Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,742
- Thread starter
- #101
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-23
"Kwa maelezo yako, huko Nchi ya Wachawi wanajua usahihi wa jambo unaotakiwa kuwepo ni upi ila wao kazi yao kubwa ni kupotosha, si ndiyo?"
"Hawapotoshi, bali wanapambana na utaratibu sahihi wa Mungu."
Nikamsimamisha mwingine ambaye aliuliza:
"Kumbe kama ni hivyo hakuna haja ya kuwa wachawi maana tunakubaliana kuwa, tunaunga mkono wale wanaompiga Mungu ambapo siku ya mwisho, tutakwenda motoni."
Wakati huyu mchawi akiongea hivyo, upepo mkali ulitokea ukampaisha angani.
ENDELEA MWENYEWE
Tulibaki tumemtumbulia macho kule alikokuwa akielekea, lakini sekunde chache baadaye hatukuweza kumwona tena.
"Jamani mwenzetu ametoweka!" Mzee mmoja alisema kwa sauti yenye mshtuko.
Wengine hawakusema lakini walibaki wameshika midomo kwa mshtuko uliowapata. Hakuna aliyejua nini kimetokea, ingawa ukweli ni kwamba, utowekaji wa yule mchawi mwenzetu ulitokana na maneno yake, hasa kuonesha mbele ya watu kwamba, anapingana na kitendo cha wachawi kumwabudu shetani wakati siku ya mwisho watakwenda motoni.
Kauli yake ilionesha kuwa, kumbe shetani hana nguvu kubwa kumpita Mungu, ingawa ukweli ni huo lakini siku zote mamlaka za kuzimu hutaka zionekane kuwa, zenyewe zina nguvu kubwa kuliko utawala wa Mungu juu ya ardhi.
Hili nalithibitisha hivi; Hata enzi za mapambano ya Mtawala wa Misri, Farao na Mtumishi wa Mungu, Musa, utawala wa kuzimu ulikuwa ukionesha nguvu zake hadharani, lakini Mamlaka ya Mungu ikawa inashinda kwa kishindo.
Basi, niliinua mkono wa kushoto juu ili kuwaweka sawa wachawi wote waliokuwa pale ambao walionekana kushtuka kwa tukio lile.
"Tulieni jamani," nilisema kwa sauti yenye mamlaka.
Wote wakatulia na kuniangalia, lakini wapo baadhi ya wachawi waliendelea kugeukageuka kuangalia ule upande ambao mwenzao alitowokea.
"Naomba macho yote yawe kwangu," nilisisitiza.
Nikaanza kwa kusema: "Kwanza napenda kusema lililotokea si tukio la kawaida wala la kupuuzia, kwani mpaka sasa mwenzetu si wetu tena."
Watu wote wakashtuka kwa kusema: "Haaa! Jamani."
"Ukweli ni huo. Na kwa uzoefu wangu yule amepelekwa mamlaka za kuzimu.
"Haaaa! Woyeee, tumekwisha sasa," walisema kila mmoja kivyake na kusababisha hali fulani isiyo na utaratibu.
Mara sauti nzito, sauti yenye mtetemesho ilisikika ikisema:
"Kila aliye hapa amekula kiapo cha kutumika kwenye mamlaka ya kuzimu. Hivyo, kwenda kinyume na kiapo ni sawa na usaliti. Na sisi katika utawala wetu msaliti ana adhabu moja tu, ni kutangulia kwenye ziwa la moto."
Wakati hayo yakisemwa, wachawi walianguka chini kwenye udongo kasoro mimi ambaye nilishatoka kushuhudia mazito zaidi ya yale.
Kufuatia tukio hilo la wachawi kulala chini, aliyekuwa akitoa ile sauti alijitokeza mbele yangu na kusimama sanjari na mimi.
Alikuwa mrefu wa wastani, mweusi tii. Pua yake ilichongokea mbele na kuwa kama ndizi, katikati ya paji la uso alikuwa na kipande cha pembe kikiwa kimekatika kwa mbele.
Na kila alipokuwa akinisemesha, kinywani alitoa cheche za moto huku zikianguka chini na kuzimika.
"Hakikisha hili lililotokea hapa leo halijitokezi tena. Sisi tuna uwezo wa kuwasikia wanadamu wanavyosema sehemu yoyote kwani dunia ni mali yetu."
Niliitikia kwa kutingisha kichwa, halafu akakunja sura na kusema:
"Yule mzee uliyempa tama ya kulala na binti yake mkubwa hukumfanyia haki. Yule ni mwenzako, sasa tatizo lilikuwa wapi. Ulikingwa na cheo chako, lakini kama si hivyo na wewe ungerudi tena kule kule lakini safari hii si kwa mema."
Nilishtuka kusikia maneno hayo, nikajikuta nikianguka ghafla na kupoteza fahamu.
Sikumbuki ni muda gani aliondoka, ila nilipokuja kuzinduka nilijikuta nimesimama haraka kama vile sikupenda wachawi wenzangu wajue kwamba nilianguka.
Na wao hakuna kati yao aliyekuwa anajitambua na walikuwa wamelala kule na huku kama watu waliokunywa sumu katika mlo wa pamoja.
"Inukeni," nilisema kwa sauti ya juu, na yenye mamlaka.
Wote walisimama, karibu wote wakawa wanajipukuta vumbi kutokana na kulala chini.
"Leo nimeambiwa mambo makubwa sana hapa. Kwa hiyo nitakuwa mkali na makini. Kama mtu hataki kuwa mchawi ni kwanini aliapa kutumikia?" Nilihoji nikiwaangalia kama kuna mwenye hoja.
Mzee mmoja akanyoosha mkono.
"Ndiyo, unasemaje?"
"Ukifuatilia kwa undani tatizo lililompata mwenzetu lilisababishwa na maneno yako na wala si ufahamu wake."
"Maneno yangu? Maneno gani hayo?"
"Kumbuka ulichokuwa unataumbia kuhusu huko ulikokwenda?"
Huyu naye wakati akisema hayo, upepo ule ule ulivuma tena kwa sekunde kadhaa huku wote tukimwangalia yule mzee ili kujua kama atatwaliwa au la.
"Jamani jamani jamani ee," alipiga kelele.
Je, nini kilitokea hapo? Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua Kesho...