Hadithi ya kusisimua: Nchi ya wachawi-1

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI -1

BUNDUKI YA KICHAWI.jpg




BUNDUKI NDOGO.jpg





Picha za Juu mfano wa picha za bunduki za kichawi.

"Kwa jina naitwa Israeli, lakini si yule mtoa roho za watu, hili ni jina ambalo linapatikana katika utaratibu wa maisha ya kila siku duniani.

Nimezaliwa mwaka 1950, (kwa sasa 2010 ana miaka 60) wilayani Misungwi, mkoani Mwanza, ni mtoto wa kwanza katika familia yenye kujiweza kidogo kimaisha, ikiwa na watoto tisa, wote wanaume. Wazazi wangu (sasa marehemu) walikuwa wacha Mungu sana.

Kama kweli kuna uhai baada ya kifo na wakayajua mambo yangu ya duniani, naamini nimewaumiza sana wazazi wangu.

Kwa sasa naishi Mbagala, jijini Dar es Salaam na familia yangu yenye mke na watoto saba, wote wa kike. Mke wangu pia kwao ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto tisa, wote wanawake.

Nimelazimika kusimulia mkasa huu wa kichawi baada ya watu wengi kusimulia mikasa yao wakidai waliwahi kuwa wachawi wakaacha kwa sababu mbalimbali ambazo wengine huzisema, wengine hufanya siri kubwa.

Naweza kusema kwamba, karibu wote waliokuwa wakisimulia maisha yao ya kichawi na mikasa yake, hakuna hata mmoja aliyewahi kufikia hata robo ya maisha ya kichawi ya kwangu.

Mimi niliishi maisha hayo kwa miaka kumi, na nilifika levo' ya mbali, mfano kuwa Mkuu wa Kikundi na kusafiri sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya mikutano mikubwa ya kimataifa ya wachawi.


Niliporudi, nilikuwa nakutana na wachawi wakubwa wa hapa nyumbani Tanzania na kuwapa maagizo ya utendaji katika makundi yao sehemu mbalimbali za nchi.

Katika kipindi chote cha kuwa mchawi nilibaini mambo makubwa mawili, kwamba, maisha ya wachawi katika ulimwengu wao hayana tofauti yoyote na maisha ya watu wasio wachawi katika ulimwengu huu wa macho ya kawaida.

Maandiko yanaposema kuwa, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana ni kweli kabisa. Wachawi wanaamini kwamba, vitu visivyoonekana pia vilikuwa na siku sita katika uumbaji wa Mungu, siku ya saba akapumzika.


Na hiyo ndiyo sera ya mchawi mara tu baada ya kujiunga katika kazi hiyo inayolaaniwa na wengi ulimwenguni kote.

Kabla sijaenda mbele zaidi nataka kusema kuwa, kama kuna shughuli mbalimbali za binadamu zinazoonekana kwa macho ya kawaida duniani, pia kuna shughuli kama hizo hizo zisizoonekana kwa macho ya kawaida, lakini zinashirikisha wachawi na mambo yao.

Itaendelea Mukinipa
(Like) Kazi kwenu .......
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-2

ILIPOISHIA:
Kabla sijaenda mbele zaidi nataka kusema kuwa, kama kuna shughuli mbalimbali za binadamu zinazoonekana kwa macho ya kawaida duniani, pia kuna shuguli kama hizo hizo zisizoonekana kwa macho ya kawaida, lakini zinashirikisha wachawi na mambo yao.
SASA ENDELEA…


Wachawi wana kila kitu, wana mikutano ya nchi, mikutano ya kimataifa, ya kanda ya mabara na pia wana mabenki, japokuwa kwa macho tunazungumzia mabenki ya pesa, wao wana mabenki ya damu, nyama na dawa za kienyeji.

Huwa wanakopeshana, wanalipana na wapo wasiotaka kulipa ambapo huchukuliwa adhabu mbalimbali kulingana na makosa. Zipo nchi ambazo wachawi wake wanafukuzwa katika uanachama, zipo zinazoingizwa, wapo wakuu wa wachawi wa nchi wanaopinduliwa wengine hata kuuawa na pia kunakuwa na uchaguzi mkuu kila baada ya miaka mitano kuchagua viongozi wa kichawi wa nchi husika ambapo wapiga kura huandikisha majina yao na kuwa na vitambulisho vya kupigia kura.

