Haki za wanyama zinasemaje??

Leornado

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,529
196
kiumbe huyu kakosa nini?
164324_193047410709458_100000126027936_806035_4181596_n.jpg
 
Huyo sio mnyama. Ni ndege.
Viumbe hai vimegawanyika katika makundi makuu matatu. Ukiendelea kunyumbua utakuta kuku ni mnyama lakini katika kundi la ndege (kingdom animalia)....... au sio? biology std six umesahau?.
 
hata panzi ana nyama ila sio mnyama.
Atakachotendewa baada ya hapo naona ni kikubwa zaidi ya hicho.
Ah! Hivyo eh! Mi nilikuwa sijui kuwa hata panzi ana nyama pia...!

Kwa hiyo ivyo alivyotendewa huyo kuku ni sawa sio?
 
Tangu lini kukawa na haki za wanyama bongo??Hayo ndio maisha halisi ya hao viumbe!!!
 
Huyu muhusika akikamatwa anaweza kushtakiwa kwa kukiuka sheria ya ustawi wa wanyama, na adhabu yake ni faini ya kuanzia Tsh 20,000 - 100,000 hapo kwa papo au kwenda kutumikia kifungo cha mwezi mmoja Jela.
 
Huyo sio mnyama. Ni ndege.

Husninyo mamii umesoma biology kweli? OK hata kama si mnyama we unaona ni sawa huyu kuku alivyofungwa hivyo?

Lizzu,I guess haki za wanyama zipo hata hapa Bongo tatizo ni kwamba watu wengi hatujui haki zetu ndio iwe za wanyama?
 
kuchinja na kumla mnyama ni halali, lakini kumtesa ni unethical, si halali kabisa, kunapoza upendo wako na wa wanaoshuhudia. kunadhihirisha usivyo na huruma, yaani kunaonyesha ulivyo katili. kama utafanya mbele ya watoto waweza kukuogopa na kukuchukia maisha yao yote na hata wao wenyewe waweza kuwa watu katili sana ukubwani. its a complicated psychological disorder
 
Viumbe hai vimegawanyika katika makundi makuu matatu. Ukiendelea kunyumbua utakuta kuku ni mnyama lakini katika kundi la ndege (kingdom animalia)....... au sio? biology std six umesahau?.

nafikiri wewe ndio umesahau ila sitaki kubishana sana. Kama akipita mwana biology hapa atatuondolea huu utata.
 
Husninyo mamii umesoma biology kweli? OK hata kama si mnyama we unaona ni sawa huyu kuku alivyofungwa hivyo?

Lizzu,I guess haki za wanyama zipo hata hapa Bongo tatizo ni kwamba watu wengi hatujui haki zetu ndio iwe za wanyama?

hata mimi sipendi alivyofanyiwa hivyo.
Nyama yake yenyewe naipenda ikiwa ishaiva.
Huwa siwezi kuangalia akichinjwa pia. Nina kahuruma.
 
nafikiri wewe ndio umesahau ila sitaki kubishana sana. Kama akipita mwana biology hapa atatuondolea huu utata.

Husninyo,
ukiangalia kibiologia huyu kuku,ng'ombe, mbwa, panya,binaadamu, mijusi,chura, samaki, ngisi, panzi, mbu nk wote wako kwenye kundi moja na hilo kundi linaitwa Animalia.Tumewekwa kwenye kundi moja kwa sababu kuna sifa tunazo share...refer animal classification kupata mwanga kwenye hilo.
nadhani Leonardo ametumia kigezo hicho kumuita kuku mnyama.
 
Back
Top Bottom