hii hadithi inaonekana itakuwa tamu sana mbeleni
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI -1
![]()
![]()
Picha za Juu mfano wa picha za bunduki za kichawi.
Kwa jina naitwa Israeli, lakini si yule mtoa roho za watu, hili ni jina ambalo linapatikana katika utaratibu wa maisha ya kila siku duniani.
Nimezaliwa mwaka 1950, (kwa sasa 2010 ana miaka 60) wilayani Misungwi, mkoani Mwanza, ni mtoto wa kwanza katika familia yenye kujiweza kidogo kimaisha, ikiwa na watoto tisa, wote wanaume. Wazazi wangu (sasa marehemu) walikuwa wacha Mungu sana.
Kama kweli kuna uhai baada ya kifo na wakayajua mambo yangu ya duniani, naamini nimewaumiza sana wazazi wangu.
Kwa sasa naishi Mbagala, jijini Dar es Salaam na familia yangu yenye mke na watoto saba, wote wa kike. Mke wangu pia kwao ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto tisa, wote wanawake.
Nimelazimika kusimulia mkasa huu wa kichawi baada ya watu wengi kusimulia mikasa yao wakidai waliwahi kuwa wachawi wakaacha kwa sababu mbalimbali ambazo wengine huzisema, wengine hufanya siri kubwa.
Naweza kusema kwamba, karibu wote waliokuwa wakisimulia maisha yao ya kichawi na mikasa yake, hakuna hata mmoja aliyewahi kufikia hata robo ya maisha ya kichawi ya kwangu.
Mimi niliishi maisha hayo kwa miaka kumi, na nilifika levo ya mbali, mfano kuwa Mkuu wa Kikundi na kusafiri sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya mikutano mikubwa ya kimataifa ya wachawi.
Niliporudi, nilikuwa nakutana na wachawi wakubwa wa hapa nyumbani Tanzania na kuwapa maagizo ya utendaji katika makundi yao sehemu mbalimbali za nchi.
Katika kipindi chote cha kuwa mchawi nilibaini mambo makubwa mawili, kwamba, maisha ya wachawi katika ulimwengu wao hayana tofauti yoyote na maisha ya watu wasio wachawi katika ulimwengu huu wa macho ya kawaida.
Maandiko yanaposema kuwa, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana ni kweli kabisa. Wachawi wanaamini kwamba, vitu visivyoonekana pia vilikuwa na siku sita katika uumbaji wa Mungu, siku ya saba akapumzika.
Na hiyo ndiyo sera ya mchawi mara tu baada ya kujiunga katika kazi hiyo inayolaaniwa na wengi ulimwenguni kote.
Kabla sijaenda mbele zaidi nataka kusema kuwa, kama kuna shughuli mbalimbali za binadamu zinazoonekana kwa macho ya kawaida duniani, pia kuna shughuli kama hizo hizo zisizoonekana kwa macho ya kawaida, lakini zinashirikisha wachawi na mambo yao.
Itaendelea Mukinipa (Like) Kazi kwenu .......
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-6
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Huyu msichana naye alikuwa binadamu kwa asilimia zilezile kwani hata yeye alikuwa kama yule mwanamke, pengine tofauti kubwa ilikuwa kwenye umri tu na mavazi.
Yeye alivaa sketi ya kimini, miguu, yaani makanyagio ni kwato za ngombe, juu alivaa kikoti kinachofanana na sketi, au niseme alivaa suti.
Kukosa kuwa na pembe ya katikati ya paji la uso na weusi tii, angekuwa msichana mzuri mfano hakuna. Alipotabasamu, meno tu ndiyo yalionekana, kwani yalikuwa meupe sana.
Mzee wangu, sidhani kama nitaweza kuvumilia kuwepo eneo hili ambalo linatisha, nilimwambia mzee Madume.
Hapana, hatua uliyofikia ni nzuri sana kijana wangu, kuwa mvumilivu tu, alisema yule mzee.
Mle ndani, mlikuwa na watu wengi sana wakionekana kama sisi, nao walikuwa na shida kama sisi.
Ghafla, yule msichana alisimama na kusema:
SASA ENDELEA
Karibuni sana ndugu, jamaa na marafiki zetu. Kwa wale wageni kabisa, sasa mko katika taifa linalojitegemea kwa kila kitu, nina maana kwa raia wake, utawala wake na hata sayari yake. Wote mliofika humu, hakuna uhusiano wowote kati ya duniani na huku, hivyo kama una wasiwasi jisikie una amani na uko huru.
Alipomaliza kusema hivyo, alitoka kwenye lile eneo lake akiwa ameshika kitu kama faili, akatembea kwa kuliza mlio kama wa viatu ambapo baadaye nikaja gundua kuwa, naye alikuwa na kwato kama za ngombe badala ya miguu ya binadamu.
Ko ko ko ko! Ndivyo mlio wake ulivyosikika, akazama sehemu. Pale kwenye meza yake pakabaki tupu.
Ukimya uliotawala baada ya yule msichana kuondoka hakuna mfano wake. Ilikuwa kama tumemwagiwa maji ya baridi kwenye msimu wa baridi.
Nilimsogelea yule mwenyeji wangu, mzee Madume na kumuuliza:
Sasa huku mwanga unatoka wapi, maana hakuna jua.
Tusikilizane mara moja jamani, yule msichana alirejea akiwa ameongozana na mwanaume mmoja, mnene sana. Mweusi sana. Meno yote nje, katikati ya paji la uso ana pembe la ngombe, si kwamba ameipachika, bali imeotea hapo. Kwa kweli alikuwa anatisha sana, sana!
Yule msichana ambaye mimi naweza kusema ni katibu Muhtasi au Sekretari wa kule.
Huyu ni msaidizi wa Mkuu wa taifa hili, yeye ndiye mwenye ujumbe wa kutoka kwa Mkuu mwenyewe, anayo ya kusema. Namwachia yeye sasa.
Alipomaliza kusema, aliinama kidogo kama ishara ya utii kwa mkubwa wake, kisha akainua shingo kuwa kama kawaida.
Kulisikika mkoromo kama wa spika ambayo ina matatizo. Lakini spika haikuwepo wala dalili za waya.
Santeni sana, santeni sana, ndivyo alivyoanza kusema, badala ya asanteni akasema santeni.
Akaendelea: Mimi ni mtoa maagizo tu, lakini mwenyewe atafuatia muda kidogo. Kuna wale waliokuja toka duniani kwa lengo la kuwa matajiri, waende kule, alisema akinyoosha kidole mahali ambapo alitaka watu hao waende.
Mimi nilianza kusimama, lakini mzee Madume akanishika shati na kunikalisha chini vilevile kama mwanzo.
We huhusiki, alisema, akanishangaza sana, kwani maongezi yetu toka mwanzo ni mimi kuwa tajiri, yaani kupata pesa nyingi kupitia biashara ya uvuvi wa samaki.
Khaaa! Nilimshangaa sana kwa kukoroma.
Unashangaa nini, si nimekwambia bado.
Sawa mzee.
Haya, wale waliokuja ili wawaue wabaya wao waende pale, yule mtu aliendelea kusema.
Watu wakatoka kwenda sehemu iliyoelekezwa, kundi hili lilinishangaza sana, lilikuwa na watu wengi sana.
Oke, santeni sana. Santeni sana. Wale waliokuja wakitaka kuutawala uchawi watoke huku, waje nyuma yangu.
Mzee Madume alinishika mkono na kunivuta kwa nguvu, nikataka kukataa, lakini akanizidi nguvu.
Wakati huo, bado watu walikuwa wanaingia kwa wingi toka duniani kiasi kwamba, niliamini kuwa, kuna wakati dunia inakosa watu, kwani wengi wanakuwa wamekwenda huko.
Na hapa nataka kusema jambo, sitaki kuitaja jina siku, lakini katika siku saba za wiki, kuna siku mbili, watu wengi wanakwenda huko, iwe kwa kupelekwa au kujipeleka. Lakini wengi huenda huko. Ukitaka kuamini, fuatilia, utakuta katika kila wiki, hizo siku mbili watu huwa wachache sana mijini, hata foleni za magari si kubwa na kunakuwa hakuna shida sana ya usafiri.
Siku moja ipo mwanzomwanzo mwa juma, nyingine mwishomwisho mwa juma. Kazi kwako kuzijua siku hizo mbili.
