- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na taarifa mdau mmoja amechapisha picha ya mtu akiwa amempigia magoti aliyekuwa Rais wa Zambia , Edgar Lungu kuwa alikuwa ni hakainde Hichelema.
- Tunachokijua
- Edgar Lungu alikuwa Rais wa 6 wa Zambia kati ya mwaka 2015 hadi 2021 na baadaye akafuatiwa na Rais Hakainde Hichilema mwaka 2025. Lungu amefariki Juni 5, 2025.
Madai
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X alichapisha taarifa iliyoambatana na picha inayomuonesha Rais wa awamu ya 6 wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amepigiwa magoti na Rais wa awamu ya saba Hakainde Hichelema wakati huo akiwa bado siyo Rais. Miongoni mwa maneno yaliyoambatana na picha hiyo ni;
“Aliyepiga Magoti ni Hakainde Hechilema, alikuwa kiongozi mkuu wa Upinzani nchini Zambia, mwaka 2017 alishitakiwa kwa Makosa ya Uhaini akakaa gerezani kwa miezi minne, Mwaka 2021 akashinda kiti cha Urais dhidi ya Edgar Lungu, aliyekaa kwenye kiti.”
Uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo inapotosha kwani anayeonekana pichani akiwa amempigia magoti Rais wa wakati huo wa Zambia Edgar Lungu si Hakainde Hichilema ambaye ni Rais wa sasa wa Zambia bali ni Micheal Katambo aliyekuwa waziri wa uvuvi na ufugaji.
Kwa kutumia Google reverse image search JamiiCheck imebaini kuwa picha hiyo ilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook na X (Twitter) Machi 21, 2017. Tovuti ya Lusaka Times ilichapisha taarifa yenye kichwa chenye tafsiri ya “Picha ya Waziri Katambo akiwa amepiga magoti imesambaa mitandaoni” taarifa hiyo iliambatana na picha husika Machi 21, 2017.
Tovuti hiyo inabainisha kuwa aliyepiga magoti pichani ni Waziri wa uvuvi na ufugaji wa wakati huo Michael Katambo mbele ya Rais Lungu walipokuwa ndani ya ofisi ya Paroko wa parokia ya Mary Immaculate Lusaka baada ya ibada Jumapili iliyopita (Machi 19, 2017).
Micheal Katambo amekuwa mbunge wa jimbo la Msaiti nchini Zambia kuanzia mwaka 2011 na baadaye kuteuliwa kuwa waziri wa ufugaji na uvuji mwaka 2016 hadi 2018 na kisha wizara ya kilimo hadi mwaka 2021