Waliosema maisha ni safari ndefu hawakukoseaInaendelea
Samahani kwa kuchelewa Kuweka muendelezo ubize wa utafutaji unasababisha niwe free wikendi ila tajitahidi niwezavyo tumalize hii stori
Tuendelee.........
Ndani ya huo mwaka 2011 Kaka angu ( mtoto wa Bamkubwa) aliharibu huko bush alipokua anakaa alitorokea home kwetu Mzee wangu alimpokea vzr tu.Bro na Sister Walienda kusomea kwa ndugu zetu mmoja Dom mwingine Tanga,Me ndo nilibaki kijana mkubwa mpk alipokuja huyo broh wangu mwingine ( mtoto wa bamkubwa ) nilifurahi kubaki me ndo mkubwa ila pia nifurahi zaidi kwa ujio wa huyu bro maana damu zilkua zinapata kinoma tofauti na bro wangu wa damu kwanza nilifurahi alivyoondoka.
Huyu bro wangu ( mtoto wa bamkubwa) alikua anavuta ndumu,sigara na tungi anakunywa japo ilikua kisiri baadae akazoea mpk leo bado anatumia hivyo vitu.Nilijikuta me nae naanza kuvuta ndumu alizokuwa akinipa nimuashie.Tulikua tunalala nae chumba kimoja ko muda mwingi nilkua nae alafu hicho chumba kilikua kimejitenga na kilikua na mlango wa nje.
Mdogo mdogo nikawa mzoefu kwenye ndumu lakin ckuta wazazi wajue wadogo zangu walikua wanajua lakin walikua sio WANAA.Shule ikawa kwa machale ila nilijitahid nikafanya mtihani wa Taifa form 2 majibu yalikuja vizur tu maisha yakasonga.
Mwaka 2012 nikiwa form 3 ndo mambo yalikua yanazid kuharibika, hapo home kulikua kuna banda moja lilitumika kwa ajili ya parking ya gari.Kipindi hicho sio mzee wa yule mtoto wa mwenye alie kuwa na gari ko banda lilikua tu lipo free.Bro wangu aliamua kulifanya liwe Jim ( gym) siku moja alileta nondo ( ckujua hata alitoa wapi ) ko tukawa tunapigiapo tizi mida ya jioni.Kuna siku moja alikuja na muhuni mmoja wa kundi la JAMAICA MOCKERS pale gym.Huyo muhuni walikua wamehamia pale Mtaani kwetu japokua nyumba zetu zilkua mbali kidogo.Huyo muhuni alikua na tabia chafu balaa ( yaani kwa kifupi familia yake walinyanyua mikono juu.) kuiba na kujeruhi watu ndo ilkua raha yake.Nilkua nikipiga nae story anasimulia tu matukio yake ya kukata watu sime ( zuna ) na kupora.Nilikua na vutiwa na story zake sana ( Huyo muhuni now ni marehemu 2014 ndo alifariki ).
Nakumbuka tukio la kwanza kushirikiana nae huyo muhuni tulimwibia bishoo mmoja simu ( dingi ake alikua ni mfanyakazi wa TRA ).Huyo bishoo tulimchorea ramani me na huyo muhuni maana ilikua kila jioni anapita home kwetu kwenda kwa manzi ake.
Tulimchorea ramani vizuri tu me muhuni alinambia nimdanganye huyo bishoo aingie King ( yaani nimlete gym ) na kweli hatukuchukua siku nyingi nikawa nimemleta bishoo gym.ilikua saa 12 kuelekea saa Moja jioni.Muhuni alimwomba bishoo simu aione ilivyo, Alivyopewa tu Akasepa nayo mazima.Bishoo alisubir wap mtu atokei ( wakati huo niko nae ) alivyoona muhuni atokei akasepa huku akisema atamkomesha.Basi bna mida ya Saa Tano usiku muhuni alikuja yeye na Bro wangu wakaniamsha walinipa 10k kwa kazi niliyoifanya
Kesho yake tukiwa hatuna hili wala lile tunavuta zetu ndumu, mara Baba ake na huyo bishoo wako na wazee wakazi mbele yetu.Muhuni yeye aliwai kusepa tukawa tumebaki me na bro wakatushika ilikua ni purukushani siku bro anakataa yeye ajaiba me nilishikwa na Baba ake huyo bishoo nilkua sileti usumbufu wakati huo najitetea kuwa sikuiba mimi.Na kweli bishoo alinitetea kuwa me sikushiriki wakaniachia wakabaki na broh wanamlazimisha awapeleke kwao na huyo muhuni, cjui alifanyaje akawachoropoka maafande mbio alizotoka angefaa awakilishe taifa kwenye Olympic.
Hili tukio Wazazi walivyopata taarifa walinipiga marufuku kutembea na huyo muhuni na hyo gym wakaipiga marufuku.Ila hata baada ya hilo tukio kuisha bado niliendelea kutembea na huyo muhuni sasa hapo ndo kuteka watu simu n.k ilikua imeshamiri.kipindi cha Umiseta tumewachuklia Wanafunzi simu sana tunauza bei ya hasara.Ilifikia mahala hata nilipokua mwenyewe mazingira yakiniruhusu kukuteka nakuteka vizuri na kusepa.Mzee wangu alinikanya mpaka kuna siku alitufukuza kwake mimi na huyo bro angu ila tena akaturudisha home ( alikua na huruma sometimes )
matukio ni mengi tuliyoyafanya kipindi hicho lakini hili sitokuja kulisahau ilikua kidogo tufe.
Siku hyo tumeenda Club Club House ( Metro ) kama kawaida yetu tulikua wanne ikiwe bro wqngu na huyo muhuni na jamaa mmoja hivi.Sasa midaa ya saa 9 usiku tuliamua kurudi magheton kulala, kilindi tunatoka huyo muhuni alimuona kuna mdada kasimama pekee ake karibu na wanapouza magazet.Muhuni alisema tu nisubirin nikaongee na yule demu ( alikua anamjua ) sisi tulimsubir pembeni tulikua na pikipiki ( XL ) bro aliazima alipokua anafanyia kibarua chake.zilipita kama dakika kadhaa muhuni bado anaongea na yule demu mara ghafla wakaanza kuzozana, Muhuni alimchukilia yule demu kimkoba chake......acha yule demu apige kelele za mwizi, muhuni akaanza kukimbia tulipo bahati nzuri aliwai kukalia pikipiki mapema, bro akaiwasha ili tukimbie kucheki nyumba mabodaboda walikuwa wanatufata wako kwenye boda zao.tulifukuzana nao walikua bampa to bampa nasisi.Hapo sasa mimi mpk tungi imeisha kichwani nawaza tu mazishi yangu na wakati huo namuomba Mungu kimoyomoyo atusaidie.
Tulikimbilia barabara ya kwenda Majita road ila hatufika kabisa Majita road kuna sehem panaitwa kwa ILIJi ndo dereva wetu alikatiapo kona ( kuna njia hapo inaenda mtaani kwetu ) Pikiki ilimshinda dereva ( kinjia kilikua ni chembamba sana pikipik kupita ) bahat nzuri tulianguka kwenye bustani ya mboga mboga.Wale boda walitukosa maana tuliwaacha hatua nyingi sana ndo ikawa pona yetu.pikipiki iliharibika hand cater moja.Ila me peke angu niliumia ( niliumia mguu wa kushoto sehemu ya ugoko ckumbuki hata ni nini kiliniumiza vibaya vile).Wazazi niliwadanganya tu nimeanguka kwenye Jiwe wakakubali na maisha ykazid kusonga.
Nitaendelea
Sawa kaka jambaziHabarini Wapendwa hope mko njema licha hili janga linalo tukumba Mungu ni mwema sana.
Leo naomba kushare story ya Maisha yangu Mimi holy holm.Wiki chache zimepita nilileta humu thread ya jinsi nilivyoanza mahusiano ya kimapenzi na jimama na nilihaidi kuwaletea story nyingne ya maisha yangu, basi kwa hiari yangu sina budi kuwaletea.
Hii story ita base Katika Mji wa Musoma maana ndo nimeishi sana huku.Baadhi ya majina ya watu sitayataja hii ni kuwalindia heshima lakini ikibidi nitawaja. Tuweni tu wavumilivu maana story ni ndefu kidogo na nitakua naitoa vipande ili iweze kueleweka vizuri.
