Hakuna anayependa kukuona unafanikiwa

Hakuna anayependa kukuona unafanikiwa

Kuna wengine kila siku anapiga picha akiingia ofisini, anweka status za kazi hadi mood zake ktk mtandao hii unampa enemies kujua your tracks....siku ukianguka wanajua a to z yako kupiyia mtandao tuu
watu wa hivi hua wananishangaza sana....yani utajua maisha yake yoooote kupitia status...kama amelala njaa utajua...kama katiwa/katia jana utajua...yani utajua hadi mida hii yupo sehemu flani...yani no privacy at all duh....me hua naogopa eti...
 
Watu wana roho mbaya jamani acheni mchezo.. Kuna wengine etii humu humu id fake kila kitu fake.. Lakini anamchukia balaa mtu bila hata sababu za msingi.
 
Kinachosikitisha hizi tabia zipo hadi kwenye familia kuna hadi wazazi wanapenda ona watoto wao wanahangaika alafu wanajifanya wao ni manabii eti nilisema mimi nachukia sana Aina hizi za familia
Mkuu wewe umeleta hoja nyingine nzuri na iliosahauli, kuna baadhi ya wazazi ambao pia wanakuwa kikwazo cha mafanikio ya watoto wao kwa makusudi kabisa hata hao kina mama ambao kila mtu huonyesha kuwaamini asilimia nyingi..mifano hai ipo! muhimu ni kuwa makini zaidi na mtu yeyote linapokuja swala zima la harakati za kimafanikio.
 
Hivi kwanini binadamu amepewa macho, masikio, mdomo, pua, mikono na miguu nk; na kichwa chenye ubongo? Halafu mungine nae anavyo timamu lakini havitumii halafu anamlaumu mwenzake kwa kuvitumia kujikomboa.
Wazungu wasingekuwa wachoyo utumwa na ukoloni usingetokea. Asili ya binadamu ni uchoyo na ubinafsi. Ubepari.
Ila wenzetu wana umoja katika kulinda maslahi yao wote pamoja (common interests) bila kusalitiana. Angalia weusi! Shida!
 
Umesema kweli tupu Mkuu. Na hasa namba moja nimejikuta naielewa mno Mkuu.

Sema sasa inapotokea umepambana kwa siri na wakaona wakati umeshafanikiwa bado chuki zao zinakuwepo vile vile. Kiukweli binadamu hatuna jema na kwa hali hii inabidi tuzoweane tu kwa kweli.
Nakubaliana na wewe Dada angu
 
Chuki lazima iwepo bila wivu na ubaya hakuna mafanikio ,Tufurahie kupambana na wabaya wetu ili tuwape Changa moto waumie zaidi !
 
Kweli tena sana....aisee kuna rafiki yangu nasoma nae the age almost the same...sasa tunamaliza chuo na mm nina kakazi kananipaga tu pesa ndogo ya kula....aisee yaan nikiwa na maisha tofauti tu yeye kisa namzidi vipesa nasikia anatangaza naishi maisha fake....nimeshangaaaa kweli yaan
 
Asee nikwelii kunawatu naviatu ktk dunia hii namengi ila ntaludi
 
Ni aina ya watu unaoshirikiana nao ndio tatizo!.
Nilifanikiwa kabla ya wenzangu, mmoja alikuja kaa kwangu mpaka alipopata kazi yake na akaenda jitegemea, wengine tumeshiriki kujengana!.
Matter of fact wao ndio walihusika kunitambulisha wabaya wangu nisipokuwepo same to me!, tuna matatizo yetu sehemu nyingine lakini sio katika kutafuta mafanikio!..
Aina ya marafiki na jamaa ulionao ndio tatizo lako!.
 
Kuna mfanyakazi mwenzangu mmoja hivi hapendi kabisa ufanikiwe yaani umzidi kimafanikio. Kimya kimya nimekodi shamba nimelima matikiti nimekuja kushangaa baada ya muda ananiuliza kwa kejeli hivi eti matikiti yanaendeleaje nikamjibu tu fresh.
Kwake itakuwa furaha sana nisipopata maana mpaka sasa naamini anajua hata yanaendeleaje ila nikija kufanikiwa lazima nije nimwonyeshe kuwa nimefanikiwa
 
Kuna mfanyakazi mwenzangu mmoja hivi hapendi kabisa ufanikiwe yaani umzidi kimafanikio. Kimya kimya nimekodi shamba nimelima matikiti nimekuja kushangaa baada ya muda ananiuliza kwa kejeli hivi eti matikiti yanaendeleaje nikamjibu tu fresh.
Kwake itakuwa furaha sana nisipopata maana mpaka sasa naamini anajua hata yanaendeleaje ila nikija kufanikiwa lazima nije nimwonyeshe kuwa nimefanikiwa
Duh makazini wapo wengi sana.

Hata kama unafahamu kitu fulani, yeye hakifahamu, ukisema atasema nioikuwa nataka kusema hivyo ameniwahi wakati alikuwa hajui.
 
Maisha yetu wanadamu yanasiri kubwa mnoo, pia nimeamin tumeumbwa kwa mioyo yenye chuki na husda, hii ni baada ya kufanya uchunguz takriban wa miaka minne nimegundua katika swala la mafanikio hakuna mwema, labda tu (mama yako mzazi).
Hili limejidhihirisha kwa marafiki zangu wa karbu, ambao tume husttle pamoja kwa muda mrefu ,lakin linapokuja suala la maanikio yangu wameoneshwa kutopendezewa kabisa na wengine kushindwa kuficha hisia zao na kuaonesha chuki za waziwaz kwangu au kufuta urafiki kabsa.
SOMO:-
i/Tambua hakuna anaependa umpite kimaendeleo au uwe na mafanikio makubwa kuzidi ww, chakufanya Pambana kwa siri sana mpaka pale utakapo fanikiwa waone wenyewe kwa macho yao
ii/Epuka kuweka mipango yako/mfumo(USIRI) wako wa kimaisha kwao, maana ni sawa na kuuza raman ya vita kwa adui yako
iii/Usimpe faida mtu asiye kupa faida katika maisha yako
iv/Soma tabia za marafiki / ndugu zako ili ujue unaishi nae vipi ili asiwe kikwazo katika njia yako ya mafanikio
v/Epuka kutumiwa kama daraja la mafanikio ya wengine hapa ni kuwa mtu wa kutoa ushaur sana au kupanga mipango ya mafanikio kwa kushirikisha hawa wasio wema kwako
vi/HAKUNA MWEMA KWENYE MAISHA YAKO.
Umenena ukweli mtupu
 
Back
Top Bottom