Hakuna atakayeachia ngazi sakata la Escrow

Hakuna atakayeachia ngazi sakata la Escrow

Status
Not open for further replies.
Ulipewa ngapi?

Sijapewa chochote lakini kwenye hii nyuzi nnamwambia Habinder Sing Sethi na mwenzake Rugamalira (sijui kama nimeliandika sawa hilo jina) wanione japo ki 40m tu, napoteza usingizi wangu kuwa wakili wao wa kujitolea wa JF.

You never know.
 
huyu katoka wapi watanzania wasasa kwa elimu zetu za msingi ambazo ni form four huwezi kutudanganya huku tunajua namna ya kuyabainisha yanayotekea.
 
Mahakama ilishaamuwa hakuna tatizo na wamemalizana na ikaamuru kuwa kila linaloihusu IPTL kwa sasa litabebwa na PAP na PAP wamekubali kama kuna madeni yoyote wao ndiyo watayalipa, na mikataba ikasainiwa baina yao na TANESCO na Serikali na ndiyo sababu kubwa mpaka leo kuna B 90 hawajalipwa, ikiwa kuna madai yoyote zitatoka kwenye hizo, wanachodaiwa according to Zitto si zaidi ya B30. Sasa fikiri una B30 zao unasema wamekwepa kodi ya B30? haiingii akilini.
Usikimbie sana tupe mwongozo,kulikuwa na taratibu gani hadi PAP wabebe lolote lile kuhusu IPTL?
 
mpaka ccm wakubali kwamba huo ni wizi mpaka rais achukue hatua, bila hivyo watasema mafisadi ni wale waliochunguza huo wizi
 
Kwa hiyo CAG,TAKUKURU na TRA wamechemsha kusema zile pesa ni za Uma .
Hawajasema ni za umma wao wenyewe hawana uhakika.tra amesema hatujalipwa vat.
CAG AMEDAI ANA HAKIKA KATIKA PESA HIZO KUNA ZA UMMA na za iptl,na hataji idadi ipi ni za umma,maana yake ni kwamba kumbe hata mahesabu hajui au mzee huyo amehongwa apindishe ukweli.
takukuru hawana ushaidi wa kutosha kwamba mhongo,pinda,maswi wamekula rushwa.
 
Hakuna mahala nilipoona kuwa Mwanashera Mkuu kabariki wizi. Nnachokiona ni fitna tu.

Mwansheia anatuhumiwa kuwa kamwaamuru Gana alipe, wakati huohuo Gavana ndiye wakala wa walipaji na walipwwaji, sasa kama Gavana iweje aamriwe na AG? atakuwa ni punguani huyo Gavana.

Shutuma nyingine niliyoisikia ni kuwa eti kwanini AG kaseema hio pesa zi za umma? khaa! what a rubbish point, kama zilikuwa za umma kwanini zikae escrow account? fikiri.

Hizo ndiyo tuhuma kwa AG zilizozosikia na zote ni bogus si za kumfanya mtu aachie ngazi, kama unazijuwa zingine nifahamishe.
alimwambia gavana kwamba pesa za escrow zimelipiwa kodi hivyo zitoke kumbe uongo. watu wa serikali hufuata ushauri wa sheria kwa wanasheria wa serikali hivyo werema alimpotosha ndullu. pia kwa makusudi au uzembe kama mwanasheria mkuu alitafsiri kimakosa uamuzi wa mahakama kuhusu pesa za escrow kumbuka gavana hawezi na hana mamlaka ya kutafsiri sheria.
 
una roho ya paka hufi haraka lakini safari hii zote zitatoka. time will tell. TRA CAG TAKUKURU wote hao yaelekea ni wafuasi wa zito au sio?

ndo tumshangae huyu mtetea uozo. zitto na kamati wamechambua taarifa na kuwasilisha.
 
Hadi jana ulikomaa kwamba Report haiwasilishwi leo,
haya imewasilishwa, unapambana na mapendekezo ya kamati!

Samahani sana lakini nasikitika kukuita muongo. Kama u mkweli kwa hilo, onesha ni wapi nilikomaa kuwa ripoti haiwasilishwi leo, daima nimeandika humu kuwa watu wasiandikie mate na wino upo, wangoje ripoti rasmi.

Wacha uongo, nioneshe hiyo post unayodanganya nimesema hivyo.
 
Sihangaiki bali natoa mawazo kwa muono wangu kama wewe unavyotoa mawazo yako kwa muono wako.

bora uokolewe kifikra bado unafikira finyu ya upembezi wa mambo muhimu..... vipesa vya misimu wanavyokupatia ndivyo unatetea uendelee kupata huku ndugu zako wakitaabika kuwa na hurumu.
 
Sijapewa chochote lakini kwenye hii nyuzi nnamwambia Habinder Sing Sethi na mwenzake Rugamalira (sijui kama nimeliandika sawa hilo jina) wanione japo ki 40m tu, napoteza usingizi wangu kuwa wakili wao wa kujitolea wa JF.

You never know.

j(ames) Ruge(mali)ra: nipe mpesa namba yako haraka sana. ahahahaha
 
Wewe unayemwita Chenge ni kichwa lazima umetegesha mrija wako siyo bure. Consultation 1.6 Billion? halafu unathubutu kusema Chenge ni kichwa acha porojo wewe binti FF

Hata kama chanzo cha ugali wako ni ccm si kutetea kila kitu.

ajitambue
 
Hapo sasa.

