Tatizo hujibu wewe unapeleka kwenye AI kwahyo unajikanganya sana kwenye maelezo yako, sielewi unapinga nini unakanusha nini, kwanza swali la kukuuliza ni mafundisho yapi ya mitume wote yaliyobakia hata hii leo? maana mgogoro unakuja kwasababu ya mabaki ya torati na injili na zaburi, viko wapi vitabu vingine na maneno mengine ya mitume wote waliotangulia? hata uhoji kuwa eti muendelezo wa mafundisho ya kina aadi na thamudi yako wapi? sijakueleza hapo juu kuwa hakuna kilichobakia katika kizazi chao?.
Bali ni utaratibu wa kawaida baada ya muda fulani ujumbe wa mtume husika unapotea, kisha anakuja mtume mwingine kuuhuisha, isipokuwa ujumbe wa Qu'ran huu umebakia mpaka leo hii kwasababu hakuna mtume mwingine baada ya mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake, ila waliotangulia wote ujumbe wao umeguswa na kupunguzwa na kubadilishwa na hii ni michezo ya mayahudi.
Unakiri kuwa mayahudi walihamia madinah kumsubiri mtume waliyeahidiwa kwenye vitabu vyao isipokuwa alivyokuja wakagundua sio yeye, haya madai yako una ushahidi nayo upi? una ushahidi utupe? ijapokuwa wakati huo huo umekiri kuwa walikuwa wanamsubiri aliyetabiriwa kwao, basi tupe ushahidi wa kihistoria na kimaandiko unaoonesha mtume mwingine alikuja badala ya mtume muhammad hapo madinah kama ambavyo alitabiriwa kwao, au kama hakuna mtume mwingine maana yake utabiri haukutimia, je maneno yaliyoandikwa kwenye torati na injili hayakuwa ya kweli?.
Na kukuweka sawa Qu'ran si muendelezo wa mafundisho ya biblia, hakuna kitabu cha Allah kinachoitwa biblia bali vitabu tulivyotajiwa ni ZABURI, TORATI, INJILI na SAHIFA ZA IBRAHIM NA MUSA kitabu kinachoitwa biblia sisi hatujatajiwa, na wewe unajua zaidi huu mkusanyiko unaoitwa biblia ulitoka wapi.
"Na hawakumtukuza Allah haki ya kumtukuza, pale waliposema mayahudi "hakuteremsha Allah juu ya mtu yeyote kitu chochote" waambie! ni nani aliyeteremsha kitabu ambacho amekuja nacho Musa? hali ya kuwa ni nuru na muongozo kwa watu, mnachokifanya ni karatasi, mnaziweka wazi na mnayaficha mengi na mmefundishwa ambayo hamkuyajua nyinyi wala baba zenu, waambie ni Allah{ndiye aliyeteremsha kitabu kwa Musa} kisha waache wao katika upuuzi wao wakicheza."
Qu'ran 6:91
Kama unakiri mitume wa aadi na thamudi walikuwepo na wametajwa, mgogoro wa upagani unatoka wapi? kwani ujumbe wao na ujumbe wa yesu una tofauti gani? unasema mitume wa kiislamu, kwani kuna mtume wa kikristo? unaye? labda paulo.
Hakuna ulichouliza hujajibiwa ,halafu mm sipend hizo Al maana ni za makafiri, Nina vitabu pdf nimepakua vingi sana nasoma masaa mengi sana ,
Unasema Paulo ni wa uongo, na wakati huohuo unakubali mitume kama Hud na Saleh ambao hawapo kwenye historia yoyote ya kale, si ya Mayahudi, si ya Wakristo, si ya wapagani, wala maandiko ya asili – hapo ndipo kuna mkanganyiko wa kweli. Hakuna ushahidi wa maandiko ya kale (Taurati, Injili, au hata maandiko ya kihistoria) yanayomtaja Hud au Saleh, lakini Biblia ina mashuhuda wa kihistoria walioandika kwa wakati wao, na majina yao yanajulikana hadi leo.
Unasema kwamba ujumbe wa mitume hupotea baada ya muda fulani halafu Qur’an ndiyo pekee umebaki. Swali ni hili kama Mungu anatuma ujumbe halafu unaruhusu upotee, huyo ni Mungu wa namna gani? Anashindwa kuhifadhi Neno lake mwenyewe?😂😂
Yesu alisema: “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita.” (Mathayo 24:35). Ikiwa unadai kwamba ujumbe wa awali wote ulipotea, basi unasema Mungu alishindwa jambo ambalo Qur’an yenyewe halikubali, maana inathibitisha kwamba Allah ndiye aliyeleta Taurati na Injili kama nuru na mwongozo kwa watu (Qur’an 3:3, 5:46-47).
Sasa kama ilikuwa nuru, nani aliizima? Allah mwenyewe au wanadamu? Na kama wanadamu waliweza kuizima, basi Qur’an iko hatarini vilevile.😂😂
Kuhusu hoja ya Mayahudi kumsubiri Mtume kule Madinah hiyo si madai yangu binafsi, ni ushahidi wa kihistoria.
Rejea vyanzo vya Kiislamu kama Ibn Ishaq (Sira), ambaye anasimulia kwamba Mayahudi walikuwa wakitamka kuwa atakuja Mtume, na walikuwa wanawaambia Waarabu
"Mtume atakuja, tutawaua kama walivyokufa wa Ad na Thamud!" lakini walipogundua kuwa Mtume huyo ni kutoka kwa Quraysh, si kizazi chao, wakamkataa.
Huo ni ushahidi kuwa walikuwa na matarajio lakini yaliyotimia hayakuwa kama walivyotegemea.
Bado haimaanishi Muhammad ndiye aliyekuwa katika vitabu vyao, maana hawakumtambua kama yule waliyesoma habari zake.ndio maana walipogundua ni tapeli walimkana na kumpinga ...KASOME HISTORIA YA DINI YAKO
Halafu unazungumza kama kwamba Biblia ni kitabu bandia kwa sababu haina jina "Biblia" ndani yake. 😂,
Lakini tunakubaliana kuwa Qur’an haikutaja neno "Qur’an" kwa maana ya jina la kitabu lote katika sura ya mwanzo kabisa. Lakini hiyo haibatilishi ukweli wake kwa wafuasi wake, siyo?
Biblia ni mkusanyo wa vitabu vilivyovuviwa na Qur’an yenyewe inavitaja hivyo: Taurati, Zaburi, Injili.
Hiyo ndiyo Biblia. Jina "Biblia" ni neno la Kigiriki likimaanisha "vitabu" si jina la uongo. Wewe unaona jina, sisi tunaona maudhui na ufunuo wake.
Umesema pia kuwa Qur’an si mwendelezo wa Biblia lakini Qur’an ndiyo inayodai kuwa inaendelea na mafundisho ya Musa, Daudi, na Yesu.
Qur’an 5:46 inasema “Tuliwapa Isa mwana wa Mariamu Injili, iliyomo humo mwongozo na nuru...”
sasa kama Qur’an ni mwendelezo wa hiyo nuru, kwa nini inatofautiana kwa msingi na Injili ya Yesu?
Yesu anafundisha upendo, msamaha wa dhambi, kuwa Mwana wa Mungu, na wokovu kwa njia ya msalaba lakini Qur’an inakanusha yote hayo.
Hii haijaitwa “muendelezo,” bali kubadilisha ujumbe.,QURANI ni utapeli
Kuhusu manabii wa A’d na Thamud hakuna tatizo kusema waliwahi kuwepo.
Lakini hoja yangu ni hii👇👇👇
mbona ujumbe wao haukuhifadhiwa wala kufundishwa na manabii waliokuja baadaye kama Musa au Yesu?
Kwanini hakuna ushahidi hata mmoja wa maandiko au mapokeo yaliyowahusu kabla ya Qur’an?
Hii ni ishara kuwa waliingizwa baadaye kwenye simulizi za Qur’an si kwamba walitoka kwa Mungu yuleyule wa Biblia.
Na ukisema kuwa hakuna mtume wa “Kikristo,” basi jiulize
👇👇👇👇
Yesu alimtuma nani baada yake?
Mathayo 28:19-20 Yesu alisema: “Nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi...”
hao ni mitume wake. Akina Petro, Yohana, na hata Paulo walikuwa wajumbe wake waliotumwa, na maandiko yao yanahifadhi mafundisho ya Yesu hadi leo.
Hilo ndilo jambo ambalo Qur’an haikuweza kufuta kwa sababu lina mizizi ya kihistoria.