masai dada
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 17,382
- 19,289
ni nomaa sana
Mzizi mkavu najiunga bando ya bb kwa ajili ya hii story,weka hata part mbili kwa siku plssssssssssssssssssssHADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-25
ILIPOISHIA:
Alirudiwa na fahamu baada ya tukio kutulia, alipoombwa kwenda kwenye kaburi akaangalie kumetokea nini alikataa kwa kuhofia maisha yake. Ilionekana uchawi uliotumika pale ulikuwa mkubwa kuliko uwezo wa nguvu zake za kiganga.
Mzee Andendekisye na mkewe walipagawa na kumshtumu moja kwa moja kwa sauti kuwa Amangise baba wa Ambakisye ndiye aliyefanya vile na kuapa kula naye sahani moja. Alijikuta akisema kwa sauti na kujisahau yupo mbele za watu.
Wewe si umefanya hivi basi moto utakuwakia, nimeanza na mtoto sasa nafagia ukoo mzima.
SASA ENDELEA...
Kauli ile ilifanya watu wote makaburini wagune na kuanza kunongona chinichini kuonesha kumbe yeye ndiye muhusika wa kifo cha Ambakisye mpenzi wa mwanaye. Walijiuliza alifanya vile ili iweje na kujiuliza kama aliyefanya yake makaburini ni Amangise amefanya kwa faida gani. Wapo waliojiuliza anajiamini nini kusema hadharani yeye ndiye kamuua Ambakisye.
Kwa vile ndani ya kaburi hakukuwa na kitu zaidi ya jeneza lililoloa damu walishindwa kuzika. Baadhi ya watu waliamua kutoka makaburini kukiwa na sintofahamu huku mzee Andendekisye na mkewe wakisema hawatoki makaburini mpaka wamuone mtoto wao.
Wazee wa kijiji ilibidi waitane pembeni ili kutatua tatizo lile, mmoja alitoa wazo wamfuate mtaalamu kijiji cha Mbako kabla giza halijaingia ili wajue hatima ya mwili wa Atuganile ni nini kwani ilikuwa wiki ya miujiza. Walitumwa vijana na baiskeli kwenda kijiji cha Mbako kumfuata mtaalam.
Kukiwa na sintofahamu baadhi ya watu waliotoka makaburini mtu wa karibu na Amangise walikwenda kumwambia maneno aliyosema Andendekisye makaburini baada ya tukio la kushangaza na kutisha katika kaburi la Atuganile. Baada ya kumsikiliza alisema kwa masikitiko.
Hivi mimi nimuue Atuganile ili iweje?
Basi mwenzako anatamba kamuanza mtoto, sasa anahamishia majeshi kwenu na atahakikisha unaufagia ukoo mzima.
Unasema watu wote msibani wamesikia?
Ndiyo, yaani namshangaa sana jamaa yule kujisifia kwamba kamuua Ambakisye kwa vile wewe ulimuua mwanaye na pia wewe ndiye uliyetuma mamba kumla mwanaye makaburini.
Kwa kweli Mungu ndiye anayejua kama mimi ndiye niliyetia mkono kumuua Atuganile atanihukumu. Ni kweli mwanangu nilimtafutia mchumba baada ya siku moja kwenda Kilasilo na kumuona mtoto wa Ambokile, Bupe.
Kwa kweli binti wa Ambokile alinivutia kwa heshima aliyonionesha na kupenda awe mkwe wangu. Nilizungumza na wazazi wake wakanikubalia na kuanza mipango ya kuoa mara moja. Ni kweli nilikuwa najua mwanangu ana uhusiano na mtoto wa Andendekisye lakini hakuna hata siku moja mwanangu alinieleza kuwa anataka kumuoa.
Tumeona watoto wangapi wanaanzisha uhusiano na baadaye kila mtu kufanya mambo yake. Kama mzazi niliamini nilitakiwa kumtafutia mwanangu mke bora hasa kwa historia ya familia yake na yeye mwenyewe. Bupe alikuwa binti ambaye kila mmoja anamsifia kama mzazi unataka nini kama una mtoto wa kiume si kumtafutia amuoe.
Ni kweli.
Basi nilianza maandalizi na kupeleka posa kisha nilimbeba mwanangu kwenda Kilasilo kuonana na mchumba wake. Ni kweli mwanangu alishtuka kusikia nimemtafuta mwanamke mwingine wakati ana mpenzi wake. Nilimweleza sikuwa na lawama kwa vile sikuona malengo yao.
Kibaya zaidi wakati huo Atuganile alikuwa na ujauzito ambao baadaye kwa bahati mbaya ulitoka. Hapo ndipo wenzetu wakasema tumeutoa na kuanzisha vita ya kishirikina iliyopelekea kumuua mwanangu bila kosa, mzee Amangise alijitetea kwa uongo wenye ukweli kidogo.
Sasa ndugu yangu akumulikae mchana usiku anakuchoma, kama ulikuwa hujui basi kamuanza mwanao sasa mnafuata wenyewe. Kwa hiyo liwahi neno kabla halijadondoka chini.
Itabidi niondoke baada ya mazishi ya mwanangu ili niwawahi kabla hajaniwahi.
Wewe Amangise, uzembe wako ndiyo uliofanya umpoteze mwanao. Mwenzio kajipanga wewe unafanya mchezo. Sasa tegemea kumpoteza mkeo kisha wewe mwenyewe, Amangise alipewa tahadhari.