Kinachowauma zaidi ni kuwa TANESCO walifunguwa kesi na kesi ikakaa miaka mingi sana, inabidi capacity charges zilipwe tu hata kama haitumiki.

Huo ndiyo ujinga wa TANESCO.

Kweli kuna kusikia na kusikiliza, yaani huo ndio uelewa wako kwenye hii taarifa? Basi unasafari ndefu kujua kilichozungumziwa.

Kwa kifupi, fedha za escrow hazikutakiwa kutoka mpaka kuwe na maridhiano kuwa ni kiasi gani kinagharamiwa kama capacity charge. Baada ya kukokotoa ndipo kila muhusika achukue chake.

Mpaka sasa PAP haijawakilisha hati halisi za kununua hisa za Mechmar kwani hati hizo zipo mahakama ya BVI.

Kwa maana hiyo PAP kuwa inachkua madeni ya IPTL ni utapeli. Inawezekana kuwa PAP ni kampuni halali lakini kwenye hili la IPTL imenunua dili hewa ili ifanikishe kukwiba fedha.

Hao waliolipwa na JL kwa nafasi zao na kama watumishi wa umma na kwa mujibu wa maadili ya viongozi walipaswa ku-declare zawadi walizopokea. Kwa kutokufanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
 
alimwambia gavana kwamba pesa za escrow zimelipiwa kodi hivyo zitoke kumbe uongo. watu wa serikali hufuata ushauri wa sheria kwa wanasheria wa serikali hivyo werema alimpotosha ndullu. pia kwa makusudi au uzembe kama mwanasheria mkuu alitafsiri kimakosa uamuzi wa mahakama kuhusu pesa za escrow kumbuka gavana hawezi na hana mamlaka ya kutafsiri sheria.

Kuna Billion zaidi ya 90 ambazo hazijalipwa, umeshajiuliza kwanini? na ilitakiwa ziwepo kwenye hiyo account, na hayo kayasema Zitto leo hii, si mimi kwanini hajasema zanini zile? kwanini kababaisha na kusema tu ilikuwa ziwekwe billion 306 na zimewekwa billion 182 tu, billion 142 zimewekwa na Tanesco Billion 40 zimewekwa na Serikali, kwenye escrow account. Kwanini zimebaki na hazikuwekwa zote?
 
Wewe mtetezi wa wahuni na mafisadi utata utauona wapi!!!! Si ajabu nawe umo kwenye list ya kupata mgawo awamu ya pili baada ya kuonekana ukitoa povu zito karibu kila siku kuwatetea hao wezi.

Sijaona utata kwenye hayo malipo. Naona watu wanayafanya yaonekane yana utata.
 
Kweli kuna kusikia na kusikiliza, yaani huo ndio uelewa wako kwenye hii taarifa? Basi unasafari ndefu kujua kilichozungumziwa.

Kwa kifupi, fedha za escrow hazikutakiwa kutoka mpaka kuwe na maridhiano kuwa ni kiasi gani kinagharamiwa kama capacity charge. Baada ya kukokotoa ndipo kila muhusika achukue chake.

Mpaka sasa PAP haijawakilisha hati halisi za kununua hisa za Mechmar kwani hati hizo zipo mahakama ya BVI.

Kwa maana hiyo PAP kuwa inachkua madeni ya IPTL ni utapeli. Inawezekana kuwa PAP ni kampuni halali lakini kwenye hili la IPTL imenunua dili hewa ili ifanikishe kukwiba fedha.

Hao waliolipwa na JL kwa nafasi zao na kama watumishi wa umma na kwa mujibu wa maadili ya viongozi walipaswa ku-declare zawadi walizopokea. Kwa kutokufanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Hilo lilishaamuliwa na ICSID, msikilize tena Zitto.
 
JAMAA WA CAG HAWANA UHAKIKA NI PESA YA UMMA AMA YA IPTL...

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
¡°... Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu. Kundi la kwanza hiyo fedha ilikuwa na kodi ndani yake kwa hiyo tungesema kulikuwemo na fedha ya Serikali kwa maana ya kodi. Kwa upande mwingine, kwa sababu mpaka ESCROW inafunguliwa kulikuwa na dispute, kulikuwa na kutokubaliana juu ya charges, kwa hiyo kuna fedha ambayo inaweza ikawa ni ya TANESCO na kuna fedha ambayo inaweza kuwa ni ya IPTL ...¡±
Kamishna Mkuu wa TRA
¡°... TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT. Kwa hiyo, kulikuwa na VAT Component ambayo haikutakiwa kwenda kule
 
Wewe mtetezi wa wahuni na mafisadi utata utaona wapi!!!! Si ajabu nawe umo kwenye list ya kupata mgawo awamu ya pili baada ya kuonekana ukitoa povu zito karibu kila siku kuwatetea hao wezi.

Hapana sijapata chochote, njoo na hoja usije na viroja.

Lakini wakiniona hapa kina Habinder Sing Sethi na James, wakinifikiria sizikatai lakini zisiwe chini ya 40m.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom