Hadithi za wapagani wa kiarabu ndani ya Quran

Hadithi za wapagani wa kiarabu ndani ya Quran

Hizo picha ni ustaarabu wa Nabateamu, si ya Thamud kama jamii ilivyotajwa kwenye Qur’an.,Acha upotoshaji

Pale hakuna ushahidi wazi wa uraia wa Thamud kupata makazi ya miamba kabla ya Firauni ni tafsiri tu za kisiri ambazo wataalamu wengi hawaziamini kwa msingi wa uthibitisho.
Hakuna uthibitisho wa arkeolojia unaoonyesha kwamba Thamud walijenga majumba na makazi kama inavyoelezwa na Qur’an badala yake ni mabaki ya taifa la Nabateamu nje ya historia halisi.

Acha Taqya
 
Wewe hamis77 umekua mwiba mchungu kwa Muslims namshukuru Mungu kwa Jina la Yesu Kristo umekuja kupiga kwenye mshono uongo wa Dini ya Waqurash,
Kihistoria Uislam umejaa uongo na propaganda na nilikua nashindwa kuja kushusha nondo kuuhusu sababu nilikua sija I master Quran in deep,wewe ndio umekuja tokea pembeni ashukuriwe Roho Mtakatifu aliyekutoa jikoni uje sebuleni umeonekana kwa kazi nzuri!
#Spanaziendelee
 
Al Kaaba ina pembe 4.
Kuna pembe ina jiwe jeusi. (Hajarul-asward)
Na Kuna pembe inaitwa pembe ye Yemen (kumtukuza dini za Kiyemen pamoja na Manabii wa kipagan uliowataja hapo juu na kuonyesha ushirikiano na makabila yote ya Yemen)

kabla ya mtume kuzaliwa kulikuwa na Al Kaaba nying tu.
(Ref watu wa As habul fiyl . walijenga Al kaaba nyingne Yemen mji wa Sanaa)

na Al kaaba zote hizi zlikuwa zinaabudiwa na wapagani.

Hii Al kaaba ya Meccah hadithi zinasema ilijengwa na Ishmael na baba yake Ibrahim(Refers Historia ya Kabila la Jurhum kutoka Yemen na ushirikiano wa kabila hili na Ishmael)

Soma pia historia ya Wakuresh (wapagan ) walivyokuwa wanaiheshimu Al kaaba .(kabla ya mtume kuanzisha Uislamu).

Al kaaba ya meccah ndio ilikuwa maarufu kwa sababu watu kutoka sehem mbalimbali walikuwa wanaenda kuona kugusa jiwe jeusi kwa kutoa chumvi au dhahabu ili wasamehewe dhambi zao. na ilikuwa inamilikiwa na wapagani.

Hadithi zinasema Miaka mamia mbele Al kaaba ikabomolewa kwenye Vita na kubaki Rundo la udongo.

Hii yote kabla Mtume hajazaliwa.
Naam mkuu Castle_Lite nikirudi kwako kuhusu ulichoandika uhalisia sio kama huo unaojaribu kutueleza, na hii iwe warning light kwako uangalie sources zako naona hawa watu wanataka kukuaibisha kwa makusudi.

Ama alkaaba haijajengwa na nabii Ibrahim na mwanae ismail amani iwe juu yao, bali wao waliinua tu kuta zake baada ya kuwa imebaki msingi tu kutokana na kukutwa na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini alkaaba imejengwa tangu enzi ya Aadam amani iwe juu yake, na hapa ni mahali pa khilafu baina ya wanachuoni baadhi wameenda kuwa imejengwa na Aadam mwenyewe na baadhi kuwa imejengwa na malaika na nyumba hii ndio nyumba ya kwanza hapa ardhini kuwekwa kwa ajili ya ibada.

"Hakika nyumba ya kwanza waliyowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko makkah, hali ya kuwa ni yenye kubarikiwa na hali ya kuwa ni uongofu kwa walimwengu wote."
Qu'ran 3:96

Baada ya hayo nikufahamishe sasa kuwa alkaaba imekaa katika umbile la mraba, kwa maana ina pande nne kama ambavyo tumesoma darasa la tano, sielewi imekuwaje umehusisha hizi pande na upagani na miungu? upande mmoja unaitwa nguzo ya upande wa sham, ambayo hii imeelekea upande wa Syria ya leo ambao ni upande wa magharibi, upande mwingine ni nguzo ya Yemen ambao huu ni upande ulioelekea usawa ya Yemen huku ni kusini , na upande mwingine ni nguzo ya Iraq hii imeelekea upande wa Iraq ambao huu ni upande wa kaskazini, na upande wa mwisho ni nguzo nyeusi ambayo yenyewe imeelekea upande wa mashariki.

Hivyo waislamu dunia nzima wanapata mahala pa kuelekea wakiswali kwani ni amri kuelekea kwenye nyumba hii kongwe na tukufu, kama alivyosema Allah aliyetukuka:

"Kwa hakika tumeona unavyogeuza geuza uso wako mbinguni, basi tutakuelekeza kwenye uelekeo uupendao, nasi elekeza uso wako upande wa msikiti mtakatifu wa makkah na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo na hakika wale waliopewa kitabu{mayahudi na wakristo} wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa mola wao, na Allah si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda."

Qu'ran 2:144

Hivyo kauli ya kutukuza upande wa Yemen eti kisa mitume wa kipagani, haya ni madai ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuyaandika, kwanza wakishakuwa mitume wanakuwaje wa kipagani tena? au tumeacha kukubaliana kuwa wapagani ni wale wasiokubali dini zote za mbinguni?.

Ama kuhusu kutukuzwa alkaaba kabla ya kuzaliwa mtume muhammad ni kweli, nyumba hii kama nilivyoeleza iko hapo tangu enzi ya Aadam swala na amani ziwe juu yao, sasa kuhusu hoja yako kuwa zilikuwepo alkaaba nyingi kabla ya uislamu haya ni madai ya uongo kabisa, kama una ushahidi leta madai hayo, alkaaba ni moja pekee katika dunia hii na ni katikati ya dunia kwa pande zote, huu ni muujiza mwingine ukisimama juu kabisa ya dunia utaona center ya dunia ni hapo, na ndio maana ni uelekeo wa waislamu wote wakiswali dunia nzima.

Ama suala la watu wa tembo ulilolitaja ni kweli lilitokea, ila kwa sura tofauti na uliyoitaja, alikuwepo mfalme kutoka Ethiopia aliyeitwa Abraha muda kidogo kabla ya kuzaliwa mtume muhammad, yeye alijenga kanisa na akataka watu waelekee kanisa lake, akakusudia kwenda kuivunja alkaaba kwa jeshi lake la tembo, kilichomkuta ndio kimetajwa katika Qu'ran ndani ya suuratul fiyl pale Allah aliyetukuka aliposema:

"Je hukujua namna gani alivyowafanya mola wako wenye ndovu? je hakuvifanya vitimbi vyao ni vyenye kupotea bure? na akawapelekea juu yao ndege makundi makundi, wanawapiga wao kwa mawe yanayotokana na udongo mkavu, akawafanya wao kama majani yaliyoliwa na wadudu."

Qur'an 105:1-5

Habari yake ikaishia hapo, na mpaka leo hii hajatokea mtu wa kuthubutu kuifanya chochote alkaaba ukiachana na mabadiliko machache yaliyotokana na hali ya hewa na uvamizi wa hajaaj bin yuusuf enzi ya Abdullah ibn zubayr Allah amridhie, ukifika makkah utaona kuwa alkaaba iko bondeni hivyo zamani imepata mashambulio ya mafuriko mara kadhaa.
 
The writer of the quran is a real joker.
How can Aaron's sister be Jesus' mother when infact in real Jesus was born 1600 after Moses😂
Ama kuhusu suala hili hii ni cheap argument na lazima ujichanganye kwasababu huna unachoelewa kuhusu Quran zaidi ya copy na kupaste kutoka kwenye vitabu vya hao walimu wako.

Hiyo aya imeeleza kuwa maryam mama yake issa amani iwe juu yake ameitwa "....ewe dada yake harun.."

walikuwa watu hao wema katika wana wa israeli wanajiita kwa majina ya manabii wao na watu wema wao, hivyo walimuita hivyo kumtahariza kwamba wewe dada yake mtu mwema harun imekuwaje umekuja na mtoto mchanga hali ya kuwa hujaolewa kwa ndoa? na ndio maana ukamilifu wa aya hiyo ni huu:

"Ewe dada yake haruna! baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba."

Qu'ran 19:28

Bali hakuna ulazima kuwa huyo ni haruna yule ndugu yake musa, kwani baina ya zama za maryam na zama za kina mussa swala na amani iwe juu yao ni zaidi ya miaka 500, iweje Qu'ran iliyoandikwa kwa ustadi wa hali ya juu ije na mistake dhaifu kama hii, kama una ushahidi kuwa maryam ni dada yake haruna kabisa ndugu yake na mussa tuletee.
 
"Na laiti ungeliwaona malaika wanapowafisha{chukua roho} za wale waliokufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao, na {wakiwaambia} ionjeni adhabu ya kuungua! hayo ni kwasababu ya yale yaliyotangulizwa na mikono yenu na hakika Allah si mwenye kuwadhulumu waja {wake}."

Qu'ran 8:50-51
Yani unaniletea nukuu ya daftari la vilaza?
 
Nimenukuu kutoka kwenye hadith mojawapo

"Alipojulishwa juu ya uamuzi huo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wasallam) (hii ilikuwa kabla ya kupewa utume) alikubali, na kwa utulivu akaomba kiletwe kitambaa, akakitandaza na kuliweka jiwe jeusi juu yake, kisha akawataka viongozi wa makabila yote kila mmoja akamate upande wa kitambaa, kisha wanyanyuwe kwa pamoja. Wakalinyanyua na walipopafikia mahali pa kuliweka, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wasallam)) akalinyanyua yeye kwa mikono yake miwili na kulirudisha mahali pake.
Kwa njia hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wasallam) aliweza kulitatua tatizo lililokaribia kuleta umwagaji wa damu mkubwa baina ya Makabila ya Kikureshi, na kila mmoja aliondoka hapo akiwa ameridhika."

Mwisho wa Kunukuu.

Kama hizi hadithi ni za kweli. ina maana jiwe jeusi Lilikuwa na Heshima sana na Lilikuwa linaabudiwa.
Kabla hata Utume wake na Kuanzisha Uislam .

Mohamed alikuwa analithamini.
Ama suala la jiwe jeusi, hili lipo kwenye kona ya alkaaba jirani na mlango wa alkaaba na upande sambamba na nguzo ya yaman ruknul yamaani, jiwe hili ni jiwe la peponi na hili limetajwa katika maneno sahihi ya mtume swala na amani ziwe juu yake, kwa sasa hivi limebaki vipande kama nane kwani ni la zamani sana na kutokana na uvamizi wa qaraamitwa ambao waliliiba wakakaa nalo kwa makumi ya miaka, kwa sasa limeunganishwa kwa ambari na miski na ukizoom utaona hivyo vipande vilivyobaki, ni mwenendo na mafundisho ya mtume kulibusu hilo jiwe.

Hiyo habari uliyonukuu ni kweli, kila ukoo katika makabila ya kiquraysh walitaka kupata heshima ya kulirudisha hilo jiwe mahali pake, ndio mtume swala na amani ziwe juu yake akaja na hilo wazo la kufanya hivyo ili kuepusha mizozo na vita kisha yeye ndo akalirudishia mahali pake baada ya wao kuliinua kwa pamoja kama ulivyoeleza.

Ama mwisho, hakuna muislamu anaeabudu hilo jiwe, na hii hapa kauli ya swahaba Umar allah amridhie:

"Hakika mimi ninajua wewe ni jiwe tu haudhuru wala haunufaishi, laiti kama nisingemuona mtume wa allah anakubusu nisingekubusu."

Kumalizia hizi ni ibada na utiifu wa waislamu kwa mtume wao, swala na amani ziwe juu yake.
 
Umekuja kwa jazba sana,ni wazi hizi hoja ni ngumu sana kwako

Kwanza naomba nianze kwa kusema kuwa mimi siandiki haya kwa chuki, kejeli, wala dhamira ya kuwadhalilisha Waislamu, bali kwa sababu nimeamua kuchunguza kwa kina madai ya Uislamu na kuyapima dhidi ya historia, maandiko, na ushahidi wa kweli.

Ninaandika kwa sababu napenda ukweli siyo kwa kufurahisha upande wowote bali kumfikia Yule Mungu aliye hai na ambaye historia inamshuhudia kwa uwazi.

Niseme pia kuwa hoja nilizowasilisha hazijabuniwa, hazijatungwa, na wala si propaganda kama unavyodai,

Kila nukuu niliyoitumia inatoka katika kazi za watafiti waliotambuliwa kimataifa, wanaoheshimika katika fani za historia, lugha za kale, na maandiko ya dini. Hii ni njia ya kitaalamu ya kutafuta ukweli, si chuki kama ulivyodhani.

Kweli haifai kutishiwa au kujibiwa kwa jazba na kejeri, kweli inapaswa kuchunguzwa na kuthibitishwa.

unasema napoteza muda mwingi kuupiga vita Uislamu,

Kama ninavyochunguza Biblia kwa kina, vivyo hivyo nimeamua kuichunguza Qur'an na historia ya Uislamu kwa makini maana pia Mimi ni muislamu niliyezaliwa ndani ya familia ya kiislamu,nimesoma madrasa na elimu ya Uislamu,.

Hivo kumbuka, mtu hawezi kukosoa kitu asichokijua. Kwa hiyo kama unakuta nakosoa, basi ujue tayari nimekifahamu vizuri.

