Hakika Wachina wana Mungu wa Kweli

Supermind

Supermind

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
200
250
Habarini wanajamvi.

Nimekuwa nikitafakari siku nyingi juu ya uwepo wa Mungu. Lakini majibu bado ni utata mkubwa na kujazwa imani kila kukicha.

Watu weusi ndio kizazi pekee chenye imani ya dhati juu ya huyu Mungu asieonekana ambae tusadiki ndie Mungu wa kweli. Lakini cha kushangaza sijui tunakwama wapi. Tumekuwa tukizama kwenye maombi juu ya vitu vingi lakini matokeo ni sisimizi (yaani kidogo sana au hamna kabisa).

Ila wenye imani huzidi kukutia moyo na kukwambia maombi yatajibiwa tu sio lazima wee ujue. Au watakwambia yalishajibiwa ila wee huna jicho la kiroho pengine hukujua. Kwa kweli ni mafumbo mengi na imani tuu na kudhania dhania ndiko kumetawala. Kimsingi nimechunguza binafsi imani hii, mtu maskini wala haimsaidii kiviile, sana naona ndo wanazidi kuwa maskini tu, sjui kwa nini.

Wenzetu WACHINA tumekuwa nao sawa kimaendeleo na kiuchumi mwanzoni mwa vita vya pili vya dunia. Hawa watu inasadikika hawana imani wala dini yeyote nchini mwao. Muasisi wa Taifa lao bwana Mao Tse dong inasemekana alipiga marufuku dini zote wakati wa ujenzi wa ujamaa wa china. Nchi ilipiga hatua kwa kasi ya ajabu hadi leo ni tishio duniani kiuchumi na maendeleo.

Maswali magumu ya kujiuliza, kwa hawa wachina;

1. Ni nani anawabariki wakati hawaamini katika Mungu na wala hawasali.?
2. Mbona kila siku wanafanya maendeleo makubwa wakati hata misikiti na makanisa hawana.?
3. Mbona sisi Waafrika tunamwamini Mungu wa Mbinguni na tunasali sana lakini hatupati baraka kama za wachina?
4. Waafrika tunakosea wapi hasa.? Au tunakosea namna ya kuabudu na kuendesha hizi dini.?

Wachina wameendelea kuishangaza dunia.

*Wameweza kujenga hospitali/ karantini kubwa duniani ya wagonjwa wa corona kwa wiki moja tu.
*Wameweza ku-wipe out/kuifutilia mbali corona kwa mda wa mwezi mmoja tu
*Wachina wanazidi kuwa tishio kiuchumi na kimaendeleo duniani kote kila kukicha.

Je, ni nani hasa Mentor wao? Kwanini hawa watu wanaodaiwa kukosa imani ya Mungu tumuabuduye sisi wanazidi kuchanja mbuga kwa kila kitu, ili hali sisi tuaminie tunazidi kuwa masikini?

Kwa maoni yangu kuna haja ya kufanya research juu ya huyu Mungu wa uchina awasaidiae ili kama vip nasi tu-adapt/tuige. Maana si kwa kufanikiwa huko.

Sijataka kuzama sana kwa undani kuhusu uchina kuepuka kuwachosha wasomaji na wachangiaji. Ila kimsingi wachina wanavitu ni hatari.

Karibuni wanajamvi tujadili kwa ajili ya kubadili mind set na kupanuana kifikra.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
October man

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,208
2,000
Duu Mungu hatimaye anapimwa kwa maendeleo aliyonayo mtu.

Basi USA ndio wana mungu kweli.

MoDewji ana Mungu wa kweli kwasababu tajiri ila mbona Mungu huyohuyo ndio wangu then mimi masikini basi sio mungu wa kweli.
 
Mr Big

Mr Big

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
478
1,000
Theory yako haiko applicable,its only materialistic...

Hebu fanya utafiti vyema then uje na hoja za msingi zaid kuhusu hili...
 
tang'ana

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
8,746
2,000
hawa wachina nafanya nao kazi..sisi tukiwa tunasali wao wanatushangaa tu,wanatuuliza how can you pray for something that you can't see it?but pia wanaheshimu sana imani za watu hasa mkiwa maeneo ya kazi.
 
W

wise-comedian

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
3,207
2,000
Usiwe narrow minded, wachina hawajawahi kuwa sawa kimaendeleo na jamii yeyote ya Africa katika kipindi chochote cha maisha ya dunia, walikuwa na ancient civilization iliyokuwa na philosophers wa kubwa wanaoheshimika mpaka leo, traditional medical experts waliobobea, architectural designs za kuushangaza ulimwengu refers to great wall, na mengineyo kibao yanayowazidi hadi mabeberu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkulima gwakikolo

mkulima gwakikolo

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
594
500
Hoja ipo hapa..Waje manabii na maskofu..waseme hapa!!Mungu akubarki na Mungu hatakubark kama humuchi..je Kwanini Mungu huwabark wabudu sanamu? Wachina wengi huubudu sanamu na Manyoka na Mavyura makubwa from Everest mountains!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nzi ni nyuki mjinga

Nzi ni nyuki mjinga

JF-Expert Member
Jan 13, 2020
818
1,000
Kutokuamini MUNGU si tatizo maana ni uchaguzi. Ila kuishawishi jamii isiamini MUNGU ni tatizo sana na inaweza kutishia hata uwepo wa kiumbe binadamu duniani.

Embu fikiri tu, tugeuze mafundisho yote ya dini kuwa kinyume, mfano usiue, usizini, usiibe n.k.

leo hii ikikubalika kwamba hakuna MUNGU unajua nn kitafuata? Binadamu wataabudu binadamu aliye na nguvu. Kutakuwa hakuna maraisi bali kuna mungu wa Tz, Kenya, Ug au mungu wa Africa.

Kama ww ni mpenzi wa documentaries na movies lazima itakuwa umeshakutana na jamii zinazoabudu binadamu zinavyokuwa.

Uwe muamini au la, tunahitaji jamii ambayo watu wake na viongozi wana hofu ya MUNGU.
 
No retreat no surrender

No retreat no surrender

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
1,898
2,000
Jibu la mleta mada liko pale pale kwamba hata huku Africa ili uwe tajiri lazima uloge! China pamoja na kwamba hawamjui Mungu wa wakristo na yule wa waislamu lakini wanaimani zao za miungu ya sanamu kwenye temple zao katika ngazi ya familia na koo! Wanatraditions za kuabudu za juuu sana na zimejengewa masanamu na mahekalu watu uabudu na kuzitolea sanaka!

Kwa mukutadha huo China wanaabudu miungu yao ya sanamu na mwingine ana sura ya kiongozi wa kwanza Mao The Tung na anaabudiwa katika ngazi ya juu sana kama mungu! Kwa wakristo tunaamini kama huna Yesu waliobaki wote ni miungu (mashetani) na yana nguvu ya kutajirisha ndo maana hata katika ujenzi wa majengo makubwa na madaraja wachina ufanya makafara usiku!
 
Baba Joseph17

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,342
2,000
Supermind,
Wachina wanadini zao ambazo ndizo zinazotawala mila zao, tofauti yao na sisi no kuwa huku Afrika tukipatwa na janga tunahimiza maombi wanjilishaji wanajitokeza kujifanya wao wanaliweza wanasingizia Zambi wao Wachina wakipata janga wanafanya tafiti za kisanyansi ili kupambana nalo
 
semper saratoga

semper saratoga

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
967
1,000
Supermind,
mkuu wachina ni watu wa dini kama watu wengine tu duniani. Tofauti yao ni kuwa hawaaamini katika dini za wajukuu wa Abraham(uislamu na ukristo/ujudea(judaism). Wana imani zao za mababu na dini zenye asilia ya kwao au majirani zao wa karibu India.

China kuna mahekalu (temples) makubwa sana tu ya dini zao za u buddha (Buddhism), Taoism na Confucianism. Dini za mashariki ya kati (uislam/ukristo/judaism) pia zina wafuasi wengi tu ingawa zinapigwa vita kwa kiasu kikubwa.
 
Actions Speak Louder

Actions Speak Louder

Member
Nov 12, 2019
87
125
hawa wachina nafanya nao kazi..sisi tukiwa tunasali wao wanatushangaa tu,wanatuuliza how can you pray for something that you can't see it?but pia wanaheshimu sana imani za watu hasa mkiwa maeneo ya kazi.
kweli kabisa wanaheshimu hawataki kuingilia imani za watu wao ni KAZI TU
 
J

juma mpemba

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
1,974
2,000
Jibu la mleta mada liko pale pale kwamba hata huku Africa ili uwe tajiri lazima uloge! China pamoja na kwamba hawamjui Mungu wa wakristo na yule wa waislamu lakini wanaimani zao za miungu ya sanamu kwenye temple zao katika ngazi ya familia na koo! Wanatraditions za kuabudu za juuu sana na zimejengewa masanamu na mahekalu watu uabudu na kuzitolea sanaka!