Nimezaliwa Musoma mjini nilikua naishi Kata ya Iringo mimi na familia yangu,tuko watoto sita.Kwa wanaoijua mitaa ya musoma enzi hizo ilikua sio mitaa salama sana kwa usalama hii ni kutokana na wimbi la makundi ya kihuni yaliyokua yameshamiri nahisi ni kuanzia 2010 mpka 2014 au 2015 kama sikosei mwenye kumbukumbu nzuri ataliweka sawa hilo.Binafsi yangu mimi sikua kwenye hayo makundi ila nilkua na marafiki ndani ya hayo makundi.
Tumelelewa kwenye maadili mema tu mimi na familia yangu ila wazazi wetu walikua wako busy sana na shughuli zao Baba alikua mwalimu na Mama alikua anauza nguo za mitumba (Nyasho) so muda mwingi tulikua tunabaki home wenyewe tu mpk jioni wazazi wakirudi.
Mwaka 2004 nilianza darasa la pili shule ya Musoma ambapo niliamishwa kutokana na maendeleo hayakua mazuri nikaamia Mwisenge primary tena nikahama kuja iringo ( B ) primary.Kwenye hii shule nilkutana na marafiki ambao tulikua tunaishi nao mji mmoja walikua ni jirani zangu.Kama mnavyojua kwa mlio kaa mtaa wa iringo enzi hizo kulikua na wahuni sana tena hasa kule kastamu milimani ulikua ukijichanganya angazao imekula kwako.Mimi na hao rafiki zangu tuliokua tunasoma nao nakumbuka tulkua na mtindo wa kukaa na hao wahuni japo wazazi walikua hawataki kukaa nao lkn haikuwa rahisi kutuzuia maana mda mwingi walikua kwenye shuguli zao.
Mara nyingi hao wahuni walikua wanatutuma tukawaitie mademu ambao walikua wanawataka wao muda mwingine wanatutuma bangi kwa mapusha wao kipindi hicho sisi hatuvuti sigara wala bangi tena walikua wanatukataza wao wenyewe....Kipindi hicho tulikua tumepanga nyumba ya vyumba viwili na sebule,chumba kimoja walilala wazazi na kingne alilala sista na wadogo zangu wawili wa kiume mimi na bro wangu tulikua tunalala kwa jirani kila mtu sehemu tofauti.Mimi nilikua na lala kwa na rafiki yangu tulikua tunasoma nae darasa moja.kiukweli huyu rafiki tabia zake hazikua nzuri alikua na tabia ya wizi ambayo aliniambukiza kimtindo nikajikuta na mimi nishakua kezi.
Nakumbuka siku ya kwanza mimi kuiba japo tulikamatwa siku, tulikua tunaenda shule ( darasa la pili tulikua tunaenda saa nne ) njia tuliyopita kuliku na Mmama mmoja anakibanda chake anauza vitu bidhaa za dukani pamoja na matunda.Sasa bna huyo rafiki angu akanambia twende tuchukue hela hapo kibandani,kulikua na utulivu yaani kulionekana hakuna mtu hapo maana tulivyofika tuliita kama mara tatu kibandani....kibandani....kibandani...tulivyoona hakuna mtu anae kuja jamaa angu alinambia niangalie usalama wakati yeye muda huo alipanda kwenye hicho kibanda na kupitia kwenye kale katundu ambako wanapitishia bidhaa, moja kwa moja kwenye kopo la hela akakomba zote ile anatoka tu anataka kushuka yule mama cjui alitokea wapi akaanza kupiga yowe la wezi.
Tukiwa na uniforms zetu za shule tulikimbia vibaya mno kuelekea shuleni bahati nzuri watu hawakua wengi sana ( hiyo ndo nature ya iringo asubuhi watu sio wengi sana mtaani ) tulikimbia mpka tukampotea yule Mama hatukuenda shule moja kwa moja tulipitia yale maeneo ya Afilux hotel kujua tulikua na shingap alizochukua kucheki zilikua ni sh 18000 na vijisenti me nilipewa buku 6000 yeye nae akachukua buku 6000 iliyobaki tukaingia kwanza kwenyee ka mgahawa kupoteza mawazo,tulikula siku hyo donati za kutosha baada ya hapo tukaenda pale stendi kwa wamachinga me nilinunua saa zile disco zilikua ni jero pamoja vile vikamera ambavyo ukichungulia unaona wanyama mbalimbali, Rafiki angu yeye alinunua karedio na vile vigemu fulani hivi ndo vilkua vina trend kipindi hicho.Baada kufanya hiyo shopping tulielekea shuleni sasa tukiwa hatuna wazo kama huko nyuma tumefanya msala.