Wakati tunapita mbele, yule Mkuu akasema:
Nyiye wengine mngejua kwamba, hakuna kundi zuri kama la wale wanaotaka kuutawala uchawi, naamini wote mngetaka kundi hili. Lakini si mbaya, santeni. Santeni sana. Aligeuka, akaondoka akimwacha yule msichana pale. Naye akaendelea:
Haya, kundi la kwanza mkaingie chumba namba tatu, kundi la pili, chumba namba moja, na kundi la tatu, chumba namba mbili.
Alipomaliza kusema akawa anayaangalia makundi yote kama anataka kuhakikisha kwanza maagizo yake yanatekelezwa au la.
Ilikuwa ni miingiliano, watu wa kundi hili wakienda kundi lile, wa kundi lile wakija huku, ili mradi tu.
Kulipotulia, mimi na yule mzee tulikuwa ndani ya chumba tulichotakiwa kuwepo.
Kilikuwa chumba kikubwa sana, umbali wa kutoka chini hadi juu darini ni kama umbali wa uwanja wa mpira toka goli moja hadi jingine.
Mapana yake, kama viwanja vitano vya mpira na bado tulibanana kwa sana tu.
Mwanga ulikuwa hafifu sana kiasi kwamba, haikuwa rahisi kumtambua wa mbele yako kwa umbali wa mita kumi.
Kwa mbali ilikuwa kama kuna AC kwa ajili ya kuweka hewa ya baridi badala ya joto, mlio wa AC ulisikika kwa mbali sana, lakini kila nilipojaribu kuchunguza huku na kule, sikuona AC wala dalili zake.
Mambo niliyoyaona katika chumba hicho yalinishangaza sana, nilitamani kumwuliza mwenyeji wangu kuhusu mahala pale nikasita.
Nikiwa nipo katika hali hiyo, ghafla mwanga mkubwa sana ukamulika kote, lakini bila kuwepo kwa taa, wala mishumaa, wala mlio wa Jenereta, nikazidi kupigwa butwaa.
Je, nini kitaendelea? Usikose kesho......
Kma kawaida ikinoga utuache hewani...
umenikosha sana mtu wangu kwanzia mwanzo hadi mwisho ila kama inawezekana weka vipengele viwili viwili.HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-6
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Huyu msichana naye alikuwa binadamu kwa asilimia zilezile kwani hata yeye alikuwa kama yule mwanamke, pengine tofauti kubwa ilikuwa kwenye umri tu na mavazi.
Yeye alivaa sketi ya kimini, miguu, yaani makanyagio ni kwato za ng'ombe, juu alivaa kikoti kinachofanana na sketi, au niseme alivaa suti.
Kukosa kuwa na pembe ya katikati ya paji la uso na weusi tii, angekuwa msichana mzuri mfano hakuna. Alipotabasamu, meno tu ndiyo yalionekana, kwani yalikuwa meupe sana.
"Mzee wangu, sidhani kama nitaweza kuvumilia kuwepo eneo hili ambalo linatisha," nilimwambia mzee Madume.
"Hapana, hatua uliyofikia ni nzuri sana kijana wangu, kuwa mvumilivu tu," alisema yule mzee.
Mle ndani, mlikuwa na watu wengi sana wakionekana kama sisi, nao walikuwa na shida kama sisi.
Ghafla, yule msichana alisimama na kusema:
SASA ENDELEA…
"Karibuni sana ndugu, jamaa na marafiki zetu. Kwa wale wageni kabisa, sasa mko katika taifa linalojitegemea kwa kila kitu, nina maana kwa raia wake, utawala wake na hata sayari yake. Wote mliofika humu, hakuna uhusiano wowote kati ya duniani na huku, hivyo kama una wasiwasi jisikie una amani na uko huru."
Alipomaliza kusema hivyo, alitoka kwenye lile eneo lake akiwa ameshika kitu kama faili, akatembea kwa kuliza mlio kama wa viatu ambapo baadaye nikaja gundua kuwa, naye alikuwa na kwato kama za ng'ombe badala ya miguu ya binadamu.
"Ko ko ko ko!" Ndivyo mlio wake ulivyosikika, akazama sehemu. Pale kwenye meza yake pakabaki tupu.
