Kazakh destroyer
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 4,105
- 8,493
Amekufa Qu'ran haipo? sasa walikuwa wanasoma nini? sikiliza mkuu laiti ungejua hata maneno kiasi kwenye kiarabu ningekufafanulia kwa namna fulani ungeelewa zaidi, ila nnachotaka kukwambia ni kuwa namna ya kutunza vitu katika karne ya kwanza ilikuwa ni kwa kifua zaidi, watu walikuwa na uwezo mkubwa wa kukariri, huo ukusanyaji ulifanywa chini ya usimamizi wa waandishi wa mtume swala na amani ziwe juu yake, na hakuna herufi moja iliyopunguzwa wala kuongezwa, Qur'an imewekwa kwa uandishi wa kiungu hata ukisoma unaona haya maneno si ya mwanaadamu, na laiti ingekuwa hivyo isingebakia kama ilivyo kwa miaka zaidi ya 1400 sasa bila kubadili hata tone, wachilia mbali wakati ambao maswahaba wako hai na maandishi yapo ya asili.Bro Kazakh destroyer nadhan unajua kuwa Mtume alikufa na Quran haikuwepo.
Ni Khalifa Abu Bakr baada ya kushauriwa na 'Umar ibn Khattab(r.a).
(Soma Hadith zao).
Ndio walikusanya vipande vipande vilivyokuwa kwa mtu mmoja mmoja ambal Mtume aliwaandikia kwa kusaidiwa na wasaidizi wake maana yeye hakuwa anajua kusoma wala kuandika.
Una uhakika aliyokuwa anasema ndio yote yameandikwa?. (Tuwe neutral kwenye hili).
Una uhakika gan walikusanya maandiko yote?.
Wanadai Quran haijaandiksa kuwa imeshushwa coz mtume asingewza kuandika. lakina kuna hadith mtume alikuwa anatuma ujumbe kwa baadh ya wafalme kupitia magome ya miti.
Alikuwa anaandikiwa bila shaka.
Kwahiyo Quran ndan ya miaka 23 ya Utume wake na wakata anapata wahyi na kuwambia wafuasi wake waandike.
So dhana kuwa imeshushwa bila kuandikwa sio kweli.
Ukisema imeshushwa na kuandikwa na Binadam nitakubaliana na ww. and kwemye kuandika kuna kukosea heruf . mantik nk nk
Pili, usiseme vipi kama ilibadilishwa? leta ushahidi wa mahali palipobadilishwa au kupunguzwa baada ya kufa mtume swala na amani ziwe juu yake, ama hilo suala la kusimamiwa na watu wengine naam limeelezwa kwenye Qur'an yenyewe.
"Kisha tumewarithisha kitabu wale ambao tuliwateuwa miongoni mwa waja wetu......."
Qu'ran 35:32
Soma historia utaona kuwa njia iliyotumika kuhifadhi elimu ilikuwaje katika karne ya kwanza na enzi ya mtume swala na amani ziwe juu yake, kuna kitu kinaitwa isnaad hii ni chain of narrators ni kitu pekee kinachosifika kwa umma huu, hakuna watu wengine wowote walipewa jambo hili na ni elimu na watu wamebobea katika hiyo fani, hata huo usomaji huyo mwenzio aliokuwa anapigia kelele kila mmoja umepokewa kwa sanad mpaka kwa mtume alayhi ssalaam.
Na huyo abubakar na Umar na uthmaan na ally allah awaridhie hawa mtume mwenyewe ametuambia tuchukue wanayotupa, hivyo hilo la kukusanya Qu'ran wamefanya wao na sisi hatuna namna isipokuwa kunyenyekea kwenye wasia wa mtume alayhi ssalaaam, tumepokea msahafu na tunaisoma Qu'ran na tunaiamini na tunaamini hakuna herufi moja iliyo tofauti na Qu'ran aliyoteremshiwa mtume alayhi ssalaam kwa kupitia malaika jibriyl amani iwe juu yake, kisha waandishi wake wakaiandika kwenye waliyoandika juu yake na haikushushwa kama kitabu.