Nitarudi kuendelea maana story ni ndefu ndugu zangu.
Au nasema uwongo ndugu zangu![]()
kipindi hicho nilkua bado young ila makundi sio asee na washkaji zangu wamekufa wengi tuMwaka 2006 kuna dogo wetu mmoja kwa jina la mdogo Chale aliuwawa na makundi ya kihuni akitokea kwenye tamasha CCM Kirumba Mwanza na yeye alikuwa ni mwenyeji wa Musoma
Dogo alikuwa anaishi Kitaji kama sijakosea, nilipomaliza Tarime Second alikuwa form 1kipindi hicho nilkua bado young ila makundi sio asee na washkaji zangu wamekufa wengi tu
😊😊 Me binafsi nilkua muda mwingi tukiteka nakuwa na huyo muhuni mwangu ( r.i.p kwake )nakumbuka umiseta mwaka 2012 kama sikosei uwanja wa karume baada ya kushinda 4 kwa 3 nikiwa kama streka wa Mara boys nilipiga hatrick
Bac ile tunarudi shule nyuma kidogo tu ya ule uwanja walitokea vijana wadogo kama wa 4 ivi na masime wakampokonya mwanafunzi mwenzetu simu na pesa
Wengine tulikua hatujui nini kinaendelea mpaka tuliposikia mikwaruzo ya sime hapo tukagawanyika makundi mawili, waliokua mbele wakakimbilia shuleni sisi wa nyuma tukaanza kukimbia ovyo mjini , wenye hela wakawa wanadandia boda boda kurudi shule cc wengine tunakimbia ovyo tu
Cha kushangaza kuna wazee wanapishana na wale madogo hata hawawasumbui wakawa wanatwambia nyie watoto wagonjwa kweli yani mko mia mnatishwa na watu wanne?
Nakumbuka sana tukio hilo
Sema mtoa mada nataka nikuulize hukuwemo kweli katika hao madogo?
Ooh shit kipaji kimepotea hiki lost talent ukwenda hata Toto Africa ahaaaaa hatrick heronakumbuka umiseta mwaka 2012 kama sikosei uwanja wa karume baada ya kushinda 4 kwa 3 nikiwa kama streka wa Mara boys nilipiga hatrick
Bac ile tunarudi shule nyuma kidogo tu ya ule uwanja walitokea vijana wadogo kama wa 4 ivi na masime wakampokonya mwanafunzi mwenzetu simu na pesa
Wengine tulikua hatujui nini kinaendelea mpaka tuliposikia mikwaruzo ya sime hapo tukagawanyika makundi mawili, waliokua mbele wakakimbilia shuleni sisi wa nyuma tukaanza kukimbia ovyo mjini , wenye hela wakawa wanadandia boda boda kurudi shule cc wengine tunakimbia ovyo tu
Cha kushangaza kuna wazee wanapishana na wale madogo hata hawawasumbui wakawa wanatwambia nyie watoto wagonjwa kweli yani mko mia mnatishwa na watu wanne?
Nakumbuka sana tukio hilo
Sema mtoa mada nataka nikuulize hukuwemo kweli katika hao madogo?
dah itakua nlikuona sema sikukujua tu ningekupiga jiwe la mdomoMe binafsi nilkua muda mwingi tukiteka nakuwa na huyo muhuni mwangu ( r.i.p kwake )
Tena hapo karume huo huo mwaka 2012 kwenye umiseta kuna mademu 4 tuliwateka simusasa wanafunz wengine kuona hivyo walikimbia kila mtu na njia yake.Just imagine tulikua Watu wawili tu
acha tu yan nipo nacheza ligi za mbuzi tu saivOoh shit kipaji kimepotea hiki lost talent ukwenda hata Toto Africa ahaaaaa hatrick hero