Pia kuna bendara ya umoja wa wachawi barani Afrika, Ulaya na duniani kote. Aidha, kila nchi ina bendera yake inayoonesha utambulisho wa kitaifa. Mfano, bendera ya kichawi ya Tanzania ni rangi nyekundu, nyeusi na kahawia, katikati ina picha ya mnyama Twiga.
Nchi ya Nigeria, bendera yake ya kichawi ina rangi nyekundu bila mchanganyiko, katikati ina picha ya mkono mweusi umeshika kibuyu chenye shanga.

Kuna wachawi wanaofanya biashara za kimataifa, mfano kutoa dawa za kienyeji Tanzania kupeleka India kwa njia za kichawi na kule mchawi anaweza kununua ngozi za wanyama akaja kuuza Tanzania, Kenya au Uganda kwa wachawi wengine ambao hawana mitaji mikubwa.

Ilikuwa mwaka 1980 nikiwa na umri wa miaka thelathini tu, ndipo niliposhawishiwa na mzee mmoja, sasa marehemu kujiunga na wachawi. Huyu mzee namtaja kwa jina moja la Madume, tulikutana kwenye shughuli ya uvuvi samaki ziwani Victoria, alitokea kunipenda sana kutokana na tabia yangu njema na kuwa kama kijana wake.
Usiku mmoja nikiwa nimelala alinijia katika ndoto, lakini baadaye niligundua ilikuwa 'laivu'.

"Kijana wangu Israeli, unaoenekana unaweza kukifanya kile ambacho mimi ninacho, nitafurahi sana kama utakipenda ili nikupe," aliniambia kwa sauti ya utu uzima.
"Kwa wewe baba nitapenda, na ikibidi naomba unipe sasa," nilimjibu.

Mzee Madume akanishika mkono na kunivuta, nikasimama. Tulisimama sanjari, akanisogezea uso wake kwenye uso wangu, kwa hiyo pua yake ikagusa pua yangu, midomo yake ikawa kwenye midomo yangu, paji lake la uso halikadhalika, kuna wakati alitembeza uso wake mpaka kidevu chake kikagusana na changu.

Kufumba na kufumbua, tukawa kwenye nyumba ya udongo, dhaifu kwa kila hali, katika chumba ambacho koroboi ndiyo ilikuwa ikitoa mwanga hafifu uliofanya tuonane kwa tabu. Tulikuwa watatu, mimi, mzee Madume na mtu tuliyemkuta ndani ya chumba kile.

"Kaa chini kijana wangu," mzee Madume aliniambia kwa sauti ileile niliyoizoea.
Nilikaa chini kwenye ngozi nyeusi, kila nilipokuwa nikimkamata sura yule mtu tuliyemkuta mle ndani, kibatari kilipoteza nuru na kumfanya aonekane kwa tabu kidogo, hivyo kuna wakati nililazimika kufumbua macho mpaka mwisho ili nipate nafasi ya kuona sawasawa.
"Fumba macho," mzee Madume aliniambia, lakini si kwa amri.

Nilifumba macho na kusubiri tamko jingine kutoka kwa mzee huyo au yule mwenyeji wetu. Nilihisi hali ya kama maji yakinigusa mwilini, kuanzia shingoni kuteremka na uti wa mgongo hadi kiunoni. Yalikuwa ya baridi mfano wake hakuna, nikasema siiiii.

"Sii nini kijana wangu? Wewe sasa ni mtu kama mimi, utaishi kama mimi na wala hakuna binadamu yeyote atakayekuweza," mzee Madume aliniambia lakini tukiwa palepale kwenye kitanda alichonikuta.

"Ha!" Nilisema na kushtuka.


Je, nini kitatokea? Usikose Itaendelea Kesho
 
👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI-3-

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Nilifumba macho na kusubiri tamko jingine kutoka kwa mzee huyo au yule mwenyeji wetu. Nilihisi hali ya kama maji yakinigusa mwilini, kuanzia shingoni kuteremka na uti wa mgongo hadi kiunoni. Yalikuwa ya baridi mfano wake hakuna, nikasema siiiii.
Sii nini kijana wangu? Wewe sasa ni mtu kama mimi, utaishi kama mimi na wala hakuna binadamu yeyote atakayekuweza, mzee Madume aliniambia lakini tukiwa palepale kwenye kitanda alichonikuta.
Ha! Nilisema na kushtuka.
SASA ENDELEA


Ha nini kijana wangu?
Si tulikuwa kwenye..!

