Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

Kwa mtazamo wangu,

Hua ni msomaji wa vitabu vyote ninavopata vya dini, kuanzia Biblia, Quran, Torah (torat) na hata vya Monks. Na ni mpenzi wa vitabu vya falsafa na siasa.

Nashukuru kwa kunisaidia mwandishi kwa kuweka vipande vya Biblia katika uzi wako.

Ningependa kuwakumbusha haya machache ambayo niliyakuta katika Quran kuhusu wazazi (Yani Baba Na Mama)

Sura ya 17: 23... Inasema hivi "Na mungu wenu amewa amrisha msimuabudu yoyote isipokua yeye tu, na fanyeni wema kwa WAZAZI wenu. Na kama mmoja ama wote wawili (WAZAZI) wamefikia umri wa UZEE (wamezeeka) basi msi wasimange na wala msi wakemee kwa hasira, wala msiwaambie aaarghh, ongeeni nao kwa wema na upole"


Mama kakubeba miezi 9 kwa shida tumboni mwake, na kakuzaa kwa machungu makali sana, Baba kakulea kwa shida mpaka umekua mtu mzima (pengine kakusomesha mpaka chuo).

Sasa, hizi ndio fadhila za mema waliotufanyia wazazi toka tulipokua wadogo, tuwalipe kwa kuwaita majina machafu kama hili la "BABA JINGA" ????????


Mkuu tunawapenda Baba zetu lakini hatupendi ujinga na maovu yao. Tutawajibu kwa adabu, upole na kuwatendea mema lakini si kuzidi uwezo wetu. Hata wewe sasa fanya kazi, wekeza ili baadaye usiwe mzigo kwa wanao na wajukuu. Mbona iko wazi sana.
 
Back
Top Bottom