Hadithi ya kusisimua: Nchi ya wachawi-1

Hadithi ya kusisimua: Nchi ya wachawi-1

HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YAWACHAWI-12

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Niliuweka pale na kushuka ambapo nilipokelewa na watu wawili lakini weupe, waliovaa kama mimi, yaani nguo nyeusi (kaniki) ya kukata lubega nao walikuwa wamejichafua mwili mzima kwa masizi. Chini walikuwa pekupeku.

Kutoka? Mmoja wao akiwa ameshika vikadi vingi vilivyoandikwa mambo mbalimbali ambayo haikuwa rahisi kusoma kwa hatua za mbali ikizingatiwa kwamba, ilikuwa usiku.
Tanzania, nilijibu nikiwaangalia kwa umakini wa hali ya juu.

Ooo, Taifa Kuu TZN, alisema yule mwenye vikadi huku akinipa kikadi chenye kamba na kuniambia nivae shingoni na ile sehemu yenye maandishi iwe mbele wazi, nikafanya hivyo.
Nilichukuliwa hadi nje ya uwanja ambako kulikuwa na giza nene na la ajabu.

ENDELEA MWENYEWE


Tembea kuelekea mbele hatua kumi na tano utakutana na ukumbi wa mikutano, aliniambia yule mtu.
Nilitii agizo lile kwa kutembea huku nikihesabu hatua moja baada ya nyingine, moja baada ya nyingine mpaka nilipofika hatua kumi na nne, ikiwa imebaki moja, ghafla nilijikuta nimetokea kwenye eneo lenye taa nyingi na majumba mbalimbali. Ni mji kabisa, kwani watu mbalimbali ambao hawafanani sana na binadamu walikuwa wakipitapita kila mmoja na hamsini zake.

Nilipokanyaga hatua ya kumi na tano, nikajikuta nimezungukwa na watu wengi wenye kufanana na wale walionipokea na wale waliokuwa wakiendelea na hamsini zao.
Basi, walinichangamkia sana huku wakiniuliza habari za nitokako.

Niliwajibu ni nzuri sana, mmoja wao akanishika mkono wa kushoto huku akiniambia nakaribishwa kuingia kwenye jumba la mikutano la nchi ya Mpingaji huku akisema sijachelewa sana kwani nusu ya wajumbe kutoka pande zote za dunia wameshafika, nusu bado.

Lakini ratiba ya mkutano inasema wakishafika robo tatu ya wajumbe wote, kikao kinafunguliwa, aliniambia yule mtu, au naweza kusema kiumbe kwani ni kama mtu lakini si kwa kufanana na sisi binadamu.

Nje ya jumba la mikutano kulikuwa na watu wa sampuli ile ile wakipiga ngoma na wengine kucheza kwa furaha.
Nje ya jumba, mlangoni kwa juu palikuwa na tambara kubwa jeusi, maandishi meupe yanayosomeka; Mkutano Mkuu wa Dunia wa Kujadili Mambo Mbalimbali. Karibuni nchi ya Mpingaji.

Pembeni ya tambala na maandishi kulikuwa na picha ya kichwa cha mtu, alionekana hadi usawa wa shingo tu. Masikio marefu mfano hakuna, naweza kusema yalipita kichwa kama ya Sungura. Macho ya pembe tatu, makubwa na mbaya au cha kutisha zaidi alikuwa na pembe moja kwenye paji la uso, midomo mirefu kama mdomo wa kibuyu. Tafsiri ya haraka ungeweza kusema ni mnyama na si binadamu.

Nilikazia macho zaidi chini ya ile picha kwani kulikuwa na maandishi. Nikasoma yakiwa yameandikwa; Mkuu wa Nchi ya Wachawi.

Mheshimiwa karibu sana, tuingie ndani, mtu mmoja miongoni mwa watu wale wa ajabu aliniambia akinielekeza kwa mkono mlango mkuu.

Niliingia ndani ya ukumbi ambapo nyuma ya mlango tu nilikutana na watu watano walionipokea na kunisindikiza sehemu ya kukaa.

Macho yangu yalistaajabu sana kuona ukumbi umepambwa kama inavyokuwa kwa kumbi za ninazozifahamu mimi. Kifupi ulipambwa kama kumbi za sherehe mbalimbali, ikiwemo harusi.

Ndaki ya ukumbi kulikuwa na meza kubwa moja na pana na kuna watu mchanganyiko walikaa kasoro viti vitatu vya katikati.

Ninaposema watu mchanganyiko walikaa maana yangu ni kuwa, kulikuwa na binadamu wa kawaida kama mimi. Pia kulikuwa na watu wa kule ambao kama nilivyosema, hawakuwa wamefanana na binadamu sisi.

