SoC02 Haja ya kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia na kujifunzia katika nyanja zote za elimu nchini Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition
Jul 29, 2022
16
15
Wenu Mtambo Mtoka mbali

utangulizi.

Makala haya imeandikwa kwa kuzingatia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanazuoni,tume ya makweta (1982),taasisi ya haki elimu (2008),tamko la waziri mkuchika (2010), na mjadala unaoendelea saizi nchini kwetu juu ya lugha ya kufundishia na kujifunzia mashuleni na vyuoni.

Lugha kama chombo na nyenzo muhimu katika mchakato wa utoaji elimu {kufundishia na kujifunzia}. Mapema baada ya Tanganyika(sasa Tanzania) kujipatia uhuru wake toka mikononi mwa mkoloni (uingereza). Kiswahili kilirasimishwa kama lugha ya mawasiliano nchini Tanzania na lugha ya taifa . Bila kusahau mchango wake kipindi cha kupigania uhuru wa nchi yetu.

Kiswahili imekuwa lugha ya kwanza kwa wazawa wengi wa mjini hasa katika karne ya ishirini na moja, vile vile Kiswahili ni lugha ya pili kwa wazawa wengi wa vijijini (hasa wale waliopata elimu ya shule za msingi na wengineo.

Ingawaje, imekuwa ni ngumu kujua rasmi,lugha ya Kiswahili inawazungumzaji wangapi,kwasababu kwenye sense zote zilizofanyika nchini Tanzania tangia mwaka 2002,2012 na ingawa sensa ya 2022 imejaribu kuulizaz maswali kuhusu lugha ambazo0 mtanzania anaweza kuzungumza(kiswahili au kiingereza au zote). Hata hivyo, kutojua idadi kamili ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili,haiwezi kufuta ukweli kuwa Kiswahili kinazungumzwa na kueleweka na wakazi wengi nchini Tanzania.

Lakini,hii haibadilishi umuhimu wa lugha za kigeni katika elimu,bali kutaka kufanya elimu yetu iwe na tija kwa mwanafunzi,jamii na taifa kwa ujumla

HADHI YA KISWAHILI NA KIINGEREZA KATIKA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA NCHINI TANZANIA(SASA).

Baada ya uhuru, Kiswahili kilifanywa kuwa lugha muhimu ya mawasiliano na lugha ya taifa nchini Tanzania .kiswahili kimeendelea kutumika katika shughuli mbalimbali za shule za msingi,serikali,bungeni, kuendeshea mijadala ya kesi mahakamani,na kufanyia kampeni za kisiasa . ilhali, kiingereza imebakia kuwa lugha mahususi katika elimu ya sekondaqri hadi elimu ya juu, ambapo masomo yote yakifundishwa kwa lugha ya kiingereza isipokuwa kwa somo la Kiswahili tu.

Vilevile shule nyingi zimeenda mbali zaidi kwa kutoa adhabu kwa wanafunzi wanaoshindwa kuzungumza kiingereza,pia wengine wamekuwa wakikosa msaada au huduma wanayo ihitaji toka kwa walimu wao au wahudumu wa hapo shuleni.

Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanazuoni,taasisi na wizara husika zimebainisha wazi madhara ya kuendelea kutumia lugha za kigeni katika kufundishia na kujifunzia katika Nyanja zote za elimu kwa mfano (wanazuoni kama Quoro (2003),tume ya makweta (1982-1983),taasisi ya haki elimu (2008) n.k

Tafiti zote zimeainisha majibu yasiyopisha na kwa ukubwa ,kuwa matumizi ya kiingereza katika kujifunzia na kufundishia katika elimu ya nchini Tanzania kuna leta madhara makubwa katika elimu. Vile vile maarifa, na stadi lengwa zinashindwa kufikiwa na wanafunzi walimu, pamoja na taifa kiujumla.

KWANINI LUGHA YA KISWAHILI IWEZESHWE KUTUMIKA KATIKA NYANJA ZOTE ZA ELIMU?.

Mosi,lugha ya kiswahili inaeleweka vizuri na wanafunzi wengi sambamba na walimu. Kutokana na hoja hii,kiswahili kinaweza rahisisha mchakato wa kujifunza na kufundisha mashuleni na vyuoni. Kwa mujibu wa Rubanza (1979) na Mekacha (1977) wanaonesha kwamba watoto wengi wa mjini na vijini wenye uelewa wa lugha ya kiswahili (kama lugha ya kwanza na pili) umeongezeka.

