Mkuu Mimi Binafsi sitakujibu Hizi hoja zako za uongo ila naskitika kuona unapoteza muda mwingi sana kupambana na uislam,unajitahidi kutafuta kila namna kuuchafua/kuufifisha uislam,unajitahidi kutengeneza makala ndefu ndefu na references zisizo na tija wala ukweli ili uaminike na watu wa mlengo wako.
Unaonekana hulali na muda mwingi unaupoteza Kwenye kutafuta namna yoyote kuufubaza uislam.
Lakini pia Naona unapambana sana kuanzisha nyuzi nyingi ambazo ukizichunguza zimejaa chuki zaidi badala ya elimu.
Mkuu nikufahamishe jambo Moja muhimu sana kwamba Juhudi kubwa unayoitumia kuusoma UISLAM UNGEWEKA PEMBENI HIYO "CHUKI" DHIDI YA UISLAM NAAMINI UNGEKUWA MTU WA TOFAUTI NA WA MAANA SANA na ungeifurahia hiyo juhudi ya kuusoma uislam.
NIKUHAKIKISHIE PIA WEWE SIYO WA KWANZA KUUCHAFUA UISLAM,WEWE SIYO WA KWANZA KUTAMANI UISLAM UPOTEE/UFUTIKE/USIWEPO,UISLAM ULIANZA KUPIGWA VITA KUANZIA HUKO KARNE NA KARNE...UISLAM ULIANZA KUPIGWA VITA NA MAJITU YENYE NGUVU NA UWEZO NA YENYE MAMLAKA KUBWA LAKINI MWISHO WAO WALISHINDWA NA WENGINE WALIISHIA KUINGIA KATIKA UISLAM.
KWA JINSI UISLAM UNAVYOPIGWA VITA INGEKUWA NI DINI YA UONGO UNGESHAPOTEA KITAMBO SANA..
UISLAM NI DINI YA KWELI NA NI DINI YA MUNGU MUUMBAJI,ameapa kuulinda Mpaka mwisho wa Dunia hii,ndomana Unaona pamoja na harakati zote mnazozifanya ajabu UISLAM ndo unazidi kustawi kwa kasi kubwa...Ingekuwa DINI ya uongo msingehangaika kiasi Hiki mpk mnashindwa kulala,unauanzishia uislam nyuzi mpk usiku wa manane...mbona huanzishi nyuzi kushambulia uhindu,ubudha nk?
Unashambulia UISLAM kwavile unauelewa kwamba ni UKWELI MTUPU na umegundua
UISLAM Umekuja kuweka bayana HAKI NA BATILI ila chuki ndo imekujaa na shetani amekuoambia kuuchukia DINI hii ya kweli,Uislam haumlazimishi mtu kuufuata mkuu,ni wewe na hiari yako.
WEWE NI MTU MDOGO SANA MKUU,UONGO,CHUKI NA FITNA ZAKO DHIDI YA UISLAM SOON ZITAKUGHARIMU KWA SABABU HUNA MUDA MWINGI UTAONDOKA KWENYE HII DUNIA NA HIKI UNACHOKIANDIKA HAPA UTAKIKUTA,nakuonea huruma siku utakapogundua Huu ukweli wa DINI hii na muda utakuwa umeshapita na Upo chini ya ardhi.
Umekuja kwa jazba sana,ni wazi hizi hoja ni ngumu sana kwako
Kwanza naomba nianze kwa kusema kuwa mimi siandiki haya kwa chuki, kejeli, wala dhamira ya kuwadhalilisha Waislamu, bali kwa sababu nimeamua kuchunguza kwa kina madai ya Uislamu na kuyapima dhidi ya historia, maandiko, na ushahidi wa kweli.
Ninaandika kwa sababu napenda ukweli siyo kwa kufurahisha upande wowote bali kumfikia Yule Mungu aliye hai na ambaye historia inamshuhudia kwa uwazi.
Niseme pia kuwa hoja nilizowasilisha hazijabuniwa, hazijatungwa, na wala si propaganda kama unavyodai,
Kila nukuu niliyoitumia inatoka katika kazi za watafiti waliotambuliwa kimataifa, wanaoheshimika katika fani za historia, lugha za kale, na maandiko ya dini. Hii ni njia ya kitaalamu ya kutafuta ukweli, si chuki kama ulivyodhani.
Kweli haifai kutishiwa au kujibiwa kwa jazba na kejeri, kweli inapaswa kuchunguzwa na kuthibitishwa.
unasema napoteza muda mwingi kuupiga vita Uislamu,
Kama ninavyochunguza Biblia kwa kina, vivyo hivyo nimeamua kuichunguza Qur'an na historia ya Uislamu kwa makini maana pia Mimi ni muislamu niliyezaliwa ndani ya familia ya kiislamu,nimesoma madrasa na elimu ya Uislamu,.
Hivo kumbuka, mtu hawezi kukosoa kitu asichokijua. Kwa hiyo kama unakuta nakosoa, basi ujue tayari nimekifahamu vizuri.
Kama kweli Qur’an inadai kwamba Muhammad ametajwa katika Biblia (Qur’an 7:157), basi ni halali kabisa kuuliza yuko wapi?
Kama Hud, Salih, na Thamud ni manabii wa kweli, kwa nini hawapo hata kidogo kwenye Biblia, wala katika historia ya Uyahudi na Ukristo? HIZI NDIO HOJA NILITEGEMEA UZISHAMBULIE
Unasema Uislamu umepigwa vita tangu kale lakini haujapotea. Ni kweli kwamba dini nyingi zimepingwa, hata Ukristo ulipigwa vita vikali na Warumi kwa karne tatu kabla ya kushamiri.,KASOME HISTORIA YA ZAMA ZA GIZA,kipindi hicho hata uislamu haupo kabisa ,
Uwepo wa dini hauonyeshi kuwa ni ya kweli hata dini za kipagani kama Hindu, Budha, au dini za wazawa wa Amerika na Afrika zimeendelea kwa karne nyingi bila kupotea.
Kwahiyo hii haimaanishi kuwa ni kweli za kimungu bali inaonesha nguvu ya tamaduni na siasa.
Umeandika kuwa “Uislam ni dini ya Mungu na ametamka kwamba atauhifadhi,hii ni propaganda ndani ya Uislamu,
Naomba tuchunguze hilo. Kama kweli Qur’an ilihifadhiwa moja kwa moja kutoka kwa Mungu, mbona kuna nakala nyingi tofauti zilizowahi kuwepo kabla ya Uthman kuziunguza?
Mbona kuna maandiko ya kale kama Sana’a Manuscripts ambayo yana tafsiri tofauti na Qur’an ya sasa? Kwa nini hakuna hata shahidi mmoja wa kihistoria aliyesikia ufunuo huo wa malaika kwa Muhammad? Na je, si kweli kuwa Muhammad alikulia mazingira ya wapagani na alifundishwa baadhi ya masimulizi ya Biblia,stori za apokrifa za wayahudi na wakristo waasi,kwa masikio tu, bila kuyaona kwa maandiko?HIZI NI HOJA HUWEZI KUZIJIBU
Unasema mimi ni mdogo na haya yatanigharimu baada ya kifo. 😂😂 Unafanya nicheke sana,Mimi nipo ndani ya Yesu,
Ndugu yangu, ni kwa sababu hiyo hasa nimeamua kuchunguza ukweli sasa kabla sijafa. Sitaki kuamini bila hoja, au kwa sababu tu nimerithi ,Mimi NARUDIA nimezaliwa kwenye uislamu na nimekulia humo ila niliukana uislamu ndani ya MSIKITI baada ya Sala ya ijumaa baada ya kuuliza maswali hayakujibiwa,kiukweli sijawahi kujuta,for ndio maamuzi Bora nimewahi kufanya katika maisha yangu,
Sitaki kuwa mfuasi wa dini ambayo manabii wake wengine wamechukuliwa kutoka kwenye simulizi za wapagani bila uthibitisho wa kihistoria wala maandiko ya awali. Hilo si jambo la kuchukulia juu juu.,
Mwisho, nakushukuru kwa kuniambia nisichukie lakini naomba na wewe usikimbie hoja kwa kujiingiza katika lawama au matusi.
Kama kweli dini yako ni ya kweli, basi ikabili hoja na si mtu. Hoja haijibiwi kwa hisia, bali kwa ushahidi.
Sitaki nifuate dini kwa hisia, bali kwa msingi wa ukweli ulio wazi na unaothibitishwa kihistoria.
Na kama uko tayari kujadiliana kwa msingi wa hoja na heshima, mimi niko tayari.
Tufungue Biblia na Qur’an, tusome historia ya Kiyahudi na Kiarabu kabla ya Muhammad, tulinganishe, tuangalie.
Hapo ndipo tutakutana kwenye ukweli, hata kama ni mchungu.