Nakujibu moja baada ya jengine kama ulivouliza. Mwanamke kuwa na digirii ni faida, lakini sio haimalizi kila kitu katika kumkamilisha kama mwanamke. Awe na digirii yake lakini ajue digirii haikuumbwa, kaisomea tu imsaidie lakini yeye ni mwanamke, alinde utu wake wa kike. Asikubali digirii ikampora uhalisia wake wa kike..
Nimkupata kabisa, tuko sawa hapa.
Labda swali la nyongeza, huu 'utu wa kike' ni ukoje? Unapimwaje? Na unadhani unafanana dunia nzima?
Au utu wa kike wa Saudi Arabia ni sawa na utu wa kike wa Italia?
Hata kama mama hana digirii, anapaswa kujitahid wanawe wapate maendeleo makubwa ikiwemo hiyo digirii, lakini pia awalelee vyema watakapopata hiyo digirii isije ikawapoteza, maana wapo walopotezwa na digirii zao wenyewe. Ni kama kumnunulia mwanao gari halafu akaliendesha rafu likamuua. Gari ni faida lakini kifo ni hasara. Kwa hivo lazima umsaidie mwanao maendeleo yasimpotoshe..
Nimekubaliana na wewe kabisa hapa, sina swali
Wanawake wenye digirii waliofanikiwa katika maisha yao ni wale walotambua kuwa ndoa hainaga digirii, na kwamba digirii haitunzi mume.
Nafasi ya mwanamke katika jamii wala si ya kuuliza, ni kubwa. Lakini akiweka mbele kiburi na nyodo kuwa ati nina digirii sijui kitukitu gani hiyo nafasi mwenzangu nakwambia itamshinda. Sasa kama digirii unaitumia kuvunja nyumba yako, hapo ndo umeienzi nafasi ya mwanamke au umechemsha dada hebu sema mwenyewe. Na kama kwa digirii hiyo, hata unapokosea hujikubali kurekebika ati kisa digirii, sasa hiyo ni digirii au majanga? .
Hivi kutokubali kurekebishwa ni sababu ya digrii au ni tabia ya mtu?
Hamna wanawake wasio na digrii na bado wana kiburi na wabishi?
Au unamaanisha kuwa digrii inampa mwanamke nafasi ya kuonesha kiburi chake zaidi? Lakini wakati huo huo kiburi ni nini? Ni mambo gani mtu afanye yakubalike ni kiburi na mengine yakubalike ni kulinda nafasi yake kama mke?
Bibiye unapoishi na mwanaume elewa ana hisia, usipomjali lazima atapindukia kule anapopata wa kumjali. Basi kama la kumjali limekushinda, mshukuru yule aliyekusaidia kumjali, hili nalo linahitaji digirii?.
Halihitaji digrii kwa kweli, labda nisaidie kuchora mstari, niruhusu hadi wapi ili nionekane namjali na si mtumwa tena? Kuna mwanamke alikuwa anampa GoTi mmewe ili asiachike. Alionyesha kujali kwa hali ya juu, lakini was it worthy?
Watoto wa mumeo ni wanao, hili nalo unapinga? Kama ukipinga wanao mwenyewe watakuumbua maana watasema hawa ni kaka zao. Kama digirii yako haikusaidii kutambua hili, ni ya kazi gani hiyo digirii? Mwanamke tumia digirii yako kujenga jamii si kubomoa, likikushinda hili basi digirii zako ni bure..
Ha ha a ha, Da Sophy bana. Kukubali mtoto wa nje wa mme ni matokeo ya mambo mengi, makuzi yanachangia sana. Kama umetoka kwenye jamii ambayo mitala ipo, sio ish kukubali mtoto wa nje wa mme. Na hii wala haihusiani na digrii kabisa, hii inahusiana na hisia zaidi. Ukute nyie mnamwambia akubali watoto wa nje wa mumewe wakati yeye bado yuko kwenye maumivu makali, is it fair? Jivalishe viatu vyake uone.
Ujue ni rahisi sana kushea mume ukiwa nyumba ndogo, kwa nini? Sababu unajua fika nyumba kubwa ipo na umekubali ukiwa unajua hilo. Ila ni vigumu sana kuwa nyumba kubwa wakati kuna nyumba ndogo, ni dhahiri kabisa 'nchi' yako onakuwa imeingiliwa. Ni sawa na rais wa nchi asikie kuna mtu mwingine kajotangaza rais wa nchi hiyo hiyo. Kwa hapa, jaribu kumpa muda huyo mnayeshea naye. Ukweli ukiingia akili na kukubaliana na matokeo hamtagombana kiasi kikubwa, utabaki wivu wa kike wa kawaida tu.
Ni sawa na wewe usikie sasa hivi huyo bwana ana ingizo jipya na wamezaa, utajisikiaje?
Labda nikuulize, je ulipoamua kuwa na uyo bwana, ilikuwa sababu ya kumkomoa mkewe au mlipendana tu? Kama sababu ilikuwa kumkomoa mkewe, basi endelea kumfanyia huyo bi mkubwa kila aina ye sinema, sababu ndio lilikuwa lengo.
Ila kama sababu nimlipendana nyie kwa raha zenu, msaidie mwenzio maisha yake yawe marahisi. Labda hata hukujua kama mkewe ndiye huyo, angeweza kuwa mwanamke mwingine yeyote. Kwa hiyo kiuhalisia wewe na huyo nyumba kubwa hamna ugomvi, ila aliyewakosanisha ni huyo mwanamme. Na kama umeshamauumiza kwa kumchukua mumewe, sasa ya nini azidi kuumia kwa vitimbi? Hivi unadhani ukimuona chini ya futi 6 utafurahi? Unaweza furahi kwa muda ila mbeleni kuna muda wa kujuta, si unajua ujana nao una mengi. Mchunie tu, hata kama ana vitimbi, tayari wewe ushabeba kombe, unaweza kuta hata mengine anayafanya akiwa hajui.
(Nimetumia nafsi ya pili -wewe, simaanishi wewe kama wewe, ni ili tu ujumbe wangu ufike)