Wale walionipokea walinielekeza hadi kwenye kiti kimoja kule mbele, lakini si kati ya vile viti vitatu vya katikati. Nilikaa kwenye kiti ambacho mbele yake kulikuwa na kibao kilichoandikwa; MWAKILISHI TAIFA LA TZ.

Nilipokaa tu, nikapewa maelekezo ya kutumia waya nyembamba headphone kwenye masikio endapo nitataka, lakini naweza nisitumie pia.

Mimi nilisema situmii, kwani sikupewa ufafanuzi zaidi wa madhara ya kutumia au faida zake.
Wageni waliendelea kuingia, wakati fulani waliingia kwa mpigo kama saba, wakapewa viti vya kukaa.

Lakini ikumbukwe pia kulikuwa na viti vilivyopangwa mbele ya meza kuu. Watu wengine walikuwa wanakwenda kukaa huko, wengine wakiwa na kamera, wengine na mabegi tu wengine mafaili na kalamu.
Nusu saa baadaye ukumbi wote ulikuwa umejaa, sauti ikasikika ikisema:

Sasa tunaomba utulivu kwani wakati wowote Mkuu atatokea ili kuanza kikao chetu.
Hii ilikuwa sauti isiyotoka kokote, yaani ilisikika tu, lakini msemaji hakuonekana licha ya kwamba alikuwa mwanamke kulingana na sauti.

Ukimya ulitawala, kilichokuwa kikisikika ni watu kukohoa au makaratasi kukaa vizuri, pengine na watu waliokuwa wakidondosha vitu mbalimbali.
Mara, mlango mmoja kulia kwa meza niliyokaa ulifunguliwa.

Ghafla ulitangulia mwanga mkali, halafu mlio wa viatu vya ngozi vilivyoashiria kuwa, visigino vyake vilikuwa, ama vya chuma au vya kitu kigumu sana kwani mlio ulisikika kwa sauti na pia kwa wingi kuonesha kuwa, hakuwa na mtu mmoja.
Mara, watu watatu walitokea, wawili wakiwa pembeni kwa yule mmoja ambaye ni wazi alikuwa ndiye Mkuu wa nchi ile ya Wachawi.

Mkono mmoja alishika kitu kama chupa au labda almasi kwani ilikuwa ikiwaka sana, mkono mwingine wa kushoto alishika chupa kubwa mfano wa zile za pombe kali kama za whisky.


Je, nini kitaendelea? Kesho usikonde........
 
brothher ulionana na lusifa uso kwa uso ?je watu wa dini uliwakuta huko kuzimu?
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-13

ILIPOISHIA
Mara, watu watatu walitokea, wawili wakiwa pembeni kwa yule mmoja ambaye ni wazi alikuwa ndiye Mkuu wa nchi ile ya Wachawi.
Mkono mmoja alishika kitu kama chupa au labda almasi kwani ilikuwa ikiwaka sana, mkono mwingine wa kushoto alishika chupa kubwa mfano wa zile za pombe kali kama za whisky.

Kila walipopita, mwanga ulitawala kuwazunguka mpaka wanafika kwenye viti vyao kukaa. Yule Mkuu alikaa kiti cha katikati kati ya vile vitatu, wale aliofuatana nao walikaa pembeni yake kulia na kushoto.
Nilijiuliza maswali mengi sana kwamba, ni kwanini Mkutano ule upo kama wa kimataifa wa duniani. Pia nilijiuliza kule ni wapi.

Mkuu wa nchi ndiyo ameingia, nashukuru wageni wote, naomba tukae. Ile sauti iliyotuambia tutulie ilisema kwani wakati Mkuu anaingia tulisimama wote.

Tukasikia mlio wa viatu ukitembea kutokea kusikojulikana kuelekea katikati ya ukumbi ambapo kulikuwa na mimbari ya kuhutubia.
SASA ENDELEA


Habari zenu mabibi na mabwana, leo tunafanya Mkutano wetu mkuu wa kimataifa hapa. Karibuni sana wageni waalikwa na wageni wa heshima, ilianza kusema ile sauti.

Pale pale nilibaini mambo mawili makubwa muhimu. Kwanza nilibaini kuwa, aliyekuwa akiongea ingawa hakuonekana sauti yake ilionesha ndiye alikuwa MC wa Mkutano ule. Pia nilibaini kwamba, kila mtu mle ndani alikuwa akimsikia MC kwa lugha yake mwenyewe. Yaani mimi nilimsikia kwa Kiswahili, Mwingereza naye alimsikia kwa Kiingereza, vivyo hivyo kwa Mfaransa, Mhindi na kadhalika.

Hapa pia nataka kusema kuwa, nilibaini utaratibu wa kidunia wa wajumbe wa mikutano kutumbukiza viwaya sikioni ili kuweza kusikia kinachoongelewa kilitokana na mfumo wa nchi hiyo.