Hivyo basi kuna haja ya msingi kabisa kwa serikali kuruhusu na kurasimisha matumizi ya lugha ya kiswahili katika kufundishia katika nyanja zote za elimu( elimu ya awali hadi elimu ya juu). Hii itawawezesha wanafunzi kuelewa vyema kile wanachofundishwa, yote kwasababu mwalimu atafundishwa kwa udadavuji mada husika na kwa mifano dhahiri.

Pili,Walimu wengi kutotumia lugha ya kiswahili kufundishia masomo yote,huchochea kutokueleweka vyema darasani, kwa mujibu wa Mwinsheikhe (2003). Hii inatokana na walimu wengi kukosa umahiri na ujuzi wa kutosha katika kutumia kiingereza . swali dogo linakuja,unawezaje kutumia walimu wasio mahiri katika lugha husika kufundishia masomo ya lugha husika? Je, wanafunzi watapata maarifa na ujuzi uliokusudiwa?. Jibu ni fupi tu,hapo hakutakuwa na ufundishaji kusudiwa. Ikumbukwe ya kuwa,walimu wengi wanaotumia lugha ya kiingereza tu kufundishia darasani,wengi wao huwa hawaeleweki vyema.

Pia, walimu wanaochanganya lugha mbili (kiswahili na kiingereza) katika kufundishia huwa wanaeleweka kiasi,ingawaje wanakuwa wanakinzana na Sera ya elimu ya nchi yetu katika lugha ya kufundishia katika shule za sekondari na elimu ya juu. Kipindi nikiwa kwenye mafunzo kwa vitendo mwaka 2020,katika shule fulani jijini Mbeya,wanafunzi walidiriki kuniomba kufundisha kwa kuchanganya lugha ya kiswahili na kiingereza (kiswanglish) ili somo lieleweke. Nami nilifanya hivyo,na nilieleweka vyema kabisa,hivyo kiswahili kinahitajika sana katika kuhakikisha mwalimu anaeleweka darasani na katika shughuli nyinginezo za elimu.

Tatu,Lugha ya Kiswahili ni nyenzo na chombo sahihi kulifikisha taifa katika maendeleo ya sayansi na teknolojia. Kwa mujibu wa Quoro (2003),anasisitiza kuwa lugha ya kwanza ni chombo muhimu kumwezesha muhusika kung'amua(kudadisi) na kueleza mtazamo na hisia za ndani kuhusu maarifa. Hivyo kupitia uwezo huo wa kung'amua / kudadisi hapo ndipo ugunduzi na ubunifu mbalimbali huanzia.

Hivyo, kiswahili kinaweza kuwafanya wanafunzi kugundua na kubuni vitu na mambo mbalimbali. Ikumbukwe kuwa hamna nchi iliyoendelea sana kiteknolojia bila ya mchango wa lugha inayoeleweka. Lugha ya kiingereza imechangia sana kuzalisha wanafunzi wanao kariri tu kile wanachofundishwa ili wafaulu mitihani yao,bila kuwa na maarifa yoyote ya msingi katika ugunduzi na uvumbuzi. Hivyo kiswahili kinaweza kuwa mwarobaini wa hili tatizo.

Nne,kuanza kutuimiwa kwa lugha ya Kiswahili katika Nyanja zote za elimu,kutasaidia kukomboa fikra na tamaduni za jamii yetu. Kutokana na kuendelea kutumia lugha ya kiingereza katika elimu ya sekondari na chuo kikuu , kumechochea wanafunzi wengi kudharau lugha ya Kiswahili na tamaduni zetu njema,pia, kumeendeleza utumwa wa kifikra kwa wananchi, wasomi wengi(wasomi kasuku),na wanasiasa.

Kitendo hiki kimefanya mtu ajione ni msomi kwa kuzungumza “kiswanglish”. Wananchi wengi wamejikuta kwenye ukoloni mamboleo kwa kulinganisha uwezo wa kiakili na uwezo wa kuzungumza kiingereza,jambo ambalo ni la hovyo kabisa. Izingatiwe ya kuwa ukombozi wa fikra ndio nyenzo sahihi kufikia mageuzi mbalimbali katika jamii yetu.

Hitimisho, ningependa kutoa rai kwa serikali na wizara ya elimu na sayansi na teknolojia kuzingatia majibu ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu mbalimbali juu ya lugha ya kufundishia katika Nyanja ya elimu. Lakini pia , ikumbuke kuwa mabadiliko yoyote yana gharama yake,lakini gharama ya kuendelea kutumia kiingereza katika kufundishia na kujifunzia katika elimu ya sekondari hadi elimu ya juu ni gharama kubwa zaidi kwa taifa.

" Elimu yetu,maendeleo yetu"
 
Back
Top Bottom