Kama kweli Qur’an inadai kwamba Muhammad ametajwa katika Biblia (Qur’an 7:157), basi ni halali kabisa kuuliza yuko wapi?

Kama Hud, Salih, na Thamud ni manabii wa kweli, kwa nini hawapo hata kidogo kwenye Biblia, wala katika historia ya Uyahudi na Ukristo? HIZI NDIO HOJA NILITEGEMEA UZISHAMBULIE

Unasema Uislamu umepigwa vita tangu kale lakini haujapotea. Ni kweli kwamba dini nyingi zimepingwa, hata Ukristo ulipigwa vita vikali na Warumi kwa karne tatu kabla ya kushamiri.,KASOME HISTORIA YA ZAMA ZA GIZA,kipindi hicho hata uislamu haupo kabisa ,

Uwepo wa dini hauonyeshi kuwa ni ya kweli hata dini za kipagani kama Hindu, Budha, au dini za wazawa wa Amerika na Afrika zimeendelea kwa karne nyingi bila kupotea.

Kwahiyo hii haimaanishi kuwa ni kweli za kimungu bali inaonesha nguvu ya tamaduni na siasa.

Umeandika kuwa “Uislam ni dini ya Mungu na ametamka kwamba atauhifadhi,hii ni propaganda ndani ya Uislamu,

Naomba tuchunguze hilo. Kama kweli Qur’an ilihifadhiwa moja kwa moja kutoka kwa Mungu, mbona kuna nakala nyingi tofauti zilizowahi kuwepo kabla ya Uthman kuziunguza?

Mbona kuna maandiko ya kale kama Sana’a Manuscripts ambayo yana tafsiri tofauti na Qur’an ya sasa? Kwa nini hakuna hata shahidi mmoja wa kihistoria aliyesikia ufunuo huo wa malaika kwa Muhammad? Na je, si kweli kuwa Muhammad alikulia mazingira ya wapagani na alifundishwa baadhi ya masimulizi ya Biblia,stori za apokrifa za wayahudi na wakristo waasi,kwa masikio tu, bila kuyaona kwa maandiko?HIZI NI HOJA HUWEZI KUZIJIBU

Unasema mimi ni mdogo na haya yatanigharimu baada ya kifo. 😂😂 Unafanya nicheke sana,Mimi nipo ndani ya Yesu,

Ndugu yangu, ni kwa sababu hiyo hasa nimeamua kuchunguza ukweli sasa kabla sijafa. Sitaki kuamini bila hoja, au kwa sababu tu nimerithi ,Mimi NARUDIA nimezaliwa kwenye uislamu na nimekulia humo ila niliukana uislamu ndani ya MSIKITI baada ya Sala ya ijumaa baada ya kuuliza maswali hayakujibiwa,kiukweli sijawahi kujuta,for ndio maamuzi Bora nimewahi kufanya katika maisha yangu,

Sitaki kuwa mfuasi wa dini ambayo manabii wake wengine wamechukuliwa kutoka kwenye simulizi za wapagani bila uthibitisho wa kihistoria wala maandiko ya awali. Hilo si jambo la kuchukulia juu juu.,

Mwisho, nakushukuru kwa kuniambia nisichukie lakini naomba na wewe usikimbie hoja kwa kujiingiza katika lawama au matusi.

Kama kweli dini yako ni ya kweli, basi ikabili hoja na si mtu. Hoja haijibiwi kwa hisia, bali kwa ushahidi.

Sitaki nifuate dini kwa hisia, bali kwa msingi wa ukweli ulio wazi na unaothibitishwa kihistoria.

Na kama uko tayari kujadiliana kwa msingi wa hoja na heshima, mimi niko tayari.

Tufungue Biblia na Qur’an, tusome historia ya Kiyahudi na Kiarabu kabla ya Muhammad, tulinganishe, tuangalie.

Hapo ndipo tutakutana kwenye ukweli, hata kama ni mchungu.
Hakuna aya kwenye Qu'ran inayosema kuwa mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake ametajwa kwenye biblia, kwanini unapenda kutunga hoja na kuziandikia maneno mengi ili ionekane ni za kweli?.

Nilikuuliza kwenye ile post nyingine na ntaenda kutizama umejibu nini maana napitia post moja baada ya nyingine sijatizama umesemaje, mtume asipotajwa kwenye vyanzo vya mitume wa wana wa israeli ndio anakuwa mtume wa kipagani? mbona hiki kipimo ni kipimo ambacho hakijazingatia uadilifu.

Unadai ni muislamu halafu hapohapo unakuja na hoja za kujaribu kuutia uislamu kwenye upumbavu, halafu katikati ya maneno yako tena unadai yesu yuko ndani yako, mara ulikanusha uislamu msikitini siku ya ijumaa baada ya kuuliza maswali ambayo hayakujibiwa, ni maswali gani hayo? na je kama ni kweli maana nyinyi irhaabiyyuun huwa mna hoja nyingi za kuwavuta wasio na maarifa, hukujua kuwa sio lazima watu wote wawe na maarifa ya kukujibu? je msikiti huo mmoja ulioswali ulitosha kukuonesha kuwa mambo haya uliyonayo hayana majibu?!.

Ama mas'ala ya Qur'an na msahafu wa uthmaan na hizo chapa za san'aa na uturuki sisi tumekujibu kwa hoja nzuri kwenye ule uzi wako wa makala maalumu na ulishindwa kujitetea hatima yake ukang'ang'ania maneno ya maalik na malik hoja nyepesi kabisa kuliko ubawa wa mbu.

Qu'ran ni moja na hakuna pahala imepata kubadilishwa hata herufi moja, na itabaki hivyo mpaka siku Allah atakapoiondoka katika zama za mwisho.
 
Ama suala la jiwe jeusi, hili lipo kwenye kona ya alkaaba jirani na mlango wa alkaaba na upande sambamba na nguzo ya yaman ruknul yamaani, jiwe hili ni jiwe la peponi na hili limetajwa katika maneno sahihi ya mtume swala na amani ziwe juu yake, kwa sasa hivi limebaki vipande kama nane kwani ni la zamani sana na kutokana na uvamizi wa qaraamitwa ambao waliliiba wakakaa nalo kwa makumi ya miaka, kwa sasa limeunganishwa kwa ambari na miski na ukizoom utaona hivyo vipande vilivyobaki, ni mwenendo na mafundisho ya mtume kulibusu hilo jiwe.

Hiyo habari uliyonukuu ni kweli, kila ukoo katika makabila ya kiquraysh walitaka kupata heshima ya kulirudisha hilo jiwe mahali pake, ndio mtume swala na amani ziwe juu yake akaja na hilo wazo la kufanya hivyo ili kuepusha mizozo na vita kisha yeye ndo akalirudishia mahali pake baada ya wao kuliinua kwa pamoja kama ulivyoeleza.

Ama mwisho, hakuna muislamu anaeabudu hilo jiwe, na hii hapa kauli ya swahaba Umar allah amridhie:

"Hakika mimi ninajua wewe ni jiwe tu haudhuru wala haunufaishi, laiti kama nisingemuona mtume wa allah anakubusu nisingekubusu."

Kumalizia hizi ni ibada na utiifu wa waislamu kwa mtume wao, swala na amani ziwe juu yake.

Bro Kwann wasilitoe jiwe basi pale kwenye Al kaaba kama kweli hamlithamini?.

Mnalitukuza jiwe.
Na huo ndio ukweli.

1. Madai kuwa Adam alijenga Al kaaba ndio kwanza nasikia kwako😂😂😂😂.

2. Zilikuwa Al Kaaba nying. Ukiacha hiz za ethiopia. Kuna nyingne ilijengwa Yemen . Mji wa Sanaa . Na ni kuabudu Miungu mingine ya kipagani.
Unajua maana ya synagogi?.
Majengo yetu ya kumcha Mungu kwa kipindi hiki. (Msikikiti /kanisa)
Ni mfano wa synagogi.

Yalikuwepo zaman kabla ya Yesu na Mtume ila kabla ya hawa. bas hizo synagogi zilikuwa zinatumika kuabudu Miungu mingne.

Wengne ndan waliweka masanamu na wengine waliweka jiwe.

Hili jiwe lilikuwa la kipekee coz halikuwa na mfano wake.

(Imekuja kufahamika ni Kimondo tu kama lile jiwe lilioko Mbozi - ambalp ofcoz hata mababu wetu wa Mbozi waliliabudu)

Wakuryeshi walikuwa wanaabudu jiwe jeusi. Na ndio hilo jiwe jeusi lililoko Maccah mpaka leo . wapagan hao walikuwa wanaliabudu.

Hebu google bro. upate uelewa zaidi
 
Quran ni moja na hakuna pahala imepata kubadilishwa hata herufi moja, na itabaki hivyo mpaka siku Allah atakapoiondoka katika zama za mwisho.

Bro Kazakh destroyer nadhan unajua kuwa Mtume alikufa na Quran haikuwepo.

Ni Khalifa Abu Bakr baada ya kushauriwa na 'Umar ibn Khattab(r.a).
(Soma Hadith zao).
Ndio walikusanya vipande vipande vilivyokuwa kwa mtu mmoja mmoja ambal Mtume aliwaandikia kwa kusaidiwa na wasaidizi wake maana yeye hakuwa anajua kusoma wala kuandika.

Una uhakika aliyokuwa anasema ndio yote yameandikwa?. (Tuwe neutral kwenye hili).
Una uhakika gan walikusanya maandiko yote?.

Wanadai Quran haijaandiksa kuwa imeshushwa coz mtume asingewza kuandika. lakina kuna hadith mtume alikuwa anatuma ujumbe kwa baadh ya wafalme kupitia magome ya miti.

Alikuwa anaandikiwa bila shaka.
Kwahiyo Quran ndan ya miaka 23 ya Utume wake na wakata anapata wahyi na kuwambia wafuasi wake waandike.

So dhana kuwa imeshushwa bila kuandikwa sio kweli.

Ukisema imeshushwa na kuandikwa na Binadam nitakubaliana na ww. and kwemye kuandika kuna kukosea heruf . mantik nk nk
 
Hakuna aya kwenye Qu'ran inayosema kuwa mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake ametajwa kwenye biblia, kwanini unapenda kutunga hoja na kuziandikia maneno mengi ili ionekane ni za kweli?.

Nilikuuliza kwenye ile post nyingine na ntaenda kutizama umejibu nini maana napitia post moja baada ya nyingine sijatizama umesemaje, mtume asipotajwa kwenye vyanzo vya mitume wa wana wa israeli ndio anakuwa mtume wa kipagani? mbona hiki kipimo ni kipimo ambacho hakijazingatia uadilifu.

Unadai ni muislamu halafu hapohapo unakuja na hoja za kujaribu kuutia uislamu kwenye upumbavu, halafu katikati ya maneno yako tena unadai yesu yuko ndani yako, mara ulikanusha uislamu msikitini siku ya ijumaa baada ya kuuliza maswali ambayo hayakujibiwa, ni maswali gani hayo? na je kama ni kweli maana nyinyi irhaabiyyuun huwa mna hoja nyingi za kuwavuta wasio na maarifa, hukujua kuwa sio lazima watu wote wawe na maarifa ya kukujibu? je msikiti huo mmoja ulioswali ulitosha kukuonesha kuwa mambo haya uliyonayo hayana majibu?!.

Ama mas'ala ya Qur'an na msahafu wa uthmaan na hizo chapa za san'aa na uturuki sisi tumekujibu kwa hoja nzuri kwenye ule uzi wako wa makala maalumu na ulishindwa kujitetea hatima yake ukang'ang'ania maneno ya maalik na malik hoja nyepesi kabisa kuliko ubawa wa mbu.

Qu'ran ni moja na hakuna pahala imepata kubadilishwa hata herufi moja, na itabaki hivyo mpaka siku Allah atakapoiondoka katika zama za mwisho.
Kwanza wanaosema tapeli Muhammad ametajwa katika Biblia ni wanazuoni wa Kiislamu wakinukuu vifungu kama Kumbukumbu la Torati 18:18 na Yohana 14:16, wakidai kuwa "nabii kama Musa" au "Msaidizi mwingine" ni Muhammad. ,Nashangaa Leo unakana 😂😂

Lakini hoja hizi ni tafsiri za kulazimisha, zikiwa hazina muktadha wa maandiko. Kumbukumbu 18:18 inazungumza kuhusu nabii kutoka miongoni mwa ndugu zao Waisraeli, si Waarabu. Hii ni tofauti kubwa sana, na tafsiri yoyote ya kulazimisha haiwezi kubadilisha msingi wa kifasihi wa maandiko.

Jambo la pili ni hili kama kweli Qur’an inadai kwamba Muhammad ametajwa katika Taurati na Injili (Qur’an 7:157), basi ni wajibu wa Muislamu kuthibitisha wazi wapi hilo lipo katika maandiko yenyewe.,NI MOJA YA HOJA ZANGU AMBAZO MNAZIKIMBIAKIMBIA

Biblia haimtaji Muhammad popote kwa jina wala kwa maelezo yanayoendana na yeye. Na si kosa kuuliza Kama Qur’an inasema ametajwa, mbona Biblia yote haina jina lake hata mara moja? Kama maandiko ni ya kweli, basi uthibitisho wa kweli pia unapaswa kuwepo.

Uislamu unadai jambo, halafu ukikosa uthibitisho, watu wanapigwa Changa la macho kuwa BIBLIA imetiwa mikono, na bla bla kibao, Huko ni kukwepa hoja.