Pia naomba niseme na nieleweke kuwa, ukumbi tuliokuwemo kulikuwa na watu wa rangi mbalimbali. Katika maisha yangu mpaka wakati huo nilikuwa sijawahi kumwona binadamu ana rangi ya njano, lakini siku hiyo niliwaona, tena wafupi sana. Baadaye niliambiwa kuwa, watu hao walitoka katika nchi iliyopo Kaskazini mwa dunia, inaitwa Visiwa vya Barafu (Iceland) mji wao mkuu unaitwa Reykjavik.

Nasema hivi kwa sababu kila mtu alipokaa, kulikuwa na kibao cha jina la nchi yake na mji mkuu, sasa sijui kama ilikuwa lazima iwe mji mkuu hata kama mjumbe alitokea mji mdogo. Mfano, mzee mmoja kama Mhindi, alikaa kwenye kibao kilichoandikwa Ulan Bator halafu mbele kukaandikwa jina la nchi, Mongolia. Mwingine kibao kiliandikwa Bangkok halafu jina la nchi Thailand.

Mimi mwenyewe jirani yangu alikaa mtu mweupe, yaani mzungu na kibao chake kiliandikwa Brussels mbele kukaandikwa Belgium (Ubelgiji).
Basi, mara ile sauti ikasema:

Naamini waalikwa wote mmekaa kila mmoja katika sehemu yake na kupata huduma zote, namwita kwenu msaidizi Mkuu wa nchi hii aongee na nyinyi kabla na yeye hajamkaribisha Kiongozi Mkuu wa Nchi ya Wachawi.

Lakini kitu cha kushtua kilijitokeza kwamba, wakati ile sauti inaendelea kuongea kutokea pale kwenye mimbari, ulianza kuonekana uso wake, baadaye shingo, yakafuata mabega na kumalizikia na tumbo huku sehemu za chini nazo zikianza kujitokeza.

Tukio hilo lilitufanya baadhi ya watu kumtumbulia macho mpaka alipomalizika kuonekana mwili mzima na kusimama kwa miguu miwili.

Alitembea taratibu akiacha kifaa cha kuongelea juu ya mimbari lakini wakati huo huo mtu mmoja kati ya wale waliokuwa na Mkuu wa Nchi alionekana kusimama na kuelekea mbele alikotoka yule MC.
Kwa sauti, MC ungeweza kusema ni msichana mrembo, mwenye sura ya mvuto na umbile la kumfanya atazamwe, lakini sivyo.

Alikuwa mzee wa kama miaka 75, ngozi ya uso wake imejikunja-jikunja, mbele alionekana ana meno mawili tu, masikio kama wenzake, marefu yaliyopita kichwa halafu alikuwa mweusi kama mkaa ambao haujaingia jikoni.

Yule mtu alipofika mbele aliweka sawa vipaza sauti na kuweka kando kinasa sauti kile cha kuongelea alichokuwa akitumia yule MC. Alisimama na kuangalia kulia kwake, kushoto, akageuka kuangalia nyuma walikokuwa wamekaa Mkuu na watu wengine.

Alianza kwa kusalimia wote huku akipunga mikono hewani na tukio hilo liliambatana na hali ya umeme kama wa radi kuwaka kwenye mikono yake.

Akaanza kwa kusema kuwa, hayupo tayari kupoteza muda kwa vile tulikuwa pale kwa ajili ya kuelimishana, kupeana uwezo na kutahadharishana.

Akasema: Kwa nyinyi mliopata nafasi ya kuwakilisha nchi zenu, tunapenda kuwahakikishia kwamba, kwanza mtabadilika, kutoka kwenye uwezo wa kuwa mchawi hadi kuwa pepo wachafu.
Kusita kwake kuongea kunaonekana kulitokana na ukweli kwamba, kila mtu alionekana kushtuka, akaendelea:

Ninaposema kuwa pepo wachafu nina maana kwamba, mtakuwa juu zaidi kupita wachawi. Nyinyi mtaweza kubadilika kutoka maumbile hayo na kuwa kitu chochote, upepo, moto, ndege, kisiwa, bahari, ziwa, yaani kitu chochote kile.

Akaendelea: Kuna mikakati mingi na mikubwa sana kuhusu nyinyi, kifupi mnatakiwa kuwa na uwezo wa kuwa kama majini sasa ambayo nguvu za uchawi haziwezi kushinda na wao ndiyo wanaosimamia kazi za majini.

Alipomaliza kusema, akamkaribisha Mkuu wa Nchi ambapo sote tuliokuwemo mle ndani tulitakiwa kusimama wakati kiongozi huyo akienda mbele na yule aliyekuwa mbele akirudi nyuma.

Tulisimama, akaenda mbele akitembea kama mtumishi wa Mungu anayekwenda kutoa Neno la Bwana kwa kondoo wake. Alipofika, alisimama wima na kwa heshima zote.


Je, nini kitaendelea? Usikose Kesho.....
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-14

Na leo hii akitokea Mchungaji akahubiri acheni dhambi mwende peponi, utakuta kanisa lake halijai, maana shetani amewafanya watu watafute ufalme wa duniani na si mbinguni.

Utakuta muumini anashuhudia mbele ya kanisa alivyopata gari la kisasa, alivyokubaliwa kupata mkopo wa mamilioni ya pesa peke yake wakati walikuwa waombaji hamsini, anaamini ni muujiza wakati haenendi katika roho, msengenyaji, mzinzi, mnafiki, hana heshima, huyo Mungu anayekutendea muujiza ni yupi kama si ibilisi?
Basi, Mkuu wa nchi akaendelea:

"Kwa tathimini ya hivi karibuni kabla ya kikao hiki, tumefanikiwa kwa sehemu kubwa sana kuyafanya makanisa yote ya kilokole kuwa kama yale mengine tu, kwani ndani ya makanisa haya siku hizi watu wote wapo, wapo wazinzi, wapo walevi, wapo wasengenyaji, wapo wezi. Kifupi si makanisa ya kiroho tena, ila tumewaziba akili wasijue wameshika kisichoshikika.
SASA ENDELEA…


"Lakini pia mnatakiwa kujua kuwa, mkiwa wenye uwezo wa kuwa pepo wachafu mtahakikisha mnabadili ratiba za vipindi vya Televisheni, Redio na Makala za kwenye magazeti, nyingi wapewe nafasi wanawake kujieleza, kuwe na vipindi vya wanawake kujikomboa, wanawake wawe wanamtaka wazi kuwa, ni wakati wa usawa.

Hii hali itadakiwa na wakuu wengine, sasa shughuli za kikazi, nyingi zinafanywa na wanawake, hata kama watakuwa hawawezi, lakini tutafanya mazingira ya kufumba macho na akili za watu ionekane kuna kuweza.

Hilo jingine, lakini kuna hili la kuhakikisha uchumi wa dunia unashikwa na wanawake, hili lazima lipigiwe vita kwa nguvu zote, lengo letu ni kupingana na utabiri wa vitabu vya aliyeumba nchi, yeye alisema siku za mwisho wanawake wengi watakuwa wakiishi na mwanaume mmoja na kujitegemea kwa kila kitu, lakini sisi tuhakikishe siku hizi za mwisho, mwanamke mmoja ndiyo aishi na wanaume wengi.

Kuhusu vifo, tunatakiwa kuelewa kwamba, kipindi hiki ndicho kwetu tunatakiwa kuvuna kwa wingi zaidi roho za watu, hivyo hakuna namna zaidi ya kuhakikisha watu wanaangamia kwa kila njia, kila namna.

Mtakuwa mkipita kwenye kingo za mito, bahari na maziwa na kuzifungua ili nchi ikumbwe na mafuriko, mtakuwa mkipaa angani na kuangusha ndege zenye abiria wengi, mtakuwa mkisababisha matetemeko makubwa sehemu na sehemu ili kuyasawazisha maghorofa yawe kama nyumba za kawaida na hivyo kuleta madhara.

Lakini kingine nilipitiwa kuwaambia, ndoa nyingi duniani zinalindwa na watoto. Huu ni utafiti tulioufanya kwa kutuma roho zetu mpaka kwenye jamii, kila kona na kila pande za nchi.

Katika kila ndoa kumi za halali zilizovunjika, ndoa tano zilichangiwa na kukosekana kwa watoto, ndugu wengi walichukua madaraka kwa kumshinikiza mwanaume amwache mke na kuoa mwingine."
Yule Mkuu wa nchi alipofika hapo, kuna mjumbe alinyoosha mkono. Huyu hakuwa na kibao kilichoonesha alitoka nchi gani.

Mkuu: Enhe, wewe, una swali?
Mjumbe: Ndiyo Mkuu.
Mkuu: Uliza utajibiwa.
Mjumbe: Sasa, ndoa kuvunjika, kutukuwepo watoto na mume kuoa mke mwingine, sisi tunapata faida gani?

Mkuu: Sawa, lengo letu ni kuvuruga utaratibu wa aliyeumba nchi na kuondoa amani duniani, watu wengi watakuwa hawaendi na maagizo ya aliyeumba nchi, hivyo tutafanikiwa kuwapotosha wengi na watakwenda motoni na sisi.

"Pia, mume akimwacha mkewe na kuoa mwingine si atakuwa anavunja ile amri yao na mnajua aliyeumba nchi hakuna kitu kinamkera kama kuachana."

Yule mjumbe alikaa, Mkuu akaangalia pande zote ili kuona kama kuna mtu mwingine ana swali.
Ilionekana hakuna mwenye swali, wote tulibaki kimya na ndiyo Mkuu aliendelea:

"Hakuna kati yenu ambaye atadhurika, kwani uwezo tunaowapa sisi ni mkubwa sana. Si wa kichawi ila ni wa kiroho, mtakuwa mnaweza kuingia sehemu yoyote ikiwa ni pamoja na kwenye mwili wa binadamu na kukaa moyoni mwake na kumgeuza mawazo, kutoka yale ya kumpendeza aliyeumba nchi na kumfanya awaze mabaya tu muda wote.

Kuhusu wanawake kutokuzaa, nyinyi mtakuwa mkiingia kukaa kwenye matumbo ya uzazi ya wanawake na kuharibu mfumo wa uwezo wa kupata ujauzito."

Alipomaliza kusema, alitoka kwenye mimbari na kuelekea walikotokea, wale aliokuja nao wakamfuata kwa nyuma na kupotea moja kwa moja.
Mara, akatokea yule mwanamke mwenye sauti nzuri lakini sura ya kutisha.

"Hatujafikia mwisho wa Mkutano wetu, sasa anakuja kiongozi mwingine ambaye anawafundisha jinsi ya kupata uwezo wa kuwa roho wanaoweza kuingia ndani ya mwili au mishipa ya fahamu ya binadamu na kuharibu uwezo wake na kufanyia kazi matakwa yenu.

Alipita mbele haraka mzee mmoja aliyekuwa amevaa suti ya kitambaa cha kaniki. Hii suti ilikuwa haina kola ya shingoni na alionekana amechoka kwa kufanya kazi kwa bidii au nzito.
Akasimama, akatuangalia kisha akapiga makofi mara tatu alipomaliza akaanza kwa kusema:

"Sina salamu ya mazoea, ingekuwa mlikotoka (duniani) ningewasalimia kwa kila mtu na jinsi anavyojua yeye.

Lakini nataka kuwaambia kuwa, ni wakati wa mavuno huu na si wa kuchezacheza. Nyinyi mlioamua kuwa kwetu na iwe hivyo, mpaka mmekuja huku naamini mmepitia mengi makubwa na mmeshinda, hakuna aliyekuja kwa upendeleo kwa sababu huku hakuna upendeleo wala rushwa, huku kila mtu anakuja kwa jinsi alivyokwishakataliwa na yule aliyeumba nchi."

Hapo nilishtuka sana, nikanyoosha kidole haraka.
Kiongozi: Una swali?
Mimi: Ndiyo.
Kiongozi: Uliza, utajibiwa.

Mimi: Umesema tuliokuja huku ni wale waliokwishakataliwa?
Kiongozi: Ndiyo. Swali lako liko wapi sasa?
Mimi: Ina maana sisi tulishakataliwa na Mungu?
Kiongozi: We! Acha.

Baadhi ya wajumbe: Wee, kelele ala!
Mara yule mwanamke ambaye yupo kama MC alisimama mbele, yule kiongozi akaondoka zake akitembea kama anachechemea.
Yule mwanamke alionekana kukasirika sana, aliniangalia kwa kunitumbulia macho na kushindwa kuongea.


Je, nini kitaendelea? Usikose Kesho.....
 
Kumbe hawaruhusiwi kumtaja Mungu (aliyeumba nchi)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-15

Lakini nataka kuwaambia kuwa, ni wakati wa mavuno huu na si wa kuchezacheza. Nyinyi mlioamua kuwa kwetu na iwe hivyo, mpaka mmekuja huku naamini mmepitia mengi makubwa na mmeshinda, hakuna aliyekuja kwa upendeleo kwa sababu huku hakuna upendeleo wala rushwa, huku kila mtu anakuja kwa jinsi alivyokwishakataliwa na yule aliyeumba nchi."
Hapo nilishtuka sana, nikanyoosha kidole haraka.

Kiongozi: Una swali?
Mimi: Ndiyo.
Kiongozi: Uliza, utajibiwa.
Mimi: Umesema tuliokuja huku ni wale waliokwishakataliwa?

Kiongozi: Ndiyo. Swali lako liko wapi sasa?
Mimi: Ina maana sisi tulishakataliwa na Mungu?
Kiongozi: We! Acha.

