Hakimu ajitoa kusikiliza kesi ya Tsh. Milioni 315 baada ya mshtakiwa kumkataa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,117
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Kisutu, Richard Kabate, amejiondoa kusikiliza kesi ya kujipatia Sh315 milioni kwa njia ya udanganyifu, baada ya mshtakiwa Prepetua Gondwe (25) maarufu kama Annastazia kudai kuwa hana imani na hakimu huyo.

Annastazia anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kughushi nyaraka na kujipatia Sh315 milioni kutoka kwa Ritha Remi, ambaye ni mstaafu kwa madai kuwa anataka kufanya biashara, wakati akijua ni uongo.

Uamuzi wa hakimu Kabate kujitoa kusikiliza kesi hiyo ya jinai namba 114/2022 umetolewa leo, Aprili 12, 2022 na yeye wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya usikilozwaji.

Hakimu Kabate amejitoa kusikiliza shauri hilo ambalo tayari shahidi wa kwanza ameshatia ushahidi wake na leo upande wa mashtaka walikuwa na shahidi na waliomba kuendelea na shahidi, lakini kutokana wakili wa mshtakiwa kutokuwepo kesi hiyo imeshindwa kuendelea.

"Kesi hii imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara kutokana na wakili wako wewe mshtakiwa kutokuwepo mahakamani hapa, pamoja na yote mshtakiwa wewe umekuwa ukilalamikia mahakama kuwa inachelewesha kesi yako bila kuwa na sababu ya msingi," amesema Hakimu Kabate.

Hakimu aliendelea kusema kuwa hata ziara ya Jaji Kiongozi Mustapher Siyani alipotembelea magereza, mshtakiwa huyo alipata nafasi ya kutoa malalamiko yake juu ya ucheleweshaji wa kesi yake wakati anajua wazi anayechelewesha kesi hiyo isiendelee na usikilizwaji ni wakili wake.

"Hata leo hii kesi hii haiwezi kuendelea kwa sababu wakili wako hayupo na huna taarifa zake. Unakumbukwa kesi hii ilifutwa kwa hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa baada ya wewe kushindwa kuhudhuria kesi yako na kuruka dhamana ndio ikaletwa kwangu?

"Ni vizuri ukatafakari malalamiko yako unayotoa juu ya kesi hii, mimi najitoa kusikiliza kesi hii kuanzia leo na jadala la kesi hii ninalirudishwa kwa hakimu Mfawidhi wa Mahakama hii kwa ajili ya kulipangia hakimu mwingine, hivyo kesi yako itatajwa April 25, 2023," amesema Hakimu huku akifunga jalada na kumpatia karani.

Hakimu Kabate alisema mshtakiwa huyo ataendelea kubaki rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Katika kumbukumbu za mahakama kesi hiyo imewahi kuahirishwa na kushindwa kuendelea na usikilizwaji kati ya Januari 18, 2023; Machi 14, 2023; Machi 27, 2023, April 6, 2023 na leo April 12, 2023 kutokana na wakili wa mshtakiwa kushindwa kufika mahakamani hapo.

Awali Kabla ya kujiondoa kwa hakimu huyo, Wakili wa Serikali Ashura Mnzava alieleza Mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa ushahidi na upande wa mashtaka wanae shahidi mmoja.

Kuruka dhamana

Agosti 19, 2022 mshtakiwa huyo alifutiwa kesi na kufunguliwa nyingine yenye mashtaka hayo, baada ya kuiomba Mahakama hiyo urudie kusikiliza ushahidi kuanzia shahidi wa watatu hadi wa sita wa upande wa mashtaka ambao tayari walishatoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa.

Inadaiwa kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo ya mwanzo, mshtakiwa huyo aliruka dhamana, hali iliyosababisha kesi hiyo kuendelea bila kuwepo mshtakiwa mahakamani.

Mshtakiwa baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, anayekuwa anasikikiza shauri hilo, Huruma Shaidi alimueleza mshtakiwa kuwa aliruka dhamana na kushindwa kuhudhuria kesi yake hadi alipokamatwa na kupelekwa mahakamani.

Hakimu Shaidi alisema ili mshtakwa aweze kupata nafasi ya kusikiliza upya ushahidi huo, ni vizuri kesi hiyo akaifuta ili ifunguliwe nyingine.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom