Sijasema mtu asiwasaidie wazazi wake ila nimesema ni Aibu kwao kusaidiwa na watoto. Watu wangejua nini maana ya Baba wasingepinga hii Mada. Sema wazazi wa siku hizi wamekuwa wavivu, watu wa anasa, watu wabadhirifu na wabinafsi. Mzazi ni mtoaji mtoto ni mpokeaji siku zote bila kujali umri wa mtoto.
Hata hivyo ujumbe huu unanihusu mimi na wewe kijana wa sasa. Ikiwa utazembea sasa hivi eti kisa umezaa watoto hata Mungu aliyekuumba atakushangaa. Mungu anahitaji watu wenye akili na wenye kumtii yeye na kumuiga.