Haijawahi kutokea; asiye na mikono,miguu...kufunga ping za maisha

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
remote_image_1329301350.jpg
Nicholas Vujicic ‘Nick’ (wa kwanza kulia) wakati wa harusi yake na Kanae Miyahara.

remote_image_1329301347.jpg
Nick akiwa na mpenzi wake Kanae.

KIJANA Nicholas Vujicic ‘Nick’, hawezi kuisahau Februari 10, mwaka huu kwani ndiyo siku aliyofunga ndoa na msichana Kanae.
Siku ya ndoa yao, watu maalum walialikwa na baada ya hapo waalikwa walijichana kwa vinywaji na chakula baadaye maharusi hao wakaenda kufunga fungate Hawaii, Marekani.
Wazazi wa Nick, Dushka na mumewe Boris wenyeji wa Australia wanasema siku alipozaliwa mtoto wao huyo miaka 29 iliyopita walikata tamaa kama angeweza kuwa na maisha mazuri.
Hata hivyo, Mungu alimjaalia, akasoma na sasa ana shahada ya kwanza ya Mipango na Uhasibu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Griffith, Logan, Australia.
Anaweza kuandika kwenye kompyuta na anamudu kusugua meno yake kwa kutumia mdomo.
Jijini Logan, amefungua shirika lake lisilo la kiserikali la watu waishio bila mikono na miguu yeye akiwa afisa mtendaji mkuu (CEO) na ni mhubiri wa Neno la Mungu na amekwisha tembelea nchi zaidi ya 25 duniani. “Nimekuwa nikiwapa matumaini watu wenye ulemavu kwamba wanaweza kuishi maisha mazuri,” anasema Nick.
 
niliwahi kusikia habari za huyu bwana siku nyingi nikawa najiuliza hivi anaishije. Nashukuru Mungu amepata msichana anayempenda na kukubali kufunga naye ndoa. Mungu awajaaliye familia bora.
 
Huyu jamaa ni inspirational speaker na kwa kweli ananipa motisha juu ya yale ninayoona siwezi. Ila hiyo picha ya harusi hapo anaonekana kama msimamizi wa harusi na sio bwana harusi. Angalia bibi harusi kamkumbatia huyo bwana kushoto na sio Nick. Na huyo jamaa kakwida kiuno cha bi harusi kwa bashasha. Sina hakika sana kwa kweli.
 
Tambua kwenye harusi picha zapigwa nyingi na hii inawezekana walibadilisha pozi picha ipigwe.
Hiyo nyingine mbona hujaizungumzia
OTIS
 
kama anazalisha msongo wa kilowatts/megawtts/kv 3300 songas kuunganisha kwenye grid ya taifa kuna tatizo gani mkuu?hujawahi kuona umeme bila nguzo?au transformer iliyochimbiwa chini lakini megawatts ni zile zile?tena huyu jamaa inaonyesha ni mkali sana kwamba umeme ukikatika anaweka change over switch anamuwashia generator na huenda ndio alichompendea.kitu honda aisee exhaust haitoi moshi inanguruma tu
 
niliwahi kusikia habari za huyu bwana siku nyingi nikawa najiuliza hivi anaishije. Nashukuru Mungu amepata msichana anayempenda na kukubali kufunga naye ndoa. Mungu awajaaliye familia bora.

Aombe huyo msichana awe anampenda kweli, asije akamdanganya na hatimaye kumuacha njia panda.
 
kama anazalisha msongo wa kilowatts/megawtts/kv 3300 songas kuunganisha kwenye grid ya taifa kuna tatizo gani mkuu?hujawahi kuona umeme bila nguzo?au transformer iliyochimbiwa chini lakini megawatts ni zile zile?tena huyu jamaa inaonyesha ni mkali sana kwamba umeme ukikatika anaweka change over switch anamuwashia generator na huenda ndio alichompendea.kitu honda aisee exhaust haitoi moshi inanguruma tu

Mhmmm!!! Haya bwana.
 
Hata kama jogoo anawika unadhani atafanyaje bila ya kuwa na mikono wala miguu?

Kuna staili nyingi, nyingine hazihitaji hiyo mikono wala miguu, big-up bi harusi, huwezi kuibiwa huyo mume, ni wako peke yako, wenzio wanajuta kuwa na mijidume yenye miguu na mikono, haitulii nyumbani, kutwa kuhama baa tu.
 
Mhmm!!! Lakini kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom