Hadithi ya kusisimua: Nchi ya wachawi-1

Hadithi ya kusisimua: Nchi ya wachawi-1

HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-7

Akatokea mtu mmoja, yeye weusi wake si kama wenzake, alikuwa zaidi. Alikuwa mweusi kama chungu kilichozeeka.
Akiangalia hivi, macho yake yalikuwa kama yanatoa mwanga hafifu huku kichwa kikiwa kipara chote.
Kilichonishangaza zaidi ni kitendo cha mtu huyo kuwa na rangi hiyo, lakini eti alivaa kanzu nyeupe sana.
Sasa ile rangi nyeusi ya mwili na ile rangi nyeupe ya kanzu, akaonekana kutisha sana, hasa ikizingatiwa kuwa, naye kwenye paji la uso alikuwa na pembe refu lenye kama mita moja.


Alisimama akatuangalia kama vile aliyetaka tunyamaze ili aanze kusema ingawa hakukuwa na watu wanaosema sema, pengine ni kutokana na wasiwasi na hofu iliyokuwepo eneo lile, hasa pale kila mtu mgeni alipojua eneo tulilokuwa si duniani.


Lakini mimi kwa akili zangu nilijua ni duniani, bali ni chini ya dunia. Maana hata ndani ya dunia ni dunia. Nje ya dunia, ingekuwa sayari nyingine, kama vile Uranus, Venus, Mercury au Jupiter.
Basi, ukimya ulitawala, yule mtu akiwa amesimama pembeni ya yule msichana PS, akasema:
Kazi yangu kubwa si kutoa elimu, bali uwezo. Kama ni elimu mtapewa huko huko duniani kila mmoja kwenye eneo lake.


Alipomaliza kusema, akamgeukia yule msichana huku akinyoosha mkono kupokea kitu. Yule msichana akainama, akanyanyua ndoo nyeupe kama kioo cha kujitazamia, akampa, naye akapokea na kuishika mkono mmoja.


Huyu mtu alikuwa mrefu kidogo, kwa sisi wote tuliokuwa ndani, hakuna aliyekuwa mrefu kama yeye, hata yule msichana hakuwa mrefu kama yeye, ingawa na yeye kati yetu hakuna aliyemfikia kwa urefu.
Akiwa ameshika ndoo ya maji, alichovya mkono, akachota maji akayarusha kwetu, yakaja kama maji yayorushwa na mpira wa kumwagilia.


Yalitupata wote na tulilowa sana, lakini wapo waliolowa zaidi na wapo waliolowa kidogo, mimi nililowa zaidi.
Hongera sana kijana wangu, umekuwa mtu mwingine sasa, si kama ulivyokuwa wakati hatujaingia humu ndani, mzee Madume aliniambia huku akiniangalia kwa macho yenye kunipa pongezi.


Kwa hiyo inakuwaje? Nilimuuliza.
Kuanzia sasa, wewe ni jasiri, una nguvu za ajabu na una uwezo wa ajabu.
Nitajuaje? Nilimuuliza.


Tukifika duniani utajua tu.
Mara sauti ya yule mtu ikatukatisha:
Kuanzia sasa, kila neno kutoka kwenye vinywa vyenu litakuwa na maana, kila mtakachotenda kwa kutegemea nguvu hii pia kitafanyika.


Alipomaliza kusema hivyo aligeuka na kurudi. Kama nilivyosema, ukumbi ulikuwa mkubwa kama viwanja vya mpira, kwa hiyo mpaka anaondoka tulimkazia macho hadi anapotea zake.
Pale alibaki yule msichana, lakini naye baada ya yule mzee kupotea, aligeuka na kutoka ndani ya ule ukumbi tukisubiri amri nyingine ya juu.


Mara alitokea yule mwanamke ambaye naye ni wa ajabu aliyetupokea na kutuingiza mle. Akasimama mbele ya watu wote na kupaza sauti akisema:
Hiki ni kipindi cha wageni kupotezana, sasa kila aliyekuja na mwenzake amshike mkono, mnatoka nje kabisa, huko kila mmoja anakutana na maelekezo mengine.


Alipomaliza kusema, akageuka na kuondoka zake.
Kwa haraka sana nilichojifunza mimi ni kwamba, utawala wa kule ulikuwa kama wa duniani, kwa maana kwamba, kulikuwa na protokali. Kila mtu alitambua jukumu lake ni lipi na linaanza kufanya kazi wakati gani.


Basi, tulianza kutoka nje na kila aliyekuwa na mwenzake alimshika mkono, mimi mzee Madume alinishika mkono. Tukaongozana hadi nje kabisa ambako tulikuta watu, wanawake kama yule aliyetuamuru kutoka nje, lakini wakiwa wengi sana. Kila mmoja alikuwa na ubao mweupe, maandishi mekundu yakisomeka mahali mtu alipotokea.


Sisi wetu yule pale, aliniambia mzee Madume baada ya kusoma ubao wa mtu yule ambao uliandikwa Wavuvi Mwanza.
Tulimfuata yule mwanamke, naye alipotuona akasimama ghafla, kisha akageuka kutupa mgongo huku akisema:
Nifuateni.
Tulimfuata kwa nyuma hadi nje ya geti kubwa la jengo hilo, akatuonesha njia akisema:
Hii njia inafika mlikotoka, ifuateni moja kwa moja. Tahadhari, msikate kulia wala kushoto, alisema akisimama pembeni ili kutupa nafasi sisi ya kuanza safari.


Tulitembea umbali wa mita kama mia moja hivi, njia ilikuwa ya kupita kwa miguu tu na si gari, halafu udongo wake kama mchanga wa pwani mweupe.
Tukiwa tunazidi kwenda, tulifika eneo fulani mbele yetu tuliona ukomo wa njia. Kwa maana kwamba, endapo tungeendelea kwenda tungetumbukia, mzee Madume akasimama na kusema:


Tatizo la huku bwana ni hili. Kila ukija kunakuwa na ugeni wa jinsi ya kuingia na jinsi ya kutoka, sijawahi kuja nikatoka kwa mtindo huu wa kukutana na gema kama hili, sasa mbona njia hapa imefika mwisho na yule alituambia moja kwa moja, tumekosea wapi?
Mimi sikumjibu kitu zaidi ya kukaa kimya, maana kama ni kujua yeye mwenzangu ndiye alikuwa mwenyeji zaidi.
Nimesema nyoosheni, sasa mnasita nini, nyoosheni, sauti ile iliyotupokea ilisema huku ilikotokea hakujulikani.


Mzee Madume alinishika mkono, akanivuta, tukanyoosha hadi kwenye mwisho wa njia ambapo ni gema kubwa na kwa chini kulikuwa kunaonekana mawingu ya bluu. Yaani ilikuwa kama vile sisi tupo juu ya dunia.
Sasa rukeni hapo mrudi kwenu, sauti ilisema.


Je, nini kitaendelea? Kesho tena
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-7

Akatokea mtu mmoja, yeye weusi wake si kama wenzake, alikuwa zaidi. Alikuwa mweusi kama chungu kilichozeeka.
Akiangalia hivi, macho yake yalikuwa kama yanatoa mwanga hafifu huku kichwa kikiwa kipara chote.
Kilichonishangaza zaidi ni kitendo cha mtu huyo kuwa na rangi hiyo, lakini eti alivaa kanzu nyeupe sana.
Sasa ile rangi nyeusi ya mwili na ile rangi nyeupe ya kanzu, akaonekana kutisha sana, hasa ikizingatiwa kuwa, naye kwenye paji la uso alikuwa na pembe refu lenye kama mita moja.


Alisimama akatuangalia kama vile aliyetaka tunyamaze ili aanze kusema ingawa hakukuwa na watu wanaosema sema, pengine ni kutokana na wasiwasi na hofu iliyokuwepo eneo lile, hasa pale kila mtu mgeni alipojua eneo tulilokuwa si duniani.


Lakini mimi kwa akili zangu nilijua ni duniani, bali ni chini ya dunia. Maana hata ndani ya dunia ni dunia. Nje ya dunia, ingekuwa sayari nyingine, kama vile Uranus, Venus, Mercury au Jupiter.
Basi, ukimya ulitawala, yule mtu akiwa amesimama pembeni ya yule msichana PS, akasema:
“Kazi yangu kubwa si kutoa elimu, bali uwezo. Kama ni elimu mtapewa huko huko duniani kila mmoja kwenye eneo lake.”


Alipomaliza kusema, akamgeukia yule msichana huku akinyoosha mkono kupokea kitu. Yule msichana akainama, akanyanyua ndoo nyeupe kama kioo cha kujitazamia, akampa, naye akapokea na kuishika mkono mmoja.


Huyu mtu alikuwa mrefu kidogo, kwa sisi wote tuliokuwa ndani, hakuna aliyekuwa mrefu kama yeye, hata yule msichana hakuwa mrefu kama yeye, ingawa na yeye kati yetu hakuna aliyemfikia kwa urefu.
Akiwa ameshika ndoo ya maji, alichovya mkono, akachota maji akayarusha kwetu, yakaja kama maji yayorushwa na mpira wa kumwagilia.


Yalitupata wote na tulilowa sana, lakini wapo waliolowa zaidi na wapo waliolowa kidogo, mimi nililowa zaidi.
“Hongera sana kijana wangu, umekuwa mtu mwingine sasa, si kama ulivyokuwa wakati hatujaingia humu ndani,” mzee Madume aliniambia huku akiniangalia kwa macho yenye kunipa pongezi.


“Kwa hiyo inakuwaje?” Nilimuuliza.
“Kuanzia sasa, wewe ni jasiri, una nguvu za ajabu na una uwezo wa ajabu.”
“Nitajuaje?” Nilimuuliza.


“Tukifika duniani utajua tu.”
Mara sauti ya yule mtu ikatukatisha:
“Kuanzia sasa, kila neno kutoka kwenye vinywa vyenu litakuwa na maana, kila mtakachotenda kwa kutegemea nguvu hii pia kitafanyika.”


Alipomaliza kusema hivyo aligeuka na kurudi. Kama nilivyosema, ukumbi ulikuwa mkubwa kama viwanja vya mpira, kwa hiyo mpaka anaondoka tulimkazia macho hadi anapotea zake.
Pale alibaki yule msichana, lakini naye baada ya yule mzee kupotea, aligeuka na kutoka ndani ya ule ukumbi tukisubiri amri nyingine ya juu.


Mara alitokea yule mwanamke ambaye naye ni wa ajabu aliyetupokea na kutuingiza mle. Akasimama mbele ya watu wote na kupaza sauti akisema:
“Hiki ni kipindi cha wageni kupotezana, sasa kila aliyekuja na mwenzake amshike mkono, mnatoka nje kabisa, huko kila mmoja anakutana na maelekezo mengine.”


Alipomaliza kusema, akageuka na kuondoka zake.
Kwa haraka sana nilichojifunza mimi ni kwamba, utawala wa kule ulikuwa kama wa duniani, kwa maana kwamba, kulikuwa na protokali. Kila mtu alitambua jukumu lake ni lipi na linaanza kufanya kazi wakati gani.


Basi, tulianza kutoka nje na kila aliyekuwa na mwenzake alimshika mkono, mimi mzee Madume alinishika mkono. Tukaongozana hadi nje kabisa ambako tulikuta watu, wanawake kama yule aliyetuamuru kutoka nje, lakini wakiwa wengi sana. Kila mmoja alikuwa na ubao mweupe, maandishi mekundu yakisomeka mahali mtu alipotokea.


“Sisi wetu yule pale,” aliniambia mzee Madume baada ya kusoma ubao wa mtu yule ambao uliandikwa Wavuvi Mwanza.
Tulimfuata yule mwanamke, naye alipotuona akasimama ghafla, kisha akageuka kutupa mgongo huku akisema:
“Nifuateni.”
Tulimfuata kwa nyuma hadi nje ya geti kubwa la jengo hilo, akatuonesha njia akisema:
“Hii njia inafika mlikotoka, ifuateni moja kwa moja. Tahadhari, msikate kulia wala kushoto,” alisema akisimama pembeni ili kutupa nafasi sisi ya kuanza safari.


Tulitembea umbali wa mita kama mia moja hivi, njia ilikuwa ya kupita kwa miguu tu na si gari, halafu udongo wake kama mchanga wa pwani mweupe.
Tukiwa tunazidi kwenda, tulifika eneo fulani mbele yetu tuliona ukomo wa njia. Kwa maana kwamba, endapo tungeendelea kwenda tungetumbukia, mzee Madume akasimama na kusema:


“Tatizo la huku bwana ni hili. Kila ukija kunakuwa na ugeni wa jinsi ya kuingia na jinsi ya kutoka, sijawahi kuja nikatoka kwa mtindo huu wa kukutana na gema kama hili, sasa mbona njia hapa imefika mwisho na yule alituambia moja kwa moja, tumekosea wapi?”
Mimi sikumjibu kitu zaidi ya kukaa kimya, maana kama ni kujua yeye mwenzangu ndiye alikuwa mwenyeji zaidi.
“Nimesema nyoosheni, sasa mnasita nini, nyoosheni,” sauti ile iliyotupokea ilisema huku ilikotokea hakujulikani.


Mzee Madume alinishika mkono, akanivuta, tukanyoosha hadi kwenye mwisho wa njia ambapo ni gema kubwa na kwa chini kulikuwa kunaonekana mawingu ya bluu. Yaani ilikuwa kama vile sisi tupo juu ya dunia.
“Sasa rukeni hapo mrudi kwenu,” sauti ilisema.


Je, nini kitaendelea? Kesho tena

Mzizi mkavu we ni sooooooooo!!!!!!!
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-8
ILIPOISHIA
"Tatizo la huku bwana ni hili. Kila ukija kunakuwa na ugeni wa jinsi ya kuingia na jinsi ya kutoka, sijawahi kuja nikatoka kwa mtindo huu wa kukutana na gema kama hili, sasa mbona njia hapa imefika mwisho na yule alituambia moja kwa moja, tumekosea wapi?"
Mimi sikumjibu kitu zaidi ya kukaa kimya, maana kama ni kujua yeye mwenzangu ndiyo alikuwa mwenyeji zaidi.

"Nimesema nyoosheni, sasa mnasita nini, nyoosheni," sauti ile ile iliyotupokea ilisema huku ilikotokea hakujulikani.
Mzee Madume alinishika mkono, akanivuta, tukanyoosha hadi kwenye mwisho wa njia ambapo ni gema kubwa na kwa chini kulikuwa kunaonekana mawingu ya bluu. Yaani ilikuwa kama vile sisi tupo juu ya dunia.
"Sasa rukeni hapo mrudi kwenu," sauti ilisema.

SASA ENDELEA…


"Mzee Madume alinishika mkono, tukaruka, lakini mimi huku nikipiga kelele.
"Haa!" Nilihamaki kwani kufumba na kufumbua tulikuwa pale pale tulipoondokea.
Mzee Madume akawa anacheka.
"Ha ha ha haaa! Ulijua tunakufa leo?" Aliniuliza kwa utani. Lakini sikumjibu.

Maisha yalianza kubadilika hapo. Nilirudi kwenye makazi yangu, mzee Madume naye alirudi kwake. Lakini akiniambia kuwa, kila nitakapotaka kumfanyia ubaya mtu niwe nanuiza kwa maneno ya kumtaka mkuu wa nguvu za giza ambaye ni shetani aitwaye Lusifa.

"Kama kuna mtu anakusumbua unataka tumbo lake livimbe, unasema "Lusifa nataka tumbo la mtu fulani livimbe", basi kufumba na kufumbua litakuwa limevimba na litaendelea kuvimba kutokana na unavyotaka," mzee Madume aliniambia huku tukiachana.

Nikiwa nyumbani, upepo mkali sana ulivuma kiasi kwamba, niliamini unaweza kuezua paa. Nilivumilia kwanza, lakini hali ikaendelea mpaka nikaanguka chini na kujikuta niko kwenye ulimwengu mwingine.
Huko nilikutana na watu kibao kama mimi, yaani vijana vijana sana.
Kila mmoja alionekana anakaa kwenye sehemu kwa ajili maalum. Kama vile kuna mgeni alikuwa akisubiriwa.

Na mimi nikatafuta sehemu yangu, nikakaa.
Mara akatokea mtu mmoja, mrefu sana, mweupe kama mwarabu, amevaa kanzu nyeupe, inaburuza chini sakafuni. Alipotembea, mwili wake ulizungukwa na mwanga kama miale ya jua.
Uso wake wakati mwingine ulionekana kama unawaka, wakati mwingine kama giza, nywele zake zilikuwa ndefu sana, lakini zikionekana zenye matunzo mazuri.

Huyu mtu alikuwa peke yake na mwendo wake ulikuwa wa taratibu sana huku mikono ameshika kwa mbele jirani na kifuani kama vile ishara ya unyenyekevu.
Aliposimama akatugeukia, ndipo nikamwona kwa uzuri zaidi na pia nikabaini tofauti kubwa kati yake na binadamu sisi.

Macho yake yalikuwa ya pembe tatu, midomo mipana sana, kidevu kirefu kupita kawaida na masikio kama ya sungura.
Alikohoa kidogo, moto ukatoka kinywani, akapiga chafya, pia moto ukatoka puani. Na wakati anakohoa na kupiga chafya, lile jengo tulimokuwemo lilitikisika kama kuna tetemeko la ardhi.

Aliinua mikono juu, mikono ya kanzu ikashuka hadi mabegani, kitu cha ajabu sana kikajionesha, mikono ilikuwa myeusi tii tofauti na usoni. Kwa hiyo ni kama alikuwa na sura mbili ya mtu mweupe na mtu mweusi.

"Kila mmoja ainue mikono kama mimi," alisema.
Mara, mikono ya watu wote ikawa juu.
"Pokeeni nilichonacho," alisema.

"Sawa," tulisema.
Nikashtuka na kujikuta nipo nyumbani kwangu, chumbani kama nilivyokuwa kabla.
"Khaa!" Nilishangaa.

***
Ilikuwa ni asubuhi ya siku iliyofuata tukasikia habari ya maiti za wavuvi wawili zimepatikana ziwani zikielea. Mimi nilijua ni wale wavuvi waliosukumwa majini na mzee Madume.
Nilikutana na mzee Madume ziwani, alionekana mchangamfu sana huku akisema ana mpango wa kubadili shughuli, badala ya uvuvi anataka kununua matrekta ili awe anakodisha kwa watu kulimia mashamba. Hapo tulikuwa tumekaa na wavuvi wengine kama sita.

"Hivi jana mlikuwa wapi nyinyi?" Mvuvi mmoja aliuliza, wengine wakadakia.
"Tena kweli."
Kusema ukweli hakuna aliyeweka wazi, si mimi wala si mzee Madume aliyekuwa tayari kuanika safari yetu.

"Jamani, si tunawauliza nyinyi?"
Mzee Madume akawa anacheka tu.
Zamu ya kuanza kazi ilifika, nikaingia mtumbwini. Tuliingia watu watatu, lakini mzee Madume hakuwepo.
Siku hiyo tulivua samaki wengi sana, sana tu. Kiasi kwamba hata mtumbwi ulielemewa na mzigo mkubwa wa samaki.

Njiani wakati tunarudi, wenzangu wakawa wananitania.
"Au mwenzetu mlikoenda jana na mzee Madume ndiyo majibu yake haya nini?"
Nilicheka tu, lakini sikuwafungulia moja kwa moja kwamba, ni kweli yale ndiyo yalikuwa majibu ya safari tuliyokwenda jana yake au la!

Tulipofika ufukweni, tulikuta wenzetu wengine nao wakiwa wamerudi. Mtumbwi wa mzee Madume nao ulijaa samaki wengi kiasi kwamba, maswali yakawa kibao kwa wavuvi wengine.
"Mh!" Mvuvi mmoja aliyekuwa kwenye mtumbwi mmoja na mimi aliguna, mguno huo uliashiria kuwa, alishangazwa na wingi wa samaki kwenye mtumbwi wa mzee Madume. Kusema ukweli hata kama ningekuwa mimi ningeshangaa, kwanini mitumbwi ambayo sisi tuliokuwa hatupo jana yake ndiyo iwe na mapato ya samaki kwa wingi vile?!

Kifupi biashara ilikwenda vizuri kwa upande wangu kiasi kwamba, maisha yangu pia yalibadilika. Ikafika mahali, nikafungua duka kubwa mjini Mwanza, akawa anauza mke wangu. Wakati huo mzee Madume alishahamia Kagera ambako alikuwa akimiliki matrekta na magari ya kubeba abiria toka mjini Bukoba kwenda Muleba.

Baada ya muda nilifungua duka jingine la pili kubwa sana kuliko lile la kwanza. Nikawa nauza mwenyewe, hapo ndipo maisha yangu ya uchawi yaliponoga.


Je, nini kitaendelea? Usikose Kesho...........
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-9

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA

"Mh!" Mvuvi mmoja aliyekuwa kwenye mtumbwi mmoja na mimi aliguna, mguno huo uliashiria kuwa, alishangazwa na wingi wa samaki kwenye mtumbwi wa mzee Madume. Kusema ukweli hata kama ningekuwa mimi ningeshangaa, kwanini mitumbwi ambayo sisi tuliokuwa hatupo jana yake ndiyo iwe na mapato ya samaki kwa wingi vile?!

Kifupi biashara ilikwenda vizuri kwa upande wangu kiasi kwamba, maisha yangu pia yalibadilika. Ikafika mahali, nikafungua duka kubwa mjini Mwanza, akawa anauza mke wangu. Wakati huo mzee Madume alishahamia Kagera ambako alikuwa akimiliki matrekta na magari ya kubeba abiria toka mjini Bukoba kwenda Muleba.

Baada ya muda nilifungua duka jingine la pili kubwa sana kuliko lile la kwanza. Nikawa nauza mwenyewe, hapo ndipo maisha yangu ya uchawi yaliponoga.
SASA ENDELEA…


Siku moja nikiwa dukani, nikagundua kuwa, duka lililopakana na mimi linaingiza wateja wengi kuliko mimi, jambo hilo lilinikasirisha sana. Haraka sana, nilifunga duka nikarudi nyumbani nikipitia kwa mke wangu kumlalamikia.
Nilimweleza haiwezekani watu wafanye biashara kubwa kupita mimi wakati mimi nina uwezo mkubwa kuliko wao.

"Sasa utafanyaje baba Masu?" Mke wangu aliniuliza.
"Najua mimi mama Masu," nilijigamba huku nikipigapiga mkono kifuani.
Nilipofika nyumbani, nilifungua kabati langu. Nikisema kabati langu nina maana kwamba, funguo la kabati hili nakaa nazo mimi na mke wangu nilishamwambia kuwa, humo naweka vikorokoro nyangu tu, sitaki tuchanganye.

Nilitoa kitu fulani mfano wa kitambaa cheusi, nikakishika mkononi, nikafumba mkono kisha nikaondoka kurudi dukani.
Niliiingia dukani, lakini kabla sijafungua, nilikitembeza kile kitambaa mwilini huku nikisema:
"Mimi ndiye mwenye nguvu kuliko wote hapa, nataka niendelee kuwa na nguvu. Wateja wote walione duka langu kama nyuki wanavyoona maua."

Baada ya kusema hayo, niliinua mguu mmoja juu kisha nikaupiga chini puu.
Nikawa si mimi katika mwili, hapo ina maana sikuwa naonekana kwa macho ya kibinadamu.
Nilikwenda kusimama nje ya duka la yule jirani yangu, lakini alishtuka na kusema:
"Ushindwe katika jina…"

Kabla hajamaliza, nilirudi kwangu, ndani. Nikajibadili kuwa kawaida, lakini sikufungua duka. Nilijiuliza ina maana yule bwana ni mtu wa Mungu au vipi? Na kama ni mtu wa Mungu mimi nimchukulie hatua gani ili nimzidi nguvu:
"Oke, nimejua la kufanya," nilijiambia mwenyewe.
Baada ya hapo nilifungua duka langu na kuendelea kuuza.

Ukweli ni kwamba, wateja walianza kuja kwangu kwa wingi huku nikifurahia moyoni. Mara, yule jirani yangu ambaye ana madevu mengi na nywele ndefu zinazoonesha hazichanwi kwa ufasaha, alikuja dukani kwangu na kusimama mbele yangu.
"Kijana, huu ni moto wa gesi, acha kabisa kucheza na mimi."
Kisha akaondoka zake kurudi dukani kwake.

Mbaya zaidi wakati anasema maneno yale, walikuwepo wateja wawili walioingia kila mmoja kivyake.
"Huyu mzee vipi kwani?" Mteja mmoja aliniuliza.
"Khaa! Kama kichaa!" Mwingine alisema.
"Aa! Mwanza hii bwana," wa tatu alisema huku akitoka nje, pia iliashiria kuwa, alichotaka ndani ya duka langu hakikuwepo.

"Hata mimi namshangaa," nilijikaza na kusema.
"Kwani humfahamu?" Aliniuliza mmoja.
"Namfahamu, si mwenye duka la pili hapo," nilisema lakini kwa sauti iliyokuwa ikitoka nje kwa wasiwasi mkubwa.

Baada ya wateja hao kuondoka, nilisimama mlangoni, nikainua mkono juu kuashiria nasimamisha mara moja ujaji wa wateja ili nishughulikie suala la jirani yangu kwanza.
Nilirudi ndani na kukaa kwenye kiti nikiwaza, lakini sikufunga duka. Katika maamuzi yangu niliamua kumuumiza yule jirani kwa kumpiga upofu asione tena na hivyo kumfanya amweke mtu mwingine wa kuuza pale dukani ambapo niliamini atakuwa mwepesi ‘kiroho' kuliko yeye.

Nilipopata uamuzi huo, nilirudi mlangoni, nikanyoosha tena mkono na kufanya alama ya kuita, yaani nikafungulia wateja waingie.
Nilitoka nje kidogo, nikasimama kwenye kizingiti cha mlango.
Nilitoa kichwa kuchungulia nje, nikamwona yule jirani yangu naye amesimama kwenye kizingiti kama mimi, nikarudisha uso nyuma kwa ghafla. Lakini sehemu kubwa ya mwili ilikuwa tayari nje.

Kumbe na yeye alifanya kama mimi, alirudisha uso nyuma na sehemu kubwa ya mwili ikabaki mbele, kisha akawa anatoa uso kwa kuibia na mimi vivyo hivyo. Ilifika mahali nikajikuta nacheka.
"Kumbe mwoga," nilijisemea moyoni.

Nilirudi ndani kwani kuna mteja aliingia akitaka katoni ya sabuni ya kufulia. Wakati nampa, aliingia mtoto mmoja akitaka nimuuzie sindano za kushonea ishirini.
"Unasema?" Nilimuuliza kwa mshtuko. Hata yule mteja pia alishangaa.
"Wewe, sindano zote hizo za nini?" Mteja alimuuliza.
"Si za kushonea…"
Mimi nikasikia sauti ya upole ikiniambia.

"Shtuka kijana, usikubali kumuuzia."
Nilimalizana na yule mteja wa kutaka sabuni, alipoondoka nikamgeukia yule mtoto.
"Enhe, amekutuma nani?"

"Ah! Unamtakia nini?" Aliniuliza na yeye.
Kimyakimya niliinua mguu mmoja juu, nikaupiga chini.
"Nakuuliza ili nikuuzie, au hutaki tena?"


Je, nini kitaendelea? Kesho....
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-6


Na hapa nataka kusema jambo, sitaki kuitaja jina siku, lakini katika siku saba za wiki, kuna siku mbili, watu wengi wanakwenda huko, iwe kwa kupelekwa au kujipeleka. Lakini wengi huenda huko. Ukitaka kuamini, fuatilia, utakuta katika kila wiki, hizo siku mbili watu huwa wachache sana mijini, hata foleni za magari si kubwa na kunakuwa hakuna shida sana ya usafiri.

Siku moja ipo mwanzomwanzo mwa juma, nyingine mwishomwisho mwa juma. Kazi kwako kuzijua siku hizo mbili.
Wakati tunapita mbele, yule Mkuu akasema:



Bila shaka siku hizi ni Jumapili na Juma tatu. Maana zina tabia hiyo....


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-10

ILIPOISHIA

Ilifika mahali kile kivuli kikasimama na yule mtoto aliponiona nimekazia macho nje, naye akageuka huku akiniuliza.
"Unashangaa nini?"
"Wewe unaona nini?"

"Sioni kitu," alinijibu kwa ujasiri japo ni mtoto.
Kwa kukiangalia kivuli, nilibaini kuwa, licha ya kusimama, huyo mtu mwenye kivuli alikuwa akicheza kwa kunesanesa kulia na kushoto, wakati mwingine akiinua juu mguu mmoja baada ya mwingine.

Mara alisimama na kuchezacheza kwa kukata kiuno.
Nilichoamua, nilitoka ili kumshuhudia mtu huyo kwa mwili wake kabisa badala ya kivuli.
ENDELEA SASA…


"Naweza kusema ilikuwa kitu cha ajabu sana kwa macho yangu kwani badala ya kumwona mtu kama nilivyoona kivuli chake, sikuona kitu chochote kila na badala yake yule jirani yangu alikuwa amesimama nje ya duka lake.

Niligeuza kurudi ndani, lakini ajabu nyingine yule mtoto sikumwona, nikamsaka ndani kote hakuwepo. Nilistaajabu sana.
Ili kuweka mambo sawa, niliamua kujiweka sawasawa na mimi. Nikasimama katikati ya duka, nikatumbua macho pima, nayo yakatoka mbele sana kiasi cha nusu futi, nikayashika polepole kisha nikayarudisha ndani, nikanyanyua mkono kama askari anayepiga saluti.

Pale pale nikawa si mimi tena, nilipata nguvu ya ajabu ya uchawi, nikatoka nje, nikatembea hadi nje ya duka la yule mtu, nikasimama kumwangalia kwa kumtumbulia macho tena. Nikayatoa mbele umbali wa futi moja nzima huku nikiyashikilia.

Safari hii yeye hakuwa na ubavu wowote wa kuniona wala kutambua kuwa, kuna mchawi amesimama mbele yake. Nilipeleka mguu mmoja wa kushoto mbele, kisha nikapeleka wa kulia na kuingia ndani.
Hapa nataka kusema kitu, mara zote mchawi anapotaka kutembea huanza na mguu wa kushoto ilimradi kwenda kinyume na utaratibu mwingine uliozoeleweka na pia kutimiza amri za Mkuu wa Wachawi Duniani ambaye ni Shetani Mkuu, Lusifa.

Hata wewe binadamu wa kawaida, unapotaka kutembea ukaanza na mguu wa kushoto hukawii kujikwaa, hata ukifuatilia kuanzia sasa, wengi wanaojikwaa walipoanza kutembea walianza na mguu huo.

Basi, niliingia ndani ya lile duka, nikapita nyuma yake na kusimama sambamba na bidhaa zake. Yeye akiwa hajui lolote, akatoka na kusimama mlangoni akikata shingo kulia kuangalia kwangu bila kujua kuwa, nilikuwa ndani ya duka lake.
Nilichofanya sasa, nilichukua bidhaa moja moja na kunipitisha kwenye makalio yangu mfano wa kutawaza.

Hapa pia naomba niweke wazi jambo moja, mara zote ukiona mtu anamiliki duka, lakini wateja hawatokei, au wateja wanatokea wanaulizia bidhaa, wanaomba kuziona kwa kuzishika tu kisha wanarudisha tambua kuwa, bidhaa hizo zimetawaziwa na mchawi. Kwa hiyo kila mnunuzi anaiona bidhaa hiyo kama kinyesi tu.

Basi, nilifanya hivyo kwa muda mrefu, miongoni mwa bidhaa nilizozitawazia ni pamoja na maboksi ya biskuti, dawa za meno, vocha za simu nakadhalika.
Kuna wakati baadhi ya wateja walikuja pale na kumuuliza:
"Huyu bwana yuko wapi?"

"Sijui," alijibu yule mwenye duka jirani yangu wakati mimi naendelea kutawazia bidhaa zake.
Nilipojiridhisha, nilitoka kwa mwendo ule ule wa kutupa hatua ndefu mbele. Wakati wote huo macho yangu yalikuwa mbele kama nilivyokwisha yatoa.

Nilipofika dukani kwangu, nilijirejesha kama kawaida na kuendelea kuuza huku wateja wengi wakiwa wanakuja na kununua huku wakimkwepa mwenzangu.

Baada ya miezi tisa tu, duka la jirani yangu likafungwa kwani bidhaa nyingi zilipoteza sifa ya kuuzwa (expire) na kuzitupa. Nilisikia baadaye kwamba, aliamua kwenda kufanya biashara ya samaki Ukerewe.
***
Baada ya mwaka mmoja kupita, kwa kutumia uchawi wangu niliweza hata kuua watu mbalimbali, wakiwemo ndugu zangu ili biashara zangu zikuwe na pia nilikuwa nakutana na wachawi wenzangu kwa ajili ya kufanya maangamizi katika jamii.

Siku moja, usiku wa saa saba, nikiwa nimelala na mke wangu kitandani, nilisikia mlio wa ndege, nikashtuka na kukaa kitandani. Mara ule mlio ukasikika chumbani, lakini hakuonekana ndege.
Nilipeleka mkono kwa mke wangu ili nimwamshe, lakini kabla sijamgusa, nikajikuta mkono umenata.
"Usithubutu kufanya hivyo," ilisema sauti bila kutokea kokote.

Niliacha kushangaa kwani nilijua nini kinaendelea sasa.
"Kuanzia leo, utakuwa Kiongozi Mkuu wa Wachawi Kitaifa. Majukumu yako utaambiwa utakapokuwa umelala," sauti ile ilisema, ikakatika kisha mlio wa ndege ukasikika na kupotea.

Nilirudia kulala, nikiwa usingizini nikaota ndoto. Nilikuwa kwenye chumba kikubwa mfano wa shule, lakini sikuwa peke yangu. Mwalimu aliyesimama mbele yetu alikuwa yule dada Sekretari wa kule dunia nyingine tulipokwenda. Alikuwa akisema:
"…pia kila mmoja ambaye ni kiongozi kwenye nchi yake atakuwa akihakikisha hakosi kwenye semina za kimataifa, kuhudhuria mikutano ya kuangamiza afya na mafunzo ya kuhujumu ndoa zilizoshibana.

"Kila mwakilishi atapewa barua ya mwaliko kupitia njia yoyote ile, lakini muhimu kuhudhuria ili kuifanya nchi yako kuwa mbele kimaendeleo katika sekta hii ya uchawi.

"Mikutano mikubwa ya kanda itakuwa ikifanyika katika nchi husika, kwa kanda na mabara ya ulimwengu na nchi itakayokuwa mwenyeji itawajibika katika kubeba mzigo wa maandalizi kwa maradhi, chakula na usafiri kwa wajumbe watakaohudhuria."

Je, nini kitaendelea? Usikose Kesho...
 
Kwenye hiyo mikutano yao wanaongeaga lugha ganiii
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-11

ILIPOISHIA JANA
Barua kubwa ilidondoka chini katikati ya wachawi wote, mmoja akataka kuishika, nikamkataza asifanye hivyo. Niliifuata mimi na kuiokota huku nikisema maneno ambayo, kama barua ile ingekuwa na madhara nisingedhurika.

Nilipoiweka mikononi niliifungua na kukutana na maneno yaliyoandikwa kwa biki nyekundu yakisomeka hivi:

"Kwa Mkuu wa wachawi upande wa taifa kuu, unatakiwa kuhudhuria mkutano maalum wa dharura utakaofanyika nchini Indonesia Juni 5. Maandalizi yote kule tayari.

Lengo la mkutano huo wa dharura ni kupanga mkakati wa kupandikiza roho ya chuki kati ya viongozi na wananchi ili kuweza kuleta machafuko zaidi duniani kote. Kufika kwako ni muhimu kuliko kutokufika."
SASA ENDELEA


"Kusema ule ukweli nilishtuka sana japo nilijua ni barua iliyonilenga mimi moja kwa moja kwa sababu nilishataarifiwa mapema."

Lakini wakati nikifikiria mambo yatakavyokuwa, mara nikasikia sauti ikisema:
"Usafiri wako utakuwa unauamrisha, utataja nchi unayokwenda na mkutano unaohudhuria, utafikishwa hapo. Kwa sasa funga mkutano wako hapo waache wanakundi wakalale."

Nilitii, niliwaambia wenzangu wakalale, lakini nikiwa nimemwachia madaraka mzee mmoja ambaye kabla ya kutawanyika alisimama mbele yangu nikamwapisha.
Nikiwa nyumbani usiku huo, nikawaza jinsi ya kuondoka kwani Juni 5 ilikuwa usiku huo huo kuelekea Juni 6 ya mwaka huo.