Kwenye nini kijana wangu? Nimekukuta hapa na hata sasa tuko hapahapa, alisema, lakini safari hii akiachia tabasamu pana kidogo tofauti na mara zote, nikajua ananitania tu, lakini ukweli tulikwenda mahali.
Nahisi kama naota, kwanza umeingiaje humu ndani kwangu? Nilimuuliza.

Aa, hata wewe utaweza kijana wangu, ndiyo maana nimekwambia wewe sasa ni mtu kama mimi, utaishi kama mimi na wala hakuna binadamu yeyote atakayekuweza.

Nilitaka kumwambia kitu, lakini sikumwona mle ndani, nikashtuka zaidi na kujikuta nimekaa kitadani. Sasa jasho jembamba lilinichuruzika mwilini, hofu ilinipanda, niliamini niliingiliwa na kiumbe wa ajabu aliyejifanya binadamu ninayemfahamu. Niliangalia huku na kule lakini sikuona mtu.

Nilitoka nje, nikasimama kwa muda mlangoni kuangaza kama ningeona kiumbe cha ajabu, pengine kama mtu, lakini mwenyewe akiwa na mguu mmoja, mkono mmoja, jicho moja na kalio moja, lakini hakukuwa na dalili yoyote. Hivyo nilirudi ndani nikifunga mlango kwa uhakika na kujiami, moyoni nikisema: Simfungulii mtu yeyote akitaka kuingia.

***
Nilishtuka asubuhi ya saa kumi na mbili, nikatoka kitandani haraka sana, nilikwenda nje nikiwa na shuka tu. Nilipofika niliangaza huku na kule, nikaona mambo ni shwari, nikarudi ndani.

Nilijiandaa kwa ajili ya kwenda ziwani ambapo nilipofika mtu wa kwanza kukutana naye ni mzee Madume ambaye alinilaki kwa furaha sana huku akinisifu kwa kuwahi kuliko siku nyingine.

Kijana wangu, umewahi, hongera sana. Good.
Nilimkubalia huku nikiuonesha uso wangu kuwa, hauna amani kama siku zote. Naamini hata yeye alinijua kwani alionekana kusinyaisha sura yake.

Kikubwa ambacho alinishangaza ni kitendo cha kunisifia kuwahi wakati ilikuwa kawaida yangu. Labda mimi ndiyo ningeshangaa kwa yeye kuwahi kwani haikuwa kawaida yake, mara nyingi alikuwa akifika jua liko juu.
Basi, nilibadili nguo, kwa kuvua nilizokwenda nazo na kuvaa za kazi, yeye alikuwa ameshabadili za kwake. Wakati navua nguo ili nivae, alinisogelea na kunishika begani na kuniambia:

Uko tayari ufanye majaabu kwa kazi hii ye leo?
Nilisitisha nilichokuwa nakifanya na kumkazia macho ya mshangao:
Wewe nijibu kwanza, unashangaa nini? Wewe kijana wangu bwana.

Nilimkubalia kwa kutingisha kichwa kisha nikatulia kumsikiliza alitaka kuniambia nini. Wakati huo huo akili ikanikumbusha lile tukio la usiku na mzee huyo huyo, nikataka kumuuliza, lakini nikasema moyoni, si ndoto tu.
Kabla hatujaanza shughuli nenda kasimame pale, aliniambia akionesha kidole kwenye mashua moja chakavu saana.
Nilikuwa nimemaliza kuvua na kuvaa nguo nyingine, nikaenda mpaka pale aliponielekeza palikuwa na umbali wa kama hatua kumi za miguu ya mtu mzima.

Wakati nakwenda niligeuka kumwangalia nikiamini kuwa na yeye anakuja nyuma yangu, lakini kumbe ilikuwa ni mimi tu ndiyo nikasimame pale.

Baada ya kusimama niligeuka kumwangalia, yeye naye akawa anageuka huku na kule kuangalia wenzetu wengine kama wanakuja, kasha akaniambia:

Sasa kijana wangu, mimi nakuja huko huku kama nakimbia kidogo, na wewe fanya hivyo hivyo, njoo kama unakimbia, tukikutana tunagonganisha vifua vyetu, halafu utaona matokeo yake tukiingia ziwani.
Nilimkubalia kwa kutingisha kichwa, akaanza kuja huku kama anakimbia, na mimi nilianza kufanya kama yeye, tulikutana katikati ya umbali, tukagongeshana vifua tii.

Rudi kinyumenyume hadi pale pale kisha tunaanza upya, mara tu ndiyo kipimo chake, alisema akiwa anarudi bila kuangalia nyuma.

Wakati tunakimbia kwa mara ya tatu, kabla hatujakutana, wavuvi wawili walitokea na kutushangaa.
Ha! Nyiye, huo ni uchawi au mazoezi? Mmoja alisema, mwenzake akasisitiza kuwa, ni uchawi na kuanza kulalamika kuwa, kumbe ndiyo maana amekuwa akifanya vibaya kazini kumbe kuna watu wanaroga.

Alisema maneno machafu sana licha ya yule mzee kumwomba samahani tena akimwomba asije kusema kwa wavuvi wengine wa eneo letu, lakini yule mzee hakutaka kuelewa, aliendelea kutoa maneno ya kejeli na shutuma.
Nilimwona Mzee Madume ameanza kukasirika huku akiinama na kuchota mchanga mwingi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto, akakifumba na mchanga wake kisha akaumwaga pale pale alipouchota.

Sijui nini kilitokea, lakini ghafla wale watu, wote wawili walikimbilia majini na kujirusha huko kimyakimya.
Licha ya kuingia wenyewe, walijitahidi kupiga mbizi ili wasinywe maji, lakini wapi! Wakazama na kutoonekana tena juu.

Niliogopa sana, nilimwogopa sana mzee Madume na kitendo kile. Ilibaki kidogo na mimi nianze kutimua mbio kurudi kwangu. Wakati huo, mke wangu na watoto wawili walikuwa kijijini kwa wazazi wangu kutokana na ugumu wa maisha niliokuwa nao kwa wakati huo.

Kijana wangu usikimbie, mimi si mbaya kwako, ila hawa walitaka kutuhadhiri, we unadhani ingekuwaje leo baada ya wavuvi wengine kufika na kuambiwa? Aliniambia mzee Madume akiwa amenitumbulia macho.
Je, nini kitatokea?


Usikose kufuatilia Kesho wakati kama huu................
 
HADITHI YA KUSISIMUWA NCHI YA WACHAWI -4

Sijui nini kilitokea, lakini ghafla wale watu, wote wawili walikimbilia majini na kujirusha huko kimyakimya.
Licha ya kuingia wenyewe, walijitahidi kupiga mbizi ili wasinywe maji, lakini wapi! Wakazama na kutoonekana tena juu.
Niliogopa sana, nilimwogopa sana mzee Madume na kitendo kile. Ilibaki kidogo na mimi nianze kutimua mbio kurudi kwangu. Wakati huo, mke wangu na watoto wawili walikuwa kijijini kwa wazazi wangu kutokana na ugumu wa maisha niliokuwa nao kwa wakati huo.
Kijana wangu usikimbie, mimi si mbaya kwako, ila hawa walitaka kutuhadhiri, we unadhani ingekuwaje leo baada ya wavuvi wengine kufika na kuambiwa? Aliniambia mzee Madume akiwa amenitumbulia macho.
SASA ENDELEA


Hapana, wewe si mwema kwangu, nilimwambia.
Simama kijana wangu.
Sisimami mzee.

Hapana, nakutakia mema tu.
Mema si hayo mzee wangu.
Ungesimama basi ili unisikie kwa umakini.

Sina haja kwani nimeona kwa macho.
Hujaona kijana, simama uone sasa.
Niliendelea kukimbia hadi kwenye kibanda kimoja jirani kabisa na akina mama wanauza chakula, nikasimama pale.

Kwa hali yangu ilivyokuwa, wale akina mama waliniuliza nini kilinipata.
Hakuna kitu.
Hakuna kitu wakati unaonekana haupo sawa?

Nipo sawa mama zangu.
Unafukuzwa na nani?
Hata, nakimbia mwenyewe tu.

Nilipoangalia kwa mbali upande niliotokea, nilimwona yule mzee akija mbio.
Kwa vile nilikuwa na watu wengine sikuona sababu ya kukimbia, nilisubiri afike ili nimsikie, lakini pia sikuwaambia wale watu habari za yule mzee.