Baadhi ya wajumbe: Wee, kelele ala!
Mara yule mwanamke ambaye yupo kama MC alisimama mbele, yule kiongozi akaondoka zake akitembea kama anachechemea.
Yule mwanamke alionekana kukasirika sana, aliniangalia kwa kunitumbulia macho na kushindwa kuongea.
ENDELEA SASA…


Karibu kila aliyekuwemo ndani ya ukumbi aliniangalia mimi, lakini wapo walioonekana kuniangalia kwa macho ya kutojua kitu, wengine walionekana kujua.
Kusema ule ukweli mimi mwenyewe sikujua kwanini palitokea hali ile. Sikujua nini nilikikosea mpaka kuonekana wengine wakinishutumu wengine wakiniangalia kwa macho makali.
Kingine kilichonishangaza sana ni kitendo cha yule kiongozi kuondoka akitembea kwa mwendo wa kuchechemea.

Yule mwanamke akaniamuru nisimame, nikatii kisha akaniuliza kama nilipokuwa napita niliingizwa kwenye chumba cha sharti kuu, nikajibu sikumbuki.
Akaitwa mtu aliyenileta mpaka nje ya ukumbi huo, alipofika aliulizwa hivi:
"Huyu Mwakilishi kutoka nchi ya Tz ulimleta wewe?"
"Ndiyo."

"Ulimpeleka chumba cha sharti?"
"Hapana, nilisahau."
Ghafla Mkuu kabisa wa Nchi ile alitokea akiwa anatembea kwa kasi mpaka pale mbele na yule mwanamke akampisha kwenye eneo la kuzungumzia.

"Ni kwanini hukumpeleka kwenye chumba cha sharti wakati unajua kile ndiyo chumba muhimu sana kuliko vyote humu ndani, unataka tupate madhara siyo?"
Yule mtu alitulia tu kwa muda huku akiwa ameinamisha kichwa.

""Nisamehe Mkuu," hatimaye alisema akiwa bado ameinama, alikuwa haangalii popote pale.
"Sasa mchukue mpeleke, kisha mrudishe hapa haraka sana, kosa ni lako na utaadhibiwa wewe kwa sheria za Nchi hii," alisema Mkuu huku akiwa amemkazia macho.

Yule mtu, au tuseme yule kiumbe aliniangalia mimi kwa macho ya kunitaka kumfuata.
Njiani nilijiuliza maswali mengi sana, ni sharti gani hilo ambalo haikuwezekana mimi kuambiwa mle mle ukumbini mpaka nifike kwenye chumba hicho?
Alitembea mimi nikimfuata kwa nyuma mpaka akasimama mbele ya jengo moja la wastani, kwa nje lilionekana kama ofisi nzuri na ya kisasa.

Na mimi nikasimama nyuma yake, akafungua mlango na kuniambia:
"Ingia humu ndani, utakutana na tangazo kubwa jeupe ukutani, ukishalisoma hutakiwi kutoka na kuuliza swali jingine kwa sababu maelekezo yake yako humo kwenye tangazo mwanzo hadi mwisho."
Nilikubali kwa kutingisha kichwa. Akaendelea:

"Ufanye haraka kwa sababu kule hawawezi kuendelea na kikao mpaka wewe urudi."
Pia nilikubali kwa kutingisha kichwa huku nikiingia lakini nikiwa gizani na kitu ambacho nitakikuta huko ndani.

Baada ya kuingia, nilikutana na mlango mwingine tena, huu ni wa kioo, kioo cha kujiangalia lakini nikiwa nashangaa shangaa, ghafla mlango huo ulifunguka wenyewe na kunipa nafasi ya mimi kupita.

Nikaingia na kutokea kwenye chumba cha wastani, ukutani kulikuwa na tangazo lenye maandishi makubwa yanayosomeka hivi:
"UKIWA KWENYE NCHI YA WACHAWI EPUKA KUTAJA NENO MUNGU, UNAWEZA KUUAWA USIRUDI ULIKOTOKA. KUANZIA SASA FUNGA KINYWA CHAKO KUHUSU JINA HILI."

Nilijikuta nikiguna bila kutarajia, kila kitu kwenye mwili wangu kililegea, mara nikasika mlio wa kengere kisha kwenye lile tangazo kukawaka taa nyekundu, lakini ilikuwa ikimulika kama ‘indiketa' ya gari.

Nilitoka mbio, nikamkuta yule mtu ananisubiri akiwa anaonekana kukasirika sana. Aliponiona tu aligeuza na kuanza kuondoka. Ina maana aliamini kuwa, kwa kitendo cha yeye kugeuka mimi nitajua natakiwa kumfuata nyuma kurudi kule ukumbini.

Basi, tulikwenda kwa mtindo ule ule, lakini njiani alianza kulia jambo ambalo lilinishangaza sana mimi.
"Unalia nini sasa?"
Nimekwisha," alinijibu.
"Umekwisha! Umekwishaje?"

