Haitoshi! - Chenge jiuzulu na Ubunge!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Ni kweli yawezekana kuwa kujiuzulu Uwaziri kumepokelewa kwa furaha na wengi (mimi mmoja wao). Yawezekana kwa kufanya hivyo uchunguzi utakuwa huru (sidhani alikuwa anazuia uchunguzi anyway); yawezekana kujiuzulu kwake kumekuwa ni kitulizo cha kelele dhidi ya ufisadi; Yawezekana kujiuzulu kwake kumeonesha ufisadi wa viongozi wa serikali ya JK na hivyo kumuondoa kumeonesha jitihada za kusafisha serikali hiyo;

Hata hivyo, hadi hivi sasa CCM haijalipa gharama yoyote ya viongozi wake kuhusishwa na ufisadi na hakuna wakati hadi hivi sasa ambao wao kama CCM wamechukua hatua za viongozi wa serikali waliofanya vitendo vya ufisadi wakiwa ni wanachama wake.

Ni kwa sababu hiyo basi naamini kujiuzulu kwa Chenge toka serikalini hakutoshi bali lazima kufuatiwe na kujiuzulu toka Ubunge. Kwanini?

a. Kiasi cha fedha anachodaiwa kukutwa nacho kingeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wa Jimbo lake lakini aliwaficha wapiga kura wake.
b. Kwa kukiita kiasi hicho "vijisenti" kwa kisingizio cha "usukuma wake" ni tusi kwa wasukuma wengine ambao hawajui maana ya "vijisenti" hasa baada ya yeye mwenyewe kuelezea kuwa "kila mtu ana kiwango chake".
c. Mwakilishi wa wananchi anapotajwa na kuhusishwa na kitendo cha matumizi mabaya ya nafasi yake, nafasi ambayo imetokana na kuchaguliwa na wananchi hao, basi anapojiuzulu nafasi yake basi hana budi kuachia kiti chake ili ampishe mtu mwingine kushika nafasi hiyo.

Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey. Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.

JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!
 
Mkjj, hawa mawaziri wanafanya unafiki mkubwa wa kujiuzulu uwaziri wakati wakiendelea kuwa wabunge wanaolipwa mishahara na marupurupu manono. Kwa kusema hivyo basi tuanze kuwashinikiza akina Lowassa, Msabaha, Karamagi na huyu Chenge ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine na mikataba ya kifisadi kwamba haitoshi tu kujiuzulu uwaziri bali pia tunataka wajiuzulu ubunge na ujumbe wa halmashauri kuu kama wana wadhifa huo pia.
 
Kama kawaida yao, baada ya kujiuzulu atakwenda jimboni mwake kujitetea jinsi 'alivyoonewa' na baada ya hapo atatumia 'vijisenti' vyake kujisafisha kupitia vyombo vy habari vya Bongo.
 
Kwa Chenge lengo ni kuhakikisha anajiuzulu Ubunge au anavuliwa uanachama wa CCM. Wakifanya hivyo mapema watajipunguzia aibu iliyoko mbeleni, na niwaambie ni aibu. Wasisubiri hadi SFO waoneshe ushahidi ambao yeye mwenyewe anajua upo. Sasa atafanya vizuri kama aidha yeye mwenyewe atajiuzulu au Rais amuite na kumwambia ajiuzulu Ubunge kwani hiyo milioni moja ni kidogo. Yeye anajua na SFO wanajua. Haikuwa hela ya mshahara, na wao wakitaka hadi "mwisho" basi wajue wanajiandaa vibaya.
 
........

Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey. Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.

JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!

Kujizulu pekee haitoshi, bali sheria ichukue mkondo wake na hivyo VIJISENTI vyetu turudishiwe. Mbona yule aliyekuwa balozi wetu Italy, prof. ..., wamemburuza mahakamani kwa VIJISENTI hivyo???
Bwana Chenge na nduguzo tunataka vijisenti vyetu tukajengee japo zahanati
 
Kama kawaida yao, baada ya kujiuzulu atakwenda jimboni mwake kujitetea jinsi 'alivyoonewa' na baada ya hapo atatumia 'vijisenti' vyake kujisafisha kupitia vyombo vy habari vya Bongo.

"Vijisenti" vyote alivyotuchukulia na kuviweka kwenye accounts zake mbali mbali zikiwemo za mkewe na watoto wake zilizo ndani na nje ya nchi aturudishie ili vitusaidie Watanzania wote.
 
Hapana inatosha kujiuzulu uwaziri, duniani tuna mifano mingi falling from grace kwa viongozi ni ngazi ya uwaziri kuwa back bencher aghalabu kuona hili unless na sisi tanzania tunataka kuset new ethical standards!
 
Katika moja ya mambo ambayo JF inaweza kujivunia ni kwamba Serikali ya JK inajua wazi NGUVU ya JF na inafuata kwa njia moja au nyingine kile tunachopendekeza humu ndani ya Baraza.

Kuna mwanachama mmoja hapa kapendekeza kuwa tutumie pressure kuwang'oa Lowassa na wenzake kwenye Ubunge. Mie naungana naye kwa asilimia 500, these guys know JF FULL PRESSURE. Hivyo nawashauri wana JF wenzangu tutumie hii JF-FP kuhakikisha mafisadi hawa waachie ubunge wao ili watu waadilifu waweze kupata nafasi ya kuwatumikia wananchi wao. Inaweza kuwa ngumu kidogo kutokana na SISIEMU kuogopa kuachia hayo majimbo kwa sasa ukitilia maanani kuwa wananchi sasa wana Uchungu kutokana na UPUPU unaofanya na hicho chama. Lakini ninaamini tukiungana na tukatumia hii nguvu tuliyonayo hapa, wataona aibu wenyewe.
 
Hawa Wasukuma wanatutia aibu sisi wengine. Kaanza kubambwa Mahalu..sasa huyu Chenge...na sijui wangapi wengine ambao bado hawajabambwa? Halafu kwa nini kesi kama hizi (kwa mfano ya Mahalu) zinachukua muda mrefu namna hii? Huyu Chenge hizo akaunti zake za huko visiwani zingegandishwa mara moja wakati uchunguzi ukiendelea.
 
Ni kweli yawezekana kuwa kujiuzulu Uwaziri kumepokelewa kwa furaha na wengi (mimi mmoja wao). Yawezekana kwa kufanya hivyo uchunguzi utakuwa huru (sidhani alikuwa anazuia uchunguzi anyway); yawezekana kujiuzulu kwake kumekuwa ni kitulizo cha kelele dhidi ya ufisadi; Yawezekana kujiuzulu kwake kumeonesha ufisadi wa viongozi wa serikali ya JK na hivyo kumuondoa kumeonesha jitihada za kusafisha serikali hiyo;

Hata hivyo, hadi hivi sasa CCM haijalipa gharama yoyote ya viongozi wake kuhusishwa na ufisadi na hakuna wakati hadi hivi sasa ambao wao kama CCM wamechukua hatua za viongozi wa serikali waliofanya vitendo vya ufisadi wakiwa ni wanachama wake.

Ni kwa sababu hiyo basi naamini kujiuzulu kwa Chenge toka serikalini hakutoshi bali lazima kufuatiwe na kujiuzulu toka Ubunge. Kwanini?

a. Kiasi cha fedha anachodaiwa kukutwa nacho kingeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wa Jimbo lake lakini aliwaficha wapiga kura wake.
b. Kwa kukiita kiasi hicho "vijisenti" kwa kisingizio cha "usukuma wake" ni tusi kwa wasukuma wengine ambao hawajui maana ya "vijisenti" hasa baada ya yeye mwenyewe kuelezea kuwa "kila mtu ana kiwango chake".
c. Mwakilishi wa wananchi anapotajwa na kuhusishwa na kitendo cha matumizi mabaya ya nafasi yake, nafasi ambayo imetokana na kuchaguliwa na wananchi hao, basi anapojiuzulu nafasi yake basi hana budi kuachia kiti chake ili ampishe mtu mwingine kushika nafasi hiyo.

Bw. Chenge amewaangusha wapiga kura wake, na amekiletea aibu kubwa chama chake. Kati ya wote walioatajwa katika tuhuma za ufisadi ni yeye pekee ambaye tunajua angalau kiasi gani che fedha kimefichwa huko Jersey. Kwa sababu hiyo basi Chenge siyo tu ajiuzulu Uwaziri kama alivyofanya bali pia ajiuzulu Ubunge wake na Uwakilishi wake ili mwana CCM au mtu mwingine aweze kuwawakilisha wananchi wa Bariadi Magharibi.

JIUZULU UBUNGE BW. CHENGE, UMEKUWA AIBU YA TAIFA LETU!

ahh kamnda ukimkomalia mtu mpaka ujue mwisho wake.ulimkomalia EL na ndege yake inayopaa mpaka ukaiangusha,now umeamua kula sahani moja na WASUKUMA akina chenge.
 
yah ni kweli aachie na ubunge ili ashitakiwe kwa urahisi na kufikishwa mahakamani>>>JIZI LIKUBWA<<< sijui limefundishwa na nani wizi???!!!!!?? maana wasukuma hatuko hivyo bwana..aaaaahhhh....umetutia aibu wasukuma...ukimalizana na umaa wa watanzania una kesi ya kutujibu wasukuma kwa kututumia kujitetea upuuzi wako....CHENGE UKOME....
 
Nyani, kumbe "vijisenti" ndiyo msemo wa bangosha.. imekuwa ni chengumanule wa chenge!

Mimi sishangai kabisa kwa yeye kutumia hilo neno la "vijisenti". Mdingi wangu mwenyewe huwaga anatumia hilo neno akimaanisha hela irregardless of the amount. So I'm willing to give him a pass on it....
 
Ni jambo la kusikitisha na kuudhi, eti kufurahi kwa chenge kujiuzuru uwaziri wkt bado ni mbunge! Kama tumedhamiria kuondokana na uchafu na kujenga dhana mpya kuwa uongozi ni usafi na dhamana adimu ambayo gharama yake ni imani ya umma kwa uadilifu usio na hata chembe ya kusingiziwa tuhuma. Lowasa, chenge, karamagi, msabaha wavuliwe ubunge! Tumedhamiria kutoa fundisho kuwa, kamwe imani ya umma kwa viongozi haiwezi kuchezewa au kununuliwa kwa fedha! Hatuna imani nao tena! We r not cheap as they think(ccm),hata wakibaki na unec au ucc kwny chama chao, watajuana wao,but tanzania siyo ya ccm! ni ya watanzania! Lakin pia tutakuwa tumewafundisha waone umuhimu wa kuwa na mawaziri ambao si wabunge. Tukatae hila na ghiliba zao eti kuachia uwaziri inatosha BADO!
 
Tanzania inahitaji "MAPINDUZI" na sio tumabadilko twa danganya toto!We need "Total revamp"
 
Mimi sishangai kabisa kwa yeye kutumia hilo neno la "vijisenti". Mdingi wangu mwenyewe huwaga anatumia hilo neno akimaanisha hela irregardless of the amount. So I'm willing to give him a pass on it....
No way!Ni tofauti!Kwanza mdingi wako anapo mention "vijisenti" sidhani kama alikuwa akiulizwa kuhusu tuhuma za wizi!Unless u clarify hilo then tutakuwa on the same page!
 
No way!Ni tofauti!Kwanza mdingi wako anapo mention "vijisenti" sidhani kama alikuwa akiulizwa kuhusu tuhuma za wizi!Unless u clarify hilo then tutakuwa on the same page!

Umeshindwa kabisa kunielewa nilikuwa nasema nini...
 
Umeshindwa kabisa kunielewa nilikuwa nasema nini...
Nyani umesema ujashangazwa na usemi wa vijisenti kwasababu dingi yako huwa anatumia the same word regardless of the amount of money!Na mimi nikasema issue ya Chenge na dingi yako kutumia usemi mmoja ni issue ambazo haziwezi kulinganishwa kwasababu Chenge yeye alikuwa akiulizwa swali la msingi kuhusu tuhuma za wizi wa vijisenti hivyo..where as hatujui bado kama dingi yako naye alipolitumia neno hilo la vijisenti alikuwa akijibu tuhuma za wizi ama ilikuwa kwenye maongezi mengine ya kawaida!Pls be specific.
 
Ninahisi tuko kwenye transition, mapinduzi yako njiani
Transition only if Mh rais akijitoa muhanga na kulishughulikia hili suala la ufisadi kishujaa!Akiyumba tu then..tunaweza kusema mengi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom