Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Maswali yako yananitia kizungu zungu ujuee.....

Kwanini mama?

Nahitaji kitu ambacho unacho na unataka kuninyima tena maksudi kabisa
Huo ni ubinadamu kweli?
 
you are just sharing with us a story. mwanaume hawezi kuhitaji msaada kwenye issue direct kama hii.jambo ambalo halihitaji hata ushauri, hata mtoto mdogo angejua chakufanya ili kuepuka matatizo mbeleni. tafakari halafu jiulize mtakuwa wangapi?
 
Kwanza ninakawaida ya kuwapenda watoto sana bila kujali kama ni wa jinsia gani,kwangu nawakubali wote sana na wamekuwa marafiki wangu wa ukweli sana kwakuwa hawajui kupenda kwa masharti na wakikupenda wanakupenda ki-ukweli hasa

Sasa uswahilini kwetu kuna katoto kamoja ka miaka mi-4 hivi,jinsia yake ni ya kike huwa napenda sana siku nikiwa nyumbani au nikiwahi kurudi huwa nakaa nako na kupiga story nako sana na hunifanya mastress yangu ya kutafuta hela kuisha kama sio kupungua

Katoto haka kananipenda sana nami nakapenda sana kwani ni karafiki kangu sana,tatizo linakuja kwa mama yake,anadai kuwa inafika wakati wa usiku kanalia kaletwe kwangu nae anadai anakuwa hataki

Lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba huyo mama yake anadai eti napendeza sana kuwa baba yake huyo mtoto na anadai kwakuwa mtoto wake ananipenda nae ananipenda na ameanzisha visa wakati mwingine hukaleta hako ka rafiki kangu usiku wa saa 4 hadi 5 usiku akidai eti kanalia akalete nami huwa nakapokea na kukaa nako hadi kanapolala kisha nampa mama yake na kisha kuondoka

Mama wa haka karafiki kangu alikuwa ameolewa lakini ameachika kwa mumewe kwa sababu yule jamaa hakuwa ametulia

Sasa hizi vurugu zimekuwa zinazidi sana hadi naanza kukereka kwasababu sina mpango kabisa na huyo dada kwani ana mahusiano na jamaa mmoja hapa mtaani na nafahamiana nae sana

Naanza kuwaza kukakatia line kale ka rafiki kangu lakini roho inaniuma sana

Nimejaribu kumwambia aache tabia hiyo lakini naona kama nampigia mbuzi gitaa

Sijaamua kuchukua maamuzi yoyote hadi sasa lakini naona kama huyu dada ananiharibia urafiki wangu na huyu mtoto na hili sio halali na halikubaliki kabisaaa

Yaani hapa nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake


Enyi akina dada hebu mtuache na hawa marafiki zetu na msituvurugie urafiki wetu bana!
...sicko!
 
Back
Top Bottom