Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,742
- Thread starter
- #81
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YAWACHAWI-17
Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua, yule Mkuu alirefuka huku tunamwona, masikio yake yakawa marefu kama ya mnyama, sura yake ilibadilika pia, jicho lake moja lilikaa juu ya paji la uso, halafu akaota mapembe mawili kwa kila upande mmoja.
Meno yake yalichomoza kwa mbele urefu wa wembe na kidevu kilishuka kwa urefu wa chupa ndogo ya chai. Tukiwa tunafikicha macho kwa kutoamini tulichokuwa tukikiona, mara akatokea yule dada MC, yeye alikuwa kituko zaidi, alikuwa mwembamba mfano wa katuni mbaya, kiuno chembamba sana, miguu nilidhani ni vidole vilivyopata uwezo wa kusimama.
SASA ENDELEA
"Mnaona hamuoni?" Alituuliza akionekana kuringia umbile lile.
Tulipiga makofi, lakini kwa kujikaza, maana kusema ule ukweli alitisha sana. Mimi mwenyewe nilijiuliza itakuwa vipi kama siku moja nitakutana na kiumbe kile, niliamini nitapoteza fahamu.
Lakini akaendelea kusema:
"Utaratibu wetu umeharibiwa na mtu mwenye kukiuka maadili na adhabu kali imeshachukuliwa. Sasa sina sababu ya kumwita yule aliyekuwa akiongea kwani karibu mambo yote ya msingi tumeshakubaliana nayo kinachotakiwa sasa ni utekelezaji wake tu, sawa jamani?"
"Sawa," tuliitikia wote kwa pamoja huku tukipiga makofi kwa nguvu.
"Sasa tutakwenda kwenye meza ya chakula, baada ya mlo kila mmoja atarudi kwake duniani, halafu utekelezaje wa yale yote niliyoyasema uanze mara moja. Mtasaidiwa na roho kutoka huku."
Aliposema maneno hayo alisita kidogo, kisha akaendelea:
"Mnaonekana wengi mmeshtuka niliposema mtasaidiwa na roho kutoka huku, kweli?"
"Kweliii," tulimjibu.
"Kwa hiyo mnataka kuwaona hao roho wa huku?"
"Ndiyooo."
Pale pale alipiga au tuseme alipuliza winja wengine wanaita mbinja, wengine wanaita mluzi, kufumba na kufumbua, viumbe wa ajabu walijaa mbele yetu. Walikuwa wengi sana, wafupi kama paka, lakini wanasimama mfano wa binadamu, wakawa wanatembea kwa kurukaruka hapa na pale.
Walionekana hawana habari na sisi. Pia walionekana hawaogopi kitu na zaidi sana walionekana wamezoea kazi wanayoifanya.
Mkuu wa Nchi akasema kuwa, roho wale ndiyo wenye uwezo wa kujibadili na kuingia kwenye mwili wa binadamu na kumsaidia kuwaza au kuamua mambo ya kufanya, hasa yale mabaya.
Akasema: "Kuna roho wa kila aina hapa. Kuna roho anayeshughulika na maamuzi mabaya, ngoja asimame mbele."
Kiumbe kimoja kilipita mbele ya wenzake na kusimama kwa pozi. Mkuu akasema anataka kuonesha mfano wa roho huyo anavyofanya kazi, akamwamuru akaingie kwa mzee mmoja aliyekuwa amevaa majani ya njano peke yake kama nguo za kwenye mkutano ule.
Kwanza, yule kiumbe pale mbele alipotea ghafla, kisha sekunde tano tu mbele, yule mzee akatoka alipokuwa na kufuata watu kisha kuanza kuwapiga huku akijisifia kuwa, yeye ni bondia wa ukweli hakuna wa kumuweza.
"Hata wewe Mkuu huniwezi mimi, eeeh! Mimi ndiyo Tyson wenu."
Nilishangaa sana tena sana, nikawaza mambo mengi, kwamba, kumbe wale watu ninaowaona duniani wakiwa wakorofi, si wao. Kuna roho wamewaingia na ndiyo wanawaelekeza kufanya vile.
Kilichotokea sasa, Mkuu akasema anatuma roho mwingine anayeshughulika na maamuzi mabaya akaingie kwa mtu mwingine ili tuone kitakachotokea.
"Lengo langu mkitoka hapa mkajue ni jinsi gani sisi tulivyo na uwezo mkubwa," alisema Mkuu huku akiwaangalia wale roho.
Roho mmoja akasimama mbele, akamwamuru akamwingie mzee mwingine aliyekuwa amevaa kaniki kukatiza kiuno, kichwani ana mvi tu.
Kufumba na kufumbua, yule mzee akaanza kumjia juu yule wa kwanza akimwambia hana lolote mbele yake, na anaweza kumuua kama ataendelea kutamba kwamba, yeye ni Tyson.
Mzozo mkubwa ulitokea, yule anayejiita Tyson akiendelea kutamba na sasa akawa anamfuata yule mzee wa mara ya pili ambapo alimrushia ngumi, yule mwingine akakwepa.
"Basi basi basi jamani. Naamini mmekubaliana na mimi."
Wale wazee wakawa katika hali zao za kawaida na kurudi kwenye viti huku wakionekana kujishangaa wenyewe.
Mkuu: Basi sasa nendeni mkale chakula, kisha baada ya hapo mtawanyike, kila mmoja arudi kwenye nchi yake na kusubiri utekelezaji wa maagizo ya huku.
Mkuu alipotea pale pale akawa haijulikani alikoingilia wala kutokea. Viumbe wengine wale walitangulia kutokomea kabla ya Mkuu.
Kwenye foleni ya chakula sasa, meza ilikuwa kubwa, lakini si ya mbao, ilipambwa kwa ngozi ya mnyama mwenye manyoya mengi kama mbwa.
Chakula chenyewe kilikuwa ni mapande ya nyama ya kuchoma huku kwenye chupa ndogo za plastiki kukiwa na kinywaji chekundu. Harufu kali ilitawala mahali hapo kiasi kwamba nilitaka kuziba pua.
Je, nini kilitokea hapo? Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua Kesho......