeye tu, na fanyeni wema kwa WAZAZI wenu. Na kama mmoja ama wote wawili (WAZAZI) wamefikia umri wa UZEE (wamezeeka) basi msi wasimange na wala msi wakemee kwa hasira, wala msiwaambie aaarghh, ongeeni nao kwa wema na upole"


Mama kakubeba miezi 9 kwa shida tumboni mwake, na kakuzaa kwa machungu makali sana, Baba kakulea kwa shida mpaka umekua mtu mzima (pengine kakusomesha mpaka chuo).

Sasa, hizi ndio fadhila za mema waliotufanyia wazazi toka tulipokua wadogo, tuwalipe kwa kuwaita majina machafu kama hili la "BABA JINGA" ????????
....Point! Huyu Mkuu ninahisi kuwa bahati mbaya mdingi wake akaumwa Kisukari na BP, itakuwa Ndio Safari tu, maana Mtoto wake huyu ni Dhahiri ataona Ubahili kumtibu Baba Jinga wake!
Tumuombe tu aombe radhi kimoyo moyo!!!
 
sijui
baba alifyatua watoto 12 wewe wa kwanza amekusomesha kwa kuuza mashamba na mifugo
leo hii umepata kazi take home laki 6, hapo unatakiwa usomeshe wadogo zako na usaidie nyumbani
wewe upo mjini umepanga una mke na mtoto , mke hana kazi na ndugu zake wanakutegemea
Natabasamu utafikiri mazuri
 
Ushasema kawekeza kwangu kwa nini asile alichowekeza. Huwezi vuna usipopanda hiyo ni kanuni katika mfumo wa maisha. Asiyefanya kazi na asile.

Kama umefika kidato cha nne huwezi shindwa elewa mantiki ya mada hii. Lakini kama madarasa ni machache huwezi kunielewa.
Mkuu Bora umeelewa kuwa Kuna watu wazto kuelewa mapema , umeongea ukweli mno Ila tambua pia Kuna watu huwa wanachangia mada kutokana na hisia zao na sio uhalisia , pia Kuna wabishi , wapumbavu na wajinga wanabisha ili waelewe Zaid , Aslimia kubwa ya wazee wetu walijitahd kuwekeza kwenye mashmba na elimu za wanae , tatzo kubwa litakuja kuanzia kwa sisi vjna wa kileo wakwepa mimba, Wala mirungi masharobaro , wachagua kazi na wavivu , kwa tabia hizi huna haki ya mtoto alie ishi maisha ya kuunga kukusaidia kwa chochte , labda hyo mtoto awe na roho ya kipekee tu , Akikusaidia hatopata chchte , pia asipo kusaidia hatopata chchte
 
Back
Top Bottom