Ukimya uliotawala baada ya yule msichana kuondoka hakuna mfano wake. Ilikuwa kama tumemwagiwa maji ya baridi kwenye msimu wa baridi.
Nilimsogelea yule mwenyeji wangu, mzee Madume na kumuuliza:
"Sasa huku mwanga unatoka wapi, maana hakuna jua."
"Tusikilizane mara moja jamani," yule msichana alirejea akiwa ameongozana na mwanaume mmoja, mnene sana. Mweusi sana. Meno yote nje, katikati ya paji la uso ana pembe la ng'ombe, si kwamba ameipachika, bali imeotea hapo. Kwa kweli alikuwa anatisha sana, sana!
Yule msichana ambaye mimi naweza kusema ni katibu Muhtasi au Sekretari wa kule.
"Huyu ni msaidizi wa Mkuu wa taifa hili, yeye ndiye mwenye ujumbe wa kutoka kwa Mkuu mwenyewe, anayo ya kusema. Namwachia yeye sasa."
Alipomaliza kusema, aliinama kidogo kama ishara ya utii kwa mkubwa wake, kisha akainua shingo kuwa kama kawaida.
Kulisikika mkoromo kama wa spika ambayo ina matatizo. Lakini spika haikuwepo wala dalili za waya.
"Santeni sana, santeni sana," ndivyo alivyoanza kusema, badala ya ‘asanteni' akasema ‘santeni'.
Akaendelea: "Mimi ni mtoa maagizo tu, lakini mwenyewe atafuatia muda kidogo. Kuna wale waliokuja toka duniani kwa lengo la kuwa matajiri, waende kule," alisema akinyoosha kidole mahali ambapo alitaka watu hao waende.
Mimi nilianza kusimama, lakini mzee Madume akanishika shati na kunikalisha chini vilevile kama mwanzo.
"We huhusiki," alisema, akanishangaza sana, kwani maongezi yetu toka mwanzo ni mimi kuwa tajiri, yaani kupata pesa nyingi kupitia biashara ya uvuvi wa samaki.
"Khaaa!" Nilimshangaa sana kwa kukoroma.
"Unashangaa nini, si nimekwambia bado."
"Sawa mzee."
"Haya, wale waliokuja ili wawaue wabaya wao waende pale," yule mtu aliendelea kusema.
Watu wakatoka kwenda sehemu iliyoelekezwa, kundi hili lilinishangaza sana, lilikuwa na watu wengi sana.
"Oke, santeni sana. Santeni sana. Wale waliokuja wakitaka kuutawala uchawi watoke huku, waje nyuma yangu."
Mzee Madume alinishika mkono na kunivuta kwa nguvu, nikataka kukataa, lakini akanizidi nguvu.
Wakati huo, bado watu walikuwa wanaingia kwa wingi toka duniani kiasi kwamba, niliamini kuwa, kuna wakati dunia inakosa watu, kwani wengi wanakuwa wamekwenda huko.
Na hapa nataka kusema jambo, sitaki kuitaja jina siku, lakini katika siku saba za wiki, kuna siku mbili, watu wengi wanakwenda huko, iwe kwa kupelekwa au kujipeleka. Lakini wengi huenda huko. Ukitaka kuamini, fuatilia, utakuta katika kila wiki, hizo siku mbili watu huwa wachache sana mijini, hata foleni za magari si kubwa na kunakuwa hakuna shida sana ya usafiri.
Siku moja ipo mwanzomwanzo mwa juma, nyingine mwishomwisho mwa juma. Kazi kwako kuzijua siku hizo mbili.
Wakati tunapita mbele, yule Mkuu akasema:
"Nyiye wengine mngejua kwamba, hakuna kundi zuri kama la wale wanaotaka kuutawala uchawi, naamini wote mngetaka kundi hili. Lakini si mbaya, santeni. Santeni sana." Aligeuka, akaondoka akimwacha yule msichana pale. Naye akaendelea:
"Haya, kundi la kwanza mkaingie chumba namba tatu, kundi la pili, chumba namba moja, na kundi la tatu, chumba namba mbili."
Alipomaliza kusema akawa anayaangalia makundi yote kama anataka kuhakikisha kwanza maagizo yake yanatekelezwa au la.