"Unadhani ni adhabu gani nitapewa?"
"Sijui, kwani ni adhabu gani?"
"Kifo tu, ndiyo adhabu kubwa ya huku!"
Nilishtuka sana, nikamuuliza:

"Wewe umejuaje?"
Akanigeukia na kusema:
"Ndiyo adhabu kubwa ya huku."
"Kwanini kusiwe na adhabu nyingine?"
"Hakuna, kama ipi?"

"Kupigwa viboko, kunyimwa chakula."
"Viboko hatuumii, chakula huwa hatuli, hata ukinipiga na panga hapo huwezi kunikata mimi."
Kusema ule ukweli nilishangaa sana, lakini bado nikawa na dukuduku, kama alivyokuwa anaongea ni kweli, sasa wataamuaje?
"Sasa kama ni hivyo utauawa vipi?" Nilimuuliza.

"Nawekewa mkono kichwani kisha nasemewa maneno fulani."
Mpaka hapo tukawa tumefika kwenye geti la kuingilia ndani ya jengo la mkutano.
Nje, tulikutana na kiumbe kimoja kina sura mbaya sijapata kuona hata kwenye michoro ya hadithi za kutisha.

Alikuwa na sikio moja tu, upande wa kushoto, jicho moja katikati ya paji la uso likiwa limevimba kama linataka kutoka, mdomo mrefu lakini upo upande kidogo na kidevu kilichopindia kulia.
Wakati najiandaa kumwangalia miguuni, alimshika yule mtu niliyeongozana naye mimi na kuondoka naye.

Niliogopa sana, lakini wakati niko kwenye mshangao, nilishikwa bega la kushoto na mtu au kiumbe kisichoonekana:
"Ingia ndani ya mkutano unasubiriwa wewe tu," sauti nene lakini isiyo na utulivu iliniambia.

Haraka sana nikazama ndani na kukutana na macho ya wote waliokuwemo ukumbini wakinikodolea mimi.


Je, nini kitaendelea?
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-16

Alikuwa na sikio moja tu, upande wa kushoto, jicho moja katikati ya paji la uso likiwa limevimba kama linataka kutoka, mdomo mrefu lakini upo upande kidogo na kidevu kilichopindia kulia.

Wakati najiandaa kumwangalia miguuni, alimshika yule mtu niliyeongozana naye mimi na kuondoka naye.
Niliogopa sana, lakini wakati niko kwenye mshangao, nilishikwa bega la kushoto na mtu au kiumbe kisichoonekana:

Ingia ndani ya mkutano unasubiriwa wewe tu, sauti nene lakini isiyo na utulivu iliniambia.
Haraka sana nikazama ndani na kukutana na macho ya wote waliokuwemo ukumbini wakinikodolea mimi.
SASA ENDELEA



Mpaka hapo sasa nikawa nimeshajua kwanini niliwashtua watu kwa kauli yangu ile. Kumbe jina la Mungu kwenye makao makuu ya viumbe wale ni sumu kwao inayoweza kuwaangamiza mara moja. Kama mimi nilipolitamka mara moja tu kiongozi wao akatembea kwa kuchechemea huku akishindwa kuendelea na hotuba je, ningelirudia?

Nikiwa ndani, nilisimama mbele, yule Mkuu wa Nchi akaja, alinishika na kuniangalia kwa muda, kisha akasema:
Unajua kuna mwananchi wangu ameshakufa?
Nikamjibu: Mimi sijui, kafaje?

Mkuu: Si kitendo chake cha kutokukupeleka kwenye chumba kile ulichokwenda sasa hivi. Hivi hapa kuna Msaidizi wangu Mkuu ameugua ghafla. Lakini ni salama kwako, kwani kama ingethibitika alikupeleka ungekufa wewe kifo kilekile.

Nilitamani pia kumuuliza lile jina linawaathiri vipi, lakini kabla sijafikia huko, yeye mwenyewe alisema:

Sisi huku hatutumii baadhi ya majina, kwani yana madhara na ndiyo maana tuko mstari wa mbele kuhakikisha tunawaumiza watu ili kumtesa aliyeumba nchi.

Mara, mtu mmoja ambaye naye alikuwa mjumbe kama mimi, alikurupuka na kusema:
Jina la Yesu je?

Ghafla, ukumbini kulisikika mlio kama wa bomu zito huku moshi mkubwa na mzito ukifunika na kusababisha giza nene.
Vilio kutoka kila kona vilisikika, baadhi ya watu walisikika wakisema kwa kuomboleza kwamba, wanakufa huku mimi nikiwa nimesimama palepale.

Niliangalia pale aliposimama Mkuu wa Nchi, hakuwepo! Ilinishtua sana, nilijua niliyebaki mzima ni mimi peke yangu.

