Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Ni kweli yawezekana kuwa kujiuzulu Uwaziri kumepokelewa kwa furaha na wengi (mimi mmoja wao). Yawezekana kwa kufanya hivyo uchunguzi utakuwa huru (sidhani alikuwa anazuia uchunguzi anyway); yawezekana kujiuzulu kwake kumekuwa ni kitulizo cha kelele dhidi ya ufisadi; Yawezekana kujiuzulu kwake kumeonesha ufisadi wa viongozi wa serikali ya JK na hivyo kumuondoa kumeonesha jitihada za kusafisha serikali hiyo;
Hata hivyo, hadi hivi sasa CCM haijalipa gharama yoyote ya viongozi wake kuhusishwa na ufisadi na hakuna wakati hadi hivi sasa ambao wao kama CCM wamechukua hatua za viongozi wa serikali waliofanya vitendo vya ufisadi wakiwa ni wanachama wake.
Ni kwa sababu hiyo basi naamini kujiuzulu kwa Chenge toka serikalini hakutoshi bali lazima kufuatiwe na kujiuzulu toka Ubunge. Kwanini?
a. Kiasi cha fedha anachodaiwa kukutwa nacho kingeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wa Jimbo lake lakini aliwaficha wapiga kura wake.
b. Kwa kukiita kiasi hicho "vijisenti" kwa kisingizio cha "usukuma wake" ni tusi kwa wasukuma wengine ambao hawajui maana ya "vijisenti" hasa baada ya yeye mwenyewe kuelezea kuwa "kila mtu ana kiwango chake".
c. Mwakilishi wa wananchi anapotajwa na kuhusishwa na kitendo cha matumizi mabaya ya nafasi yake, nafasi ambayo imetokana na kuchaguliwa na wananchi hao, basi anapojiuzulu nafasi yake basi hana budi kuachia kiti chake ili ampishe mtu mwingine kushika nafasi hiyo.
Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey. Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.
JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!