Halafu kusema kwamba eti kutotajwa kwa Muhammad katika Biblia ambayo ndiyo yenye Torati na Zaburi, haina maana ,utakuwa unapingana na QURANI yako,

Kama Qur’an yenyewe inasema ametajwa, basi ni wajibu wako kama Muislamu kuonesha hayo maandiko kwa uwazi. Usipofanya hivyo, basi hoja hiyo ya Qur’an inabaki kuwa haina uthibitisho wa kweli ni madai tu ya tapeli Muhammad na kikundi chake.

Sasa kama mtu anahoji kwa hoja, anapaswa kujibiwa kwa hoja, si kubezwa,tatizo la waislamu mnakosa hoja maana Quran yenu imejaa uongo mwingi.

Kuhusu nilichosema kwamba nilikana Uislamu msikitini baada ya kuuliza maswali yasiyojibiwa, wenzako Tena MASHEIKH walishindwa kujibu maswali na nilikuwa kijana mdogo sana ambaye nimeshiba neno na Nina udadisi mkubwa ,

Kwa nini Qur’an inakana kusulubiwa kwa Yesu, wakati historia nzima ya wanadamu, wakiwemo warumi, wayahudi, na hata wanazuoni wa kidunia, wanakiri kuwa Yesu wa Nazareti alisulubiwa?

Kwa nini Qur’an inasema Biblia imepotoshwa, wakati hakuna uthibitisho wowote wa kihistoria unaoonyesha kuwa Biblia imewahi kubadilishwa kabla ya Qur’an kuteremka?

Kwa nini Qur’an inakana Yesu kuwa Mwana wa Mungu, wakati hata Shetani anamkiri Yesu kuwa Mwana wa Mungu katika Biblia?

Je Kuna uthibitisho hata tone wakuokesha kuliwahi kuwepo dini ya Uislamu kabla ya Muhammad??

Nakumbuka niliambiwa Yesu alikuwa muislamu kwa hoja ya Luka 4:16 kuwa aliingia ndani ya sinagogi,kumbuka nilikuwa kijana mdogo sana ,lakini niliuliza je ni kwa tafsiri ipi Hadi sinagogi inakuwa MSIKITI ? Je kwa kiarabu Sinagogi ni masjid?

Mzozo ukaanza hapo

Hayo ni baadhi ya maswali niliuliza na hakuna aliyenipa majibu ya hoja, bali nilipigwa vijembe na kejeli.

Na kuhusu Qur’an kuwa moja na haijawahi kubadilika, hilo pia halina msingi wa kisomi.

Historia ya Uthman ibn Affan kuamuru msahafu mmoja na kuchoma nakala zingine ni ushahidi kwamba kulikuwa na tofauti.

Zaidi ya hayo, hadi leo kuna riwaya tofauti za kusoma Qur’an (qira’at) kama Hafs na Warsh ambazo zina tofauti ndogo lakini bado ni tofauti.

Hadi Leo hakuna matini au Manuscript ya Uthman popote pale....ili Hali uislamu ni dini ya juzi tu hapa

Uislamu una historia yake ya kihistoria ambayo Waislamu wengi wa kawaida hawaelezwi.

Madai kwamba Qur’an haijawahi kubadilika hata herufi moja ni propaganda, si hoja ya kisomi.

Kwa hiyo, natetea hoja zangu kwa akili, si kwa jazba. Na siyo dhambi kuuliza, kuchunguza, na kupima kwa kipimo cha mantiki.

Kama hoja haina majibu ya kisomi na yenye uthibitisho, basi mtu ana haki ya kuhoji. Huo ndiyo uhuru wa kweli wa akili na imani.

Sio tu kuaminishwa vitu bila ushahidi wowote
 
Ndugu, Mimi sina tatizo na mtu kuamini Uislamu au dini yoyote kila mtu ana uhuru wa imani.

Lakini unaponiita kafiri na kusema mimi ni kenge, ni ishara ya ukosefu wa hoja,sijui madrasa ndio mnafunzwa hivo, maana kipindi nasoma madrasa hatukufundishwa hivo, nilimaliza juzi zote 30 ,hatukufundishwa matusi na kejeli,

Nimehoji hoja zangu kwa utulivu,

Kama imani yako ina nguvu, basi ionyeshe kwa busara na si kwa maneno ya dharau.,hii inafanya hata wengine watilie mashaka Imani yenu

Umesema Qur’an haiwezi kuchafuliwa sawa, basi kwa nini mnapata hasira kila inapoulizwa?😂

Kama kweli ni ufunuo wa Mungu na umehifadhiwa, basi hoja yoyote itashindwa mbele ya ukweli wake., Lakini kama watu wanaanza kulalamika, kuporomoka kwa hasira, na kutukana basi hilo linaashiria kuna jambo haliko sawa kwenye hiyo dini.,mbona wakristo hawapo hivo

Umesema Uislamu ni dini ya haki lakini hilo ni dai, si hoja.

Kila dini duniani inadai kuwa ya haki.

Je, tunawezaje kupima haki ya kweli? Si kwa maneno ya hisia, bali kwa uchunguzi wa historia, maandiko, na matokeo ya ujumbe wake.

Mimi nimeleta uchambuzi wa manabii wa Qur’an ambao hawapo kwenye Biblia,historia,AKIOLOJIA na maandiko ya kale ya kiyahudi ,, na hoja yangu ni kuwa wametokana na hadithi za wapagani.

Kama unadhani si kweli, njoo ukanushe hoja moja baada ya nyingine kwa ushahidi, si kwa matusi.,Si mnasema QURANI imekamilika

Umesema hizi hadithi nipeleke kwa wafuasi wa Mfalme Zumaridi. Hiyo si hoja, ni dhihaka. Naomba tusifike huko, Mimi sihitaji kutoka nje ya mada na hoja zangu,

Ninazungumzia historia ya maandiko, muktadha wa Qur’an, na tofauti na Biblia.

Kama uko makini na unathamini ukweli, utajibu kwa uchambuzi si kwa mzaha.

Mwisho umesema Mimi siwezi kujua utamu wa Uislamu.

Ndugu, mtu hawezi kujua kama kitu ni cha kweli au la kwa sababu tu ni kitamu.,Halafu Mimi ni muislamu niliyezaliwa humo ,najua vingi huenda kuliko wewe,

Heroin ni tamu kwa mwenye kuitumia, lakini si dawa. Mtu anayempenda dikteta anaweza kuona utamu lakini hiyo haimaanishi yuko upande wa haki. Kweli inapimwa kwa uhalisia wake si kwa hisia za mtu binafsi.

Kwa hiyo rafiki, mimi niko tayari kujifunza na kuelewa, lakini sitakubali kuridhika na majibu ya matusi na kejeli badala ya ushahidi.

Kama dini yako ni ya kweli, basi ionyeshe kwa hoja simple tu
Hizi juzuu 30 ulizomaliza labda za kwenye forex Bible, au trading for dummies sio Qu'ran, kuna kitu nimeona hapa unasema hao mitume hawako hata kwenye maandishi ya kiyahudi ya kale, hebu tupe ushahidi hayo ni maandishi gani? kisha hata wewe kusema ni muislamu ni madai tu hakuna ubainifu wala ushahidi wa hilo kwenye maandishi yako.
 