Kama kawaida, nilitoka kitandani ikiwa ni dakika ishirini tu baada ya kurudi. Nikatumia mbinu ile ile ya kulaza kinu kitandani ili mke wangu anaposhtuka ajue nipo. Lakini hata hivyo, yeye nilimfanyia mazingaombwe ya kumlaza kwa muda mrefu.

Nilisimama katikati ya chumba, nikafunga miguu kama askari wa usalama wa raia.
Nikafumba macho nikisema:
"Hii ni safari ya kwenda Indonesia kwenye mkutano wa dharura wa kimataifa wa wachawi, nataka nifike huko."

Kufumba na kufumbua nilijikuta nipo nyuma ya nyumba, nikashangaa.
"Ina maana mpaka leo hujui kuwa, ungo ndiyo (ndege) yako?" Niliulizwa swali hilo na sauti ya mtu nisiyemwona. Nikakumbuka ungo nilishautumia mara moja, hata na usukani wake upo na pia tanki la mafuta lipo tena niliyaacha ya kutosha tu.

Nilisimama wima, nikanyoosha mkono wa kulia mbele na kufumbua kiganja. Niliita ungo, ukaja mkononi, nikauweka chini. Nikaita usukani ambao ni shanga za kike zinazovaliwa kiunoni.

Naomba hapa kabla sijaendelea niweke wazi kitu kimoja. Shanga au wengi siku hizi huita chachandu, ni kitu kikubwa sana ambacho wengi hawakifahamu.
Kumekuwa na tabia ya wanawake kuvaa chachandu kwa idadi yoyote bila kujua ni hatari au ni salama.

Wachawi wanavyojua, asili ya wanawake kuvaa chachandu ilikuwa kuwakinga na utasa au wale ambao tayari ni tasa kuwatibu, sasa ilitegemea idadi ya shanga.

Ilikuwa ukimwona mwanamke amevaa chachandu tatu, ina maanisha anakinga kupata utasa, akivaa hadi tisa jua anatibu utasa.

Siku hizi wanawake wanavaa kwa sababu ni mtindo bila kujua zina madhara na wengi wamejikuta wakijifunga na uzazi kwa sababu wanavaa idadi kubwa ya shanga kama mtindo. Sasa badala ya kutibu wanajikuta wanajiharibu kwa sababu hawahitaji tiba.

Na shangaa ilivyo, haivaliwi kwa pacha hata siku moja. Yaani, mbili, nne, sita, nane, kumi, hapana! Shanga huvaliwa moja, tatu, tano, saba, tisa, kumi na moja na kuendelea hivyo.
Basi, naomba niendelee. Chachandu nazo zilikuja, kikaja kibuyu cheusi ambacho ni kwa ajili ya mafuta sasa.

Nilipojiamini kuwa, kila kitu tayari kwa safari, nilipanda ndani ya ungo, nikajivua ubinadamu na kukanyaga kile kibuyu kisha nikazishika shanga na kuanza kupaa kwa kasi ya ajabu.
Anga usiku ule lilikuwa la ajabu sana. Kwani uzito haukuwa wa kawaida, kila baada ya dakika moja, ungo wangu ulitetemeka kuashiria kuwa, nilikuwa napita sehemu mbaya.

Ninaposema sehemu mbaya kwa wachawi ni pale ambapo chini kuna majumba makubwa ya kuabudia au kuna mkusanyiko wa watu wanaosali au kumwomba Mungu, hasa wale wenye kujifanya wanakemea mapepo wachafu, ogopa sana wale.

Kuna eneo niliona ungo unalemewa kiasi cha kutaka kupinduka, lakini unga unga mweupe niliojipaka kabla sijaanza safari uliokoa ajali kama nne.

Sikumbuki ni dakika ngapi nilichukua angani, lakini mara nikaona natua kwenye uwanja mkubwa ajabu. Nyungo nyingi zilikuwa pembeni mwa uwanja huo wenye mwanga wa taa lakini hakuna taa iliyokuwa inaonekana kwa macho.

Nilipotua chini tu, mtu mmoja alisimama mbele yangu na kupunga mkono wa kulia juu kama vile wanavyofanya askari wa Usalama Barabarani. Nikawa namfuata polepole mpaka pembeni ya barabara, akanionesha sehemu ya kuegesha ungo wangu.

Niliuweka pale na kushuka ambapo nilipokelewa na watu wawili lakini waupe, waliovaa kama mimi, yaani nguo nyeusi (kaniki) ya kukata lubega nao walikuwa wamejichafua mwili mzima kwa masinzi. Chini walikuwa pekupeku.

"Kutoka?" Mmoja wao akiwa ameshika vikadi' vingi vilivyoandikwa mambo mbalimbali ambayo haikuwa rahisi kusoma kwa hatua za mbali ingizingatiwa kwamba, ilikuwa usiku.
"Tanzania," nilijibu nikiwaangalia kwa umakini wa hali ya juu.

"Ooo, Taifa Kuu TZN," alisema yule mwenye vikadi huku akinipa kikadi chenye kamba na kuniambia nivae shingoni na ile sehemu yenye maandishi iwe mbele wazi, nikafanya hivyo.
Nilichukuliwa hadi nje ya uwanja ambako kulikuwa na giza nene na la ajabu.


Je, nini kitaendelea? Usikose Kesho
 
Back
Top Bottom