Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

Hiyo id ninayotumia ananiita hivyo mwanangu mmoja niliyemuangaikia kumsomesha elimu nzuri kwa hali yangu ya chini kwa kubangaiza baada ya kupata retrenchment nikiwa tu na miaka 7 kazini iliyokuwa NBC it was 1997 nimewasomesha wanangu international schools from primary to university levels je hizo ghalama nilizotumia tena kwa kujinyima zisingeweza kuweka investment ya kula maisha? leo hii mambo yaniendee kombo niitwe jinga!! kwa kauli km hii watoto wangu hawezi kuelewa mleta mada may be kuna jinsi mzazi wake hakumjengea future so ana hasira naye yangu hayo tu
Ulitimiza wajibu wako vizuri. Natumaini watoto wako pia watafanya hivyo kwa wajukuu wako/watoto wao.
 
sijui
baba alifyatua watoto 12 wewe wa kwanza amekusomesha kwa kuuza mashamba na mifugo
leo hii umepata kazi take home laki 6, hapo unatakiwa usomeshe wadogo zako na usaidie nyumbani
wewe upo mjini umepanga una mke na mtoto , mke hana kazi na ndugu zake wanakutegemea
Yaani km umenisemea Mimi. Ulipe kodi yako na ya kwenu. Wadogo zako wasome, that is too much, Mimi naamini Mungu hapendi umaskini. Ile tabia ya MTU kuwa mvivu alafu anadai ni mipango ya Mungu ni upumbavu mkubwa
 
Mimi huwa nakaa naumia, nakumbuka mwaka 2001 Dada YANGU wa tatu kuzaliwa alifaulu sekondari. Ila kwa vile baba hakuwa na future na mwanae form two akaishia kwa kukosa 40000 ya ada kwa mwaka mzima. Wakati huo huo ndugu zake wapo waliokuwa na uwezo watoto wao walikuwa shule za gharama. Tulivyoanza shule tulijua kajifunza, ila Mimi na kaka YANGU tumefika sekondari akaanza kumtegemea shemeji yetu kutusomesha. Shemeji alipozenguana na sister na kuoa mke mwingine ndo ukawa mwisho wetu wa kusomeshwa. Tumesoma kibishi tulipoishia ni tudiploma tu tena kwa kuomba misaada ya watu mbalimbali. Nakumbuka nikiwa chuo nilishatumia km yatima aliyefiwa na wazazi wake nikasomeshwa mpk mwaka wa mwisho. Huku mzazi akiwa hai. Nimemaliza kurudi kwenye ajira za serikali utegemezi 100% kuanzia kodi ya kila mwezi, wadogo madaftari hadi tuition za 200 kwa siku zinakosekana. Utoe mshahara wenyewe 500k hivi kwa njia hiyo kuna kuendelea. Hapo bado kuna mke, mtoto, matumizi binafsi, michango nini kitatokea. Sikatai kusaidia wazazi, ila kuna wazazi wengine wavivu na WAMEZENGUA SANA. Ni bora mzazi aliyefight kukusomesha kuliko mzazi aliyetegemea kusomeshewa watoto na msomeshaji alipokataa akawa ana future. For me ni more than pain. Maana nilijikuta nimesoma fani nisyokuwa nimeipanga, ila nilifika huku sababu ya umaskini.
 
Hiyo id ninayotumia ananiita hivyo mwanangu mmoja niliyemuangaikia kumsomesha elimu nzuri kwa hali yangu ya chini kwa kubangaiza baada ya kupata retrenchment nikiwa tu na miaka 7 kazini iliyokuwa NBC it was 1997 nimewasomesha wanangu international schools from primary to university levels je hizo ghalama nilizotumia tena kwa kujinyima zisingeweza kuweka investment ya kula maisha? leo hii mambo yaniendee kombo niitwe jinga!! kwa kauli km hii watoto wangu hawezi kuelewa mleta mada may be kuna jinsi mzazi wake hakumjengea future so ana hasira naye yangu hayo tu
Mzee hilo ni jukumu lako kuwasomesha elimu nzuri sababu umewazaa mwenyewe. Watakapojitegemea nao watakuwa na jukumu la kulea watoto wao, siyo wewe. Sababu umewekeza kwenye elimu yao ni vizuri pia ukajiwekeza angalau kidogo wapate kitu cha kukusaidia na hata kurithi. Siyo unafariki huna hata kiwanja cha kurithisha wanao, huo ni umaskini wa fikra
 
Unajua watu hawapingani na fikra zako ila maneno yako ulioyatumia hyajaleta taswira nzuri.

Mkuu watu wamezoea wakifanya mabaya wapewe lugha nyepesi lakini kwa watu wadizaini yangu hatutumii kanuni hiyo. Ukifanya uzembe maneno makali ni sehemu ya matokeo
 
Mimi huwa nakaa naumia, nakumbuka mwaka 2001 Dada YANGU wa tatu kuzaliwa alifaulu sekondari. Ila kwa vile baba hakuwa na future na mwanae form two akaishia kwa kukosa 40000 ya ada kwa mwaka mzima. Wakati huo huo ndugu zake wapo waliokuwa na uwezo watoto wao walikuwa shule za gharama. Tulivyoanza shule tulijua kajifunza, ila Mimi na kaka YANGU tumefika sekondari akaanza kumtegemea shemeji yetu kutusomesha. Shemeji alipozenguana na sister na kuoa mke mwingine ndo ukawa mwisho wetu wa kusomeshwa. Tumesoma kibishi tulipoishia ni tudiploma tu tena kwa kuomba misaada ya watu mbalimbali. Nakumbuka nikiwa chuo nilishatumia km yatima aliyefiwa na wazazi wake nikasomeshwa mpk mwaka wa mwisho. Huku mzazi akiwa hai. Nimemaliza kurudi kwenye ajira za serikali utegemezi 100% kuanzia kodi ya kila mwezi, wadogo madaftari hadi tuition za 200 kwa siku zinakosekana. Utoe mshahara wenyewe 500k hivi kwa njia hiyo kuna kuendelea. Hapo bado kuna mke, mtoto, matumizi binafsi, michango nini kitatokea. Sikatai kusaidia wazazi, ila kuna wazazi wengine wavivu na WAMEZENGUA SANA. Ni bora mzazi aliyefight kukusomesha kuliko mzazi aliyetegemea kusomeshewa watoto na msomeshaji alipokataa akawa ana future. For me ni more than pain. Maana nilijikuta nimesoma fani nisyokuwa nimeipanga, ila nilifika huku sababu ya umaskini.