Mwanamke mmoja alipomwona yule mzee anakuja huku anakimbia, aligeuka kuniangalia na mimi.
Mpo pamoja na huyu mzee?Aliniuliza.

Nilifikiria kwa muda cha kujibu, lakini likaja lenyewe.
Hapana, simjui.
Mbona anatokea ulikotokea wewe?
Kwani haitakiwi?

Yule mama akabaki kimya kwa jibu langu hilo. Lakini aliendelea kuwa matumatu kwa kuangalia kwa yule mzee na kwangu.
Inaonekana alikuwa akisoma mambo fulani usoni kwangu, kwani kuna wakati alianza kutabasamu.

Yule mzee alipofika, akanishika mkono.
Jamani namchukua kijana wangu, alisema.
Sawa, lakini mwenyewe mbona alikataa hamjuani? Yule mama alihoji akipakulia chakula wateja wake.
Aa, unajua tena, ujana unamsumbua, alisema yule mzee.

Ujana au kuna tatizo? Yule mama akauliza tena. Alionekana yeye aliguswa sana na mazingira yale kuliko mtu mwingine pale.
Ujana tu.
Sawa, lakini iwe amani siyo kesho na keshokutwa tunasikia mengine.

Wala hakuna hatari, alimalizia kusema yule mzee.
Sijui kwanini kwani nilikubali kirahisi kukokotwa na yule mzee wakati si kawaida. Niliamini ana mambo yake ya kumfanya mtu alegee kiakili.

Tulirudi mpaka kwenye kile kibanda, akaniambia nikae chini kwani hata yeye alitakiwa kukaa.
Nilikaa nikimtazama kwa macho ya woga sana.

Niambie sasa, nilisema.
Kijana, kazi tunayofanya kubwa sana na ya hatari, hivi unajua kama ziwani kuna vitu vingi sana? Kuna viumbe, samaki, maji na vingine vingi vinavyoonekana na visivyoonekana, unajua hilo?
Najua.

Enhee! Kama unajua hilo jua na hili. Ili tufanikiwe tunahitaji kufanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuisikiliza mizimu, hivi huoni mi mwenzenu ninavyoendelea kila kukicha?
Ki ukweli katika wavuvi wote, yule mzee ndiye aliyekuwa amepiga hatua sana kuliko wengine, kwa hiyo kwa kauli yake hiyo na mimi nilijikuta nikihamasika kutaka kuwa kama yeye.

Kwa hiyo mzee wangu tufanyaje?
Hilo neno. Sasa nataka wewe uwe kama mimi, unakubali? Alisema akiniangalia kwa macho ya kujiamini.
Niko tayari.

Mzee Madume alicheka sana, akataka hata kuanguka chini kiasi kwamba, niliamini alikuwa anatania kumbe, hakuna lolote.
Kwanini unacheka sana?

Ndiyo nacheka kijana wangu, unajua wengi nimetaka kuwaingiza huku wamekataa, mpaka leo wanasumbuka na maisha.
Kwa hiyo mimi sitasumbuka nikiingia huko uliko wewe mzee?
Wala, ni raha tupu!

Niko tayari mzee wangu, tunafanyaje kwani?
Hakuna cha kufanya, hebu twende mara moja, alisema akinyoosha miguu pale alipokaa.
Nilibaki nimetumbulia macho nisijue la kufanya.

Na wewe nyoosha kama mimi, alisema mzee Madume akiniangalia huku akicheka.
Nikanyoosha miguu, mara tukafutika pale, kwangu nilihisi kizunguzungu mpaka tulipojikuta tupo sehemu ya wazi. Kuna mwanga lakini hakuna jua, kuna majani ya kijani kwa wingi huku miti ikiwa sehemu kwa sehemu.
Hapa tumefika, alisema yule mzee.

Kwa hiyo kuna sehemu tunakwenda?
Hapana, tumefika.
Ni wapi? Nilimuuliza.
We unahisi wapi?

Niliangalia kulia, kushoto, juu na chini.
Moshi?
Hapana.
Iringa.

Hapana.
Basi, Dar es Salaam.
Umekosea.

Sasa wapi?
Hapa ni chini ya maji ziwa Victoria, kwa hiyo tumetoka juu tumekuja chini.
Nilishtuka sana.


Je, nini kitaendelea? Usikose Kesho......
 
Back
Top Bottom