Ilikuwa ni miingiliano, watu wa kundi hili wakienda kundi lile, wa kundi lile wakija huku, ili mradi tu.
Kulipotulia, mimi na yule mzee tulikuwa ndani ya chumba tulichotakiwa kuwepo.
Kilikuwa chumba kikubwa sana, umbali wa kutoka chini hadi juu darini ni kama umbali wa uwanja wa mpira toka goli moja hadi jingine.
Mapana yake, kama viwanja vitano vya mpira na bado tulibanana kwa sana tu.
Mwanga ulikuwa hafifu sana kiasi kwamba, haikuwa rahisi kumtambua wa mbele yako kwa umbali wa mita kumi.
Kwa mbali ilikuwa kama kuna AC kwa ajili ya kuweka hewa ya baridi badala ya joto, mlio wa AC ulisikika kwa mbali sana, lakini kila nilipojaribu kuchunguza huku na kule, sikuona AC wala dalili zake.
Mambo niliyoyaona katika chumba hicho yalinishangaza sana, nilitamani kumwuliza mwenyeji wangu kuhusu mahala pale nikasita.
Nikiwa nipo katika hali hiyo, ghafla mwanga mkubwa sana ukamulika kote, lakini bila kuwepo kwa taa, wala mishumaa, wala mlio wa Jenereta, nikazidi kupigwa butwaa.
Je, nini kitaendelea? Usikose kesho......
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-5
"Hapa tumefika," alisema yule mzee.
"Kwa hiyo kuna sehemu tunakwenda?"
"Hapana, tumefika."
"Ni wapi?" Nilimuuliza.
"We unahisi wapi?"
Niliangalia kulia, kushoto, juu na chini.
"Moshi?"
"Hapana."
"Iringa."
"Hapana."
"Basi, Dar es Salaam."
"Umekosea."
"Sasa wapi?"
"Hapa ni chini ya maji ziwa Victoria, kwa hiyo tumetoka juu tumekuja chini."
Nilishtuka sana.
ENDELEA MWENYEWE…
"Kwa hiyo kinachotakiwa hapa kijana wangu ni kuhakikisha kila kitu kinakubalika, usije ukapinga kitu cha huku, kinaweza kukuingiza matatizoni," mzee Madume aliniambia kwa sauti ya kunibembeleza sana kama vile alijua tabia yangu.
Kusema ukweli, karibu wavuvi wote walijua mimi ni mbishi na nisiyependa kushindwa na jambo lolote lile.
"Sawa, sawa," nilimjibu nikitikisa kichwa juu na chini.
Tukiwa bado tunashangaa wote, mara sauti kwa nyuma ilisikika.
"Mnataka kumwona nani?"
"Mkuu," alisema mzee Madume.
"Nifuateni," ilisema ile sauti ikiashiria kuondoka.
Mzee Madume alinishika mkono na kunivuta huku akiniambia.
"Twende inakosema hii sauti."
Nilitii, tuliifuata ile sauti kwa mtindo wa kuisikiliza.
"Hivi mzee, huku wewe ni mara yako ya kwanza kuja?" Nilimuuliza mzee Madume.
"Hapana, mara nyingi."
"Sasa watu wa huku hawaonekani kwanini?"
Kabla mzee Madume hajajibu, ile sauti ilimuwahi.
"Huku hakuna maswali, unataka kuona, unataka kumwona nani kwani?"
Nilibaki kimya, tukiendelea na safari.
Ghafla, baada ya umbali wa kama mita mia moja, nikaona jumba kubwa, jeupe mbele yetu, weupe wake ni kama bati linalopigwa na jua.
Nilipeleka mkono usoni ili kukinga ule mwanga kwani ulikuwa unanichoma sana usoni na kushindwa kuona sawasawa mbele licha ya kwamba, nilikuwa nimeshikwa mkono na yule mzee.
"Karibuni," ile sauti ilisema mbele yetu.
Kwa jinsi ya uzoefu wangu, ile sauti ilikuwa ikitafsrika kuwa, ni ya mwanamke mtu mzima, mnene sana, halafu mfupi sana, na tena alikuwa amefanya kazi ya kukaribisha wageni siku ile kwa muda mrefu kwa hiyo amechoka sana.