Shida ni kuwa watu hawataki kuambiwa ukweli. Wanasahau wajibu wao alafu hawataki kukosolewa. Asiyekosolewa ni Mungu pekee. Mzazi anaheshimiwa lakini si kwa mambo ya kipuuzi na kijanga. Wasamehe wazazi wako na uwahudumia kwa kiwango chako
 
VIPI MWANA KUMTEGEMEA BABA........NIJUAVYO HAKUNA MWANAUME ALIYEKOMAA AKILI KIUME ANATAKA KULISHE NA MWANAYE ILA HUPOKEA KAMA ZAWADI.....HAKUNA ANAYETAKA KUWA MZIGO KWA MWINGINE ILA PALE INAPOBIDI....WATU TUNAZAA ILI TUJE KUSAIDIANA HIVYO LOLOTE LAWEZA KUTOKEA HIMA BABA KUMPA MWANA AMA MWANA KUMPA BABA.....HAYA NI KATIKA MAHABA NA MAPENZI....HAYA UKAWA TAJIRI VIPI UPEWACHO NA MTU HASA MWANAO UTAKIPENDA JAPO ULIKUWA UNAJIWEZA KUMUDU KUNUNUA MWENYEWE....HUO NDIO UBINADAM NA UKIWA UNAKEREKA NA HAYO BASI UNALETA UNYAMA....MTU KATIKA KUTOA/KUSAIDIA UNATAKIWA KWANZA UANGALIE FAMILIA YAKO KISHA NDIO WATU BAKI HIVYO HIVYO HATA KATIKA KUHITAJIA MSAADA BASI UNAANZA NA NDUGU ZAKO KISHA NDIO WATU BAKI...HII PIA INATOKA NA KWAMBA NDUGU NDIO WALAU WANAWEZA KUKUTUNZIA SIRI/AIBU NA NDUGU NDIO HUWA NA UCHUNGU/HURUMA JUU YA NDUGU YAKE KULIKO MTU BAKI.......BABA ANAPOTAABIKA WATU HUANZA KUSEMA HUYU MZEE ANA WATOTO WAKUBWA WAKO HUKO MJINI WANAKULA TU BATA.....NI AIBU KUSAZA CHAKULA MZAZI HUKU HAJUI BAADA YA ____ASUBUHI___MCHANA____USIKU NAO ATALALA VIPI HUKU MWANAE ANAZUNGUSHA MEZA.........PENGINE WEWE MTOTO UMEKUWA SABABU YA UFAKAR WA BABA ALIJINYIMA ILI WEWE UPATE KITU FULANI.......SASA NISEME HIVI HATA BABA AKAWA NI KAMA BILLGATE USIACHE KUMPELEKEA SHATI NA MKEWE KITENGE......NA NISEME BABA HATA AKABWETEKA HIVI KWAKO MITHALI UNACHO CHA KUMPA MPE MUHUDUMIE AJISIKIE MANA KERO ZA KUKULEA WEWE KAZIVUMILIA NAWE MVUMILIE UZIPATE RAZ ZAKE.....KIJANA TENA WA KIAFRICA HASA SISI WA UJAMAA NDOTO ZETU NI KUJA KUWA MSAADA KWA WAZAZI WETU....HAKUNA ANYEPENDA KUOMBA AU KUWA TEGEMEZI ILA TU MAISHA NDIO HUMFIKISHA HUKO........
 
Watu wengine hovyoo sana. Hii yote ni kuendekeza uvivu. Hawa hawa ndio watakao waambia watoto wao nilikusomesha ili unisaidie. Pumbavu sana
Ngoja na wewe uwe mzee, kama watoto hawajakuita baba jinga;kila mmoja katika maisha alitegemea kuwa tajiri,lakini kutokana na changamoto za maisha wamejikuta jinsi walivyo.Nadhani wewe bado ni bachela na una mihemko ya kiujana,au ndio unaanza maisha, hebu jaribu kuwa na familia kwanza uitwe baba ndio uje na mawazo ya kiutu uzima zaidi.
 
Haina shida Mkuu, kuitwa jina hilo ni haki ya mtu mzembe kama ilivyo haki ya mtu aliyekuwa mwerevu akiwa kijana
 
Kinachosikitisha,wazee wa siku hizi wanavaa mlegezo.
hata wakilipiwa karo hawasomi wakisubiri kula
mali walizowekewa na baba zao,vyuoni ni mashindano
ya ngono na kupambana kuwa na nguvu za kiume badala ya nguvu za masomo.
kweli wazee wanaotegemea kuvuna kutoka kwa vijana wao ambao
ndio chanzo kikubwa cha umasikini wao tuwakatae.
Ningekuwa kijana wa leo ningesusa mzee wangu asinipeleke shule
kuharibu hela bali ningemshauri awekeze kwa nguvu zote ili baadaye
aniachie urithi na wanangu.
 
Kweli Mkuu
 
Back
Top Bottom