MWANAKIJIJI asante sana kwa mada yako chokozi, ina mameno mazito yenye busara. Kwangu mimi nakubaliana nawe kuwa baada ya kujiuzuru UWAZIRI, aende zake kwa kuachia UBUNGE na vyeo lukuki alivyo navyo kwenye CCM, na akienda kwa wapiga kura wake Bariadi wakampe wakati mgumu ajue Tanzania ya leo si ya mwaka 1960. Ninatamani sana kumuhimiza mgosi MAKAMBA kusoma hiyo mada ili aweze kukishauri chama chake kichukue hatua madhubuti kujisafisha mbele ya Watanzania na hatimaye kiondokane na ufisadi.
Asante OGAH kwa uchambuzi wako kuhusu huyu CHENGE kukejeli WASUKUMA inasikitisha sana. Licha ya kwamba Kiswahili kimeanzia na kinaongewa sana Pwani, si kweli kwamba Wasukuma hawajui gramar ya Kiswahili kiasi hicho ati waanze kubwabwaja VIJISETI badala ya senti, VIJITOTO badala ya watoto, VIJIMAMBO badala ya mambo. Huyu mtu alipoongea VIJISENTI alikuwa anajua anaongea nini kwani alipoulizwa kwa nini bilioni anaiita VIJISENTI alijibu na kusema KILA MTU ANA VIWANGO VYAKE. Siju kama ni kweli alikuwa amesha-panick tayari au ni ile jeuri ya pesa / ubilionare ndiyo ilimpa nguvu ya kutamka hayo. Ninavyowafahamu Wasukuma ni kuwa wakiongea kitu kwa msisitizo wanatanguliza MA na hivyo angesema MASENTI tungemuelewa. Nawasilisha