Hakuna ulichouliza hujajibiwa ,halafu mm sipend hizo Al maana ni za makafiri, Nina vitabu pdf nimepakua vingi sana nasoma masaa mengi sana ,

Unasema Paulo ni wa uongo, na wakati huohuo unakubali mitume kama Hud na Saleh ambao hawapo kwenye historia yoyote ya kale, si ya Mayahudi, si ya Wakristo, si ya wapagani, wala maandiko ya asili – hapo ndipo kuna mkanganyiko wa kweli. Hakuna ushahidi wa maandiko ya kale (Taurati, Injili, au hata maandiko ya kihistoria) yanayomtaja Hud au Saleh, lakini Biblia ina mashuhuda wa kihistoria walioandika kwa wakati wao, na majina yao yanajulikana hadi leo.

Unasema kwamba ujumbe wa mitume hupotea baada ya muda fulani halafu Qur’an ndiyo pekee umebaki. Swali ni hili kama Mungu anatuma ujumbe halafu unaruhusu upotee, huyo ni Mungu wa namna gani? Anashindwa kuhifadhi Neno lake mwenyewe?😂😂

Yesu alisema: “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita.” (Mathayo 24:35). Ikiwa unadai kwamba ujumbe wa awali wote ulipotea, basi unasema Mungu alishindwa jambo ambalo Qur’an yenyewe halikubali, maana inathibitisha kwamba Allah ndiye aliyeleta Taurati na Injili kama nuru na mwongozo kwa watu (Qur’an 3:3, 5:46-47).

Sasa kama ilikuwa nuru, nani aliizima? Allah mwenyewe au wanadamu? Na kama wanadamu waliweza kuizima, basi Qur’an iko hatarini vilevile.😂😂

Kuhusu hoja ya Mayahudi kumsubiri Mtume kule Madinah hiyo si madai yangu binafsi, ni ushahidi wa kihistoria.

Rejea vyanzo vya Kiislamu kama Ibn Ishaq (Sira), ambaye anasimulia kwamba Mayahudi walikuwa wakitamka kuwa atakuja Mtume, na walikuwa wanawaambia Waarabu

"Mtume atakuja, tutawaua kama walivyokufa wa Ad na Thamud!" lakini walipogundua kuwa Mtume huyo ni kutoka kwa Quraysh, si kizazi chao, wakamkataa.

Huo ni ushahidi kuwa walikuwa na matarajio lakini yaliyotimia hayakuwa kama walivyotegemea.

Bado haimaanishi Muhammad ndiye aliyekuwa katika vitabu vyao, maana hawakumtambua kama yule waliyesoma habari zake.ndio maana walipogundua ni tapeli walimkana na kumpinga ...KASOME HISTORIA YA DINI YAKO

Halafu unazungumza kama kwamba Biblia ni kitabu bandia kwa sababu haina jina "Biblia" ndani yake. 😂,

Lakini tunakubaliana kuwa Qur’an haikutaja neno "Qur’an" kwa maana ya jina la kitabu lote katika sura ya mwanzo kabisa. Lakini hiyo haibatilishi ukweli wake kwa wafuasi wake, siyo?

Biblia ni mkusanyo wa vitabu vilivyovuviwa na Qur’an yenyewe inavitaja hivyo: Taurati, Zaburi, Injili.

Hiyo ndiyo Biblia. Jina "Biblia" ni neno la Kigiriki likimaanisha "vitabu" si jina la uongo. Wewe unaona jina, sisi tunaona maudhui na ufunuo wake.

Umesema pia kuwa Qur’an si mwendelezo wa Biblia lakini Qur’an ndiyo inayodai kuwa inaendelea na mafundisho ya Musa, Daudi, na Yesu.

Qur’an 5:46 inasema “Tuliwapa Isa mwana wa Mariamu Injili, iliyomo humo mwongozo na nuru...”

sasa kama Qur’an ni mwendelezo wa hiyo nuru, kwa nini inatofautiana kwa msingi na Injili ya Yesu?

Yesu anafundisha upendo, msamaha wa dhambi, kuwa Mwana wa Mungu, na wokovu kwa njia ya msalaba lakini Qur’an inakanusha yote hayo.

Hii haijaitwa “muendelezo,” bali kubadilisha ujumbe.,QURANI ni utapeli

Kuhusu manabii wa A’d na Thamud hakuna tatizo kusema waliwahi kuwepo.

Lakini hoja yangu ni hii👇👇👇

mbona ujumbe wao haukuhifadhiwa wala kufundishwa na manabii waliokuja baadaye kama Musa au Yesu?

Kwanini hakuna ushahidi hata mmoja wa maandiko au mapokeo yaliyowahusu kabla ya Qur’an?

Hii ni ishara kuwa waliingizwa baadaye kwenye simulizi za Qur’an si kwamba walitoka kwa Mungu yuleyule wa Biblia.

Na ukisema kuwa hakuna mtume wa “Kikristo,” basi jiulize

👇👇👇👇

Yesu alimtuma nani baada yake?

Mathayo 28:19-20 Yesu alisema: “Nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi...”

hao ni mitume wake. Akina Petro, Yohana, na hata Paulo walikuwa wajumbe wake waliotumwa, na maandiko yao yanahifadhi mafundisho ya Yesu hadi leo.

Hilo ndilo jambo ambalo Qur’an haikuweza kufuta kwa sababu lina mizizi ya kihistoria.
AI za makafiri sio sasa mbona unazitumia? usitudanganye na kudownload vitabu vingi sijui kujisomea sana hizo ni ratiba zako binafsi, lakini mtu akisoma maandishi yako anaona kabisa si wewe mwandishi wa moja kwa moja unaedit na kutuma, si utumie kichwa chako kama wanavyofanya wengine? maana matokeo yake ni kujichanganya katikati ya hoja zako na kuthibitisha yale uliyoyakataa na kuzaa hoja nyingine nyingi zisizokuwa na uhusiano wa moja wa moja kwa moja na mada.

Kuhusu mafundisho ya mitume waliotangulia kufanywa upya hii ndio sunnah ya Allah huwa anatuma mtume kisha watu wakianza kuyasahau yale mafundisho anawatumia mtume mwingine kuja kuyafanya upya yale mafundisho, na hilo limefanyika zama zote isipokuwa mafundisho ya mtume muhammad alayhi ssalaam, haya akaahidi atayalinda na atayahifadhi kwani hakuna mtume mwingine baada yake na imekuwa hivyo.

"Kisha tukawatuma mitume wetu mmoja baada ya mmoja, kila umma alipowajia mtume wao walimkadhibisha, tukawafuatanisha baadhi yao kwa baadhi nyingine, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa, wakapotelea mbali watu wasioamini!"

