I beg to differ,
a. Chenge alipochaguliwa kuwa Mbunge hakuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Bariadi. Alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano - Hivyo kila raia wa Jamhuri hiyo ana haki ya kusema lolote juu ya uongozi wa Chenge na Ubunge wake.
Tatizo sio Chenge amechaguliwa katika bunge gani, tatizo kachaguliwa na nani? Constituency yake ni wapi? Kama Mbunge wa BAriadi anawajibika kwa watu wa Bariadi, kama Mbunge wa CCM anawajibika kwa CCM.Kwa hiyo kama kuna watu wa kuhimizwa wamuwajibishe Chenge ni watu wa bariadi na CCM.Sasa hivi kama mbunge wa Bariadi Chenge hawajibiki kwa mpiga kura siye wa Bariadi.Kama una beef naye unataka ajiuzulu ubunge ongea na watu wa Bariadi au shinikiza vikao husika vya CCM vimvue uanachama au kumshurutisha ajiuzulu vyeo vya kichama.Vinginevyo ukimwambia Chenge ajiuzulu ubunge wa Bariadi, akikuuliza ulinichagua wewe utamjibuje? Akikwambia una mandate ya chama nilichosimamia utamjibuje?
Sasa whats next? Akishajiuzulu ubunge tumwambie ajivue u board member Barricks Gold (mfano tu)wakati sisi sio hata shareholders wa Barrick Gold? Waache shareholder (CCM na watu wa Bariadi) waamue. Sisi tunaweza kuweka pressure kwenye corruption charges tu.Naona sasa tutataka mpaka kwa mkewe nako ajiuzulu kwa mtaji huu.Give CCM a chance to show how they stand, talk to them, not Chenge.
b. Chenge anapoingia Bungeni hasubiri hadi hoja zinazohusu Bariadi Magharibi ndio atoe maoni, na anapokaa kutunga sheria hatungi sheria zinazohusu Bariadi Magharibi na kukaa pembeni zinapokuja sheria za Bariadi Mashariki. Sheria anazoshiriki kutunga ni za Jamhuri nzima - hivyo kila raia wa Jamhuri hiyo bado ana haki ya kutolea maoni uongozi na ubunge wake na kutotaka kuwa na mtunga sheria kama yeye..
Kila raia ana haki ya kutoa maoni kuhusu kila kitu.Hiyo haimaanishi maoni hayo yana msingi.Kumwambia mtu ajiuzulu ni zaidi ya maoni, ni protest, ni lobbying.Unapomwambia mtu ajiuzulu -which is becoming a myopic trend here nowadays- you better be ready with facts and not only maoni.Kama wewe ukisema unataka Chenge ajiuzulu na wapiga kura wa Bariadi wakisema wanamtaka mbunge wao je, wewe utaonaje? Wewe utaonaje kama mbunge wako unayempenda (Mfano Slaa au Zitto) watu wa Bariadi wanakuja kumpigia kelele ajiuzulu, utaona hiyo fair?
c. Chenge ameongoza Idara ya Mwanasheria Mkuu kwa karibu miaka kumi na katika miaka hiyo ufisadi wa mikataba ulifikia kilele; ni kutokana na kujulikana kwake katika nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu (akiwa pia Mbunge ex officio) Chenge akaamua kwenda kugombea Ubunge na akaupata na kurudi Bungeni kama Mbunge wa Kuchaguliwa. Ni kutokana na kuchaguliwa kwake akaingizwa katika serikali kama Waziri. Maamuzi yake katika Uwaziri hayakuwaathiri watu wa Bariadi tu, na hakuna ushahidi kuwa fedha alizoficha Jersey na kwingineko ni za WanaBariadi tu. YOte yanalihusu Taifa.
Umesema vizuri, maamuzi yake kama Waziri hayakuwaathiri watu wa Bariadi tu, bali yaliathiri taifa zima.Ndiyo maana sikusema kitu kumtetea, to the contrary nili-champion call ya Chenge kujiuzulu uWaziri kwa sababu hapo nilikuwa katika constituency yake kama Mtanzania na yeye kama Waziri wa cabinet ya Tanzania, lakini hili la bariadi mimi kama sio mpiga kura wa Bariadi, na kama sio mwanachama wa CCM simo katika constituency yake na sina haki ya kumpigia kura ajiuzulu.
Ndiyo maana yule mpuuzi Alberto Gonzalez alikaa Justice Department miezi kibao overdue aki parrot "I serve at the pleasure of the president" kwa sababu alikuwa ni presidential appointee, who appoints/elects has the last say.Sasa Chenge akikwambia "I serve at the pleasure of the Bariadi people, who are behind me" utamwambia nini? Ndiyo maana nasema kama kuna mtu wa kumshawishi amtake Chenge ajiuzulu ubunge ni wanachi wa Bariadi na watu wa CCM.
NI kwa sababu hiyo basi, kama kweli amepima uzito wa tuhuma zinazomkabili na madai ambayo yameelekezwa kwake, ni wazi kuwa hatendei haki Jamhuri na Bunge letu kwa kuendelea kushika nafasi ya Ubunge na kama kweli yeye ni mwajibikaji basi wakati umefika wa yeye kuachia pia kiti cha Ubunge ili CCM iweze kumsimamisha mtu mwingine.
Kama bado unaamini kuna kupima kokote kwa aina hiyo kunakoendelea you are mistaken.The only thing Chenge anachopima ni "what can I get away with" na katika hili he can get away with being an MP if neither CCM nor the Bariadi people demands his resignation.Ndiyo maana nakwambia lobby with them, not Chenge.
Vinginevyo endapo utakuja mjadala Bungeni ambao utakuwa unamgusa kimaslahi na akaamua kushikilia shilingi au kutumia nafasi yake ya parliamentary immunity kusema na kuzua mambo mengine ambayo asingeweza kuyafanya nje ya Bunge basi ni wazi ni hatari kwa demokrasia nzima ya Bunge.
Indeed,
Lakini demokrasia hiyo hiyo ndiyo iliyowapa haki wananchi wa Bariadi kumchagua na wewe kumchagua mbunge wako.Kwa hiyo si vizuri wewe ambaye hukumchagua mbunge wa Bariadi huna mamlaka, humna moral argument, hauko katika constituency yake.Ongea na mabosi wake, watu wa BAriadi na CCM, na siyo kumtaka Chenge ajiuzulu, atakucheka tu na kukuambia unasumbuliwa na mvua na kukufanya the object of his arrogant ridicule.
Chenge ni lazima ajiuzulu pia Ubunge ili kuondoa kuonekana kwa aina yoyote kuwa suala dhidi yake ni dogo na linahusu Uwaziri tu. Kimsingi linamhusu yeye kama kiongozi wa Kitaifa.
Utaongea hivyo kama nani wakati huko katika constituency yake? Wakikwambia wanampenda BAriadi utasemaje?
CHENGE JIUZULU UBUNGE, UMELILETEA AIBU TAIFA!
Tafuta mwingine wa kumshtakia Chenge (CCM, bariadi voters) lakini si kumtaka Chenge mwenyewe ajiuzulu