Wakati anasema karibuni sana, tulikuwa kwenye geti kubwa la chuma, jeusi na nondo ndefu sana. Kwa nje sikupata picha ya haraka kwamba, ndani kulikuwa na kitu gani.
Mlango ulianza kufunguka wenyewe na kuacha nafasi ya kutazamika kwa ndani.
Kulikuwa na nyumba kubwa sana ya ghorofa moja, nayo nyeupe ikiwa na madirisha ya vioo vizuri vyenye mapambo ya kuvutia, milango mbalimbali ya mti wa mninga.
"Sasa mnakaribishwa rasmi," ile sauti ilisema huku ghafla akionekana ni kiumbe kinachofanana na binadamu kwa asilimia sabini na tano.
Kwa maana gani? Kichwa kama cha binadamu, macho, masikio, pua, lakini tofauti yeye, kwenye paji la uso alikuwa na pembe kama la ng'ombe, fupi nene.
Halafu miguu yake, yaani makanyagio, yeye alikuwa na kwato za ng'ombe badala ya miguu hii ya kibinadamu.
Alivaa nguo kama binadamu, alikuwa mwanamke kweli, kama nilivyohisi, mnene, mfupi, tena mweusi tii. Alivaa gauni lililofika chini kidogo ya magoti, ndiyo maana niliweza kuona miguu kirahisi.
Sikujua haraka ni kwanini kote, tangu kutupokea hadi kufika pale alikuwa amejificha na kuachia sauti tu.
"Sawa, tunashukuru sana kwa msaada wako, sisi tunaendelea," alisema mzee Madume akimpa mkono yule mwanamke.
Mimi naye nilinyoosha mkono wangu ili kumpa, lakini wake akaurudisha nyuma kwa haraka kama mtu asiyependa kupeana mkono na wakati huo huo, mzee Madume naye aliubetua mkono wangu kama vile nilikuwa nafanya kosa kubwa sana kumpa yule kiumbe mkono.
"Huruhusiwi kwa sasa," alisema mzee Madume huku akihema kwa nguvu kama vile alikuwa ameokoa kitu cha hatari sana kwangu.
"Sawa, sawa," nilisema kwa aibu.
Yule kiumbe alianza kuondoka, akienda getini, mara alipovuka geti akapotea.
Mzee Madume alinishika mkono na kunivuta hadi kwenye mlango mmoja wa kioo ambao kwa juu uliandikwa MAPOKEZI VI lakini maandishi yake yaligueka miguu juu, kichwa chini. Ili usome kirahisi, ilikuwa lazima uwe kama unainamisha kichwa huku ukiyaangalia, naamini unapata picha.
Ilikuwa ni ofisi kubwa sana, yenye viti vingi vya sofa, vikiwa vimezunguka meza moja kubwa sana, ambayo ilikuwa na msichana aliyeonekana ndiye mwenyeji au kwa duniani ningesema ndiye Sekretari wa eneo lile.
Ukubwa wa eneo lile unalingana kabisa na ukubwa wa uwanja, yaani ukubwa wa mle ndani Mapokezi.
Huyu msichana naye alikuwa binadamu kwa asilimia zilezile kwani hata yeye alikuwa kama yule mwanamke, pengine tofauti kubwa ilikuwa kwenye umri tu na mavazi.
Yeye alivaa sketi ya kimini, miguu, yaani makanyagio ni kwato za ng'ombe, juu alivaa kikoti kinachofanana na sketi, au niseme alivaa suti.
Kukosa kuwa na pembe ya katikati ya paji la uso na weusi tii, angekuwa msichana mzuri mfano hakuna. Alipotabasamu, meno tu ndiyo yalionekana, kwani yalikuwa meupe sana.
"Mzee wangu, sidhani kama nitaweza kuvumilia kuwepo eneo hili ambalo linatisha," nilimwambia mzee Madume.
"Hapana, hatua uliyofikia ni nzuri sana kijana wangu, kuwa mvumilivu tu," alisema yule mzee.
Mle ndani, mlikuwa na watu wengi sana wakionekana kama sisi, nao walikuwa na shida kama sisi.
Ghafla, yule msichana alisimama na kusema:
Je, nini kitaendelea? Usikose Kesho...