Kwa mukutadha huo China wanaabudu miungu yao ya sanamu na mwingine ana sura ya kiongozi wa kwanza Mao The Tung na anaabudiwa katika ngazi ya juu sana kama mungu! Kwa wakristo tunaamini kama huna Yesu waliobaki wote ni miungu (mashetani) na yana nguvu ya kutajirisha ndo maana hata katika ujenzi wa majengo makubwa na madaraja wachina ufanya makafara usiku!
Na hua wananunua misukule
..na naniliu naniii kwenye kujenga madaraja ambayo chini Kuna maji mengi na hivo ili kuyatawanya Yale maji ndo wanatumia icho kitu...na maingineer nyie mliosoma law of flotation izo makitu hamjui....hahahaahaa
 
F

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
3,220
2,000
Habarini wanajamvi.

Nimekuwa nikitafakari siku nyingi juu ya uwepo wa Mungu. Lakini majibu bado ni utata mkubwa na kujazwa imani kila kukicha.

Watu weusi ndio kizazi pekee chenye imani ya dhati juu ya huyu Mungu asieonekana ambae tusadiki ndie Mungu wa kweli. Lakini cha kushangaza sijui tunakwama wapi. Tumekuwa tukizama kwenye maombi juu ya vitu vingi lakini matokeo ni sisimizi (yaani kidogo sana au hamna kabisa). Ila wenye imani huzidi kukutia moyo na kukwambia maombi yatajibiwa tu sio lazima wee ujue. Au watakwambia yalishajibiwa ila wee huna jicho la kiroho pengine hukujua. Kwa kweli ni mafumbo mengi na imani tuu na kudhania dhania ndiko kumetawala. Kimsingi nimechunguza binafsi imani hii, mtu maskini wala haimsaidii kiviile, sana naona ndo wanazidi kuwa maskini tu, sjui kwa nini.

Wenzetu WACHINA tumekuwa nao sawa kimaendeleo na kiuchumi mwanzoni mwa vita vya pili vya dunia. Hawa watu inasadikika hawana imani wala dini yeyote nchini mwao. Muasisi wa Taifa lao bwana Mao Tse dong inasemekana alipiga marufuku dini zote wakati wa ujenzi wa ujamaa wa china. Nchi ilipiga hatua kwa kasi ya ajabu hadi leo ni tishio duniani kiuchumi na maendeleo.

Maswali magumu ya kujiuliza, kwa hawa wachina;

1. Ni nani anawabariki wakati hawaamini katika Mungu na wala hawasali.?
2. Mbona kila siku wanafanya maendeleo makubwa wakati hata misikiti na makanisa hawana.?
3. Mbona sisi Waafrika tunamwamini Mungu wa Mbinguni na tunasali sana lakini hatupati baraka kama za wachina?
4. Waafrika tunakosea wapi hasa.? Au tunakosea namna ya kuabudu na kuendesha hizi dini.?

Wachina wameendelea kuishangaza dunia.

*Wameweza kujenga hospitali/ karantini kubwa duniani ya wagonjwa wa corona kwa wiki moja tu.
*Wameweza ku-wipe out/kuifutilia mbali corona kwa mda wa mwezi mmoja tu
*Wachina wanazidi kuwa tishio kiuchumi na kimaendeleo duniani kote kila kukicha.

Je, ni nani hasa Mentor wao? Kwanini hawa watu wanaodaiwa kukosa imani ya Mungu tumuabuduye sisi wanazidi kuchanja mbuga kwa kila kitu, ili hali sisi tuaminie tunazidi kuwa masikini?

Kwa maoni yangu kuna haja ya kufanya research juu ya huyu Mungu wa uchina awasaidiae ili kama vip nasi tu-adapt/tuige. Maana si kwa kufanikiwa huko.

Sijataka kuzama sana kwa undani kuhusu uchina kuepuka kuwachosha wasomaji na wachangiaji. Ila kimsingi wachina wanavitu ni hatari.

Karibuni wanajamvi tujadili kwa ajili ya kubadili mind set na kupanuana kifikra.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na mipango mizuri, kushika sheria, kufanya tafiti, kutumia akili na kufanya kazi kwa bidii na maarifa ni UMUNGU. Yeyote afanyaye hayo ataendelea kwa maana anatimiza mambo ya Mungu hata kama hajui hivyo.
 
Top Bottom