Qu'ran 23:44

Huu ndo utaratibu na hii haimaanishi udhaifu wa ujumbe wa Allah bali wanaoyasahau hayo mafundisho si yeye bali wale waliotumiwa mitume, na wanaadamu hawatenzwi nguvu katika kuamini ukitaka amini ukitaka kufuru, ila Allah anatekeleza ahadi yake ya kuleta mitume kila ambapo kuna uhitaji wa hilo, ili hoja isimame kwa watu na si vinginevyo.

"Mitume hao ni wenye kutoa bishara njema na wenye kuonya, ili watu wasiwe na hoja juu ya Allah baada ya kuletewa mitume, na amekuwa Allah ni mwenye nguvu mwenye hekma."

Qu'ran 4:165

Ujumbe wa mitume wote ni mmoja, mitume wote walikuja kufundisha watu kumuabudu Allah na kujiepusha na kuabudu mashetani na masanamu, Qur'an imekuja kuweka ukweli wa mitume wote waliotangulia na ndio maana Allah ametaja torati na injili na zaburi kuonesha kuwa hii Qur'an imekuja kuvipa nguvu hivyo vilivyotangulia, hivyo nuru ya ujumbe huo imeendelezwa na Qu'ran kwani imewataka hao watu waliopewa torati na injili waielekee Qu'ran kwani ndio amri ya yule yule aliyewapa vitabu vyao.

"Enyi watu wa kitabu! kwa hakika amekujieni mtume wetu anayekuwekeeni wazi mengi mliyokuwa mkiyaficha katika kitabu, na anayasamehe mengi{hayaweki wazi ili msidhalilike} kwa hakika imekujieni kutoka kwa Allah nuru na kitabu kinachobainisha, anawaongoza kupitia kitabu hicho wenye kufuata radhi yake kwenye njia ya amani na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake na huwaongoza wao kwenye njia iliyonyooka, kwa hakika wamekufuru wale waliosema: Hakika Allah ni masihi mwana wa maryam. Sema: Ni nani mwenye kumiliki chochote mbele za Allah ikiwa yeye angetaka kumuangamiza masihi mwana wa Maryam na mama yake na wote waliomo katika ardhi? ni wa Allah tu! ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo baina yao, huumba anachokitaka, na Allah juu ya kila kitu ni muweza."

Qu'ran 5:15-17

Kwa maana isiwe kumuumba nabii issa swala na amani ziwe juu yake bila baba ndio ishara kwamba ana sehemu katika uungu, bali Aadam amani juu yake kabla yake alikuwa hana baba wala mama mbona hakuabudiwa? na jambo lake ni la ajabu zaidi kuliko nabii issa, kwani mama yake issa anafahamika ni maryam, yu wapi mama yake Aadam na baba yake? lau ingekuwa kuzaliwa kimiujiza ndio sababu ya kuabudiwa basi wa kwanza angekuwa Aadam na Allah ametukasika kutokana na hilo kutakasika kwa mbali kabisa.

Ama kusema mafundisho ya Qur'an yametofautiana na injili ya yesu hili si kweli, kwani wewe huna injili kwa sasa, hilo ni moja, pili kama ni utofauti wa mafundisho si yesu tu yametofautiana tangu enzi ya mitume wengine wa mwanzo wa kati na hawa wa mwisho, kila mmoja katika wao alipewa mafundisho yake, kila watu walivyokuwa wasusuwavu basi walipewa mafundisho makali zaidi, lakini mitume wote ujumbe wao ni mmoja wamekuja kukataza kutokana na ushirikiana na kumuabudu mwingine asiyekuwa muumba wa mbingu na ardhi.

"Na tumekuteremshia wewe kitabu hiki kwa haki, hali ya kuwa ni chenye kuthibitisha ukweli wa yale yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na chenye kuyalinda {pia}. Basi hukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Allah wala usifuate matamanio yao ukaachana na yale yaliyokujia katika haki, kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sheria yake na njia yake, na lau angelitaka Allah angekufanyeni nyote umma mmoja, lakini ili awajaribu kwa aliyokupeni, basi shindaneni katika mambo ya kheri, ni kwa Allah tu! marejeo yenu nyote, basi atakuja kuwapeni habari ya yale mliyokuwa mkitofautiana."

Qu'ran 5:48

Narudia tena kukwambia mtume swaalih na huud ni mitume wa zamani sana kabla ya musa na issa, bali hakuna sharti la wewe kujua muendelezo wa mafundisho yao aliupokea nani, nimekueleza kuwa kuna mafundisho yalipotea kabisa na mitume wengine wakaja kuyaweka hai tena, hata wewe huoni unazungumza habari za Musa na yesu kwani hawa ndio mitume pekee? unayo mafundisho ya Idris? Ilyas? amani iwe juu yao kwa ukamilifu kama kitabu?.

Nakariri tena hakuna mitume wa kikristo mitume wote walikuwa waislamu na hawakuja kueneza msalaba duniani, ama wanafunzi 12 wa yesu wametajwa katika Qu'ran na hawa hawaitwi mitume bali maswahaba zake.

"Na kumbuka nilipowafunulia ufunuo wanafunzi {wa issa} kwamba waniamini mimi na mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni waislamu."

Qu'ran 5:111

Huud na swaalih na shu'ayb amani iwe juu yao kutokutajwa kwenye maandishi ya kiyahudi na kikristo si ishara kwamba hawakuwepo, na Qu'ran si kitabu kinachokuja kusadikisha biblia, bali torati, injili na zaburi.

Umesema Qu'ran haikutajwa kwa jina lake, aya ziko nyingi sana na hakuna ulazima wa kutajwa katika sura za mwanzo, unampangia Allah wewe kama nani?.

"Na Qur'an tumeigawanya gawanya ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kuiteremsha {kidogo kidogo}."

Qu'ran 17:106

Qu'ran ni kitabu kimeteremshwa kwa mtume muhammad, torati ni kitabu amepewa nabii mussa, injili amepewa nabii issa, zaburi amepewa nabii daudi swala na amani ziwe juu yao wote, niambie biblia ni kitabu amepewa mtume gani?.

Naweka kituo kufupisha maneno, sisi hatutumii AI kukujibu, karibu kwenye mjadala kwa hoja na si maneno mengi yenye kujikanyaga yenyewe kwa yenyewe.
 
Inaonekana hoja zinakuelemea hivo imebaki kulalamika ,mara Al mara sijui nini,nikiona hivi najua tayari dawa inaingia hivo nazidisha dozi,

Unadai kwamba Qur’an ndiyo kipimo cha ukweli wa maandiko yote yaliyotangulia.,ngoja nicheke kwanza😂😂😂

Hili ni kosa kubwa la kimantiki.

Huwezi kuanza mjadala kwa kudai kuwa Qur’an ndiyo kigezo cha kuhukumu Biblia wakati Qur’an yenyewe inathibitishwa kupitia historia ya Biblia.