Lakini hali ilianza kutulia, ule moshi ukapungua, giza likaondoka, nilipoangalia wenzangu, wengi walikuwa hoi kama wamelewa, lakini waliokuwa wazima sana ni wajumbe tuliokwenda pale tu. Ina maana kwamba, kutajwa kwa jina la Yesu kuliwaathiri zaidi wale viumbe wa kule.

Sasa sisi tuliokuwa na afya zetu, tuliangaliana na kuulizana kwa mikono nini kifuate pale?

Tunaomba utulivu kwa wote, tafadhali sana wageni wetu, tutulie kila mmoja pale alipo akae kwa matumaini kwani hali ni salama,

sauti nyembamba, sauti ya mwanamke ilisikika bila kujua ilikotokea.
Kweli, wote tulijikuta tukitulia huku kila mmoja akiangalia pande zote za dunia. Ilikuwa hali ya kutisha sana, wengine walionekana kutulia lakini wakitetemeka sana.

Baada ya muda, Mkuu wa Nchi atafika, kwa hiyo kila mjumbe aliyoko mahali hapa atatakiwa kutega sikio kumsikiliza atakachokisema.
Ile sauti ikaendelea:

Wewe uliyesimama mbele, tafadhali sana, tena sana rudi kwenye makao yako ya awali, kwa sasa tunaongelea zaidi dharura.
Nilirejea kwenye kiti changu, nikakaa. Muda wote huo yule mjumbe aliyelitaja jina la Yesu alikuwa akilia, kichwa amekiinamisha kwa unyonge mkubwa. Alionekana kama anajutia alilolisema.

Sauti hiyo ilipokuwa kimya, tukasikia mlio wa viatu kutoka kusikojulikana ukitembea kuelekea tulikokuwa, ilifika mahali tukahisi mtu huyo anayetembea yuko mbele yetu na alibakiza hatua kadhaa amfikie aliyekuwa akimtaka au alipokuwa akipataka.

Mara yule mtu aliyetaja jina la Yesu akalia mama nakufa! Akaanguka chini, damu zikawa zinamtoka kwa wingi kinywani, puani, masikioni na kwenye macho.

Wajumbe wote tulimzunguka na kumshangaa, wengine wakamwekea mikono mwilini kumpima hali yake lakini kusema ule ukweli mpaka muda huo mwenzetu alishakuwa marehemu.

Tukiwa tunashangaa shangaa, tukasikia mlio tena wa vile viatu ukitembea kutoka pale tulipomzunguka mwenzetu kuelekea ulikotoka.
Huu mlio, kwa kweli ulisikika katika tafsiri kwamba, aliyekuwa akitembea alikuwa akivuta hatua ndefu kidogo mpaka ulipopotea masikioni mwetu.

Mara, Mkuu wa Nchi akatokea akitembea kwa mwendo wa kusuasua. Alipofika mbele alisimama na kuachia tabasamu la aina fulani, kisha akasema:

Lakini Mkutano wa mwaka huu vifo si vingi, wale waliokuwepo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka jana wanyooshe mikono yao juu.
Kisha akawa anaangalia huku na kule kama vile alitaka kuhesabu, akawa anatingisha kichwa.

Ilionesha ni nusu kwa nusu, kati yetu sisi wapya na wale waliokuwepo mwaka jana. Yule Mkuu akaendelea:

Je, mwaka jana mpaka sasa humu wangekuwa wamepoteza maisha wangapi?
Wengi tu, watu wa mwaka jana walijibu.
Wengi tu, alirudia kauli yule Mkuu. Akaendelea:

Kusema kweli hapa tunakutana kibinadamu sana, kwani tukisema sisi wenyeweji tuwe kama tunavyotakiwa kuwa mtatukimbia, ndiyo maana tunajitahidi kujibadilisha ili tuonekane nasi ni binadamu kama wengine.
Akaendelea kwa kuuliza swali:
Au mnataka tuwe kama tunavyokuwa kwa asili?

Mimi binafsi niliingiwa na shauku ya kutaka kujua viumbe wale huwa wanakuwaje?
Tukajikuta wote tukijibu:
Ndiyooo.

Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua, yule Mkuu alirefuka huku tunamwona, masikio yake yakawa marefu kama ya mnyama, sura yake ilibadilika pia, jicho lake moja lilikaa juu ya paji la uso, halafu akaota mapembe mawili kwa kila upande moja.

Meno yake yalichomoza kwa mbele urefu wa wembe na kidevu kilishuka kwa urefu wa chupa ndogo ya chai. Tukiwa tunafikicha macho kwa kutoamini tulichokuwa tukikiona, mara akatokea yule dada MC, yeye alikuwa kituko zaidi, alikuwa mwembamba mfano wa katuni mbaya, kiuno chembamba sana, miguu nilidhani ni vidole vilivyopata uwezo wa kusimama.


Je, nini kilitokea hapo? Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua Kesho.............
 
Back
Top Bottom