Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
........
Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey. Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.
JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!
Kama kawaida yao, baada ya kujiuzulu atakwenda jimboni mwake kujitetea jinsi 'alivyoonewa' na baada ya hapo atatumia 'vijisenti' vyake kujisafisha kupitia vyombo vy habari vya Bongo.
Ni kweli yawezekana kuwa kujiuzulu Uwaziri kumepokelewa kwa furaha na wengi (mimi mmoja wao). Yawezekana kwa kufanya hivyo uchunguzi utakuwa huru (sidhani alikuwa anazuia uchunguzi anyway); yawezekana kujiuzulu kwake kumekuwa ni kitulizo cha kelele dhidi ya ufisadi; Yawezekana kujiuzulu kwake kumeonesha ufisadi wa viongozi wa serikali ya JK na hivyo kumuondoa kumeonesha jitihada za kusafisha serikali hiyo;
Hata hivyo, hadi hivi sasa CCM haijalipa gharama yoyote ya viongozi wake kuhusishwa na ufisadi na hakuna wakati hadi hivi sasa ambao wao kama CCM wamechukua hatua za viongozi wa serikali waliofanya vitendo vya ufisadi wakiwa ni wanachama wake.
Ni kwa sababu hiyo basi naamini kujiuzulu kwa Chenge toka serikalini hakutoshi bali lazima kufuatiwe na kujiuzulu toka Ubunge. Kwanini?
a. Kiasi cha fedha anachodaiwa kukutwa nacho kingeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wa Jimbo lake lakini aliwaficha wapiga kura wake.
b. Kwa kukiita kiasi hicho "vijisenti" kwa kisingizio cha "usukuma wake" ni tusi kwa wasukuma wengine ambao hawajui maana ya "vijisenti" hasa baada ya yeye mwenyewe kuelezea kuwa "kila mtu ana kiwango chake".
c. Mwakilishi wa wananchi anapotajwa na kuhusishwa na kitendo cha matumizi mabaya ya nafasi yake, nafasi ambayo imetokana na kuchaguliwa na wananchi hao, basi anapojiuzulu nafasi yake basi hana budi kuachia kiti chake ili ampishe mtu mwingine kushika nafasi hiyo.
Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey. Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.
JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!
Nyani, kumbe "vijisenti" ndiyo msemo wa bangosha.. imekuwa ni chengumanule wa chenge!
No way!Ni tofauti!Kwanza mdingi wako anapo mention "vijisenti" sidhani kama alikuwa akiulizwa kuhusu tuhuma za wizi!Unless u clarify hilo then tutakuwa on the same page!Mimi sishangai kabisa kwa yeye kutumia hilo neno la "vijisenti". Mdingi wangu mwenyewe huwaga anatumia hilo neno akimaanisha hela irregardless of the amount. So I'm willing to give him a pass on it....
Tanzania inahitaji "MAPINDUZI" na sio tumabadilko twa danganya toto!We need "Total revamp"
No way!Ni tofauti!Kwanza mdingi wako anapo mention "vijisenti" sidhani kama alikuwa akiulizwa kuhusu tuhuma za wizi!Unless u clarify hilo then tutakuwa on the same page!
Nyani umesema ujashangazwa na usemi wa vijisenti kwasababu dingi yako huwa anatumia the same word regardless of the amount of money!Na mimi nikasema issue ya Chenge na dingi yako kutumia usemi mmoja ni issue ambazo haziwezi kulinganishwa kwasababu Chenge yeye alikuwa akiulizwa swali la msingi kuhusu tuhuma za wizi wa vijisenti hivyo..where as hatujui bado kama dingi yako naye alipolitumia neno hilo la vijisenti alikuwa akijibu tuhuma za wizi ama ilikuwa kwenye maongezi mengine ya kawaida!Pls be specific.Umeshindwa kabisa kunielewa nilikuwa nasema nini...
Transition only if Mh rais akijitoa muhanga na kulishughulikia hili suala la ufisadi kishujaa!Akiyumba tu then..tunaweza kusema mengi!Ninahisi tuko kwenye transition, mapinduzi yako njiani