Haiwezekani uthibitishe Qur’an kwa Qur’an halafu ukatae Biblia kwa kusema imepotoshwa bila ushahidi wa kihistoria wa maandiko ya awali yaliyoharibiwa.,Yaani hii Quran iliyoundwa na wahuni wachache hapo Al Azhar University mwaka 1924 juzi hapo Nyerere akiwa na miaka 2, ndio iwe kipimo?😂

Pili, kuhusu mafundisho ya mitume kupotea na Qur’an kuja kuyaweka sawa, hiyo ni hoja ya kudhani kwamba Mungu alishindwa kulinda Neno lake kwa maelfu ya miaka hadi ilipokuja Qur’an hii ya kina mfalme Fuad 1924 hapo Cairo misri ,maana Quran ya Uthman haipo, wala mudy hakuacha Quran .

Je, huo ni uwezo wa Mungu au udhaifu wa watu? Kama Mungu hakuweza kulinda Torati, Zaburi, Injili kwanini tukubali anaweza kulinda Qur’an hii ya 1924 hapo misri chini ya mfalme fuad?

Tatu, unapotaja Qur’an 5:111 ukisema wanafunzi wa Yesu walikuwa waislamu, lazima ujiulize, Je, Yesu mwenyewe alikuwa muislamu? Kama alikuwa, basi ni kwa mujibu wa Qur’an ambayo ni kitabu cha juzi tu hapa kinakuja watu wanakiona kimekuta historia ndefu na teknolojia ishaendelea,

Je Yesu alifundisha watu wasujudie Allah na kufunga mwezi wa Ramadhani?😂

Tuna historia na Injili zote hata zilizoko kabla ya Uislamu zinaonesha Yesu alifundisha juu ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

Hakuwahi kufundisha Shahada wala Swala tano. Hii inapingana na madai yako.,na hiyo Quran

Nne, unasema mitume wote walikuwa waislamu, hiyo si hoja bali ni tafsiri iliyopachikwa kwenye maana ya neno “kujisalimisha.” ,ni propaganda ya Uislamu,wenzako washaachana nayo maana ni hoja dhaifu sana ,

Kila nabii aliyemtii Mungu hakuwa muislamu kwa maana ya kufuata Qur’an au sharia ya Muhammad.

Yesu, Musa, Daudi walikuwa waaminifu kwa Agano la wakati wao. Hiyo haimaanishi walikuwa chini ya sharia ya Kiislamu ya karne ya 7., Uislamu umekuja na Muhammad karne ya 7,kabla hakujawahi kuwepo kitu kinaitwa UISLAMU

Tano, hoja yako ya Adam kutokuwa na baba wala mama haifuti muujiza wa kuzaliwa kwa Yesu. Hoja ya Kikristo si kwamba kuzaliwa bila baba kunathibitisha uungu wa Yesu, bali ni kuonyesha kwamba alikuja kutoka juu alikuwa Neno, naye Neno alikuwa Mungu (Yohana 1:1). Hilo ndio Neno lisemavyo

Kuzaliwa kwake ni sehemu ya kutimiza unabii wa Agano la Kale, si ajabu ya maumbile tu.,tuna unabii wa Yesu kuhusu kila kitu kuanzia Musa ,Daudi Hadi manabii wengine waliandika Hadi atakapozaliwa ..

Na mwisho, kuhusu Biblia na nani alipewa, Biblia ni mkusanyo wa vitabu vingi si kama Qur’an ambayo ni kitabu kimoja. ,ni wazi hujui maana ya neno Biblia ,hii ni aibu

Torati ilipewa Musa, Zaburi ilipewa Daudi, Injili ilifunuliwa kwa Yesu na Biblia imeyakusanya haya yote kwa mpangilio mzuri, tofauti na Quran ambayo Haina chronology,wala mantiki ya visa ,, haifuati mfululizo wa matukio wala historia.,
 
Hizi juzuu 30 ulizomaliza labda za kwenye forex Bible, au trading for dummies sio Qu'ran, kuna kitu nimeona hapa unasema hao mitume hawako hata kwenye maandishi ya kiyahudi ya kale, hebu tupe ushahidi hayo ni maandishi gani? kisha hata wewe kusema ni muislamu ni madai tu hakuna ubainifu wala ushahidi wa hilo kwenye maandishi yako.
Hivi Unajua hata kuhusu Quran yako imejaa visa vya uongo kutoka vitabu vya apokrifa vya wayahudi na wakristo waasi,

Mudy kawapoteza sana
 
Bro Kwann wasilitoe jiwe basi pale kwenye Al kaaba kama kweli hamlithamini?.

Mnalitukuza jiwe.
Na huo ndio ukweli.

1. Madai kuwa Adam alijenga Al kaaba ndio kwanza nasikia kwako😂😂😂😂.

2. Zilikuwa Al Kaaba nying. Ukiacha hiz za ethiopia. Kuna nyingne ilijengwa Yemen . Mji wa Sanaa . Na ni kuabudu Miungu mingine ya kipagani.
Unajua maana ya synagogi?.
Majengo yetu ya kumcha Mungu kwa kipindi hiki. (Msikikiti /kanisa)
Ni mfano wa synagogi.

Yalikuwepo zaman kabla ya Yesu na Mtume ila kabla ya hawa. bas hizo synagogi zilikuwa zinatumika kuabudu Miungu mingne.

Wengne ndan waliweka masanamu na wengine waliweka jiwe.

Hili jiwe lilikuwa la kipekee coz halikuwa na mfano wake.

(Imekuja kufahamika ni Kimondo tu kama lile jiwe lilioko Mbozi - ambalp ofcoz hata mababu wetu wa Mbozi waliliabudu)

Wakuryeshi walikuwa wanaabudu jiwe jeusi. Na ndio hilo jiwe jeusi lililoko Maccah mpaka leo . wapagan hao walikuwa wanaliabudu.

Hebu google bro. upate uelewa zaidi
Nigoogle ya kazi gani na tuko darasani tunayasoma kila siku, tulitoe sisi ndo tuliliweka pale!? kwenye uislamu kutukuza kile ambacho Allah amekitukuza ndio imani yenyewe, nimekufafanulia kila kitu hapo juu hizo habari za alkaaba ya Yemen leta ushahidi iko wapi, na imekuwaje ikaitwa alkaaba? ama habari za masinagogue hizo sijui zimeingiaje kwenye hii mada.

"Ndio hivyo! na yeyote anayeyatukuza matukufu ya Allah basi hilo ndiyo kheri kwake mbele za mola wake....."

Qu'ran 22:30

Hivyo sisi tunalibusu jiwe jeusi pale kwenye alkaaba kwasababu tumeamrishwa kufanya hivyo, ila sisi hatuabudu jiwe mkuu, na kila kitu nimekufafanulia sioni kama kuna ziada niliiacha kwenye maneno yangu yaliyotangulia.
 
Back
Top Bottom