Sasa nitafanyaje wakati unajua siwezi kutoka kabla ya mazishi ya mwanangu, unafikiri watu si wataamini maneno ya Andendekisye kuwa mimi mwanga na pengine mkewe au yeye afe jamii itanielewa vipi ikiwa tayari kanipaka kinyesi masikioni kwa watu kuwa nimemuua mwanaye.
Kwani unataka kwenda wapi?
Kalonga.
Huko si Malawi?
Ndiyo kuna rafiki yangu mtaalam wa mambo haya.
Unajua ninyi ndiyo mnaofanya kuonekane Tanzania hakuna watu wa kuweza kuwadhibiti watu kama hawa mpaka Malawi, kila mtu utamsikia amevuka mipaka wakati humuhumu ndani kuna watu wakali kuliko hao mnaowafungia safari.
Wengi watu wa hapa wanatibu hawawezi kulipua mabomu.
Kweli umechanganyikiwa, nani alimrudisha mtoto wa Mwakasege.
Ooh! Nilimsahau yule kijana.
Basi yule kijana kazi yake ni kulinda na kutega bomu mtu akitaka kukufanyia kitu kibaya linamlipukia.
Mi sitaki la kujilinda tu bali kulipa kisasi kwa kifo cha mwanangu kwa vile sihusiki chochote kwenye kifo cha mtu.
Hiyo vita lazima akirudisha linakupata, siku zote kilio cha kuonewa husikilizwa kuliko kujilinda mwenyewe.
Jirani moyo haunipi kujikinga tu kwani nitakuwa nimemuogopa wakati kaniulia mwanangu bila kosa.
Nataka kukueleza kitu dawa ya huyo kijana ni zaidi ya kuloga, kwa vile ameahidi kufyeka familia yako. Ukishajizindika akija kukumaliza anajimaliza mwenyewe hata watu wakienda kwa waganga kuangalia atakuwa amejimaliza mwenyewe.
Una uhakika moto utamuwakia?
Nina imani jamaa nilivyo mjua lazima usiku wa leo atasafiri kwa vile kabla ya mazishi ya mwanaye alisafiri na inaonekana majibu ni kifo cha mwanao.
Basi nipeleke.
Nitakupeleka, yaani jamaa sijui anajiamini nini kwa kusema kuwa kamuua Ambakisye? jirani wa Amangise alisema kwa masikitiko.
Anajivunia uchawi wake, aliua nguvu za kiume za mwanangu eti kwa vile anataka kuoa mwanamke mwingine tofauti na mwanaye.
Wewee! jirani alishtuka.
Yaani nimemvumilia vya kutosha sasa too much.
Sikiliza jirani usimfanye lolote wewe twende huko jibu utaniambia.
Nitafanya hivyo japo nilitaka tupambane kwa uchawi tuone nani zaidi.
Majira ya saa mbili usiku Amangise aliondoka msibani na kuwaacha watu wakiombeleza na kupanda baiskeli kuelekea kijiji cha jirani ambako alikuwepo mganga kijana ambaye hakuwa mwenyeji wa mkoa ule. Walikwenda kwa saa moja mpaka kwenye kijiji hicho.
Bahati nzuri walikuta mganga amerudi jioni ya siku ile toka Mbeya mjini alipokwenda kufanya kazi zake. Walipofika aliwapokea na kuwasikiliza shida zao. Jirani wa Amangise ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu na kueleza kilichowapeleka pale.Mganga alikuwa kijana mdogo sana, baada ya kuangalia rada zake alitikisa kichwa na kusema:
Itaendelea Kesho....
Mzizi mkavu najiunga bando ya bb kwa ajili ya hii story,weka hata part mbili kwa siku plssssssssssssssssssss
Very interesting
Genius
Binadamu bwana ni very complex. Mtu unaweza ukawa unazungumza naye na ukimwangalia ni wa kawaida sana lakini akiyaandika ayawazayo utashangaa sana! Mwingine unaweza kumwogopa ukimwona kwa mbali unaogopa kama umeona kiumbe cha ajabu sana! Sasa hapa unaweza kukuta MziziMkavu ana kichwa kidogoooo kisichoendana hata na mwili lakini chenye very 'sophisticated brain!' Shikamoo MziziMkavu!!!Sina cha kusema zaid ya kukupa hongera maana sijui ulikuwa unafikiria nini
Binadamu bwana ni very complex. Mtu unaweza ukawa unazungumza naye na ukimwangalia ni wa kawaida sana lakini akiyaandika ayawazayo utashangaa sana! Mwingine unaweza kumwogopa ukimwona kwa mbali unaogopa kama umeona kiumbe cha ajabu sana! Sasa hapa unaweza kukuta MziziMkavu ana kichwa kidogoooo kisichoendana hata na mwili lakini chenye very 'sophisticated brain!' Shikamoo MziziMkavu!!!
HADITHI YA KUSISIMUWA VITA YA WACHAWI-24
Walipoufisha mwili makaburini ilifanyika ibada nyingine ya kulibariki kaburi na zoezi la kuteremsha jeneza kaburini lilianza kwa watu kuingiza jeneza kwa kamba. Jeneza baada ya kuteremshwa kaburini na kutolewa kamba, ilifanyika misa ya mwisho kabla ya kuzika.
Padri alifungua kitabu cha sala kusoma ibada ya wafu kisha alichukua udongo na kuutupia kwenye jeneza na kusema:[/FONT][/COLOR]
"Ulitoka mavumbini na mavumbini utarudi."
Kisha alichukua chetezo chenye uvumba na kupitisha kaburini alipomaliza alichukua maji ya baraka na kuanza kunyunyizia kwenye jeneza (sanduku) huku watu wakiwa wametulia kusikiliza ibada ile.
"Ulibatizwa kwa maji..."